Historia ya Mitaa mbali mbali ya Jiji la Dar Es Salaam

Kwa nini iliitwa majina hayo?

Azikiwe, Samora, Pamba, Garden, Mkwepu, Makunganya, Shauri Moyo, Jamhuri,
Uhuru, Kongo, Chole,............ongezea mingine,

Nnamdi Azikiwe alikuwa ni kiongozi wa kwanza wa Nigeria mara baaya uhuru wa nchi hiyo. Barabara yetu ile maarufu imepewa jina hilo kama kumbukumbu yake. Alifariki mwaka 1996.

Samora Machel naye, kama Azikiwe, alikuwa ni kiongozi wa Msumbiji aliyepinga utawala wa amakaburu wa Afrika Kusini. Alifariki kwenye ajali ya ndege mwaka 1986. Mjane wake ndio mke wa Mandela wa sasa.

Hassan Omari Makunganya alikuwa kiongozi wa Wangindo (sina uhakika sana na kabila). Aliongoza watu wake kupigana na Wajerumani dhihi ya utawala wa Wajerumani. Alishirikiana na akina Kinjekitile Ngwale katika vita iliyojulikana kama Majimaji (1905 - 1907)
 
mtaa wa Lindi...
Mtaa huu ndio mrefu kuliko mitaa yote hapa Dar.

Mtaa wa Agrey...
Huu ni mtaa wa pili kwa urefu Dar.

Mtaa wa Congo...
upo Kariakoo.
Huu ni mtaa ambao una pilika na Tashtiti kuliko mitaa yote Tanzania.
Halahala, Mtaa huu ukijishaua kuzubaa tu unaibiwa.

Mtaa wa Sikukuu...
Mtaa huu ni mtaa unaouza madiko diko usiku kucha.
Nenda muda wowote mtaa huu utapata Chakula.
huu pia uko Kariakoo.

Mtaa wa Chui...
Pia nao upo Kariakoo.
Ni mtaa unaoaminika kuwa na walaji Mirungi kuliko mtaa wowote Dar es Salam.

Mtaa wa Pemba...
Upo Kariakoo.
Umelaaniwa, hauna Lami.
kwa taarifa yako mtaa huu unapita katikati ya soko kuu la Kariakoo.

Mtaa wa Swahili.
Huu mtaa upo Kariakoo.
Mtaa huu unaanzia Kariakoo Shimoni unaishia Gerezani.

Mtaa wa Twiga.
Upo Kariakoo.
Ndipo lilipo jengo la club yenye mafanikio zaidi hapa nchini.
Hapa naizungumzia club ya YANGA.

Itaendelea...
 
mtaa wa mtogole je?


Kuna haja ya kuelimishwa kutofautisha kati ya Barabara, Mtaa na kitongoji.
Mtoa mada anataka kujuwa historia ya mitaa mbalimbali hapa Dar halafu ndani ya thread yake anaweka CHOLE bila kufahamu kuwa CHOLE ni barabara na si mtaa.

Hivyo na wewe umepazungumzia kwa Mtogole.
Kwa Mtogole ni kitongoji, kama ilivyo kwa Tumbo, kwa Sadala, kwa bi Nyau, kwa Aziz Ally, au kwa Gang Chomba na si mtaa...
 
Asante Ritz kwa swali lako.
Awali ya yote napenda kukuelewesha kuwa sijasema mtaa wa Lindi ni mrefu kuliko yote Kariakoo.
Nimesema mtaa wa Lindi ni mrefu kuliko yote hapo Dar na unaanzia Mnazi mmoja mpaka Ilala...

Mkuu mtaa wa Lindi na mtaa wa Congo au Msimbazi upi mrefu au mtaa wa Agrrey.
 
Mkuu mtaa wa Lindi na mtaa wa Congo au Msimbazi upi mrefu au mtaa wa Agrrey.


asante Ritz...
Mtaa wa Lindi unabaki kuwa zaidi kwa Kongo na Agrey...
agrey unaufuatia Lindi.
Congo umeanzia Jangwani na kwenda kugota Gerezani pande za Nkrumah, ni mtaa ambao naweza kutembea bila hata kununua maji njiani.
Ila Lindi weeh...
Then kuna mtaa uko kule Masaki nao ni mrefu saana ingawa jina lake limenitoka.
Na hivi karibuni Msimbazi ulipewa hadhi ya kuwa barabara na si mtaa tena.
 
asante Ritz...
Mtaa wa Lindi unabaki kuwa zaidi kwa Kongo na Agrey...
agrey unaufuatia Lindi.
Congo umeanzia Jangwani na kwenda kugota Gerezani pande za Nkrumah, ni mtaa ambao naweza kutembea bila hata kununua maji njiani.
Ila Lindi weeh...
Then kuna mtaa uko kule Masaki nao ni mrefu saana ingawa jina lake limenitoka.
Na hivi karibuni Msimbazi ulipewa hadhi ya kuwa barabara na si mtaa tena.

Gang Chomba,
Ebu twende taratibu mtaa wa Lindi unaazia wapi na unaishia wapi? Halafu hunajua Aggrey unaanzia wapi na unaishia wapi?
 
Last edited by a moderator:
Majina ni kwa ajili ya kuwaenzi wapigania uhuru wa tanganyika na wanasiasa mbalimbali ea nchi za afrika. ali hassan mwinyi road,bibi titi mohamed road,lumumba road,nkrumah road,nyerere road, mandela road, sam nujoma road.
 
Back
Top Bottom