mtemiwaWandamba
JF-Expert Member
- May 2, 2011
- 561
- 223
Kabla ya kuitwa Independence avenue unajua ukiitwaje? Acacia street[/QUOTE
]
Aha! Ahsante Mkuu, hilo sikulifahamu.
Kabla ya kuitwa Independence avenue unajua ukiitwaje? Acacia street[/QUOTE
]
Aha! Ahsante Mkuu, hilo sikulifahamu.
Mkuu usisahau Congo inaanzia Jangwani mpaka Gerezeni. Vile vile usisahau Aggrey inaanzia Kariakoo ya Muheza mpaka Samora.
Gang Chomba,
Ebu twende taratibu mtaa wa Lindi unaazia wapi na unaishia wapi? Halafu hunajua Aggrey unaanzia wapi na unaishia wapi?
Mtaa wa Lindi ni mrefu kuliko Aggrey, unaanzia Ilala Bungoni mpaka unakutana na Nkurumah (Hapo katikati kuna jengo la Ushirika na bustani ya Mnazi mmoja).Gang Chomba,
Ebu twende taratibu mtaa wa Lindi unaazia wapi na unaishia wapi? Halafu hunajua Aggrey unaanzia wapi na unaishia wapi?
Asante Ritz kwa swali lako.
Awali ya yote napenda kukuelewesha kuwa sijasema mtaa wa Lindi ni mrefu kuliko yote Kariakoo.
Nimesema mtaa wa Lindi ni mrefu kuliko yote hapo Dar na unaanzia Mnazi mmoja mpaka Ilala...
Nnamdi Azikiwe alikuwa ni kiongozi wa kwanza wa Nigeria mara baaya uhuru wa nchi hiyo. Barabara yetu ile maarufu imepewa jina hilo kama kumbukumbu yake. Alifariki mwaka 1996.
Samora Machel naye, kama Azikiwe, alikuwa ni kiongozi wa Msumbiji aliyepinga utawala wa amakaburu wa Afrika Kusini. Alifariki kwenye ajali ya ndege mwaka 1986. Mjane wake ndio mke wa Mandela wa sasa.
Hassan Omari Makunganya alikuwa kiongozi wa Wangindo (sina uhakika sana na kabila). Aliongoza watu wake kupigana na Wajerumani dhihi ya utawala wa Wajerumani. Alishirikiana na akina Kinjekitile Ngwale katika vita iliyojulikana kama Majimaji (1905 - 1907)
Asante mhe. sana Invisible kwa kuuhuisha uzi huu tena.
Naendelea...
Sam Nujoma...(Samuel Daniel Shafiishuna Nujoma) Barabara hii imepewa kumbukumbu ya rais wa kwanza wa Namibia huru (1990-2005). Mpigania uhuru huyu aliishi Tanzania miaka hiyo akipigania uhru wa nchi yake, katika mikoa ya Mbeya na Morogoro. Ili kuwakwepa makaburu waliokuwa wakimtafuta, alipewa jina la uongo (pseudonym) la Kinyakyusa Sam Mwakangale, akiwa mkoani Mbeya.
Luthuli....Barabara hii iliyopo eneo maarufu la Ikulu, imepewa jina kutokana na mwanasiasa maarufu wa Afrika kusini (alizaliwa Zimbabwe), Albert Luthuli (1898-1967).
Lumumba....Barabara hii ilinayoambaa na bustani ya Mnazi Mmoja hadi katika makutano na barabara ya Morogoro imepewa jina la kiongozi (rais) wa kwanza wa Congo huru (Congo DRC) ndugu Patrice Emery Lumumba (1925-1961). Mtaa huu ndiko iliko ofisi ndogo ya Chama cha Mapinduzi.
Mwingine atujuze majina haya ya mitaa ya Magila, Muhonda, Aggrey. Mkwepu n.k.
Sijajua ni nani alikuwa na maamuzi ya kuzipa majina barabara zetu hizi
Mtaa wa Lindi ni mrefu kuliko Aggrey, unaanzia Ilala Bungoni mpaka unakutana na Nkurumah (Hapo katikati kuna jengo la Ushirika na bustani ya Mnazi mmoja).
Mtaa wa Aggrey unaanzia Mtaa wa Muheza (Jirani na TBL) na unaishia Mtaa wa India.