Mimi sikubaliani kabisa ukisema wachaga wanatofauti!!!/
Pili sikubaliani kabisa na kusema achanga aliwakuta wakonyingo kisha wakonyingi waka hamia Kongo!!!/hivi unajua karne ya 17 sio mbali kihivyo!??
Unaongelea miaka ya 1600s to 1700s
Halafu huo umbali wa Kongo na moshi!?????/mhhhhhhhh
Back to point yangu ya kwanza !!!
Wachaga ni wamoja na ni kabila moja!?
Wachaga kama binadamu na wabantu kuna weusi weupe warefi wanene na wembamba !! Ila kusema ni tofauti kwa sababu tajwa sikubaliani!??
Wachaga wanapishana lafudhi tuu na sio lugha!!!! Ndio maana kichaga kina fanana!!! Utofauti wa lafudhi unatokana na wagen waliopakana na maeneo ya wachaga mfano rombo walikua na wataita hivyi ni lazima lafudhi iwe tofauti halikadhalika wamachame wao ni tofauti lafudhi ila sio lugha!!!
Sababu kwann wachaga nasema ni kabila moja!??
1) angalia mila zao zote zina fanana bila kujali anatoka wapi!!
2)vyakula vyao vinafanana bila kijali anatoka wapi!!
3)pombe yao ya kienyeji ni ile ile bila kujali anatoka wapi!??
Majina yakoo yanaingiliana
4)hata ukitembelea uchagani majina ya mahali(/places) yanafanana na kuingiliana
Mitano ni mungu
Hivyo mm naamini wachaga ni wamoja ila maingiliano na makabila mengine ndio yaliyo sababisha utofauti???
We are one!!!!!
 
Wachagga (pia huandikwa Wachaga) ni kabila la watu wenye asili ya Kibantu (lakini pia mchanganyiko wa damu, hasa ya Kikushi) wanaoishi kaskazini mwa Tanzania chini ya mlima Kilimanjaro, mkoani Kilimanjaro.

Wachagga ni kabila la tatu kwa ukubwa nchini Tanzania.
Takwimu za mwaka 2003 zinaonyesha kuwa idadi ya Wachagga ni watu 2,000,000.

Makundi ya Wachagga
Wachagga wana historia ndefu ya asili yao na ya maingiliano yao na makabila mengine. Kabila la Kichagga ni mkusanyiko wa makabila madogomadogo (ya Kichagga) yaliyosambaa kijiografia kuzunguka mlima Kilimanjaro kuanzia mashariki (Tarakea, Rombo) hadi magharibi kwa Kilimanjaro (Siha, Machame).

Makabila ya Kichagga ni Wa-Rombo, Wa-Vunjo ambao wanajumuisha watu wa Mwika, Mamba, Marangu, Kilema na Kirua ambayo ndio inajulikana na wengi kama Kirua Vunjo. Ukipenda unaweza kuwagawa watu hawa wa Vunjo kama Wa-Mwika, Wa-Mamba, Wa-Marangu,Wa-Kilema na Wakirua. Makabila mengine ni Wa-Old Moshi, Wa-Kibosho, na Wa-Machame, Wa-Uru, na Wa-Siha.

Lugha ya Kichagga
Lugha ya Kichagga inabadilika kuanzia unapotoka Tarakea mpaka unapofika Siha magharibi mlima Kilimanjaro.

Kutokana na tofauti hizo Kichagga kimegawanyika katika Kimachame, Kirombo (ambacho nacho kinatofautiana kadiri unavyotoka eneo moja hadi jingine; mfano Kisseri, Kimashati, Kimkuu, Kimengwe, Kimahida), Kivunjo, Kimarangu, Kirombo, Kioldimoshi, Kingassa, Kiuru, Kikibosho, na Kisiha.

Lugha hizo zinakaribia kufanana kadiri makabila hayo yalivyopakana. Kwa mfano, Kivunjo kinafanana na Kioldimoshi. Vile vile Kisiha kinafanana sana na Kimachame ambacho pia kinafanana kidogo na Kikibosho.

Baadhi ya Wamachame walihamia sehemu za Meru, Arusha, na kuchanganyikana na Waarusha, hivyo lugha yao ikabadilika kidogo na kuwa Kimeru. Kwa sababu hiyo Wameru wanasikilizana sana na Wamachame ingawa lafudhi zao zinatofautiana kidogo.

Koo za Kichagga
Majina ya kiukoo ya Kichagga pia huashiria wanatoka sehemu gani ya Uchaga, japo si lazima kuwa hivyo: kwa mfano, familia maarufu za Kichagga nchini Tanzania ni kama ukoo wa akina Mushi, Mmasy Kimaro, Swai, Massawe, Lema, Urassa, Nkya, Ndosi, Meena hutoka Machame.

Akina Temu, Mlaki, Mlay, Lyimo, Moshiro, Mselle, Kamnde, Kileo, Kimambo, Tesha, Msaki, Assey, Kyara, Kessy, Ndanu, Macha, Mbishi, Kombe, Njau wanatoka Old Moshi na Vunjo.

Majina mengine ya Old Moshi ni kama yafuatayo: Saria, Mmari, Macha, Machange, Mshiu, Kyara, Moshi, Massamu, Kimambo, Mboro, Mlngu, Saule,Tenga, Njau, Malisa, Maro, Maeda, Ringo,Olomi, Ngowi, Lyatuu na mengine mengi.

Kavishe, Mrosso, Bongole, Mariki, Tarimo, Laswai, Mallya, Mrema, Mkenda, Massawe, Silayo, Lyaruu, Makyao, Mowo, Lamtey, Tairo, Masue, Maleto, Mramba, Kauki, Kiwango wanatoka Rombo.

Mchaki, Masawe, Sawe, Usiri, Shayo, Kiwelu, Makundi, Urasa, Mtui, Moshi, Meela, Minja, Njau,Saria, Mtei wanatoka Marangu na Kilema.

Rite, Makule, Minja, Mashayo, Chao, Shao, Makawia, Ndesano, Kimario, Tilla, Mariale, Tarimo, Mafole, Kituo, Mrosso, Lyakundia, Kessy, Mmbando, Matemba, Ndenshau, Morio, Akaro, Matowo, Towo, Mkony, Temba, Foya, Munishi, Kilawe, na kadhalika hutoka Kibosho.

Ukoo wa akina Teri wako Mamba, Chami, Chuwa, Kiria Owoya na wachache Sango, Old Moshi na wengine walihamia Maji ya Chai, Mkoa wa Arusha.

Utawala wa jadi wa Wachagga
Watawala wa Kichagga waliitwa "Mangi". Hawa walihodhi mashamba, ng'ombe na waliheshimiwa kama viongozi wa kikabila. Walikuwa na nguvu za kisiasa na utajiri. Baadhi ya Ma-mangi mashuhuri katika historia ni kama Mangi Shangali (wa ukoo wa Mushi) kutoka Machame, Mangi Rindi aliyeingia mikataba na wakoloni (Wajerumani), Mangi Sina wa Kibosho na Mangi Horombo wa Keni - waliojulikana kwa uhodari wao wa vita katika kupigana na Wamachame na kupora ng'ombe na mazao yao, hata mpaka leo makabila ya Kimachame na Kikibosho hayaoani kwa urahisi na Mangi Marealle wa Marangu na Vunjo. Mangi Meli huyu alikuwa mangi wa waoldmoshi ambaye alipigana na wajerumani na aliishia kukatwa kichwa na mpaka sasa kichwa chake kipo ujerumani alizikwa kiwiliwili tuu baada ya kumnyoga na mti aliyonyongewa upo mpaka sasa sehemu ya oldmoshi bomani karibu na kolila sekondari .

Wakoloni walipokuja Kilimanjaro waliingia mikataba na viongozi hawa wa kikabila ili kuweza kuweka misingi yao ya kikoloni. Pia ndugu na watoto wa Ma-mangi walikuwa wa kwanza kupata elimu ya kikoloni, kwa hiyo waliweza kushirikishwa katika serikali za kwanza. Hawa pia wanaaminika walikuwa kama mabepari wa kwanza wa kijadi, maana walifanyiwa kazi na watu wengine wakati wao Ma-mangi wamekaa kuhesabu mali zao.

Usemi maarufu wa "u-Mangi-meza" nadharia inawezekana kuwa umetokana na watawala hawa wa Kichagga.

Elimu kati ya Wachagga
Wachagga wanajulikana kwa uwezo wao mkubwa katika uwanja wa elimu, hususani katika masomo ya sayansi na hisabati. Moshi ni maeneo ya mwanzo ambayo wamisionari wa Ukristo walijenga makanisa na shule.

Sababu hii imefanya Wachagga kuwa kabila namba moja lenye watu wengi zaidi walio na elimu ya kisasa (elimu ya juu) na mkoa wa Kilimanjaro unaongoza kwa idadi ya shule za sekondari nchini Tanzania. Kulingana na takwimu za elimu mkoa huo una shule za sekondari zaidi ya 320. Pia mkoa una shule za msingi zipatazo 950. Idadi hii ya shule ni kubwa zaidi ya idadi ya shule katika mikoa mingine Tanzania.

Shule nyingi za sekondari ziko katika mkoa huu kwa sababu zifuatazo:
1) Hali ya hewa na vivutio vya kitalii katika mkoa huu viliwavutia zaidi walowezi na wakoloni na kuweka makazi yao hapo. Hivyo wamisionari walijenga shule za kwanza wakifuatiliwa na serikali za wakoloni
2) Serikali ya Tanzania ilirithi shule zilizojengwa na wakoloni
3) Wachagga waliobahatika kupata fedha binafsi baadaye waliwekeza kwenye ujenzi wa shule binafsi kama kitega-uchumi, wakati wakazi wa mikoa mingine kadhaa walisubiri serikali iwajengee shule.
4) Ukichanganya sababu 1, 2 & 3 utagundua shule katika mkoa Kilimanjaro zimezidi sana idadi ya shule katika mikoa mingine yote.

Ni vema pia kusema kuwa shule hizo huvutia wanafunzi kutoka Tanzania nzima, haziwasomeshi Wachagga tu.

Ardhi
Ingawa ardhi ni msingi wa maendeleo kwa watu wote, kwa Wachagga, ardhi ni mali sana kwa sababu kilimo chao ni cha mazao ya kudumu kama kahawa na ndizi hukaa shambani kwa muda wa miaka mingi.

Mojawapo ya urithi wapewayo watoto ni "kihamba". Hii ni sehemu ya ardhi ambayo mtoto anategemewa atajenga na kuanzisha familia yake. Bahati mbaya watoto wa kike walikuwa hawapewi kipaumbele katika ugawanaji wa vihamba. Uhaba wa ardhi huko Uchaga ulipelekea Wachagga wengi kuhamia mikoa mingine. Hivi leo utakuta Wachagga wakiishi Dodoma, Morogoro, Iringa, Mbeya n.k. wakiwa wamepanda migomba yao na kuendesha biashara za maduka ya vyakula.

Ukienda kwenye mikoa hiyo utakuta wamejenga jamii zao na vyama vyao vya kusaidiana wakati wa sherehe au matatizo. Aidha hata pombe ya mbege utaweza kuikuta kwenye makusanyiko ya Wachagga katika mikoa mbalimbali.

Kilimo na chakula
Wachagga hulima mazao ya chakula kama vile mahindi, maharagwe, viazi, ndizi, ulezi na mboga mbalimbali. Pia mazao ya biashara kama vile kahawa, nyanya na vitunguu.

Ndizi za Wachagga na upishi wa samaki
Wachaga wengi hawawezi kupika samaki,mihogo na wali pia Ni wakorofi Sana na wabinafsi sana

Ingawa Wachagga wa leo wanakula vyakula mbalimbali kama vile ugali, wali na viazi, chakula kikuu cha Wachagga ni ndizi.

Kuna ndizi za aina mbalimbali na kwa matumizi tofauti. Mfano ndizi sukari ni fupi na huachwa hadi ziive na huliwa mbivu kama tunda.

Ndizi mshale hukatwa zikiwa mbichi na kupikiwa vyakula mbalimbali pamoja na nyama ya ng'ombe, kondoo au mbuzi. Mara nyingine hupikwa na maharage, choroko, kunde au hata maziwa ya mtindi. Vyakula vya ndizi huja kwa ladha tofauti kama vile ndizi nyama, mtori, machalari, kiburu na kadhalika.

Aina nyingine ni ndizi ng'ombe ambazo huachwa ziive halafu humenywa na kutumiwa kutengenezea pombe maarufu iitwayo mbege. Mbege hutengenezwa kwa kutumia ndizi mbivu, maji, na ulezi.

Aina nyingine ni ndizi mzuzu. Hizi zikikomaa huachwa zianze kuiva kidogo halafu huchomwa na kuliwa kama kitafunwa pamoja na chai au pombe. Ukipita mitaa ya Dar es Salaam utaona ndizi mzuzu zikichomwa sambamba na muhogo au kuku vumbi au kiti moto. Huwa hawajui kupika samaki na ni wasiri sana

Wachagga na muhogo
Inasemekana kuwa "Mchagga halisi hali muhogo - akila muhogo atakufa". Usemi huu umetokana na historia ya mababu kuwa Wachagga waliopanda mihogo Kilimanjaro enzi za kale walikufa baada ya kuila. Historia hiyo yaweza kuwa ya ukweli kwa sababu aina nyingi za mihogo zinajenga sumu ya sianidi ndani yake; watu waliozoea kutumia mihogo huwa na njia za kuondoa sumu kwa kuiloweka mihogo katika maji kwa muda. Lakini kama Wachagga wale wa zamani, hasa wa Machame, walifanya jaribio bila kujua mbinu ya kuondoa sumu, ajali iliweza kutokea. Cha kushangaza ni kwamba hukohuko Kilimanjaro, majirani na watani wa Wachagga, yaani Wapare, walikuwa wameshazoea mihogo na ilikuja kuwa moja ya chakula chao kikuu.

Ulaji kiti-moto
Pamoja na kilimo cha mazao, Wachagga hupendelea sana kufuga nguruwe. Tabia ya kula nyama ya nguruwe ijulikanayo leo kwa jina la "kiti moto" ni moja ya mambo yaliyoenezwa na Wachagga. Ulaji wa "kiti moto" haukuwa pendeza baadhi ya wenyeji wa Pwani kama Dar es Salaam ambapo Wachagga walihamia, kwani wakaaji wengi wa Pwani ni Waislamu kwa hiyo nguruwe kwao ni haramu. Wakazi wa Dar es Salaam watokao makabila mengine na wasiyo Waislamu kwao kula nguruwe ilikuwa "ruksa".

Kuna pendekezo la kufuta kifungu kifuatacho cha makala hii. Ona majadiliano kwenye ukurasa wa majadiliano na hapa.
Maoni juu ya Wachagga
Wanawake wa Kichagga (hasa kutoka Machame) hujulikana kama wafanyakazi hodari. Huchangia sana katika mapato ya nyumbani na chakula. Ingawa wanaume wa Kichagga hupendelea kufanya kazi mbali na kwao, wake zao hukaa nyumbani (Moshi) kufuga ng'ombe na kufanya kazi za shambani. Kwa sasa kutokana na ugonjwa wa ukimwi tabia hii imepungua miongoni mwao.

Kipato cha Wachagga ni kikubwa kulingana na cha makabila mengine, hata hivyo takwimu zinaonyesha watoto wa mkoa wa Kilimanjaro huongoza kwa utapiamlo. Sababu kubwa ni wazazi kujali kazi kuliko muda wa kuwahudumia watoto. Wengi wa watoto hao ni wale ambao wazazi wao ni watu wa pombe na kipato chao kinaishia kilabuni. Utaona kwamba Uchagga una vilabu vingi vya pombe na vinaongezeka kwa sababu imekuwa biashara kubwa. Karibu kila kaya kumi na tano kuna kilabu cha pombe na kiwango cha chini kabisa cha pombe inayouzwa kwa siku katika vilabu hivyo si chini ya madebe sita au lita mia moja.

Hiyo inawezeka pia kuwa tunda la wazazi kutowalisha watoto wao chakula cha kutosha au chakula bora. Kuna sehemu nyingine za Uchagga kama Old Moshi na Kibosho ambapo watoto wadogo hupewa pombe ya mbege asubuhi, mchana na jioni.

Sababu nyingine ni kazi: mama wa Kichagga anaweza kushinda shambani kutwa na hana desturi ya kubeba watoto mgongoni kwenda nao shambani, hivyo wanakuwa nyumbani na mayaya au peke yao. Mfano ulio dhahiri ni nyakati za asubuhi na mapema kwenye vyombo vya usafiri karibu robo tatu ya abiria ni wanawake wakienda katika shuguli za biashara na kilimo na vivyo hivyo nyakati za jioni wakirudi majumbani. Hao ni nje ya wale wanaotumia usafiri wa miguu ambao ni wengi zaidi.

Pia baadhi ya kina mama wa Kichaga wanawajali waume zao zaidi kwani nyama nzuri ni ya baba. Ili kuepuka gharama baba ataandaliwa chakula kizuri, tofauti na chakula walichoandaliwa watoto, japo ni chakula kilekile.

Pia Wachagga wamekuwa na desturi ya kuwaenzi wazee wao waliotangulia mbele za haki kwa kuwatambikia kwa pombe na nyama za mbuzi pale tu wanaporudi nyumbani mwezi Desemba. Hilo limekuwa suala la kawaida sana. Wengi wao huwa wanarudi na magari, ndiyo sababu utaona ya kwamba kila mwaka ufikapo mwezi Desemba foleni za magari zimekuwa zikiongezeka kutokana na Wachagga kurudi nyumbani msimu wa sikukuu. Wengi wao wamekuwa wakitoka sehemu mbalimbali za nchi na hata nje ya nchi.

Wachagga wengi hupenda kurudi nyumbani kipindi cha Krismasi, ikiwa ni kuwatembelea wazazi wao, rafiki, au ndugu. Pia imekuwa kama desturi wanaukoo kukaa pamoja na kujadiliana mambo jinsi yalivyokwenda katika kipindi kizima cha mwaka na wakati mwingine inakuwa sehemu ya kwenda kuwatambulisha watoto kwa bibi na babu zao, hasa wale waliozaliwa mijini. Ni kipindi chenye shangwe na furaha sana: hakuna kaya utakayokuta haina furaha kwa sababu hata kama huna sherehe kuna mialiko mbalimbali ambao haihitaji kadi au michango.

Ingawa wengi hudhani kwamba Wachagga wamepokea sana dini (imani) ya Ukristo kwa kuwa wengi wao ni Wakristo na hiki huwa kipindi cha likizo kwao, inaaminika pia kuwa kurudi kwao wakati wa Krismasi ni pamoja na kutembelea ndugu zao na kujumuika pamoja katika kuumaliza mwaka baada ya kazi nyingi za kutafuta pesa mwaka mzima.

Sababu kuu za Wachaga wengi kwenda kwao mwisho wa mwaka
Kupumzika, hii ni baada ya kufanya kazi kwa mwaka mzima bila kwenda, biashara asubuhi, jioni mahesabu, kwao Desemba ni mwezi wa kutulia tu na familia ndugu na jamaa
Kuchinja mbuzi, hapa kuna za matambiko na za kula na kufurahia tu. Matambiko hayo ni kushukuru wazee wao waliokufa mapema kwa baraka walizopata kwa kipindi chote cha mwaka mzima
Sherehe mbalimbali: sherehe za wafu, maadhimisho ya ndoa mbalimbali, Krismasi, Ubatizo, Kipaimara, Komunyo, kutoa watoto jandoni na Mwaka mpya wenyewe. Kila inayoitwa sherehe hufanyika kipindi hiki, kuanzia tarehe 25 Desemba kufika tarehe 1 Januari ni shughuli tu, kula kunywa kusaza.
Utambulisho mbalimbali kwa wazee, jamaa wa nyumbani kama vile mke, mchumba, mume, gari jipya, nyumba mpya, watoto n.k.
Kukutana na watu mbalimbali ambao hamuonani baada ya kipindi hicho kama, marafiki, majirani, ndugu na jamaa. Hii ni kwa wale wanaofanya kazi mikoa tofauti (huyu Morogoro yule Mwanza mwingine katoka Dar es Salaam)
Utekelezaji wa miradi mbalimbali hapo nyumbani kama ujenzi au ukarabati wa nyumba, njia pana za magari na kukagua mashamba n.k.
Si wote wanakwenda kwa sababu hizo zote bali lazima sababu mojawapo ihusike.

Kutokana na sababu hizo wanaokwenda ni watu wote wa dini zote. Ukienda tofauti na kipindi hiki huwezi kukuta watu wengi sana. Kwanza baada ya kipindi hicho kupita kila mtu anashughulika na mambo yake (kutafuta pesa).

Kama umekwenda na huna chochote, utakumbana na ubaguzi na manyanyaso makubwa.

Hao ndio wachaga
 
mabinti wa kirombo, wengi wao utasema sio wachaga dah
 
Mtiririko siyo mzuri, mbilikimo wanahama toka Kilimanjaro mpaka Drc Congo kwa njia ipi!!
 
Kabila la Wachaga linafahamika kwa wengi kuwa linapatikana mkoani Kilimanjaro.Kwa asili, Wachaga ni mchanganyiko wa Wamasai, Wasambaa, Wataita, Wakamba na Wakahe.

Wachaga walianza kuhamia kwenye miteremko ya Mlima Kilimanjaro kwenye karne ya 17.

Walipofika wakiwa katika vikundi vidogovidogo waliwakuta wakazi, wenyeji kwenye Misitu ya Mlima Kilimanjaro walioitwa ìWakonyingo..

Wenyeji hawa ambao huitwa Mbilikimo hawakupenda kuchanganyika na wahamiaji wageni, hivyo wakahama na kuanzisha makao yao ya kudumu kwenye misitu minene iliyopo nchini Kongo.

Watu wengi wanafikiria kwamba Wachaga wanatokana na asili moja. Ukweli ni kwamba wamegawanyika katika himaya 15, wanatofautiana kwa lafudhi, lugha, rangi na mwonekano wa miili yao.Wachaga wapo katika makundi makuu matatu ya Hai, Vunjo na Rombo.

Wale wanaopatikana eneo la Hai ni Wasiha, Wamasama, Wamachame,Wangíuni, Wakibosho, Wauru na Wamoshi. Kwa wale wanaopatikana eneo la Vunjo ni Wakirua, Wakilema, Wamarangu, Wamamba na Wamwika.

Kutoka eneo la Rombo ni Wamkuu, Wamashati na Wasseri.
Hadi sasa haijulikani vizuri asili ya jina Wachaga, ila wanahistoria wanaeleza kwamba jina hilo linatokana na neno la Kiswahili linaloitwa 'Kichaka'.

Inaelezwa kwamba misafara ya wafanyabiashara iliyokuwa ikiongozwa na Waswahili pamoja na Waarabu, walipokuwa wakipita maeneo ya Vunjo waliwaona wenyeji wa huko wakiwa wamejenga vibanda vya kulinda mazao yao yasiliwe na wanyama waharibifu.

Wakawaita wenyeji hawa kwamba wanaishi vichakani na kuanzia hapo wageni wafanyabiashara na Wamisionari walipokuwa wanakuja Kilimanjaro walielekezwa na waongozaji misafara yao kwamba wanakwenda kwenye nchi ya ìUchakani,î, wakimaanisha kwamba kwa watu wanaoishi vichakani.

Hatimaye wageni wakashindwa kulitamka vizuri neno hili na kuliita ìUchagani,

Jina hili likawekwa kwenye ramani na kuitwa nchi ya ìWachaga.î Hivyo ndivyo wenyeji waliokuwa wakiishi kwenye Miteremko ya Mlima Kilimanjaro walivyopewa jina lao. Wachaga.

Maendeleo ya Wachaga
Maendeleo yao hapo awali yalitokana na zao la kahawa. Walifanikiwa kuanzisha vyama vya ushirika na hatimaye mwaka 1932 walianzisha Halmashauri ya Wachaga (Chaga Council) ambayo kwa sasa inatumiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Moshi.
Halmashauri hii iliongozwa na Mangi Mkuu ìMshumbue Thomas Marealle II.

Mwaka 1946, utawala wa Waingereza uliboresha Baraza la Halmashauri ya Wachaga. Himaya ndogo za Wachaga zipatazo 17 (himaya mbili za Wakahe na Waarusha chini zilijumuishwa kwenye Tarafa ya Vunjo) na kuundwa kwa Tarafa tatu za Hai, Vunjo na Rombo.

Halmashauri ya Wachaga ilijenga miundombinu na huduma za jamii ikiwamo kuwasomesha watoto wao kwenye shule na vyuo mbalimbali kama Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda.

Halmashauri ya Uchaga ilikuwa na bendera yake ambayo ipo hadi leo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, yenye nembo tano kuu:

1- Mlima Kilimanjaro uliochorwa katikati ya bendera ukionyesha mandhari nzuri ya kilele cha Kibo. Kilele cha Kibo kinatoa maji safi na ni kielelezo cha umoja wao.

2- Chini ya kilele cha Kibo, upande wa kushoto wa bendera kuna mgomba wenye ndizi. Hiki ni chakula kikuu cha Wachaga.

3- Upande wa kulia wa bendera ni tawi la mbuni ukiwa na matunda yake. Kahawa ni zao lililowaletea maendeleo.

4- Bendera imezungukwa na matawi ya 'sale' lenye matawi mawili (draceana plant). Matawi haya yamefanya mduara kuzunguka kilele cha Kibo, mgomba wa ndizi na tawi la zao la kahawa. Masale ni mmea unaoheshimiwa sana na Wachaga wote.

Ni alama ya amani. Masale hutumika katika sherehe na shughuli zote za kimila zinazofanywa na Wachaga. Majani yake ni kijani kibichi yanayoonyesha jinsi Kilimanjaro ilivyo na rutuba nzuri inayostawisha mazao ya kila aina.

5- Juu kidogo ya kilele cha Kibo yupo chui ambaye amejipumzisha. Chui ni alama kuu ya mamlaka ya Wachaga.

Hapo awali kwenye miteremko ya Mlima Kilimanjaro walikuwepo chui wengi wa rangi nyeusi lakini kutokana na ongezeko la watu pamoja na uharibifu wa mazingira chui hawa wametoweka.

Sikukuu ya Wachaga
Sikukuu ya Wachaga wote ilikuwa ikiadhimishwa Novemba 10 kila mwaka kama kumbukumbu ya siku ambayo Wachaga wote walipokusanyika na kumchagua Mangi Mkuu baada ya kuteuliwa na Halmashauri Kuu ya Uchaga.

Maadhimisho ya kwanza ya mwaka 1952 yalitanguliwa na uchaguzi wa Halmashauri ya Wachaga wote kuanzia kwenye ngazi ya Uchili (kijiji), Umangi ( uchifu wa eneo) na mwisho ngazi ya baraza kuu.

Sherehe ziliadhimishwa mjini Moshi ambako Wachaga wote pamoja na wageni waalikwa kutoka mataifa mbalimbali walikusanyika katika Viwanja vya Halmashauri ya Uchaga (sasa ni makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, [Kilimanjaro District Council-KDC]) kushuhudia sherehe kubwa na yenye kusisimua sana.

Jumba la Makumbusho
Upo umuhimu mkubwa wa kuhifadhi historia ya Wachaga kama kumbukumbu sahihi kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Pia, ipo haja kwa majengo ya Halmashauri ya Wilaya ya Moshi pamoja na Ikulu yakarejeshwa kwa Wachaga ili yageuzwe kuwa majengo ya kuhifadhi kumbukumbu ya kabila hilo.

Katika majengo haya patahifadhiwa nyaraka zote za Chaga Council ambazo baadhi zimeshaanza kutoweka, kutahifadhiwa pia shughuli za mila na kiutamaduni tangu enzi ya karne ya 18.

Halmashauri ya Wilaya ya Moshi haina budi kutafuta eneo la kujenga majengo mapya badala ya kuyatumia ya kihistoria.

SOURCE:MWANANCHI
=====

MAONI YA WADAU, WACHAGA NI WAYAHUDI

-------------

Sio kweli kwamba mbilikimo wa kongo walitoka kilimanjaro! Hili wamekudanganya yaani sijui kama unafahamu umbali wa kongo!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom