Hili la Godbless Lema ni la kuiga, kubeza au kuunga mkono?

aisee watu tunatofautiana kuelewa na mtazamo

mimi naamini 'confrontational politics' hazitasaidia hii nchi
sana sana zitaleta 'machafuko'
na watakaoumia ni wasio na hatia...mke wa lema anaweza kupanda ndege na watoto haooo nairobi au kampala

CCM ni kama 'machizi wenye silaha'
unahitaji kutumia 'akili' ku deal nao
na sio kuanzisha 'mapambano'

Boss unaniangusha mkuu, ina maana kwenda jela kwa hiari alikofanya Lema kutasababisha vita au? Sijaelewa hayo maandishi yako
 
aisee watu tunatofautiana kuelewa na mtazamo

mimi naamini 'confrontational politics' hazitasaidia hii nchi
sana sana zitaleta 'machafuko'
na watakaoumia ni wasio na hatia...mke wa lema anaweza kupanda ndege na watoto haooo nairobi au kampala

CCM ni kama 'machizi wenye silaha'
unahitaji kutumia 'akili' ku deal nao
na sio kuanzisha 'mapambano'
Sasa hapo ndio mnatakiwa mseme ni AKILI GANI hizo zinazotakiwa....na siyo kuishia hapo tu!
Lakini kama ni akili ya kuiba kura au kuhonga wapiga kura- big No!
Toa darsa mkuu!
 
Wewe unawasiwasi gani na kuanzishwa mapambano, hiyo akili ya kupambana nao mbona hujaitoa hapa? Unachokifanya hapa ni kutishia watu na kuwakatisha tamaa wasiikabili hiyo ccm, anyway may be is your way of earning daily bread, jiulize hao watz wa kesho watakua salama kwa utaratibu huu tunaouona? Je hicho unachopigania leo kupata na kufanikisha kesho kitakuwa na maana kama mambo yenyewe yanaendeshwa kiholelaholela hivi?

tazama Libya na walichopata baada ya mapambano
CCM ni 'wehu tu' hawana uwezo hata wa kuchambua nyakati'
kutumia nguvu nyiingi kupambana na ccm ni sawa na kutumia nguvu nyiingi kupambana na 'taahira'
lazima kuna mbinu nyingine better....mandela unamkumbuka?????
 
Broda,
Usikate tamaa...unavyowaza sivyo!
Lazima tukubali kuwa somo analotupa Lema nigumu kidogo kwenye bongo za wengi wetu!

Mimi mwenyewe niliposikia kwa mara ya kwanza nilijiuliza mara mbilimbili kuwa ana maana gani kujitakia shida hiyo!
Lakini siku hazigandi, walisema waswahili...anaweza akatoka bila pressure groups kureact kwa namna yoyote, lakini Historia tayari imesharekodi tukio hilo, hata mtoto kwasasa anajua juu ya tukio hilo, maana ndiyo burning issue nchini.

Tupende tusipende, je waliomkamata Lema last time watamwendesha au kumtishia kirahisi kwa suala la jela tena pindi akianzisha harakati mtaani siku nyingine?...ni lazimam watajiuliza sana na kutafuta altenative!

Tusitegemee mambo haya kulipuka kama petroli overnight...ni hatua...kesho tutakuwa tumesogea pale, na hatimaye nchinzima ita-take'off!

Mku hapo juuu. Mh. Lema anajua anachokifanya na anafanya hivyo kwa sababu anaijua community yake na makazi yake. Ametumia socially constructed kwamba Arusha ili utoke jela au upate dhamana inabidi uhonge hela. Lema is representing majority and incapable low socioeconomic groups ambao wengi wao ndo wapiga kura wake, wako jela huku wake zao, watoto wao na wajukuu wakiwa hawana matumaini na amani. Hivyo basi LEma sio kwamba ili atoke alipo ndiyo atoe hela au hongo, hapana.

On the other hand Kuna social pressure ya kuwa wafungwa watapiga kura siku za usoni wakati katiba itakapobadilika na kwa kujua hilo it is a positive imagination na imetokea kwa wakati muafaka yeye aende jela kama ilivyokuwa Marting Luther King JR, that "I have a dream"

Hata hivyo mkoa wa Arusha kama ulivyo batizwa na wanasiasa wa CCM ukijulikana kama ( in Political thoughts eti ni watu wakorofi na wanahitaji kwenda jela. 'wanahitaji kwenda jela kwa ajili ya haki zao.'.. shame..) Bila kificho mkoa wa Arusha kuanzia kada zote za kiutendaji kama vile polisi, chama tawala, mahakama, hata na watu kutoka nje ya mkoa huu huwaita wakazi wa Arusha ni wakorofi kwa hiyo hata vyombo vya sheria vinatuhukumu kihivyo, ilishawahi kutambulika kipindi cha nyuma eti mkoa wa Arusha unahitaji mkuu wa mkoa mkorofi na hata IGP mkorofi kama ilivyokuwa kwa Mpu.mabavu Mahita.

In respect of Charles Wright Mills (1916-1962) 'In socialogical Imagination' Things will be alright for Arushans, heko Mb. Lema na nakuhakikishia bidii zako zinakurudisha bungeni.
 
Mbunge aliyechaguliwa na wananchi anapowekwa mahabusu ina maana gani? Je, kiini cha sheria ya kumweka mtu yeyote yule mahabusu lengo lake ni nini? Je serikali yaani watawala wanalionaje hili? Je heshima ya Bunge haijawa compromised? Au ndio tatizo la serikali legelege? Je hii serikali ni ya kweli au ni serikali ya .... .... .... .... ..
 
Mbunge aliyechaguliwa na wananchi anapowekwa mahabusu ina maana gani? Je, kiini cha sheria ya kumweka mtu yeyote yule mahabusu lengo lake ni nini? Je serikali yaani watawala wanalionaje hili? Je heshima ya Bunge haijawa compromised? Au ndio tatizo la serikali legelege? Je hii serikali ni ya kweli au ni serikali ya .... .... .... .... ..
Kisheria mbunge ni kama mwananchi mwingine, unless akiwa mjengoni, akielekea au kutoka mjengoni au akiwa kwenye vibaraza na bustani za mjengoni... zaidi ya hapo anaweza kukamatwa kama sisi wengine.
 
tazama Libya na walichopata baada ya mapambano
CCM ni 'wehu tu' hawana uwezo hata wa kuchambua nyakati'
kutumia nguvu nyiingi kupambana na ccm ni sawa na kutumia nguvu nyiingi kupambana na 'taahira'
lazima kuna mbinu nyingine better....mandela unamkumbuka?????

Boss umenifurahisha hapo ulipo tumia neno taahira, taahiri lazima umpige alainike kwanza ndio akuelewe, makaburu wa SA wasingelainishwa kwanza na wapinga ubaguzi Mandela asingefanya aliyofanya, hebu fikiria mataahira wetu hapa TZ, kuwa pamoja na kelele zote za msimlipe dowans ni wizi na hatari kwenu viongozi, wapi watu wamen'gang'ania kulipa kwa lolote na liwe, sasa mataahira kama hao utaondoaje uwezekano wa kutumia machafuko, maana hawa it seems hawaelewi lugha nyingine zaidi ya risasi na kusukumiziwa mijiti kwenye masaburi yao.
 
lema ni shujaa tena shujaa na mfananisha na mkwawa aliyejinyonga asikamatwe na wakoloni naamn ipo cku tz yatatokea kama yaliyotokea tunisia,misri au libya umma kuchukua mkondo wake.hao police na ccm oneday watakuwa omega
 

Mhe Godbless Lema (MB) - Arusha Mjini

Jana huko Arusha Mbunge wa Arusha Mjini Bw. Godbless Lema alikubali kufanya kinyume chake. Alikuwa na uchaguzi wa kupewa dhamana katika kesi inayomhusu na kwenda zake nje na kufurahia uhuru au kwenda jela. Katika kitu ambacho alikipanga mapema Lema aliamua kwenda jela na kukataa kuwekewa dhamana. Uamuzi huu kwa baadhi ya watu unaweza kuonekana ni wa kujitafutia sifa na umaarufu wa kisiasa. Hilo siwezi kulipinga kwani Lema ni mwanasiasa na wanasiasa huhitaji umaarufu mara zote na si kosa.
Mkuu nalazimika kukubaliana na wewe kwa msingi niliou bold na red, ametumia haki yake.
Jana kuna mwenzako alikuja kama wewe akamfananisha Lema na Mandela, na sasa wewe umekuja tena unafananisha kitendo cha Lema ni kama alichotaka kufanya Nyerere.
Lakini tunapaswa kufikiri zaidi ya hapo, Lema tunaweza kumsifia tutakavyo lakini si kufananisha ili kuoanisha waliofanya Nyerere au Mandela ili kuzipa sapoti hoja zetu.

Kunatofauti kubwa sana kati ya kuwa mahabusu na kufungwa jela
Kuna tofauti kubwa sana kati ya faini na dhamana
Kuna tofauti kubwa sana kati ya mtuhumiwa na alietiwa hatiani
Kuna tofauti kubwa sana ya mtua aliyekataa kulipa faini aende jela na anayemlipa wakili mamilioni mkumtetea asitiwe hatiani
Sheria inaruhusu mtu yeyote kuwekwa rumande ikibidi lakini hairuhusu mtu yeyeyote kufungwa jela kama hana hatia

Kimsingi sio kama sitambui kitendo cha ki historia alichofanaya Lema isipokuwa natatiziki na jinsi kinavyojaribu kupambwa kwa nguvu zote kwa kufananishwa na watu waliofanya mambo makubwa
 
Kisheria mbunge ni kama mwananchi mwingine, unless akiwa mjengoni, akielekea au kutoka mjengoni au akiwa kwenye vibaraza na bustani za mjengoni... zaidi ya hapo anaweza kukamatwa kama sisi wengine.

Nafikiri una matatizo ya uelewa wako.
 
kama ni mapinduzi ya kweli yanaanza kwa watu kama hawa kina lema. Wanaonyesha mfano halisi wa kudai haki ya kidemokrasia na kupinga kwa dhati unyanyasaji wa kila aina dhidi ya serikali na viongozi wake. Huu ni mfano wa kuigwa si kwaraia wote kujipeleka jela la hasha bali kumuunga mkono lema kwa kutokuwa waoga na kusema hapana kwa unyanyasaji na kusimamia haki ya kweli.
 
Nafikiri una matatizo ya uelewa wako.
MAY BE, ILA UNATAKIWA ULETE FACTS NA SIYO KEJELI!!
untumia emotins and I do respect that, but facts are facts and opinions are opinions.... so what u sayin?
 
Nadhani wengi wasichoelewa ni kwamba Lema si wa kwanza kutumia mbinu hii, hata viongozi wa ANC wamewahi kuitumia na kuna kipindi walishawishi watu wafanye makosa madogo madogo makusudi ili wapelekwe jela lengo likiwa kuwa hakuna jela za kutosha ku-imprison watu wote.
 
Nafikiri hii issue mtu unaweza ukaitafsiri kwa njia nyingi. Mara ya kwanza niliposikia hii habari nilianza kufikiri hivi: Serikali imekuwa ikitishia wapinzani kuhusu kuwapeleka jela/mahabusu/fungua kesi n.k. Ni kweli watanzania wengi (including wapinzani) wanaogopa wanaposikia kukaa jela etc. Kuna watu wanaogopa maandamano, hata kama ni kitu cha maana wanachokipinga kwakuogopa kupigwa, kukamatwa na kuwekwa ndani. Kutokana na dhana hii, serikali inapata ushindi fulani inapogundua asilimia kubwa ya watanzania ni waoga wanaposikia jela. Kwa mtizamo huu; kitendo cha Lema kukataa dhamana kunaweza kuinua watu wa aina yake wengi wenye udhubutu. Hivyo basi kuweka dhana kwenye vichwa vya watu kwamba jela ni mahali pa kawaida. Kwa serikali hii ni hatari kwasababu: wanapungukiwa strategy za kuwatisha wananchi. Tuchukulie mfano mzuri vyuo vikuu. Kipindi cha Nyerere wanafunzi wa vyuo vikuu walikuwa waoga sana kugoma. Hii inatokana na jinsi Nyerere alivyolichukulia/zungumzia swala la mgomo wa vyuo. Wanafunzi wa vyuo vikuu walipoanza kugoma, walisababisha wengine tuliofuata nyuma kufanya mgomo kama ni part of life. Nakumbuka mtu unaona FFU wala huogopi tena kama ilivyokuwa mwanzo. Na sasa tunaona jinsi migomo ilivyokuwa kitu cha kawaida. That being said: hatua hii ya Lema inaweza ikaondoa woga kwa wengi; na serikali ikaona watu wengi wakiipinga bila woga. Siku Watanzania wakiondoa woga tu nafikiri serikali itakuwa na wakati mgumu sana. Wengi wetu tunaifahamu jela kwaku-hadithiwa tu, tumeizoea kama sehemu ya wahalifu na sio part of the process kwenye ukombozi. Lakini ikitokea wengi wakaenda jela na wakaona sivyo watu wanavyosema au sio hatari kiasi hicho; ni wazi fear itaondoka. I guarantee lema akitoka ndani atakuwa "highly charged" kulinganisha na alivyokuwa mwanzo. The question is: how many Tanzanian's are ready or have the voltage to handle his charges" Inawezekana kuna watanzania walio huru wanateseka hata kuliko mtu aliyeko jela i.e. hana chakula, dawa, malazi etc. Lakini kutokana na hadithi za jela wengi wetu tunaiogopa kuliko hata kifo. Siku watu wakigundua otherwise au wakapata mtizamo tofauti kuhusu jela itakuwa ngumu sana kwa serikali ku-reverse the situation.
 
Hivi wewe jelaa unakujuaa au unakusikia tu ndio mheshimiwa mbunge mwenye kuamini katika uhuru wa kweli kwa wanyonge awe amekwenda kufanya maigizo huko?

Nadhani kama alivyosema mwenzetu Mzee Mwanakijiji, kupitia lugha ya vitendo vyake, hakika Kamanda Lema kaipa taifa zima tungo tata na la ki-historia ajabu.


maigizo aisee....angeanza kugomea posho
 
kama ni mapinduzi ya kweli yanaanza kwa watu kama hawa kina lema. Wanaonyesha mfano halisi wa kudai haki ya kidemokrasia na kupinga kwa dhati unyanyasaji wa kila aina dhidi ya serikali na viongozi wake. Huu ni mfano wa kuigwa si kwaraia wote kujipeleka jela la hasha bali kumuunga mkono lema kwa kutokuwa waoga na kusema hapana kwa unyanyasaji na kusimamia haki ya kweli.

Ni dhahiri sasa kwamba tuko Watanzania wengi tunaotaka mabadiliko. Hata hivyo,tatizo letu kubwa, tunafikiri mabadiliko haya yanaweza kuja kwa siasa za upinzani za "kikondoo" na "kistaarabu". Hakuna popote katika siasa za Afrika, mabadiliko yalipotokea kwa siasa za upinzani za "kikondoo"! CHANGE IS COSTLY!

Kikundi chochote kikiwa madarakani kwa miaka makumi, hakiwezi kuachia madaraka hayo, na kukubali kukipa kikundi kingine, madaraka hayo; kirahisi, katika kisahani! Utawala wa muda mrefu, huwafanya wajione wamezaliwa kutawala! Ndiyo maana wengi wao, hutoa kauli za "tutatawala milele"! Mtaji wao wa kutawala milele, ni pale wapenda mabadiliko, wanapokuwa waoga, wakiogopa tu, virungu, mabomu ya machozi, maji ya washawasha, risasi za raba, na kufungwa jela.

Rais mstaafu wa nchi moja ya Afrika Mashariki, alipokuwa madarakani; aliwahi kuwaambia marais wenzake, "Inawezekanaje mtu kuachia utawala, wakati una nguvu zote za dola?" Hatimaye aliachia, lakini ilikuwa baada ya confrontation! Kanuni, ni hiyohiyo, kutoka Capetown hadi Cairo!

Lema ameonesha Njia - Confrontation! Hata hivyo, kazi hii ni kubwa; Lema mmoja hatoshi kuleta mabadiliko tunayoyataka. Ni mpaka wawepo mamilioni ya watu, wenye "moyo wa Lema", ndipo tunapoweza kuyaona mabadiliko tunayoyatarajia. Kinyume cha hapo, hizi zitakuwa ndoto za mchana, na hekaya za Abunuwasi!

Mtawala gani wa Afrika, atakayekubali itungwe Katiba "fair", itakayokitoa chama chake madarakani; bila kuwepo confrontation? Sahau, siyo watawala wa Afrika!

Lema ameonesha njia, nami nafuata nyayo zake!!
 
Hiyo ni "publicity stunt" na haina mshiko kwa sasa.

Inawezekana kuwa na mshiko kwa baadae. Sidhani kama amefanya hivyo for public stunt. Imeshafanywa na mtu mwingine nchini nyingine na akafanikiwa. Inaonekana Lema amedesa kwa huyo mtu. And who is that? Martin Luther King. Autobiography King inasema kuwa akiwa mwanafunzi alikamatwa na wanafunzi wengine 280 kwa kufanya maandamano ya amani kudai kuunganisha white and black lunch counters chuoni kwao. Alipokwenda mahakani aliamua kutoomba bail. Kuona hivyo, wanafunzi wengine waliokamatwa nao waliaamua kutoomba bail pia. Kwa wana usalama hii sio kitu ya kupuuza maana hata akina Mandela na ANC walikuwa wanafanya hivyo hivyo. And when the jails are full what would you do?

This is what King told the judge:

"And, sir, I know you have a legal obligation facing you at this hour. This judicial obligation may cause you to hand us over to another court rather than dismiss the charges. But, sir, I must say that I have a moral obligation facing me at this hour. This imperative drives me to say that if you find it necessary to set a bond, I cannot in all good conscience have anyone go buy my bail. I will choose jail rather than bail, even if it means remaining in jail a year or even ten years. Maybe it will take this type of self-suffering on the part of numerous Negroes to finally expose the moral defence of our white brothers who happen to be misguided and thusly awaken the dozing conscience of our community."

Na hii ni barua aliyomwandikia mkewe akiwa jela. Ina baadhi ya maneno ambayo Lema amemwambia mkewe.

LETTER TO CORETTA

Reidsville, Georgia

Hello Darling,

Today I find myself a long way from you and the children. I am at the State Prison in Reidsville which is about 230 miles from Atlanta. They picked me up from the DeKalb jail about 4 o'clock this morning. I know this whole experience is very difficult for you to adjust to, especially in your condition of pregnancy, but as I said to you yesterday this is the cross that we must bear for the freedom of our people. So I urge you to be strong in faith, and this will in turn strengthen me.

I can assure you that it is extremely difficult for me to think of being away from you and my Yoki and Marty for four months, but I am asking God hourly to give me the power of endurance. I have the faith to believe that this excessive suffering that is now coming to our family will in some little way serve to make Atlanta a better city, Georgia a better state, and America a better country. Just how I do not yet know, but I have faith to believe it will. If I am correct then our suffering is not in vain.

I understand that I can have visitors twice a month-the second and fourth Sunday. However, I understand that everybody-white and colored-can have visitors this coming Sunday. I hope you can find some way to come down. I know it will be a terrible inconvenience in your condition, but I want to see you and the children very badly.

s Eternally Yours,

Martin

October 26, 1960
 
Haina mshiko hata mkiifananisha na Martin Luther King na Mandela, they had a "cause".

Sasa Lema ana "cause" ipi? ni kesi ambayo haifanani kabisa na hizo nyingine. Wajinga ndio waliwao.
 
aisee watu tunatofautiana kuelewa na mtazamo

mimi naamini 'confrontational politics' hazitasaidia hii nchi
sana sana zitaleta 'machafuko'
na watakaoumia ni wasio na hatia...mke wa lema anaweza kupanda ndege na watoto haooo nairobi au kampala

CCM ni kama 'machizi wenye silaha'
unahitaji kutumia 'akili' ku deal nao
na sio kuanzisha 'mapambano'
mkuu hakuna namna... Viongozi wamekua deafs and wamelewa madaraka

another sierra leone in the making
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom