Hii ya wake wa viongozi wastaafu kuanza kulipwa ni zaidi ya too much

Rais akistaafu anapata 80% ,Sasa mke wa mpango,mke wa warioba,mke wa majaliwa,mke wa mkapa,mke wa sumaye,mke wa pinda,mke wa magufuli wote wapate 25% ,hesabu ya KIZIWI ni kuwa 80%+25%=105% Kwa hiyo CCM wameamua Rais aliyeko madarakani apate fedha ndogo lakini ukistaafu mshahara unakuwa mkubwa kuliko ukiwa unafanyakazi ,ni heri Wagner waje Tanzania tuondokane na hawa mashetaniiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Acheni Roho mbaya mnataka Mama Janet Magufuli aishi vipi? Ngazi ya Urais inatakiwa iheshimiwe
 
Mbona kama vile nchi hii ina Ufa mkubwa sana wa kujali raia wake?

Yaani mwanajeshi mstaafu kapigana vita Uganda na kaponea chupuchupu mara kadhaa vitani, daktari aliyestaafu miaka ya 1990 na Mungu amempa maisha mpaka leo au Mwalimu aliyekuwa anatumika kwa moyo wote miaka hiyo bahati mbaya kwa serikali HAJAFA hadi leo anapokea kutoka HAZINA shs laki moja kama pension kila mwezi lakini eti wake wa viongozi nao wawe wanalipwa mamilioni 25% ya mishahara waliyokuwa wanalipwa waume zao?

Basi nchi hii ni tajiri sana! Lakini kwa nini haiwakumbuki basi hata hawa wazee waliolitumikia taifa kwa moyo mmoja enzi hizo.

Kumbukeni nazungumzia wastaafu walio staafu zamani 1998 kwenda nyuma kabla ya mifuko ya jamii haijaanza na wanalipwa na Hazina.
Kwanza sidhani kama wastaafu hawa wanazidi 5000 nchi nzima maana wengi wametangulia mbele ya haki waliobaki ni mateso tuu.

Mara ya mwisho kiwango hiki kupanda na kuwa laki moja ni miaka 10 iliyopita wakati wa JK. Waoneeni huruma acheni uchoyo.

View attachment 2744590View attachment 2744592
NCHI YA HOVYÒ SANA HII WAJINGA NI WENGI NDIO MAANA VIONGOZI WANAWAGEUZA KAMA CHAPATI ZA MAJI NIKIFIKIRIA MAFAO WANAUOPATA RAIS MAKAMU WA RAIS NA WAZIRI MKUU KWA MAISHA YAO YOTE SERIKALI YENYE HURUMA NA WANANCHI WAKE ISINGEKUJA NA MSWAADA WA HOVYO KAMA HUU
 
Wakati huo huo wametengeneza kikokotoo cha kumuumiza mstaafu!
Lakini tutafanyaje?
Acha tuendelee kufa na tai shingoni!
 
Tulishasema kuwa kiendelea kuichagua ccm ni sawa na kujichombia kaburi sisi wenyewe.

Kuichagua ccm ni sawa na kujikaanga wenyewe kwa mafuta yetu.
Ccm ni watawala haramu kwani wanatawala bila ridhaa ya walio wengi!! Hilo linawezekana tu kwa kuwa wanatumia vyombo vya usalama; bila hivyo wasingekuwa na serikali!
 
Kazini nako waweke huo utaratibu pia mfanyakazi akistaafu basi mkewe apate pension maana hakuna utofauti
 
Ccm ni watawala haramu kwani wanatawala bila ridhaa ya walio wengi!! Hilo linawezekana tu kwa kuwa wanatumia vyombo vya usalama; bila hivyo wasingekuwa na serikali!
Kuna watu hadi sasa bado wana mapenzi na ccm na wanawapigia kura, hao ndio wenye kuwapa nguvu ccm kuendelea kuwa madarakani kuliko hata hivyo vyombo vya usalama.
 
Hakuna ukweli kuwa watu wanao ipigia kura ccm wana nguvu kuliko vyombo vya dola na tume.

Hapo hakuna ukweli mjomba.
 
Kuna watu hadi sasa bado wana mapenzi na ccm na wanawapigia kura, hao ndio wenye kuwapa nguvu ccm kuendelea kuwa madarakani kuliko hata hivyo vyombo vya usalama.
Wangekuwa na wananchi wengi wanaowapenda wasingekuwa wananunua na kuiba kura wakati wa uchaguzi!
 
Mbona kama vile nchi hii ina Ufa mkubwa sana wa kujali raia wake?

Yaani mwanajeshi mstaafu kapigana vita Uganda na kaponea chupuchupu mara kadhaa vitani, daktari aliyestaafu miaka ya 1990 na Mungu amempa maisha mpaka leo au Mwalimu aliyekuwa anatumika kwa moyo wote miaka hiyo bahati mbaya kwa serikali HAJAFA hadi leo anapokea kutoka HAZINA shs laki moja kama pension kila mwezi lakini eti wake wa viongozi nao wawe wanalipwa mamilioni 25% ya mishahara waliyokuwa wanalipwa waume zao?

Basi nchi hii ni tajiri sana! Lakini kwa nini haiwakumbuki basi hata hawa wazee waliolitumikia taifa kwa moyo mmoja enzi hizo.

Kumbukeni nazungumzia wastaafu walio staafu zamani 1998 kwenda nyuma kabla ya mifuko ya jamii haijaanza na wanalipwa na Hazina.
Kwanza sidhani kama wastaafu hawa wanazidi 5000 nchi nzima maana wengi wametangulia mbele ya haki waliobaki ni mateso tuu.

Mara ya mwisho kiwango hiki kupanda na kuwa laki moja ni miaka 10 iliyopita wakati wa JK. Waoneeni huruma acheni uchoyo.

View attachment 2744590View attachment 2744592
Huyu mke wa Kikwete alidhiki tu mbona familia yake wanaifadi hii nchi ya kutosha bado ni mbunge na bado anataka kulipwa mafao ya mumewe ya kustaafu duuh jamani Mungu atusaidie Watanzania
 
Back
Top Bottom