Muswada wa wenza wa viongozi kulipwa mafao ya kustaafu umepita vipi; mbona madai ya wastaafu Posta na ATC hawalipwi?

kisingi

JF-Expert Member
Apr 9, 2014
516
377
Bunge limepitisha haraka mswada wa kulipa mafao ya kustaafu wenza wa viongozi.

Huzuni kubwa ni kuwa bunge limeshindwa kuibana serikali kulipa madai ya kustaafu wastaafu wa Posta na ATCL. Madai halali hayalipwi lakini tayari sheria inatungwa kuwaongezea mafao katika maisha ya wenza wa viongozi wastaafu.

Kweli watu wote si sawa lakini kuweni na huruma wazee wastaafu hawa walipwe madai yao.

Mbona serikali inakwamisha kuwalipa wananchi wa kawaida wastaafu na kukimbilia kutunga sheria kwa aliyenacho aongezewe ili hali wastaafu wa kawaida wanakosa pesa za tiba, kujikimu na chakula kwa kuwa pesa zao zipo mikononi mwa viongozi fulani.

Bunge fanyeni hima hawa wazee walipwe kama mlivyosimamia kupitisha sheria ya wenza wa viongozi kulipwa mafao ya kustaafu.

Nchi hii ni nzuri lakini sasa aliyenacho huongezewa asiyenacho hukosa hata ili haki yake.
 
Hao wastaafu wa ATCL na halmashauri huko waache usumbufu. Wajiajiri tu hakuna namna
 
Inawezekana wewe ni mmoja wanao nugaika na michango ya wastaafu kwa kilipwa posho ndio maana unaita usumbufu madai halali ya wazee wastaafu. Mungu anakuona japo wazee hawa hawakuoni. Endelea kula pesa za wastaafu.
 
Hii sheria isainiwe na kuanza kazi kabla ya Disemba 2023. Tuwaenzi Viongozi wastaafu.
 
Bunge limepitisha haraka mswada wa kulipa mafao ya kustaafu wenza wa viongozi.
Huzuni kubwa ni kuwa bunge limeshindwa kuibana serikali kulipa madai ya kustaafu wastaafu wa Posta na ATCL. Madai halali hayalipwi lakini tayari sheria inatungwa kuwaongezea mafao katika maisha ya wenza wa viongozi wastaafu.
Kweli watu wote si sawa lakini kuweni na huruma wazee wastaafu hawa walipwe madai yao.
Mbona serikali inakwamisha kuwalipa wananchi wa kawaida wastaafu na kukimbilia kutunga sheria kwa aliyenacho aongezewe ili hali wastaafu wa kawaida wanakosa pesa za tiba, kujikimu na chakula kwa kuwa pesa zao zipo mikononi mwa viongozi fulani.
Bunge fanyeni hima hawa wazee walipwe kama mlivyosimamia kupitisha sheria ya wenza wa viongozi kulipwa mafao ya kustaafu.
Nchi hii ni nzuri lakini sasa aliyenacho huongezewa asiyenacho hukosa hata ili haki yake.
Hawawahusu, walikwisha lipwa buku saba wakati wa kampeni.
 
Nchi hii imejaa viongozi mashetani, makatili halafu wanajifanya kunyenyekea kwenye nyumba za ibada, wapi mafao ya waliokuwa wafanyakazi wa EAC?(jumuiya ya afrika mashariki),watumishi wale wamekufa wengi bila kulipwa fedha zao zilizoporwa na serikali kulipia vita ya Uganda tuliyojitakia, kuanzia wa bandari hadi posta na simu, elewa nchi hii ukiwa nje ya royal families, utafia Amana hosp, royal families wanatibiwa India, uk, Canada au netcare millpark.
 
Nchi hii kila mtu anajipambania mwenyewe ukiamua kumtegemea mtu huwezi kupata hata HAKI YAKO.

UBINAFSI NA UPENDELEO UPO SANA NCHI HII.
 
Hao wastaafu wa ATCL na halmashauri huko waache usumbufu. Wajiajiri tu hakuna namna

Punguza dharau. Kujiajiri ndio Nini?. Watu wanadai mafao yako kihalali na haki yao wewe unasema wakajiajiri. Tupunguze unafiki saa zingine.
 
Bunge limepitisha haraka mswada wa kulipa mafao ya kustaafu wenza wa viongozi.
Huzuni kubwa ni kuwa bunge limeshindwa kuibana serikali kulipa madai ya kustaafu wastaafu wa Posta na ATCL. Madai halali hayalipwi lakini tayari sheria inatungwa kuwaongezea mafao katika maisha ya wenza wa viongozi wastaafu.
Kweli watu wote si sawa lakini kuweni na huruma wazee wastaafu hawa walipwe madai yao.
Mbona serikali inakwamisha kuwalipa wananchi wa kawaida wastaafu na kukimbilia kutunga sheria kwa aliyenacho aongezewe ili hali wastaafu wa kawaida wanakosa pesa za tiba, kujikimu na chakula kwa kuwa pesa zao zipo mikononi mwa viongozi fulani.
Bunge fanyeni hima hawa wazee walipwe kama mlivyosimamia kupitisha sheria ya wenza wa viongozi kulipwa mafao ya kustaafu.
Nchi hii ni nzuri lakini sasa aliyenacho huongezewa asiyenacho hukosa hata ili haki yake.

Sent from my Infinix X657C using JamiiForums mobile app
 
Attachments

  • IMG-20231019-WA0005.jpg
    IMG-20231019-WA0005.jpg
    26.6 KB · Views: 3
Back
Top Bottom