Hii tabia ya kuhamisha viongozi waliofeli inazidi kuturudisha nyuma kimaendeleo

Joyboy

JF-Expert Member
Sep 16, 2023
1,364
3,408
Kuna tabia moja imekuwa inanishangaza sana kwa muda mrefu kuhusu uongozi wetu wa hii nchi. Sijui kwanini tupo hivi ila unakuta kiongozi wa serikali mfano amefanya mambo ya ajabu wizara flani baada ya kugundulika eti ana hamishwa ile wizara anapelekwa wizara nyingine.

Mfano mwingine, Unakuta Kiongozi wa wizara fulani anagundulika aliiba hela za wizara ana hamishwa pale anapelekwa kuwa mkurugenzi wa taasisi nyingine.

Nchi za wenzetu kama Japan, China, North Korea na Russia watu kama hawa huwa wanachukuliwa hatua za kisheria kama sio kunyongwa, ila sisi huku tunafuga hawa watu, eti unamuhamisha kweny sehemu nyingine, hii ndio njia sahihi ya kudeal na watu wa namna hii kweli?

Kwanini tunafuga corrupt leaders?

Je Serikali inawaonea aibu hawa watu?

Karibuni
 
Ninaposema tatizo ni mfumo wa utawala wa CCM muwe mnaelewa!! Hili mdio tatizo kubwa la maendeleo ya Nchi ya Tanzania, haiwezekan kupata maendeleo kwa mtindo huo wa kulinda mafisadi na wabadhirifu wa mali za umma!! Kiongoz kafanya madudu Badala ya kumfikisha mahakamani eti anatolewa alipo anahamishiwa kwingine 🤣🤣🤣🤣🤣🤣!! Hoja kama hiz uvccm na machawa wote humu mlipaswa mje kujibu!!
 
Yaani unataka kusema mwizi anaweza kuwa Waziri Mkuu wetu
Hapanaa mkuu cjamaanisha hvyo ,namaanisha mama ndio anateuwa na kutengua ,hvyo Kwa mtindo huu km atakaa mpk 2030 kazi ipoo maana atakuwa aingizi watu wenye mawazo mapya Bali wale wale ambao n wachumia tumboo..
 
Nahic hawa watu wanaonewa aibu na mahakama kwa sababu unakuta wengine baba zao ni waasisi wa chama cha siasa maarufu hapa nchini kama mtu fulani, wana mizizi kweny chama.
Huwaga kuna siku namkumbuka Magufuli hadi nachoka aisee.
 
Mfumo wa Serikali kumuondoa mtumishi kazini ni mtiti.Mtumishi ana visheria kibao vinamlinda
 
Hapanaa mkuu cjamaanisha hvyo ,namaanisha mama ndio anateuwa na kutengua ,hvyo Kwa mtindo huu km atakaa mpk 2030 kazi ipoo maana atakuwa aingizi watu wenye mawazo mapya Bali wale wale ambao n wachumia tumboo..
Sasa wachumia tumbo sio kutenda matendo ovu ili Hilo tumbo lipate chakula?
Na asili ya huyo kiongozi historia yake haihusishwi na wizi
 
Kuna tabia moja imekuwa inanishangaza sana kwa muda mrefu kuhusu uongozi wetu wa hii nchi. Sijui kwanini tupo hivi ila unakuta kiongozi wa serikali mfano amefanya mambo ya ajabu wizara flani baada ya kugundulika eti ana hamishwa ile wizara anapelekwa wizara nyingine.

Mfano mwingine, Unakuta Kiongozi wa wizara fulani anagundulika aliiba hela za wizara ana hamishwa pale anapelekwa kuwa mkurugenzi wa taasisi nyingine.

Nchi za wenzetu kama Japan, China, North Korea na Russia watu kama hawa huwa wanachukuliwa hatua za kisheria kama sio kunyongwa, ila sisi huku tunafuga hawa watu, eti unamuhamisha kweny sehemu nyingine, hii ndio njia sahihi ya kudeal na watu wa namna hii kweli?

Kwanini tunafuga corrupt leaders?

Je Serikali inawaonea aibu hawa watu?

Karibuni
CCM kuna mtandao wa viongozi na watoto wao, ambao wamejipatia daraja na haki ya kuongoza wao tù, nyie wengine mtaambulia ma t shirt ya kijani, kofia ya njano, vilema na wali maharage kipindi cha kampeni
 
Ninaposema tatizo ni mfumo wa utawala wa CCM muwe mnaelewa!! Hili mdio tatizo kubwa la maendeleo ya Nchi ya Tanzania, haiwezekan kupata maendeleo kwa mtindo huo wa kulinda mafisadi na wabadhirifu wa mali za umma!! Kiongoz kafanya madudu Badala ya kumfikisha mahakamani eti anatolewa alipo anahamishiwa kwingine !! Hoja kama hiz uvccm na machawa wote humu mlipaswa mje kujibu!!

Hapa aliyeweza ni magufuri tu ukiborobga kaa nje
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom