Jodoki Kalimilo
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 12,013
- 10,174
Hivi serikalini huwa wanakata asilimia (%) kwenda NHIF maana bima ya afya kwa watumishi wa serikali inatibu magonjwa mengi kuliko hizi bima za vifurushi kama wanavyoziita na ukute mtu amelipia 600,000 (laki 6), huwa najiuliza serikalini huwa wanalipa zaidi kiasi kwamba hizi za vifurushi zinapewa hadhi ya chini... kero ni nyingi sana kwenye huu mfuko. Unakatwa mshahara wako kwa lazima kulipia NHIF ila kama huna mtoto wa kumzaa huruhusiwi kuweka ndugu (mfano unayemlea); nafasi zako 4 (kama ungekuwa na watoto) zinakuwa zimekwenda bure faida kwa mfuko. Ukiuguliwa na huyo ndugu itakubidi kuingia gharama za matibabu yake ilhali kwenye mfuko una nafasi ambazo hutakiwi kumsajili.
Pili, watoto wote uliokuwa umewasajili wameshavuka 18/21; kwanini mwanachama huyu asipate nafuu ya makato? Badala yake makato yake yanabaki yaleyale. Tatu, badhi ya huduma muhimu zimepunguzwa; ukosefu wa baadhi ya dawa hivyo mhusika kulazimika kuingia mfukoni, n.k.