Hii ni Dharau kwa Fani ya Udaktari!

labda kama hujaisoma kwa makini.....ipitie tena utakutana na aya hii

''Ni kweli kwamba yeye si mtumishi wa Serikali, hivyo hakustahili kuwa sehemu ya majadiliano haya. Kulikuwa na rai ya kutaka asiwepo, lakini nilisema wamuache maadam Madaktari wanamuamini kuwa anaweza kuwasemea vizuri zaidi kuliko wao wenyewe walioajiriwa na Serikali.Na, kuhusu mgomo, Mahakama Kuu imekwishatoa amri ya kusitisha mgomo. Anayekaidi amri ya Mahakama ananunua lugomvi na mhimili huo wa dola ambao wenyewe una mamlaka ya kumtia adabu mtu huyo. ''

Hapo palipokolezwa, panajieleza vizuri zaidi, na kumfanya kuwa mtu anayefahamu yote kuhusu Dr Uli.
 
Ovyo kabisa wewe, labda kama ni mwalimu wa kufundisha mbumbumbu wenzio, kama ungekuwa professional hakika usingeandika huo upumbavu wa ku-criticize taaluma zingine. Umenitia kichefuchefu sana. Huu mgomo unahusika vipi na taaluma zingine, unaona wengine wote waliosoma taaluma zingine ni mavi siyo!

Tapika kabisa! Sas nikuoneshe umbumbumbu wako na wewe! Naam mtu alipwe kuendana na taaluma na ugumu na umuhimu wa taaluma yake kwa taifa. Kikwete mwenyewe kalisema hili. hata mimi ni mwalimu lakini ualimu na udaktari wala havikaribiani. Penda usipende. Sas nadhani umeshatapika kabisa! Mwite mama watoto afute matapishi!
 
Ozzie, simple, kuna ripoti ya hivi karibuni inaonyesha kiwango kikubwa cha brain drain...we spend a lot training docs yet we fail to retain them...only to be employed by foreign countries. Yaani tunasikitisha sana majibu yaliyotolewa kuhusu trend hiyo.

Nakubaliana na wewe, na hata CAG ameona kuwa masomo ya sayansi hayapendwi, hivi yanahitaji wasomi wenye kupewa motisha, sasa mkuu wa nchi haoni kama ni muhimu...
 
Kwa nini watu wengine wanachangia bila kufikiria, hata kama mtu amekosea kuelezea mada lakini kila kitu kuhusu madokta kinaeleweka.

Nyie mnaochangia na kukejeli madaktari mna akili finyu na uwezo mdogo sana wa kufikiria. Sina mengi ya kuwaambia ila inawezekana ni sababu ya malezi kitu ambacho sio makosa yenu, ni wazazi. Kazi wanazofanya madaktari na manesi sio za kubeza, kuna mliochangia vibaya hamuwezi hata kuingia kwenye wodi za wogonjwa achilia mbali kushindwa kufaulu masomo ya sayansi.

Daktari kama daktari, nesi kama nesi na muuguzi mwingine yoyote wa hospitali anatakiwa apewe maisha mazuri. Kitu kikubwa ni ile kitu tunaita saikolojiko tocha wanayopata madaktari hospitalini.

Mimi siungi mkono hao wanaoponda na ni vyema wangekaa kimya wangeonekana na busara.
 
Kama ni madaktari wadai tu hayo malipo, nafikiri wasihusishe fani zingine eti rahisi ama miaka mingi ama kazi ngumu, hapana nafikiri waangalie madai yao.

Sifikiri kama structural engineer amepeta kirahisi, na anafanya kazi ktk mazingira rahisi.
 
mcfm40

Mkuu kama dharua huo mshahara ni mdogo nenda kapige kazi Marekani au Ulaya.
 
Last edited by a moderator:
Acha upotoshaji wa kihuni, una hakika kuwa hao wote uliowataja hapo juu wanalipwa laki 9 kwa mtu anayeanza kazi leo.?? Hapo kuna ambao wanaanzia na laki 4.5 anapoanza kazi.
webondo awatoe Mahakama nadhani.
 
Last edited by a moderator:
kikwete mwenyewe alisema unapoangalia kiwango cha mshahara unaconsider muda wa mtu kusomea fani hiyo na umuhimu wake kwa jamii sasa umbumbumbu unautoa wapi? hata libya ya ghadafi unakuta dokta alimzidi mshahara waziri!! professa sawa kasoma muda mrefu kuliko daktari na majimarefu nae kasoma muda mrefu kuliko daktari? halafu inategemea professa wa nini huwezi kufananisha prof wa kiswahili na prof wa cardiology,

Sawa kama unaona Libya ndiyo wanatoa mshahara mnaoutaka, Rais Kikwete anawatakia kila la kheri muende huko.
 
Tujiulize, kama wanapendelewa sana inakuwaje Dk Mwinyi (Mb), Dk Prof Sarungi, Dk Kigwangala nk walikimbilia kwenye siasa?
 
Si dharau ni changamoto mojawapo ya kuwapata madaktari wazalendo na si vinginevyo,uzalendo kwa kada hii ni muhimu sana kuliko kitu chochote (bora utu kuliko kitu) hayo mengineyo ni majaaliwa ya mwenyezi mungu.
 
Nimemsikiliza Mheshimiwa Raisi nimegundua mambo yafuatayo
1. Anaongea kwa namna ya kuonyesha madaktari ndio chanzo cha matatizo na sio serikali. Nasikitika sana hotuba ya Raisi wangu ni uchonganishi na usanii wa hatari sana. Hana nia ya kweli ya kujadili na watu wenye akili. Anafanya usanii aliouzoea
2. Anatumia majina ya watu kama alivyomtaja Mgaya wakati ule kwa nia ya kuonyesha tatizo ni viongozi
3. Anatumia vitisho kuiita mgomo ni haramu
4. Siasa kwetu watanzania in sumu kali na ya kutisha naogopa
 
Tapika kabisa! Sas nikuoneshe umbumbumbu wako na wewe! Naam mtu alipwe kuendana na taaluma na ugumu na umuhimu wa taaluma yake kwa taifa. Kikwete mwenyewe kalisema hili. hata mimi ni mwalimu lakini ualimu na udaktari wala havikaribiani. Penda usipende. Sas nadhani umeshatapika kabisa! Mwite mama watoto afute matapishi!
Kilaza mwingine wewe!
 
TELO

Mimi ni mkufunzi (TA) wa Chuo kikuu kimoja hapa bongo.

Mshahara wangu wa Tutorial assistant nilianza na zaidi ya 1m, kumzidi hata Dr, na course ya undergraduate ilikuwa miaka 3. Na kazini nina nyumba, usafiri, maji, umeme. Na bado nina muda mwingi tu wa kuwa idle (si kama Dr akianza kazi hatoki mpaka usiku). Wakati mwingine Dr anafanya kazi hata weekend, mimi sifanyi.
Ni chuo gani hicho kinachomlipa tutorial assistant mshahara wa milioni moja halafu kinampa nyumba, usafiri, maji na umeme? Nitajie jina tafadhari ili na mimi niombe kazi huko. Bila shaka si chuo cha serikali. Maana vyuo vya serikali mshahara wa kuanzia wa tutorial assistant haujafika milioni moja. Acheni kupotosha.
 
Mimi sio muamini wa serikali hii kutokana na baadhi yamambo mengi ambayo hayako sawa, ila kwa hili la madakitari kutaka kulipwa mara nane ya watumishi wengine wa umma wenye elimu sawa nalikataa. Natambua umuhimu na ugumu wa kada ya udakitari, lakin haiwezi kupelekea kujenga tofauti kubwa kiasi hicho kimasilahi na kada zingine. Kupigania hali bora mazingira ya afya nchini ni muhimu, lakin hayaweza kuboreshwa kwa muda mfupi hivyo, lakini pia haiwezi kuwa sababu ya kuacha watu waendelee kufa kwa kukosa matibabu

Muarubaini nakuunga mkono,mimi pia niko idara hii ta afya lkn siungi mkono mgomo huu.Inaonekana kuwa madaktari wanataka kujenga matabaka kwa watumishi wa umma ili ionekane kuna walio muhimu na special kuliko wengine.Hili si jambo jema na haliwezi kukubaluka
 
SOMA HII KAMA UNA IQ SCORE ZAIDI YA 190
Baada ya miaka kumi tu ijayo kuanzia leo wananchi watakuwa wanaandamana kuishinikiza serikali kusolve tatizo la hospitali kutokuwa na madaktari wa kutosha kwani hamna mwanafunzi aliehitimu PCB advanced level atakae taka kusoma fani ambayo ni ngumu, miaka mingi na kipato kidogo...na afterall intellectuals ndo wanachaguliwa kusoma fani hii.. kwa kawaida mtu anasoma kwa bidii akiamini ndo anajitengenezea maisha sasa na digrii yako unapata 900,000Tshs per month nonsense hamna atakae taka fani hii... si busara na hatari zaidi kutokuwa na madaktari kuliko kuwa na madaktari wanaogoma kutaka kuongezewa mshahara na mazingira mazuri ya kazi...kama swala hili halitashughulikiwa ipasavyo unabii huu utatimia soon (2020)
 
Sijasikiliza hotuba ya Jk lkn inaonekana amezengumzia mishahara ya madk, vipi kuhusu mazingira na vifaa vya kazi? Hajasema kitu?
 
Sawa kama unaona Libya ndiyo wanatoa mshahara mnaoutaka, Rais Kikwete anawatakia kila la kheri muende huko.
libya ya ghadafi ulikuwa ni mfano wa nchi zilizokuwa zinatoa mshahara kwa kuangalia elimu ulikuwa ni mfano, sawa?hivi kwanini daktari wa NIMR apewe hela nyingi kuliko wa muhimbili? au muhasibu wa TANAPA hela nyingi kuliko wa hazina. kingine kinachowachochea madaktari ni kuona wengine wakipeta wao wakidai wanaambiwa nchi haina hela!! hili swala linaudhi sana.
 
Back
Top Bottom