Hii ni Dharau kwa Fani ya Udaktari!

Umeajiriwa serikalini na serikali kuu au umeajiriwa na Taasisi ya serikali?Kaulize daktari aliyekatika Govt agencies kama NIMR analipwa shilingi ngapi.Hebu muwe mnaumiza kichwa kabla hamjapost comments zenu humu.
Siyo kuumiza kichwa. Nafahamu agencies wanalipwa tofauti. Ila it does not make sense kufanya comparison. Waachiwe ma Dr wao na serikali, sisi wananchi tuwaombe Dr warudi kazini na si kuwatukana kwa kuwadharau, tunawavunja moyo!
 
mcfm40

Suala la muhimu ni kurekebisha mishahara na posho za wafanyakazi. Kwa mfano hakuna tija kwa mtu kusafiri na kulipwa dola karibu 600 kwa usiku mmoja wakati analala kwenye hoteliniliolipiwa na wizara ya mambo ya nje na Kula bure.

Kwa ufupi Toa posho zote zijumuishe kwenye mshahara na zikate kodi, baada ya hapo mishahara yote itakuwa mikubwa wakati huohuo serikali itaongeza mapato na kutakuwa na usawa wa malipo kwa wafanyakazi wa kada zote.
 
Last edited by a moderator:
Na kazini nina nyumba, usafiri, maji, umeme. Na bado ninamuda mwingi tu wa kuwa iddle (si kama Dr akianza kazi hatoki mpaka usiku). Wakati mwingine Dr anafanya kazi hata weekend, mimi sifanyi.

Ahsante sana kwa Tusi, si ajabu ndivyo unavyotukana hata wazazi wako na wanafunzi wako au mkeo pale wanapotofautiana na wewe kwenye hoja.

Hongera zako kama wewe unafundisha chuo ambacho unapata vyote hivyo kama ulivyovitaja. Hali ni tofauti kwa UDSM na vyuo vingine vya serikali (UDSM ambayo ndiyo ilikuwa sehemu anakofanya kazi mleta hoja). Labda wewe uko chuo binafsi. Kwa UDSM, angalia structure hiyo hapo chini na hii ni doc ya serikali kwa Academic Staff wote wa vyuo vya serikali. Kuhusu nyumba, usafiri, maji na umeme unajitegemea. Hii ni kwa wote kuanzia Tutorial Assisstant mpaka Lecturer (PhD Holder ambaye hajawa Senior). Kwa UDSM, ni Senior Lecturere tu ndiyo wenye House Allowance. Kama wewe ni TA, ASS. Lecturer au Lecturer, hakuna nyumba wala maji wala umeme wala usafiri. Na kama ikitokea umepata nyumba chuoni, basi 10 percent ya Basic salary yako inakatwa. Pia umeme na maji utajitegemea gharama zake.

Kuhusu kufanya kazi weekend, nenda UDSM hata weekend kuna tests zinafanyika. Hii si kwasababu wale waalimu wamependa,la hasha,ni kwasababu ya uwingi wa wanafunzi na vyumba vilivyopo havitoshelezi katikati ya wiki.

Ukiwa na uelewa mzuri utaweza kuona kwamba 3.5 mill. ya Drs inaangukia kwenye level ya Associate Professor (angalia rangi nyekundu kwenye Jedwali hapa chini).

1. New Salary Structure for Academic staff effective July 2010

Ngazi ya mshahara
Kianzio kwenye ngazi
Nyongeza ya kila mwaka
Kima cha juu kwenye ngazi
PUTS 12
1,080,100
55,990
1,248,070
PUTS 13
1,348,070
60,980
1,531,010
PUTS 14
1,701,010
63,000
1,890,010
PUTS 15
2,060,010
69,960
2,269,890
PUTS 16
2,439,890
76,950
2,670,740
PUTS 17
2,840,740
77,720
3,073,900
PUTS 18
3,243,900
79,110
3,481,230
PUTS 19
Fixed
3,651,230
PUTS 20
Fixed
3,821,230
PUTS 21
Fixed
3,991,230

2. Housing Allowances effective July 2010

Utaratibumpya wa malipo ya posho ya nyumba:

Watumishi wenye stahili ya kupatiwa nyumba bila ya kulipa pango ambao hawana nyumba na hawajawahi kuuziwa nyumba na Serikali au Taasisi watalipwa kiwango maalum ili waweze kupanga nyumba.
 
Ni kichekesho kwamba mganga wa kienyeji na wenzake wa darasa la saba pale bungeni anakula milioni 7, professionals wanadhihakiwa. What are our priorities?

Mkuu hapo kwenye blue ndo pana utata sana katika nchi yetu na dharau kubwa sana.

Madaktari kwa hili, hakuna kurudi nyuma pambaneni mpaka mwisho wake.
 
Nimenukuu baadhi ya maneno ya JK kwenye hotuba yake.
Yani anaposema kuwa Muajiri hana uwezo wa kukulipa so yanini Dr Kugoma.
Hii kauli inamaaana kuwa hata yale madai ya serikali kuwa wanayafanyia kazi madai yote ya Ma daktari ni Ulaghai na Usanii Mtupu, Hii inamaana kuwa Seikali ilikuwa inainawazuga tu Ma Dr ilhali haikuwa na nia ya dhat ya kutekeleza Baadhi ya Madai ya Ma Dr.

My Take
Drs Msirudi Nyuma, JK huyu huyu atakuja kuwapigia Magoti

Wasirudi nyuma kivipi wakati wameshaambiwa hawana haja ya kugoma ni bora kukabidhi mikoba na amewatakia kila la kheri huko waendako.
 
Doctors have no guts to quit their jobs, nendeni private au abroad mkapate hela nyingi...serikali miyeyusho tu....mtakuwa kama wabunge wenu matumbo makubwa!
 
Aka, mimi ndo maana nilitafakari nikaachana kabisa na somo la biology nikiwa fomu two na kufuta ndoto ya kuwa daktari.
 
Vipi TELO mbona unatokwa povu sana? Si bure!
 
Last edited by a moderator:
hizo kozi laini mnazotaka kusoma si ndo maana mmejaa mitaani hakuna kazi,lawyers kibao mtaani,nitafutieni dr ambae hana kazi,soma miaka 5 kwa shida upate uhakika wa ajira au 3 years kilaini usote mtaani,na ingekua fani nyingine wangeshafukuzwa.bado wanathaminiwa
 
Jamani mimi ni mwalimu nafundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kama Assistant Lecturer.

Kusema kweli hii nchi haijui dhamani ya madaktari na maprofeno wengine kwa ujumla. Hivi kweli unaweza kulinganisha miaka mitano ya kusomea udaktari na miaka mitatu ya digrii nyingine hizi! Nimeshangaa eti daktari anayeanza kazi analipwa laki 9. Huu ni mshahara mdogo kuliko wa tutorial assistant aliyesomea digrii yake kwa miaka mitatu tu tena digirii laini ( nimesoma mimi arts) usinitolee mimacho! ni laini tu huwezi kulinganisha na nondo za udaktari! Kusema ukweli interns wanapaswa kulipwa minimum 2m. Yaani daktari alipwe sawa na kada nyingine? You are kidding! Kazi ya udaktari ni habari nyingine jamani tusidanganyane. Kikwete anachofanya ni kujaribu kugombanisha madaktari na wananchi! Unajua watu wa kawaida hawajui nondo za udaktari zilivyo ngumu na ilivyo ngumu kufaulu! Watu mliokimbia chemistry, physics, biology mnajua habari yake, sio mchezo!
Ovyo kabisa wewe, labda kama ni mwalimu wa kufundisha mbumbumbu wenzio, kama ungekuwa professional hakika usingeandika huo upumbavu wa ku-criticize taaluma zingine. Umenitia kichefuchefu sana. Huu mgomo unahusika vipi na taaluma zingine, unaona wengine wote waliosoma taaluma zingine ni mavi siyo!

Angalia katika nyekundu hapo ulivyoandika pumba.
 
Siyo kuumiza kichwa. Nafahamu agencies wanalipwa tofauti. Ila it does not make sense kufanya comparison. Waachiwe ma Dr wao na serikali, sisi wananchi tuwaombe Dr warudi kazini na si kuwatukana kwa kuwadharau, tunawavunja moyo!

Mkuu nakubaliana na wewe lakini ndugu zetu madaktari wamezidi,nimeshtuka sana nilipoona kama madai yao yote yakitimizwa daktari atakuwa analipwa Tsh 7,700,000/= kwa mwezi kwa kuanzia na itaendelea kupanda kila mwaka.Wana madai mengine ya msingi lakini madai yao mengi yamelalia maslahi tu.Kwa kweli kwa upande wangu naona Rais amehitimisha hili suala vizuri sana.
 
Ovyo kabisa wewe, labda kama ni mwalimu wa kufundisha mbumbumbu wenzio, kama ungekuwa professional hakika usingeandika huo upumbavu wa ku-criticize taaluma zingine. Umenitia kichefuchefu sana. Huu mgomo unahusika vipi na taaluma zingine, unaona wengine wote waliosoma taaluma zingine ni mavi siyo!
 
nimechoshwa na kauli eti daktari anapendelewa kwa kulipwa sana
........hebu nisaidieni mishahara ya hawa watu kwa level ya degree wanalipwa ngapi
........tanapa
.........tra
..........bot
........bandari
.......hazina
..........msd
..........nhif
..........kilimo
..........mahakama
.........ubalozini/mambo ya nje
..........etc....etc...

ni jasiri kaktika nini
 
Vipi telo mbona unatokwa povu sana. Au mwajiriwa wa nape nini. Si bure!

Mimi napenda ukweli (facts) na siyo upotoshaji. Wewe ulipoleta hoja ya kujustify malipo ya mil.3.5 kwa madaktari wanaoanza kazi ulisema kwamba wewe ni Ass.Lecturer wa UDSM na kusema mengi. Mimi nilichofanya ni kuleta figure na ukweli wenyewe.

Mimi naomba wasomaji waelewe kwamba mimi sipingi madai ya Drs wetu, lkn najaribu kuona nini justification ya wao kudai 3.5 mil.?, ukiangalia series ya yale madai utagundua kwamba priority haikuwa mazingira ya kazi bali madai binafsi. Madai yao ni ya msingi, lkn nashawishika kuamini kwamba Drs hawakuwa na timu nzuri inayoelewa nini cha kunegotiate na serikali. Wao walikwenda kwenye negotiations kama watu wa kwenda kutoa maelekezo basi. Na hili mimi ndiyo nashawishika kuamini kwamba Drs wetu hawajafanikiwa kwenye madai yao kwasababu hawakuwa na timu iliyojiandaa na kujua nini tofauti kati ya negotiations na madai. Kwenye negotiations lazima uweze kujustify offer zako na si kutoa maelekezo.
 
Hivi kwa nini serikali ili iondoe hii sintofahamu ya mishahara na watu kuhisi wanaonewa, kwa nini isitoe hadharani ni nani analipwa nini na marupurupu yake. Kwa mfano rais analipwa tsh ngapi na marupurupu yake ni nini, waziri mkuu, mawaziri, wabunge, wakurugenzi, wakuu wa mikoa, TANESCO, TRA, TANAPA, BOT, BANDARIni, madaktari, manesi, maphamasia, WALIMU, wanyama pori, Askari polisi. Yaani iwe wazi na watu wajitambue, hii itapunguza manung'uniko au itaongeza.
 
Back
Top Bottom