Hii ni Dharau kwa Fani ya Udaktari!

Nimenukuu baadhi ya maneno ya JK kwenye hotuba yake.
Yani anaposema kuwa Muajiri hana uwezo wa kukulipa so yanini Dr Kugoma.
Hii kauli inamaaana kuwa hata yale madai ya serikali kuwa wanayafanyia kazi madai yote ya Ma daktari ni Ulaghai na Usanii Mtupu, Hii inamaana kuwa Seikali ilikuwa inainawazuga tu Ma Dr ilhali haikuwa na nia ya dhat ya kutekeleza Baadhi ya Madai ya Ma Dr.

My Take
Drs Msirudi Nyuma, JK huyu huyu atakuja kuwapigia Magoti

Sasa naanza kuelewa kuwa macho ya binadamu si kama nilivyokuwa nayajua mengine yanaona DUNIA iliyojaa MADAKTARI tuu na hakuna kitu kingine!!, Na watanzania tunawategemea wasomi wetu wenye mtazamo wa aina hiyo watoe ushauri kutuongoza watanzania!!!
 
Sitaki kukubali kuwa muandishi wa habari hii ni mwalimu wa chuo kikuu, Lazima atakuwa ni muhuni wa mtaani tu huyu.

Mshahara wa kuanzia uwe mil 3.5 kwasababu kasoma miaka mi5? (wewe hovyo sana),Hebu waulize maprofesa wa hapo UDSM wanalipwa shilingi ngapi na wamesoma kwa miaka mingapi kuufikia uprofesa.Muheshimiwa Rais kaongea vizuri sana nadhani huu mjadala ufungwe,kama daktari anataka mil3.5 ambayo hata hospitali za private kama aga khan haulipi hivyo basi aache kazi atafute sehemu inayotoa mshahara wa namna hiyo.

Siyo lazima kila pumba uliyonayo kichwani uiandike humu unaweza kaa nayo tu ukajidanganye na wenzako vijiweni.

Mwambie dhaifu na mkeo kuhusu msangi katambuliwa na Dr Uli
 
Mwambie dhaifu na mkeo kuhusu msangi katambuliwa na Dr Uli

Huwa nasita sana kujibu cheap comments kama hizi.Sijui anaongea ***** gani huyu mtu?Sasa Dr Ulimboka na Mshahara wa mil 3.5 vinauhusiano gani?
 
mcfm40,

kama chuo cha udsm ndo kina watu kama nyinyi nimepata jibu kwa nini kimepoteza mwelekeo. miaka hiyo sisi tukisoma hapo hakikuwa hivyo.
hivi we una elimu ya chuo kikuu?sasa hapa ndo umeandika nini?
Na wewe kusema ulisoma UDSM na 'judgement' yako ndo imekaa kitoto namna hiyo.nikuonee tu huruma.
Huna lolote,kuliko kuwajaji wengine ungetoa nondo zako hapa ndo ungeonekana wa maana.!c..r..a..p
 
Last edited by a moderator:
Huyu ni muongo tu. Usalama wa taifa/polisi wamehusika. Na hili lingeweza tokea kwa wanaharakati wote na wafichua mawazo kama akina
  1. Zitto
  2. Dr Slaa
  3. Mbowe
  4. Kolimba (R.I.P)
  5. n.k
Lakini sema hao ambao si red wanaulinzi wa kutosha. Maskini Dr Ulimboka hakuwa na ulinzi na alijua hili ni suala dogo kumbe wenzake walimpigia mahesabu ya kumuua. Shame on the gvt!

hawajaamua tu kuwaondoa,kati ya hao wote hakuna yeyote mwenye ulinzi wa maana!
 
Jamani mimi ni mwalimu nafundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kama Assistant Lecturer.

Kusema kweli hii nchi haijui thamani ya madaktari na professionals wengine kwa ujumla.

Hivi kweli unaweza kulinganisha miaka mitano ya kusomea udaktari na miaka mitatu ya digrii nyingine hizi!?

Nimeshangaa eti daktari anayeanza kazi analipwa laki 9. Huu ni mshahara mdogo kuliko wa Tutorial Assistant aliyesomea digrii yake kwa miaka mitatu tu tena digirii laini (nimesoma mimi Arts) usin
 
Mkikosa hoja mnaanza viroja! Jakaya Mrisho Kikwete kawafunga midomo.

time will tell tunaona wanavyoanza kubabaika angalia vizuri hotuba ya jk utapata jibu...hata hivyo mbona wanasema jambo liko mahakamani halipashwi kujadiliwa na mihimili mingine.
pili inakuwaje tena wafukuzwe kazi wakati kesi haijaisha huu ni uppuuzi
 
Hapo UDSM unafundisha school gani vile? Mimi tu kuuliza.

Acha kupotosha kwamba uko UDSM wewe kwasababu huwezi kuja bila data. TA hapo UDSM anapokea bei gani? Ass. Lecturer naye anaanzia bei gani? Je, ni sifa zipi zinamfanya mtu awe Ass. Lecturer? Ni hiyo miaka mitatu au? Wewe kama ni Ass. Lecturer, una muda gani kazini na unapata mshahara (basic) bei gani? Na mbali na mshahara wako wewe kama Ass. Lecturer, TA na Lecturers, je kuna benefits zozote anazopata huyo mwalimu? Ungekuwa Ass. Lecturer ungefahamu ni kwanini waalimu wengi wa Vyuo vikuu vya Serikali wanapiga deiwaka.

Mimi naamini wewe ni Dr., na una ndugu ambaye ni Mwalimu sasa unatafuta mazingira ya kutaka kujustify mahitaji makubwa hasa ya mshahara wa 3.5 Million kwa Drs.; wanaoanza kazi. Sasa nikuulize swali, Je 3.5 Milion ni basic ya level gani kwa chuo kikuu kama siyo Professors. Kwahiyo, unachotaka kujusstify hapa ni kwamba Interns anapaswa alipwe robo tatu ya Full Professor ambaye amekuwa kazini zaidi ya miaka 20?

Mimi madai ya Drs hasa kwenye mshahara wa Drs wanaoanza kazi kuwa 3.5 Milion is too much. Sasa najiuliza swali ,je timu ya Drs ya negotiation ilikuwa imekamilika? nasema hivyo kwasababu, kiutaalamu unapoenda kwenye negotiations, then lazima ujue kwamba huwezi kupata 100 percent ya vitu vyote unavyohitaji. Kuna kitu kinaitwa Fall Back position, ambapo unakuwa na minimum ya kiwango ambacho ikifikiwa unaweza ukakubali. Pia unakuwa na priorities, yaani unasema kama 1,2,3,4 zikikubaliwa kama tunavyohitaji, then 5,6,7 tunaachana navyo au tunapunguza ili kwamba tuweze kufikia makubaliano, na hii ndiyo inaitwa win-win negotiation. Ukienda kwenye negotiations huku ukitaka mahitaji yako yote yapite jinsi yalivyo, then hiyo sasa negotiations bali ni order ili ambayo counterpart wako anatakiwa kupokea na si NEGOTIATIONS. Mimi nilitegemea Drs walikuwa na timu ya wataalamu wa negotiations kwenye kamati yao, lkn baada ya kusoma hotuba ya Rais, nimegundua kwamba hata Drs haikuwa na kamati inayojua nini maana ya negotiations na si kutoa Instructions. Na hili inawezekana, kwani kamati yao ilikuwa na Doctors of Medicine wote kama nitakuwa sahihi, lkn haikuwa na mtu wa negotiation skills. Negotiation skills nayo ni professional, haiji automatically kama baadhi yenu wanavyofikiria.
TELO.

NB:
Siyo busara na wala huitendei haki UDSM unapoamua kujipa jina kwamba wewe ni mwalimu pale tena wa kiwango cha Ass. Lecturer lkn unajichanganya katika kile unachowasilisha hapa na makosa mengi sana. Siyo busara kuichafua UDSM kwa dhana tu kwamba ukijitambulisha uko UDSM basi mchango wako watu watahueshimu hata kama unaadika upuuzi (source: Mnyika). Watu wataheshimu mchango wako kama una mantiki hata kama ungekuwa wazi kwamba wewe ni Dr., jinsi ulivyo.

Well said, and elaborated. Need I say more? No.
 
Sitaki kukubali kuwa muandishi wa habari hii ni mwalimu wa chuo kikuu, Lazima atakuwa ni muhuni wa mtaani tu huyu.

Mshahara wa kuanzia uwe mil 3.5 kwasababu kasoma miaka mi5? (wewe hovyo sana),Hebu waulize maprofesa wa hapo UDSM wanalipwa shilingi ngapi na wamesoma kwa miaka mingapi kuufikia uprofesa.Muheshimiwa Rais kaongea vizuri sana nadhani huu mjadala ufungwe,kama daktari anataka mil3.5 ambayo hata hospitali za private kama aga khan haulipi hivyo basi aache kazi atafute sehemu inayotoa mshahara wa namna hiyo.

Siyo lazima kila pumba uliyonayo kichwani uiandike humu unaweza kaa nayo tu ukajidanganye na wenzako vijiweni.
hasira za nini mzee?tulia,acha kukurupuka.si haba,utakuwa una lako jambo...ama hujui kusoma,ama uelewa wako ni mdogo.mtoa mada kasema vizuri na hiyo laki9 ni ndogo akasuggest kama mil2 hivi na akasema anaamini kwamba madr. hawako rigid hivo kwamba it must be 3.5m....!sasa mujue hii ishu ya madr haitaisha kwa maneno ya kipuuzi ya huyo ******.nyie endeleeni tu na huo upuuzi wenu na siasa zenu za kitoto.....
 
Wabunge kulipwa mil 10 haf wabunge wenyewe akina komba,bukwimba,shibuda,maji marefu,lùsinde and co unalinganisha vp na wa2mishi wengine wa uma?

Kama Udaktari haulipi basi wagombee ubunge.
 
hasira za nini mzee?tulia,acha kukurupuka.si haba,utakuwa una lako jambo...ama hujui kusoma,ama uelewa wako ni mdogo.mtoa mada kasema vizuri na hiyo laki9 ni ndogo akasuggest kama mil2 hivi na akasema anaamini kwamba madr. hawako rigid hivo kwamba it must be 3.5m....!sasa mujue hii ishu ya madr haitaisha kwa maneno ya kipuuzi ya huyo ******.nyie endeleeni tu na huo upuuzi wenu na siasa zenu za kitoto.....

Mzee, kama unaona mshahara ni mdogo si uende private sector? Kwa nini mnang'ang'ania serikalini. Mbona sisi tumetoka serikalini tupo private na maisha yanaenda. Najua mnataka mshahara mzuri na baada ya hapo hospitali hamkai kazi kwenda kwenye vioski tu. Mnadhani watu hawajui?
 
TELO

Mimi ni mkufunzi (TA) wa Chuo kikuu kimoja hapa bongo.

Mshahara wangu wa Tutorial assistant nilianza na zaidi ya 1m, kumzidi hata Dr, na course ya undergraduate ilikuwa miaka 3. Na kazini nina nyumba, usafiri, maji, umeme. Na bado nina muda mwingi tu wa kuwa idle (si kama Dr akianza kazi hatoki mpaka usiku). Wakati mwingine Dr anafanya kazi hata weekend, mimi sifanyi.

Hata maTA nao wanatofautiana, TA wa CoET si sawa na TA wa Arts. Wa CoET sidhani kama wana huo muda kama wa kwenu!, kwahiyo either nyie mpunguziwe mshahara au wengine waongezewe pamoja na madaktari.
 
Hapo UDSM unafundisha school gani vile? Mimi tu kuuliza.

Acha kupotosha kwamba uko UDSM wewe kwasababu huwezi kuja bila data. TA hapo UDSM anapokea bei gani? Ass. Lecturer naye anaanzia bei gani? Je, ni sifa zipi zinamfanya mtu awe Ass. Lecturer? Ni hiyo miaka mitatu au? Wewe kama ni Ass. Lecturer, una muda gani kazini na unapata mshahara (basic) bei gani? Na mbali na mshahara wako wewe kama Ass. Lecturer, TA na Lecturers, je kuna benefits zozote anazopata huyo mwalimu? Ungekuwa Ass. Lecturer ungefahamu ni kwanini waalimu wengi wa Vyuo vikuu vya Serikali wanapiga deiwaka.

Mimi naamini wewe ni Dr., na una ndugu ambaye ni Mwalimu sasa unatafuta mazingira ya kutaka kujustify mahitaji makubwa hasa ya mshahara wa 3.5 Million kwa Drs.; wanaoanza kazi. Sasa nikuulize swali, Je 3.5 Milion ni basic ya level gani kwa chuo kikuu kama siyo Professors. Kwahiyo, unachotaka kujusstify hapa ni kwamba Interns anapaswa alipwe robo tatu ya Full Professor ambaye amekuwa kazini zaidi ya miaka 20?

Mimi madai ya Drs hasa kwenye mshahara wa Drs wanaoanza kazi kuwa 3.5 Milion is too much. Sasa najiuliza swali ,je timu ya Drs ya negotiation ilikuwa imekamilika? nasema hivyo kwasababu, kiutaalamu unapoenda kwenye negotiations, then lazima ujue kwamba huwezi kupata 100 percent ya vitu vyote unavyohitaji. Kuna kitu kinaitwa Fall Back position, ambapo unakuwa na minimum ya kiwango ambacho ikifikiwa unaweza ukakubali. Pia unakuwa na priorities, yaani unasema kama 1,2,3,4 zikikubaliwa kama tunavyohitaji, then 5,6,7 tunaachana navyo au tunapunguza ili kwamba tuweze kufikia makubaliano, na hii ndiyo inaitwa win-win negotiation. Ukienda kwenye negotiations huku ukitaka mahitaji yako yote yapite jinsi yalivyo, then hiyo sasa negotiations bali ni order ili ambayo counterpart wako anatakiwa kupokea na si NEGOTIATIONS. Mimi nilitegemea Drs walikuwa na timu ya wataalamu wa negotiations kwenye kamati yao, lkn baada ya kusoma hotuba ya Rais, nimegundua kwamba hata Drs haikuwa na kamati inayojua nini maana ya negotiations na si kutoa Instructions. Na hili inawezekana, kwani kamati yao ilikuwa na Doctors of Medicine wote kama nitakuwa sahihi, lkn haikuwa na mtu wa negotiation skills. Negotiation skills nayo ni professional, haiji automatically kama baadhi yenu wanavyofikiria.
TELO.

NB:
Siyo busara na wala huitendei haki UDSM unapoamua kujipa jina kwamba wewe ni mwalimu pale tena wa kiwango cha Ass. Lecturer lkn unajichanganya katika kile unachowasilisha hapa na makosa mengi sana. Siyo busara kuichafua UDSM kwa dhana tu kwamba ukijitambulisha uko UDSM basi mchango wako watu watahueshimu hata kama unaadika upuuzi (source: Mnyika). Watu wataheshimu mchango wako kama una mantiki hata kama ungekuwa wazi kwamba wewe ni Dr., jinsi ulivyo.

Note blue; Kwa hiyo na wewe unaona ni fahari kwa huyo Prof kulipwa anacholipwa???
 
Ng`wanakidiku

Umeajiriwa serikalini na serikali kuu au umeajiriwa na Taasisi ya serikali? Kaulize daktari aliyekatika Govt agencies kama NIMR analipwa shilingi ngapi. Hebu muwe mnaumiza kichwa kabla hamjapost comments zenu humu.
hilo nalo naona ni tatizo.
 
Last edited by a moderator:
Kwa mujibu wa mazungumzo ya mwisho wa mwezi yaliotolewa na raisi JK kwa watanzani,bwana ulimboka si muajiriwa wa serikali ila alichaguliwa kuwasemea madaktari!
Hii sielewi imekaaje,
yani jopo lote la madaktari nchini hakukua na mtu thabiti wakufanya hili?

Na huo ndio ukweli. Serikali na madaktari wote wameingizwa mjini. ‘Msemaji’ wa madaktari “ULIMBOKA” alikuwa ni wa kuokoteza . Chama cha madaktari ‘MAT’ sio msemaji rasmi wa mafao ya madaktari , ndio maana mwenyekiti wake alikiri mbele ya Jaji kuwa hahusiki na mgomo. Hiki ni chama cha kitaaluma zaidi. Hata hiyo inayoitwa “Jumuia ya Madaktari” sio chama rasmi cha madaktari. Kwa hiyo hata kiongozi wa mgomo hajulikani. Swali kwa nini serikali ilikaa na vikundi vidogo vodogo kujadili issues nyeti namna hii. Lessons learned…!
 
SOMA HII KAMA UNA IQ SCORE ZAIDI YA 190
Baada ya miaka kumi tu ijayo kuanzia leo wananchi watakuwa wanaandamana kuishinikiza serikali kusolve tatizo la hospitali kutokuwa na madaktari wa kutosha kwani hamna mwanafunzi aliehitimu PCB advanced level atakae taka kusoma fani ambayo ni ngumu, miaka mingi na kipato kidogo...na afterall intellectuals ndo wanachaguliwa kusoma fani hii.. kwa kawaida mtu anasoma kwa bidii akiamini ndo anajitengenezea maisha sasa na digrii yako unapata 900,000Tshs per month nonsense hamna atakae taka fani hii... si busara na hatari zaidi kutokuwa na madaktari kuliko kuwa na madaktari wanaogoma kutaka kuongezewa mshahara na mazingira mazuri ya kazi...kama swala hili halitashughulikiwa ipasavyo unabii huu utatimia soon (2020)

Acha stori wewe kwani Tanzania peke yake ndio kuna madaktari nenda India, Cuba, kaone madaktari wanavyolipwa...kuna vijana wengi wapo tayari kusoma usidhani wote wana tamaa kama wewe.
 
time will tell tunaona wanavyoanza kubabaika angalia vizuri hotuba ya jk utapata jibu...hata hivyo mbona wanasema jambo liko mahakamani halipashwi kujadiliwa na mihimili mingine.
pili inakuwaje tena wafukuzwe kazi wakati kesi haijaisha huu ni uppuuzi

Nadhani inabidi ufundishwe sheria ndo uelewe. Suala lililopo Mahakamani na swala na Drs. na Mwajiri (Serikali). Lakini kumbuka kila Hospital ina mamlaka kupitia Mabaraza ambayo yanaweza kumwajibisha Dr. kama akienda kinyume. Ndo maana Mbeya na Bugando wamewafukuza Interns na kuawarudisha kwa mwajiri wao (Serikali). Mwajiri yeye hajawafukuza. Mfano wa pili, MOI inaweza ikamtimua Dr. na kumrudisha Wizarani kwani Wizara ndo mwajiri wao (since 2010), kwa hiyo, Board ya Wakurugenzi ya MOI inaweza ikamuondoa DR. na kumwambia unatuaribia kazi rudi kwa Mwajiri wako, yeye ataamua cha kufamya. Pia elewa, kama DRs. mnajua kuwa suala lipo Mahakamani kwa nini na nyie mnagoma?
 
Hata maTA nao wanatofautiana, TA wa CoET si sawa na TA wa Arts. Wa CoET sidhani kama wana huo muda kama wa kwenu!, kwahiyo either nyie mpunguziwe mshahara au wengine waongezewe pamoja na madaktari.
Ndiyo maana nikasema si vema kujilinganisha na Dr (MD) kwenye masuala yao, serikali iwasikilize!!!
 
Jukwaa lote kimya watu wamechanganyikiwa hawana la kufanya baada ya JK kutoa kauli leo ndio mtajua JK ni rais.
 
Back
Top Bottom