Mkwawe
JF-Expert Member
- Jun 10, 2016
- 2,345
- 4,168
Hadi sasa wanajamvi sielewi kama zile taarifa za kuwa mwaka huu zaidi ya wanafunzi 220000 wanatajwa kunufaika na mkopo wa masomo kutoka heslb kuwa ni kweli, kwa sababu kila siku hapa kitaa madogo walioenda chuo kwa bashasha lote wanarudi kitaani na sura zilizokosa tumaini kabisa, yaani ni huruma na inasikitisha sana.
Hebu fikiria yaani kwa sababu tu mtu eti mtu ana wazazi wawili (ambao pengine hawana background ya kuajiriwa) hapewi mkopo kabisa au anapewa mkopo sawa na wa vicoba. Yaani mtu ameapply kusomea udaktari ambao ada take ni 1.8m halafu unampa laki mbili kweli? Mtu ameapply kusomea uhandisi ambao ada yake ni 1.5m halafu unampa laki mbili? Jamani serikali yetu pamoja na taasisi husika kuweni na utu jamani watu wanasoma kwa shida, watu wanatumia gharama kubwa sana kusomesha wengine hudunduliza hadi akiba zao za mwisho kuwasomesha watoto wao wakijua baadaye serikali itawatua mzigo lakini hiki mnachofanya ni nini?
Mwaka huu ninaamini 40% ya wanafunzi walioomba mkopo na kutaka kuanza masomo ya chuo Kikuu hawataanza maana serikali imewatupa mkono, imebaki tu kuiaminisha jamii na takwimu zao bandia za bilioni 700 na wanafunzi laki mbili.
Huu ni unyama wa kihinsia, tunajua mwenye shibe hamkumbuki mwenye njaa ila basi tumieni hata ile njaa mnayoipata asubuhi kujua kuwa Kuna watu hawali siku nzima. Yaani kwa kifupi asilimia kubwa wanafunzi walioomba mkopo wamepewa asilimia 16%, Kuna watu ada ya shilingi elfu 70 kwa mwaka walipokuwa sekondari ilikuwa inawashinda sembuse milioni 1.8? Kweli jamani!!??
Hebu bodi ya mikopo na wizara husika kaeni muangalie ni jinsi gani mtawasaidia hawa wadogo zetu, madogo wamejaa na msongo sana huku mtaani, wazazi wao ndo hawa hawa mnaowavunjia vibanda kuweni na utu jamani, dunia ni mapito hii
Poleni sana wadogo zangu hii ndo serikali inayoubutua mwingi hadi nje ya uwanja