Helicopter ya Maliasili yadondoka na kuua Kipunguni B - Ukonga Dar Es Salaam

Nilishasema nchi hii ni kama panya wa maabara. Hizi helikopta zimeletwa na rafiki zake nyalandu wamarekani kama msaada. Tuliandika kuwa ni chakavu na hazifai. Tukapuuzwa. Nyalandu kwa kuutaka uwaziri akatupuuza. Sasa yametufika. Haya madude ni mabovu. Yamepakwa rangi tu. Poleni wafiwa wote. Nyalandu ni janga jamani. Eleweni tunachosema.

Aisee...! Kumbe. tuhuma za ubadhirifu wa mali za umma na ujangili juu yake zitakuwa za kweli.
 
Watu 4 wamekufa baada ya Helkopta inayomilikiwa na Wizara ya Mali Asili namba 5HTWA kuanguka katika eneo la Kipunguni B - Ukonga jijini Dar es Salaam.



Jeshi la polisi lathibitisha kutokea kwa tukio hilo

Source: RADIO1 STEREO


Ni kweli tumepata kusikia na kuona katika baadhi ya mitandao na magroup ya whatsapp ajali yenyewe!
 
tatizo helkopta huwezi hata kujaribu kuruka maana ukifanya hivyo unajichinja mwenyewe. Tuwaombee wote waliofariki ili Mwenyezi Mungu awalaze mahali pepa peponi.
 
Harbinder Sighn Seth Yule Mmiliki wa IPTL a.k.a ESCROW Akaunti Atatupa Zingine 15 Mpya Ngojea Bunge Limalizike Leo Dodoma.

Unaongelea kupoteza helicopter je watu waliopoteza maisha yao hawana thamani? Helicopter inaweza kununuliwa mpya lakini je watu waliokufa watanunuliwa duka gani? This is very serious na hapa uchunguzi ufanyike watu wachukuliwe hatua km ilivofanyika kwa escrow
 
Mie nashangaa kuna baadhi ya watu wana dalili zote za kufurahi kutokana na ajali hiyo , maana wengine walikuwa na taarifa zisizo rasmi. Mke wangu kafiwa na kakake ktk ajali hiyo. Watu wote wa4 walokuwemo ndani ni marubani wa ki-tz, hivyo unaweza kuona taifa lilivyopoteza nguvu kazi. Leo mwili wa shemeji yangu umeagwa kinyerezi na umepelekwa Arusha- Moshono kwa mazishi
 
Helkopta za Nyalandu hizo. Ni nadra sana helcopta mpya kuanguka kizembe hivyo. Hizi chopa ni chakavu.
 
Back
Top Bottom