Tetesi: Ole Sabaya kuwa Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,850
18,260
Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha na maneno mengi. Habari zinapenya kwamba mama anatarajia kufanya mabadiliko ya wakuu wa mikoa hivi punde na kwamba Ole Sabaya ndiye atakayeteuliwa kuwa mkuu mpya wa mkoa wa Da res Salaam.

Chanzo changu cha habari kutoka viunga vya Dodoma kinabainisha pasipo shaka kuwa mama amemchoka Chalamila, hasa kwa vitimbi vyake vya mara kwa mara vinavyochochea chuki kati ya serikali na wananchi. “Tukumbuke kwamba wakati Chalamila anaapishwa kwa mara ya pili baada ya hapo awali kutupwa nje ya mfumo, mama alisema kuwa mtu huyu ni mlipukaji”. Alisikika akisema kigogo mmoja aliye karibu na utawala wa juu. “Na hata baada ya kuonywa lakini bado ameendelea kulipuka”. Aliongeza.

Taarifa hizo zinafafanua matamshi ya Chalamila ya hivi karibuni yanayoonesha kukosa umakini. Moja ya matamshi haya ni wakati wananchi wa Dar walipoingiliwa na mafuriko yaliyoharibu mali na kuua baadhi ya raia. Chalamila, akiwa mteule wa Rais, alisikika akiwabeza na kusisitiza kuwa Dar hakuna mafuriko na kwamba hao waliokumbwa na mafuriko wamejitakia wenyewe.

Tukio la pili ni lile ambalo aliwabeza wanafunzi wanaofeli ambapo alisikika akiwakejeli kwamba na wao wanaopata zero kwenye mitihani wana ‘vipaji maalumu’ (vya kufeli). Aliendelea kuwataka watendaji wa NECTA wawe wanawatambua kama vile wanavyowatambua wanafunzi wanaofaulu vizuri na kuchaguliwa kwenda shule za vipaji.

Kana kwamba hilo halitoshi, hivi majuzi ndugu Chalamila alisikika akiwataka wananchi kujichukulia sheria mikononi dhidi ya vibaka wanaovunja nyumba na kuiba. Hii inatafsiriwa kwamba Chalamila anawachochea wananchi kujichukulia sheria mkononi kwa kuwaua wahalifu badala ya kuwakamata na kuwafungulia mashtaka kwa mujibu wa sheria.

Haya matendo machache ya ulipukaji wa ndugu Chalamila, yanayochochea uvunjivu wa sheria na kuwachonganisha wananchi na serikali yao, yametosha kabisa kumfanya mama amtupe nje ya mfumo wa serikali kwani ameshindwa kujirekebisha hata baada ya kupewa nafasi kwa mara ya pili.

Hata hivyo, kurudishwa kwa Ole Sabaya kwenye uongozi inasemekana kumechagizwa na pacha wake, ndugu Paul Makonda, aliyempigia chapuo kwa mama. Wawili hawa walikuwa na nguvu kubwa sana kipindi cha uongozi wa Magufuli hadi kufikia kufanya jambo lolote bila kukemewa wala kuchukuliwa hatua zozote na mteuzi wao.

Aidha, baada ya timu ya Magufuli (Sukuma Gang) kuanza kurejeshwa uongozini taratibu, wanataka kutengeneza mtandao ndani ya serikali ili ifikapo 2025 kama hawatamuelewa mama watafute mtu wao watakayemuunga mkono kwenye uchaguzi.

Ndio maana Makonda amefanya juu chini kumshawishi mama amrejeshe Sabaya uongozini kwa kuwa wawili hawa wana ushawishi mkubwa sana kiuongozi ili waweze kujiimarisha na kuwa na nguvu ya pamoja itakayowafanya kutembea kifua mbele mwaka 2025.

MAONI YANGU
Kumrejesha Ole Sabaya uongozini wakati bado makosa aliyoshitakiwa kwayo hayajasahaulika miongoni mwa wananchi, ni kosa kubwa sana la kiufundi ambalo amelifanya mama. Sabaya akiungana na Makonda uongozini kuna hatari ya mama kupata upinzani mkubwa sana ndani ya chama ifikapo 2025.

Kumbuka wawili hawa ni kama au zaidi ya chawa. Hawaaminiki hata kidogo na wana tabia ya kiundumilakuwili. Wao hutanguliza maslahi binafsi mbele kuliko kitu chochote. Ndio maana wakati wa uongozi wa Magufuli waliutumia zaidi kujinufaisha kibinafsi badala ya kumsaidia Rais kuwatumikia wananchi.

Ningekuwa mimi ndiye mshauri wa mama nisingemrejesha uongozini Ole Sabaya kwa haraka kiasi hiki ilhali bado wananchi aliowadhulumu mali na fedha bado wana maumivu makubwa mioyoni mwao.

Nawasilisha.
 
Anaweza kurudi maana CCM kwa Sasa haina watu wenye uwezo. Ushahidi upo wa kutosha. Mwendokasi mwaka wa nane huu hawajaongeza hata Basi moja wakati inaongozwa na MTU mwenye PII HECH DII a.k.a Dr. Mhede. Na nauli wanapandisha wanavyotaka.
 
Back
Top Bottom