Maharagande: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Wajiuzulu

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
610
1,540
Hatua za uwajibikaji zichukuliwe mauaji ya raia kwenye Operesheni za Polisi nchini:

Utangulizi
Ndugu Waandishi wa Habari
Takribani siku 14 sasa tangu vyombo vya habari, wananchi mitaani na wanaharakati mitandaoni wamekuwa wakijadili juu ya Operesheni zinazoendelea za Jeshi la Polisi nchini. Wote tunakumbuka kuwa Operesheni hizo zilitokana na taarifa za kuendelea kwa matukio ya mauaji (Mfano kifo cha mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam - Shule ya Uandishi wa Habari, Maria Basso kilichotokea tarehe 14.10.2022 huko kwao Bunju) uvamizi, kujeruhi na kuporwa kwa mali za wananchi katika jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine nchini.

Matukio haya yameripotiwa kufanywa na makundi ya vijana almaarufu kama “panya road” au “panya buku” kwa nyakati mbalimbali. Kufuatia na matukio hayo wananchi walijawa na hofu, wasiwasi au hali ya amani ilianza kutetereka.

Tulishuhudia viongozi wa Serikali wakitoa maelekezo na kauli mbalimbali. Hatua iliyofuata, vyombo vya usalama vilichukua hatua za utekelezaji kukabiliana na matukio hayo ya kihalifu yanayohatarisha hali ya usalama na utulivu.

Sisi, ACT Wazalendo kama ilivyo kwa wananchi na wadau wengine tulipokea kwa faraja mwitikio huo wa vyombo vya usalama katika kushughulikia matukio ya kihalifu na kusambaratisha mtandao mzima. Lakini kinyume na matarajio hayo utekelezaji wa Operesheni hizo zimeibua hofu, wasiwasi na kuvuruga amani ya wananchi kutokana na ukweli kuwa Jeshi la Polisi limetuhumiwa kukiuka haki za binadamu na kupuuza mfumo wa sheria za nchi.

Ndugu Waandishi wa Habari,
Hadi sasa kuna mamia ya vijana wanaotuhumiwa na matukio hayo ya kihalifu wameripotiwa kukamatwa. Matukio yaliyotushtusha zaidi ni kuanzia mauaji ya watu sita (6) jijini Dar es Salaam yaliyothibitishwa na Jeshi la polisi lenyewe kupitia vyombo vya habari tarehe 18 Septemba 2022. Aidha, Polisi walithibitisha kuua watu watatu (3) huko Serengeti, Mara tarehe 21, Septemba 2022.

Mauaji haya, yalianza kuwashtua wadau na wanaharakati na kuacha maswali namna Polisi wanavyoendesha Operesheni zake. Ikiwa polisi wanajipa haki za kukamata, kuhukumu na kutoa adhabu tena adhabu za kifo kwa watuhumiwa ni dhahiri tunaruhusu ukandamizaji na ukiukwaji wa haki za binadamu. Pia, inaonekana kama tayari wameshakuhukumu (wao ndio Mahakama), wao ndio magereza (wanaosimamia adhabu na urekebishaji wa tabia).

Pamoja na kuwepo na taarifa za mauaji ya watuhumiwa wa uhalifu ambazo Polisi wenyewe wamekiri hadharani lakini polisi hawatangazi kila tukio la mauaji linalofanywa na wao katika mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.

Tukio la mauaji ya vijana watatu kutoka familia tatu tofauti waliokuwa wanaishi Tandika, Wilaya ya Temeke linadhihirisha ukweli huo. ACT Wazalendo tulifuatilia tuhuma za mauaji za vijana hao waliotuhumiwa kuwa ni “Panya road” likihusishwa Jeshi la Polisi.

Tulipofuatilia tulielezwa na familia zao kuwa vijana hawa walikamatwa na polisi wakiwa nyumbani kwao na kupelekwa kituo cha Polisi Maturubai kilichopo Mbagala. Vijana hawa hawakurudi nyumbani na baadaye ilibainika waliuawa kwa kupigwa risasi na Polisi.

Maiti za vijana hawa zilipelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kuhifadhiwa kwenye chumba cha maiti hospitalini hapo. Kitendo cha mtuhumiwa kuuwawa kwenye mikono ya Polisi, pasipo na sababu za kueleweka, siyo tu ni kinyume na Katiba ya Nchi lakini pia ni kinyume na sheria zote na kanuni na taratibu zinazotawala masuala ya utoaji haki nchini mwetu.

ACT Wazalendo kupitia Msemaji wa kisekta tulitoa taarifa ya awali mnamo tarehe 27 Septemba 2022 iliyotaka hatua za kiuchunguzi na kiuwajibishaji zichukuliwe. Lakini, Serikali haikuchukua hatua yoyote, tuliendelea kutoa taarifa ya kina ya utafiti tulioufanya kupitia Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana Ndg. Abdul Nondo siku mbili baadaye napo hatujaona wahusika wakichukuliwa hatua zozote licha ya taarifa hiyo kuenea kwenye baadhi ya vyombo vya habari.

Kutokana na tuhuma za mauaji yanayofanywa na Jeshi la Polisi taswira yake imeendelea kuchafuka sana. Jeshi la polisi limechorwa kuwa ni chombo katili mithili ya Jeshi la Kikaburu. Badala ya kuleta matuamini limeongeza hofu na mashaka, hivyo tumeona ni muhimu kulieleza hili ili kuhakikisha Polisi wanatekeleza majukumu yao ya kiupelelezi, kiuchunguzi na ukamataji katika mazingira ambayo hayazalishi hofu zaidi kwa wananchi wasio na hatia, hayaongezi matukio ya ukiukwaji wa haki za watu.

Hivyobasi, ACT Wazalendo tunaitaka Serikali ichukue hatua zifuatazo ili kuhakikisha Jeshi la Polisi na askari Polisi wanatekeleza wajibu wao huku wakizingatia haki za binadamu, weledi na sheria za nchi.

i. Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania liunde Tume ya kuchunguza mauaji yote ya raia ili kujiridhisha na hatua zilizofanywa na Jeshi la Polisi.

ii. Tunawataka maafisa wa jeshi la Polisi wanaotuhumiwa na mauaji kusimamishwa ili kupisha uchunguzi.

iii. Tunamtaka Waziri wa Mambo ya Ndani na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kujiuzulu mara moja kutokana kushindwa kuchukua hatua tangu matukio haya yametokea.

iv. Maafisa wote wanaohusika na mauaji hayo wachukuliwe hatua

Ni jambo la kusikitisha wakati nchini kote kuna kilio cha mageuzi ya utendaji na uendeshaji wa Jeshi la Polisi kuona askari Polisi wanaendelea kufanya matukio yanaongeza hasira, mashaka na kujenga uhasama baina Jeshi hilo na wananchi.

Tunaendelea kusisitiza mageuzi ya Jeshi la Polisi ili kulifanya jeshi hilo liwe linatumia utaalamu, Sayansi na weledi zaidi kuliko mateso, udhalilishaji na ukandamizaji kama zana za kubaini uhalisia, kuzuia na kukomesha matukio hayo

Imetolewa na;
Mbarala Abdallah Maharagande
Twitter : @Mbaralagande
Msemaji wa sekta ya Mambo ya ndani ya Nchi
04 Oktoba 2022.

IMG-20221004-WA0177.jpg
 
Hebu msituchoshe na nyaraka zenu ndeeefu zisizo na kichwa wa amiguu. Leo mnaandika nyaraka kesho mnaenda kuunda serikali ya umoja na hao mnaowaandikia waraka

Pambaneni na ndoa yenu
 
Hawa wanasiasa pasua kichwa sana

Ova
 
Operesheni safisha safisha ya Polisi iendelee. Naamini sheria zinafuatwa. Wanasiasa wawaache polisi wafanye kazi yao.🙏🙏🙏
 
Zitto na ACT Wazalendo

Kwa hiyo wananageuzi wa Tanzania mmegeuka kuwa watetea majambazi wa nchi hii?

Je!
Hamuoni kero zingine kubwa za kuasemea watanzania?

Je hamuoni ubadhirifu unaoendelea kwa kasi ya 4G kwenye taasisi za Umma kote nchini?

Hamuzioni Tozo za lazima kwenye akaunti na miamala ya watanzania wa kipato cha chini kote nchini?

Matetea wahalifu ambao wanaongeza umaskini na misiba kote nchini?

Kwa nini kwenye taarifa zenu hukuongelea tukio la juzi tarehe 01/10/22 huko Siha wilayani Hai.
ambapo askari Polisi alikatwa panga la kichwa.wakati akiwa katika jitihada za kumkamata mtuhumiwa wa mauaji yaliyokuwa yametokea mchana wake.

Polisi walikwenda kwa mtuhumiwa usiku,wakiandamana na mwenyekiti wa kitongoji husika.
Mtuhumiwa yule pamoja na kumtambua mwenyekiti,kupitia mazungumzo waliyoyafanya na utambulisho kupitia dirisha alilokuwa amefungua mtuhumiwa yule.

Bado aligoma kutoka nje,si hivyo tu bali aliwazuia mkewe na mtoto wao kutotoka nje.na kuwalazimu askari kutumia nguvu kuvuja mlango ili waingie ndani na kumkamata.

Lakini baada ya kubimoa mlango ule.Askari wa kwanza kuingia ndani.alikutana na pamga la kichwa na kudondokea nje.

Kilichoendelea ikawa kama movie ya "Hollywood" kwani Polisi walilazimika kurusha bomu la machozi ndani na kuwalazimu watoke.

Lakini mtuhumiwa alimtumia mkewe kama kinga(human shield)na akatokomea kusikojulikana.

Si haki kwa Polisi kuwaua raia watuhumiwa.Ila ni ukweli kwamba nao wanakumbana na mazingira magumu kwa baadhi ya matukio.

ACT kama chama cha siasa,hampaswi kuingia kwenye mkumbo huu wa kutumia matukio na kuyafanya kuwa kick ya Political mileage.

Jengeni sera mahiri,ili mpate ushawishi kwa umma na hatimae muiondowe CCM madarakani kwa kuiwajibisha.

Ni ngumu kwa raia wa kawaida kuwaelewa kwenye hili la Panya road na majambazi,zaidi ya familia za wahusika pekee.

Vinginevyo mnachofanya ni kutafuta kuichafua nchi kwenye mataifa ya nje na balozi zao ambazo zimekuwa zikiwafadhili.

Huko Marekani ndio wanaongoza kwa mauaji ya wasio na hatia

"Black Lives Matter's "
 
Hatua za uwajibikaji zichukuliwe mauaji ya raia kwenye Operesheni za Polisi nchini:

Utangulizi,
Ndugu Waandishi wa Habari
Takribani siku 14 sasa tangu vyombo vya habari, wananchi mitaani na wanaharakati mitandaoni wamekuwa wakijadili juu ya Operesheni zinazoendelea za Jeshi la Polisi nchini. Wote tunakumbuka kuwa Operesheni hizo zilitokana na taarifa za kuendelea kwa matukio ya mauaji (Mfano kifo cha mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam - Shule ya Uandishi wa Habari, Maria Basso kilichotokea tarehe 14.10.2022 huko kwao Bunju) uvamizi, kujeruhi na kuporwa kwa mali za wananchi katika jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine nchini.

Matukio haya yameripotiwa kufanywa na makundi ya vijana almaarufu kama “panya road” au “panya buku” kwa nyakati mbalimbali. Kufuatia na matukio hayo wananchi walijawa na hofu, wasiwasi au hali ya amani ilianza kutetereka.

Tulishuhudia viongozi wa Serikali wakitoa maelekezo na kauli mbalimbali. Hatua iliyofuata, vyombo vya usalama vilichukua hatua za utekelezaji kukabiliana na matukio hayo ya kihalifu yanayohatarisha hali ya usalama na utulivu.

Sisi, ACT Wazalendo kama ilivyo kwa wananchi na wadau wengine tulipokea kwa faraja mwitikio huo wa vyombo vya usalama katika kushughulikia matukio ya kihalifu na kusambaratisha mtandao mzima. Lakini kinyume na matarajio hayo utekelezaji wa Operesheni hizo zimeibua hofu, wasiwasi na kuvuruga amani ya wananchi kutokana na ukweli kuwa Jeshi la Polisi limetuhumiwa kukiuka haki za binadamu na kupuuza mfumo wa sheria za nchi.

Ndugu Waandishi wa Habari,
Hadi sasa kuna mamia ya vijana wanaotuhumiwa na matukio hayo ya kihalifu wameripotiwa kukamatwa. Matukio yaliyotushtusha zaidi ni kuanzia mauaji ya watu sita (6) jijini Dar es Salaam yaliyothibitishwa na Jeshi la polisi lenyewe kupitia vyombo vya habari tarehe 18 Septemba 2022. Aidha, Polisi walithibitisha kuua watu watatu (3) huko Serengeti, Mara tarehe 21, Septemba 2022. Mauaji haya, yalianza kuwashtua wadau na wanaharakati na kuacha maswali namna Polisi wanavyoendesha Operesheni zake. Ikiwa polisi wanajipa haki za kukamata, kuhukumu na kutoa adhabu tena adhabu za kifo kwa watuhumiwa ni dhahiri tunaruhusu ukandamizaji na ukiukwaji wa haki za binadamu. Pia, inaonekana kama tayari wameshakuhukumu (wao ndio Mahakama), wao ndio magereza (wanaosimamia adhabu na urekebishaji wa tabia).

Pamoja na kuwepo na taarifa za mauaji ya watuhumiwa wa uhalifu ambazo Polisi wenyewe wamekiri hadharani lakini polisi hawatangazi kila tukio la mauaji linalofanywa na wao katika mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.

Tukio la mauaji ya vijana watatu kutoka familia tatu tofauti waliokuwa wanaishi Tandika, Wilaya ya Temeke linadhihirisha ukweli huo. ACT Wazalendo tulifuatilia tuhuma za mauaji za vijana hao waliotuhumiwa kuwa ni “Panya road” likihusishwa Jeshi la Polisi.

Tulipofuatilia tulielezwa na familia zao kuwa vijana hawa walikamatwa na polisi wakiwa nyumbani kwao na kupelekwa kituo cha Polisi Maturubai kilichopo Mbagala. Vijana hawa hawakurudi nyumbani na baadaye ilibainika waliuawa kwa kupigwa risasi na Polisi.

Maiti za vijana hawa zilipelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kuhifadhiwa kwenye chumba cha maiti hospitalini hapo. Kitendo cha mtuhumiwa kuuwawa kwenye mikono ya Polisi, pasipo na sababu za kueleweka, siyo tu ni kinyume na Katiba ya Nchi lakini pia ni kinyume na sheria zote na kanuni na taratibu zinazotawala masuala ya utoaji haki nchini mwetu.

ACT Wazalendo kupitia Msemaji wa kisekta tulitoa taarifa ya awali mnamo tarehe 27 Septemba 2022 iliyotaka hatua za kiuchunguzi na kiuwajibishaji zichukuliwe. Lakini, Serikali haikuchukua hatua yoyote, tuliendelea kutoa taarifa ya kina ya utafiti tulioufanya kupitia Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana Ndg. Abdul Nondo siku mbili baadaye napo hatujaona wahusika wakichukuliwa hatua zozote licha ya taarifa hiyo kuenea kwenye baadhi ya vyombo vya habari.

Kutokana na tuhuma za mauaji yanayofanywa na Jeshi la Polisi taswira yake imeendelea kuchafuka sana. Jeshi la polisi limechorwa kuwa ni chombo katili mithili ya Jeshi la Kikaburu. Badala ya kuleta matuamini limeongeza hofu na mashaka, hivyo tumeona ni muhimu kulieleza hili ili kuhakikisha Polisi wanatekeleza majukumu yao ya kiupelelezi, kiuchunguzi na ukamataji katika mazingira ambayo hayazalishi hofu zaidi kwa wananchi wasio na hatia, hayaongezi matukio ya ukiukwaji wa haki za watu.

Hivyobasi, ACT Wazalendo tunaitaka Serikali ichukue hatua zifuatazo ili kuhakikisha Jeshi la Polisi na askari Polisi wanatekeleza wajibu wao huku wakizingatia haki za binadamu, weledi na sheria za nchi.

i. Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania liunde Tume ya kuchunguza mauaji yote ya raia ili kujiridhisha na hatua zilizofanywa na Jeshi la Polisi.

ii. Tunawataka maafisa wa jeshi la Polisi wanaotuhumiwa na mauaji kusimamishwa ili kupisha uchunguzi.

iii. Tunamtaka Waziri wa Mambo ya Ndani na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kujiuzulu mara moja kutokana kushindwa kuchukua hatua tangu matukio haya yametokea.

iv. Maafisa wote wanaohusika na mauaji hayo wachukuliwe hatua

Ni jambo la kusikitisha wakati nchini kote kuna kilio cha mageuzi ya utendaji na uendeshaji wa Jeshi la Polisi kuona askari Polisi wanaendelea kufanya matukio yanaongeza hasira, mashaka na kujenga uhasama baina Jeshi hilo na wananchi. Tunaendelea kusisitiza mageuzi ya Jeshi la Polisi ili kulifanya jeshi hilo liwe linatumia utaalamu, Sayansi na weledi zaidi kuliko mateso, udhalilishaji na ukandamizaji kama zana za kubaini uhalisia, kuzuia na kukomesha matukio hayo

Imetolewa na;
Mbarala Abdallah Maharagande
Twitter : @Mbaralagande
Msemaji wa sekta ya Mambo ya ndani ya Nchi
04 Oktoba 2022.
View attachment 2376985
Huyo Mr Beans anatafuta kiki.
Maria Basso liuwawa Kawe, hajui hata content ya anayoongea.
 
Naona zito anatafuta tobo atoke vipi. Raia wanaoishi uswazi ndiyo wanajua adha panya rodi.
 
Hatua za uwajibikaji zichukuliwe mauaji ya raia kwenye Operesheni za Polisi nchini:

Utangulizi
Ndugu Waandishi wa Habari
Takribani siku 14 sasa tangu vyombo vya habari, wananchi mitaani na wanaharakati mitandaoni wamekuwa wakijadili juu ya Operesheni zinazoendelea za Jeshi la Polisi nchini. Wote tunakumbuka kuwa Operesheni hizo zilitokana na taarifa za kuendelea kwa matukio ya mauaji (Mfano kifo cha mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam - Shule ya Uandishi wa Habari, Maria Basso kilichotokea tarehe 14.10.2022 huko kwao Bunju) uvamizi, kujeruhi na kuporwa kwa mali za wananchi katika jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine nchini.

Matukio haya yameripotiwa kufanywa na makundi ya vijana almaarufu kama “panya road” au “panya buku” kwa nyakati mbalimbali. Kufuatia na matukio hayo wananchi walijawa na hofu, wasiwasi au hali ya amani ilianza kutetereka.

Tulishuhudia viongozi wa Serikali wakitoa maelekezo na kauli mbalimbali. Hatua iliyofuata, vyombo vya usalama vilichukua hatua za utekelezaji kukabiliana na matukio hayo ya kihalifu yanayohatarisha hali ya usalama na utulivu.

Sisi, ACT Wazalendo kama ilivyo kwa wananchi na wadau wengine tulipokea kwa faraja mwitikio huo wa vyombo vya usalama katika kushughulikia matukio ya kihalifu na kusambaratisha mtandao mzima. Lakini kinyume na matarajio hayo utekelezaji wa Operesheni hizo zimeibua hofu, wasiwasi na kuvuruga amani ya wananchi kutokana na ukweli kuwa Jeshi la Polisi limetuhumiwa kukiuka haki za binadamu na kupuuza mfumo wa sheria za nchi.

Ndugu Waandishi wa Habari,
Hadi sasa kuna mamia ya vijana wanaotuhumiwa na matukio hayo ya kihalifu wameripotiwa kukamatwa. Matukio yaliyotushtusha zaidi ni kuanzia mauaji ya watu sita (6) jijini Dar es Salaam yaliyothibitishwa na Jeshi la polisi lenyewe kupitia vyombo vya habari tarehe 18 Septemba 2022. Aidha, Polisi walithibitisha kuua watu watatu (3) huko Serengeti, Mara tarehe 21, Septemba 2022.

Mauaji haya, yalianza kuwashtua wadau na wanaharakati na kuacha maswali namna Polisi wanavyoendesha Operesheni zake. Ikiwa polisi wanajipa haki za kukamata, kuhukumu na kutoa adhabu tena adhabu za kifo kwa watuhumiwa ni dhahiri tunaruhusu ukandamizaji na ukiukwaji wa haki za binadamu. Pia, inaonekana kama tayari wameshakuhukumu (wao ndio Mahakama), wao ndio magereza (wanaosimamia adhabu na urekebishaji wa tabia).

Pamoja na kuwepo na taarifa za mauaji ya watuhumiwa wa uhalifu ambazo Polisi wenyewe wamekiri hadharani lakini polisi hawatangazi kila tukio la mauaji linalofanywa na wao katika mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.

Tukio la mauaji ya vijana watatu kutoka familia tatu tofauti waliokuwa wanaishi Tandika, Wilaya ya Temeke linadhihirisha ukweli huo. ACT Wazalendo tulifuatilia tuhuma za mauaji za vijana hao waliotuhumiwa kuwa ni “Panya road” likihusishwa Jeshi la Polisi.

Tulipofuatilia tulielezwa na familia zao kuwa vijana hawa walikamatwa na polisi wakiwa nyumbani kwao na kupelekwa kituo cha Polisi Maturubai kilichopo Mbagala. Vijana hawa hawakurudi nyumbani na baadaye ilibainika waliuawa kwa kupigwa risasi na Polisi.

Maiti za vijana hawa zilipelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kuhifadhiwa kwenye chumba cha maiti hospitalini hapo. Kitendo cha mtuhumiwa kuuwawa kwenye mikono ya Polisi, pasipo na sababu za kueleweka, siyo tu ni kinyume na Katiba ya Nchi lakini pia ni kinyume na sheria zote na kanuni na taratibu zinazotawala masuala ya utoaji haki nchini mwetu.

ACT Wazalendo kupitia Msemaji wa kisekta tulitoa taarifa ya awali mnamo tarehe 27 Septemba 2022 iliyotaka hatua za kiuchunguzi na kiuwajibishaji zichukuliwe. Lakini, Serikali haikuchukua hatua yoyote, tuliendelea kutoa taarifa ya kina ya utafiti tulioufanya kupitia Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana Ndg. Abdul Nondo siku mbili baadaye napo hatujaona wahusika wakichukuliwa hatua zozote licha ya taarifa hiyo kuenea kwenye baadhi ya vyombo vya habari.

Kutokana na tuhuma za mauaji yanayofanywa na Jeshi la Polisi taswira yake imeendelea kuchafuka sana. Jeshi la polisi limechorwa kuwa ni chombo katili mithili ya Jeshi la Kikaburu. Badala ya kuleta matuamini limeongeza hofu na mashaka, hivyo tumeona ni muhimu kulieleza hili ili kuhakikisha Polisi wanatekeleza majukumu yao ya kiupelelezi, kiuchunguzi na ukamataji katika mazingira ambayo hayazalishi hofu zaidi kwa wananchi wasio na hatia, hayaongezi matukio ya ukiukwaji wa haki za watu.

Hivyobasi, ACT Wazalendo tunaitaka Serikali ichukue hatua zifuatazo ili kuhakikisha Jeshi la Polisi na askari Polisi wanatekeleza wajibu wao huku wakizingatia haki za binadamu, weledi na sheria za nchi.

i. Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania liunde Tume ya kuchunguza mauaji yote ya raia ili kujiridhisha na hatua zilizofanywa na Jeshi la Polisi.

ii. Tunawataka maafisa wa jeshi la Polisi wanaotuhumiwa na mauaji kusimamishwa ili kupisha uchunguzi.

iii. Tunamtaka Waziri wa Mambo ya Ndani na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kujiuzulu mara moja kutokana kushindwa kuchukua hatua tangu matukio haya yametokea.

iv. Maafisa wote wanaohusika na mauaji hayo wachukuliwe hatua

Ni jambo la kusikitisha wakati nchini kote kuna kilio cha mageuzi ya utendaji na uendeshaji wa Jeshi la Polisi kuona askari Polisi wanaendelea kufanya matukio yanaongeza hasira, mashaka na kujenga uhasama baina Jeshi hilo na wananchi.

Tunaendelea kusisitiza mageuzi ya Jeshi la Polisi ili kulifanya jeshi hilo liwe linatumia utaalamu, Sayansi na weledi zaidi kuliko mateso, udhalilishaji na ukandamizaji kama zana za kubaini uhalisia, kuzuia na kukomesha matukio hayo

Imetolewa na;
Mbarala Abdallah Maharagande
Twitter : @Mbaralagande
Msemaji wa sekta ya Mambo ya ndani ya Nchi
04 Oktoba 2022.

View attachment 2376985
ACT WAZALENDO hawana akili, mbona wakati mauji ya panyarodi yameshamili walikuwa hawaiti press ya waandishi wa habari kulaani hayo matukio ya panyarodi?!

Huyo Maragande kumbe nae Hana akili huyu bwana mdogo wa morogoro,
 
Back
Top Bottom