Mzee Mwanakijiji,
Mkuu wangu nakuomba sana ufahamu tabia na hulka za binadamu kabla hujahukumu na kitu gani kinatakiwa kufanywa kwanza ili kuondoa nafasi ya mambo yanayoweza kutokea. wazungu wanasema mahala popote ambapo diplomacy imeshindikana basi fahamu ya kwamba upo uwezekano mkubwa wa vita hata kama swala limeanzishwa na mtu mmoja. Iraq ilishambuliwa kwa sababu ya mtu mmoja tu Saadam na walokufa ktk mashambuliszi hayo wameitwa nani Collateral damage. Mtu mmoja anaweza kabisa kuimaliza jamii nzima, hivyo hekima huanza na watu wenyewe kutofundishana shari.
Binafsi yangu husema kama kuna uwezekano wa kuepusha shari Je, kuna sababu gani ya kupuuza UPENDO lakini tuwe wepesi wa kulaani matokeo wakati mbegu tulizopanda ndizo chanzo na sababu ya matokeo hayo?. Kwa nini tusijifunze kutopanda mbegu chafu ambazo matokeo yake ndio haya..Hivi kweli wewe na wengineo mlitegemea Polisi wanaweza kuua na tukawalaani kwa maneno lakini wananchi wataendelea kuvumilia kuona mauaji yakiendelea na jeshi letu likijenga Chuki na uadui baina yake na wananchi?..
Kosa la kamuhanda linaweza kabisa kuchukua sura mpya ni lazima tujifunze haya, na hivyo kosa la mtoto alokojolea Msahafu linaweza kabisa kuzua vita baina ya Waislaam na Wakristu, kosa la Chadema linaweza kuzua vurugu kubwa baina ya wanachama wa CCM ana Chadema na kosa la Chadema linaweza kuzua vifo vya raia wengine wengi..
La muhimu kwetu sisi ni kujiuliza kama kuna umuhimu wa kuendeleza vitendo vyovyote kwa gharama hizi kubwa ambazo zinajenga chuki baina yetu. Kuna tatizo gani kwa serikali yetu, viongozi wa vyama na serikali na dini kufundisha UPENDO?.. kwa nini kila unapokwenda nchini siasa ni za CHUKI tu.. aidha viongozi kutupiwa mawe, makanisani na misikitini hakuna mafundisho ya upendo isipokuwa upande wa pili ni watu gani. Ukienda Msikitini Hotuba hazizungumzii hadithi za mtume isipokuwa SIASA za chuki, Ukienda makanisani vile vile, Ofisi za CCM na Vijana ni jinsi ya kuwasambaratisha Chadema. CUF ni Uzanzibar dhidi ya bara, JF ni waislaam against wakristu, CCM against Chadema, CUF agaisnt Chadema tena kwa matusi mazito mazito. Hi kweli ndio demokraisa au tunafanya madudu mengine?..Kweli mnategemea kuwepo na AMANI?..
Leo hii katika vyama vyetu wachungaji ndio wanagombea Ubunge, I mean mkuu wangu unategemea nini kutoka kwa mchungaji anayekwenda kanisani kufundisha dini wakati ni mwanasiasa mgombea Ubunge wa jimbo lake?.. halafu tunasema nchi yetu haina dini! huyu ni mbunge ambaye kuna uwezekano mkubwa akawa Waziri kama chama chake kitaingia madarakani..Kwa nini asiache kwanza Uchungaji kama alivyofanya Dr.Slaa na kujishughulisha na siasa lakini unakuta mtu anagombea Uongoz huku akifundisha Gospel makanisani na hata ktk majukwaa ya siasa. jamani tunatafuta nini kama sio kuitaka shari sisi wenyewe?..
mambo mengine jamani sina haja ya kuyazungumza sana lakini ukweli unabakia kwamba sisi wenyewe tunafundisha a chuki, sisi wenyewe ndio tunaochochea hizi CHUKI na HuSUDA ktk mfumo mzima wa siasa zetu na Utawala. Maana sioni tatizo kabisa kwa Polisi nchini kuwalinda wananchi kama walivyoapa badala yake wananchi ndio wanakuwa maadui zao kwa makosa yalofanywa na viongozi wao halafu tutegemee watu watakaa kimya tu....
MMK Wao police ndiyo wamewafikisha hapo watz,
View attachment 68063
dada huyu ndiye mwenyewe
Correction kiongozi. Hiyo picha ni ya black american na iko kwenye website inayoongolea mambo ya unene (obesity). Sijui imefikaje Tanzania?
Back to the main point: These are trying times kwa Taifa la Tanzania na tukikosea tutaungukia upande wa pili, upande ambao ni very ugly and it may take generations to correct it. Taratibu tunaanza kubomoa mambo ya msingi yanayotuunganisha kama taifa, tunaanza kuwa na kizazi cha kuviziana na kulipiziana visasi!
Kelele za watu wakati wa mauji ya Ally Zonga, Daudi Mwangosi na wengine si kwa sababu ya taalum zao, bali ni kwa kutambua haki ya msingi ya kila mtu kuishi. It is very regrettable kwamba Tanzania tumefikia mahali tunafurahia kifo cha mtanzania mwingine. Na ndiyo nasema these are trying times.
Kunahitajika juhudi za hali ya juu kuturudisha kwenye mstari. Ni kwa kutambua haki za kila mmoja wetu ndipo mtu utakuwa na moral authority ya kunyoosha kidole pale mtu anapokwenda kinyume. Tofauti na hapo tunakuwa kama taifa la laana.
Sijui kama hili linawezekana. Lakini tungekuwa na wazee (regardless wako affiliated na itikadi,dini, kabila gani) wakae chini na uongozi wa juu wa nchi hii na kuongea kwa uwazi.Tuliona juhudu za Warioba, Dr Salim wakati wa utata wa katiba mpya na walk out ya CHADEMA. Tunaweza kuwa na juhudi za namna hiyo kwa sasa ili walau tuwe na framework ya pamoja.
Sasa hivi ni kama hatuna mwelekeo and no one anaonekana kushtushwa na hii hali. Mwezi ulipita mwandishi wa habari amelipuliwa na bomu, jana watu wazima wanamwinda mtoto mdogo wamuuwe, wengine wanachoma makanisa, leo RPC anapigwa risasi! Something must change.
Mkuu kumbe nimeingizwa chaka??kuna post inaendelea hapa jamvini inaonyesha huyu mwanamke kuwa ndiye yule aliyekuwa na kamanda!jamani!
very right...wanasema tz kuna amani lakini ukweli halisi ni kwamba hamna amani bali......kwa miaka yote hii watu wamekua wanaishi kwa harmony.....huku wakivumiliana tofauti zao.....lakini sasa imefika mahali tolerance level kwa maovu ya aina yoyote inafikia mwisho wake katika jamii ya tz....na hili limefikishwa hapa kwa kiasi kikubwa na watawala wetu...ambao jeshi la polisi liko chini ya mamlaka yao......Jamii ya mtanzania inaanza kufikia mahali kujichukulia hatua wanavyotaka maana wanaona kuwa watawala hawajali......Labda tukumbuke tu kuwa jamii nyingi zilizowahi kufikwa na machafuko pia zilipitia hatua hii ilipo tz kwasasa...mfano: nchini Kenya kabla ya yale mauaji ya kuchinjana baada ya uchaguzi..polisi wao walikuwa wanalaumiwa sana sana na raia kwa kufumbia macho maovu.....jambo lililochangia sana mauaji yale kutokea Kenya.....kama itakumbukwa katika watu waioshtakiwa kule ICC the Hague alikua mkuu wao wa jeshi la polisi(japo mwishoni aliachiwa).....Hapa kwetu tayari raia wameshapoteza imani na jeshi la polisi na kama watawala wataenddelea kufumbia macho haya mambo basi tunakoendelea only God knows......Kwa kifupi what needs to be done ni kwa jeshi la polisi kubadilika.....pamoja na watawala.......raia watanzania bado ni wapole saana......Correction kiongozi. Hiyo picha ni ya black american na iko kwenye website inayoongolea mambo ya unene (obesity). Sijui imefikaje Tanzania?
Back to the main point: These are trying times kwa Taifa la Tanzania na tukikosea tutaungukia upande wa pili, upande ambao ni very ugly and it may take generations to correct it. Taratibu tunaanza kubomoa mambo ya msingi yanayotuunganisha kama taifa, tunaanza kuwa na kizazi cha kuviziana na kulipiziana visasi!
Kelele za watu wakati wa mauji ya Ally Zonga, Daudi Mwangosi na wengine si kwa sababu ya taalum zao, bali ni kwa kutambua haki ya msingi ya kila mtu kuishi. It is very regrettable kwamba Tanzania tumefikia mahali tunafurahia kifo cha mtanzania mwingine. Na ndiyo nasema these are trying times.
Kunahitajika juhudi za hali ya juu kuturudisha kwenye mstari. Ni kwa kutambua haki za kila mmoja wetu ndipo mtu utakuwa na moral authority ya kunyoosha kidole pale mtu anapokwenda kinyume. Tofauti na hapo tunakuwa kama taifa la laana.
Sijui kama hili linawezekana. Lakini tungekuwa na wazee (regardless wako affiliated na itikadi,dini, kabila gani) wakae chini na uongozi wa juu wa nchi hii na kuongea kwa uwazi.Tuliona juhudu za Warioba, Dr Salim wakati wa utata wa katiba mpya na walk out ya CHADEMA. Tunaweza kuwa na juhudi za namna hiyo kwa sasa ili walau tuwe na framework ya pamoja.
Sasa hivi ni kama hatuna mwelekeo and no one anaonekana kushtushwa na hii hali. Mwezi ulipita mwandishi wa habari amelipuliwa na bomu, jana watu wazima wanamwinda mtoto mdogo wamuuwe, wengine wanachoma makanisa, leo RPC anapigwa risasi! Something must change.
Sio wewe uliesema humu 'umetafuna' wake za watu saba?
sasa unashangilia nini hapa?
wewe ufanywaje na wenye wake?