Hekima inapoita: Mauaji ya Barlow yanahitaji kulaaniwa, kukataliwa na yanalia "haki"

Mkuu Mwanakijiji! Umemsikia yule RPC wa Iringa alivyosema? "alikuwa anatimiza wajibu wake" yaani hadi leo anahisi yule mwandishi hakuwa na haki ya kuishi. Thanx God, Lazima nao wajaribu chungu ya jiwe. Moja imekwisha, sasa tutafute mwingine mwenye Nyumba ndogo. Wazo lilikuwa kulipiza kisasi kwao makamanda, wake zao, watoto zao, baba/mama zao au dada/kaka zao. Kwa kuwa wengi wanapatikana kirahisi kwenye Nyumba ndogo, tutawapata. Kamuhanda next
 
  • Thanks
Reactions: PhD
Siku zote dhihaka na dharau ni mbaya sana kwavile huwezi jua anaedharauliwa na kudhihakiwa inamuua kiasi gani na nn itakuwa reaction yake cause every action has its reaction...wananchi wamechoka na mdhaha na dhihaka za waliowapa dhamana kuwaongoza na kuwalinda wao na mali zao...mwanzoni tuliamini labda wataviogopa na kuviheshimu viapo vyao wanavyokula vya kubeba dhamana kubwa tuliowapa lakini kumbe imekuwa ni tofauti...Hivi tukimbilie wapi?tumeona mifano ya majaji tulionao na ripoti zao za dhihaka na mzaha ktk jambo sensitive,mkuu wa jeshi lapolisi na waziri wake wa mambo ya ndani tumeuona pia mdhaha wao na dhihaka zao ktk jambo kama la kuuwawa Mwangosi..mkuu wa nchi ameshindwa japo kutoa kauli yake kuukemea huu upuuzi...lkn alipokufa msanii wa filamu Kanumba ikulu nzima na viongozi walikuwa wakijazana kila siku kwenye msiba maeneo ya sinza na kujifutua futua kwa kutoa rambirambi mradi tu waonekane kuwa na wao wapo...ok si vibaya kuhudhuria misiba haijalishi ni ya nani lkn kama kweli mna uchungu basi mlitakiwa pia mguswe na hichi kifo cha kizembe cha mwandishi...Binafsi sina cha kuongeza wala kupunguza ktk alichokiandika mkuu wangu Mwanakijiji namuunga mkono 100% kwa yote alioandika lkn nasisitiza mdhaa sio mzuri tujenge kuheshimiana amani hii kiduchu tulionayo tukiipoteza sio vizazi vyetu wala vizazi vijavyo vitakavyoweza kuirudisha kirahisi.
 
MM wangu hayajakukuta. Wengi wanatuchukulia wake zetu wakijidai na kinga yabhuo upolisi wao. Tunapewa kesi za kijinga eti kisa mapenzi. Kwa yaliomkuta unadhan atasemaje? Na huyu kamanda RIP ni lazima alikuwa dem wake tu. We vikao gan vya saa 7 usiku imekuwa ndoabya mfalmen?
 
pinda kasema liwalo na liwe usiku huo huo ulimboka katekwa,kateswa na kutelekezwa,wakamkamata kichaa tukaona vizuri tu,hilo likapita,morogoro polisi wakaua wakasema ni kitu kizito hilo nalo likapita,mwangosi akauawa na polisi wakasema ni kitu kizito kimetoka upande wa wafuasi wa chadema,picha zikawaumbua.Je,hapo polisi wana utu?sasa kama wao wanatudhihaki je sisi ndio tuwasikitikie?
bana eeee liwalo na liwe malipo ni hapa hapa duniani tulishachoka.....
 
Kweli tunatoa pole sana kwa familia ya marehemu na ni maskitiko roho ya mtu kuondolewa tena kwa staili ya kinyama hivi. Ni kosa kubwa kushangilia kifo au tukio la namna hii no matter huyu RPC alikuwa wa aina gani kiutendaji. Si hekima kufanya hivyo.

That said; ni kweli pia kuwa si hekima kwa serikali kuangalia matukio mfululizomabaya yanayolidhalilisha jeshi la polisi na jeshi la wananchi huku kila kitu kinaendelea tu with business as usual!

Mwanakijiji wananchi tumeshangaa sana toka wafanyabiashara wasio na makosa walipouawa Dar kwa kusingizia kuwa ni wezi, tume ikaundwa na Rais ikaona makosa yaliyofanyika lakini kesi eti ikawaweka huru watuhumiwa; Askari wa kike aliuawa kituoni polisi after abuse na kutishwa eti kakosesha msafara na taarifa za uchunguzi eti zinaishia kuwa kajiua! mwandishi wa habari mahiri wa TBC aliyejishughulisha na taarifa za kiuchunguzi alipokamatwa na kushitakiwa kuwa kakutwa na pingu wakati maelezo yao yakipinda pinda; Watu wenye mali na haki ya kufurahia migodi ya nchini kwao wakauwawa machimboni na wawekezaji wezi wetu ambao wanawaweka maaskari wetu kwenye payroll kwa kuwalipa posho za kutoa ulinzi kisha polisi wakalazimisha kuchukuwa maiti na upuuzi mwingi wa kufunika kombe kwenda, kisha watu wameuawa kwenye mikutano na maandamano ya vyama vya siasa (hasa CHADEMA) bila kosa, Askari mstaafu aliuwawa Morogoro kwa kufichua jinsi polisi mkubwa anavyoshirikiana na majambazi, Makanisa yanachomwa Zanz na sasa Dar na vitu vinaporwa wakati Wakristo hawana kosa lolote wala hawajawahi kuvamia misikiti wala kutetea upumbavu wa kuwakandamiza Waislam maana ni ndugu zao, RPC ana tetea uozo wa askari wake aliyetaka kumtoa roho Afisa wa Uhamiaji kwa sababu za kutaka kupata ngono ya kulazimisha ya mke wa mwenzake! Sijataja ni vituo vingapi vya polisi vimevamiwa mwakaja na mwaka huu na raia wenye hasira!!!

Haya inapokuja kwa Jwtz, milipuko ya mabomu iliyoua na kuwafanya wananchi ama walemavu au maskini mara mbili na pia baadhi ya matukio ya maaskari jeshi kutembeza kichapo kwa wananchi wasio na hatia.

Sasa sisi tunaangali baada ya hayo yote nini kinatokea; unakuta hakuna anaye step down wala kuwajibishwa na mbaya zaidi taarifa zinazotolewa ni za UONGO mfano tume ya Waziri wa mambo ya ndani ya juzi, je ilichokitoa kama taarifa kinavumilika mbele ya wananchi ambao wamewasilikiza pia baraza la habari na wanahakati wa haki za binadamu?

Mimi Obudsman huwa sina cha kungáta maneno, nasema dhuruma ikizidi wananchi wataifatuta haki wenyewe bila kusubiri utaratibu wala sheria. Yaani ninachokisema ni kuwa waziri mwenye dhamana alitakiwa aachie ngazi na Afande Kova anapwaya sana na kwa kweli hatuhitaji kuita consultancy waje kutufanyia tathmini ya hali mbaya ya majeshi yetu kinidhanu na kiutendaji.

Najaribu kufikiri tu kile kilio cha wale akina mama wa kanisa lao matokeo ya machozi yao yatakuwa nini, siku zijazo?

Hivi leo ingekuwa ni Waislamu sisi tumechomewa Msikiti wetu wa Ijumaa na capet zetu na zaka kuibiwa ingekuwaje kutoka hapa Masjid Anuur?

Tunaweza kufikiri kuwa ni udhaifu fulani kumbe ni nguvu ya makusudi fulani ili watu wafanye kinachokusudiwa; sasa tunaendelea kutafakari na tutamshukia kila muhusika anayetuvuruga au anyayepaswa kuchukuwa hatua lakini hachukuwi toka vijijini hadi Taifa!
 
Mzee Mwanakijiji,unatakiwa urudi bongo kidogo,maana naona uko out of touch.Maneno yako ni ya "busara",lakini ungekuwa bongo na kukutana na unyama wa polisi usingesema hayo maneno.

Kuna watu ndugu zao wameuwawa bila sababu,kuna watu wako jela kwa kubambikiziwa kesi.Polisi wameshajijengea uadui na wananchi wa kawaida.

Si bora uwasemee wananchi hao wanyonge,wacha waseme wanavyojisikia,pengine ndiyo njia yao pekee ya "Retaliatory impulse", kwasababu wao ni wanyonge na wanahisi kuna mtu kawatendea haki.

Usilazimishe watu wasikitishwe na vifo vya askari wanyama na wakati wao wanauwa raia wema each and everday.

Kwanza una uhakika gani kwamba amefia mikononi mwa raia?Tofauti na tunavyojuwa sisi kuwa raia wasiokuwa na hatia wanafia mikononi mwao mchana kweupe na kamera zikimulika?
 
anamsubiri rafiki yake Benny Membe awe rais wa JAMHURI ndio arudi, kishaadiwa kuwa iwapo Membe atakuwa RAIS basi yeye ndie atamrithi rweyemamu salva kwenye ile nafasi ya kurugenzi ya mawasiliano ya rais, vifo vinavyofanywa na polisi havimuhusu mkubwa huyu MM.
 
Sijapenda kabisa hili bandiko lake,especially anapozungumza as if ni raia wema ndiyo wamefanya mauwaji hayo ya Kamanda Liberatus,nimeshangazwa sana,nadhani hafahamu kitu kinaitwa "retaliatory impulse",hakuna aliyeadhibiwa kwa mantiki ya maneno wanayozungumzia wana JF,unless awe anazungumzia kuwa wananchi ndiyo wamemwua huyo kamanda.
Mzee Mwanakijiji said:
Ni lazima tujifunze kuwa na hekima ya kutofautisha kitu kinachoitwa "collective punishment" kwamba tunaadhibu wote kwa kosa la mmoja. Labda ni kwa sababu tunaamini (bila kufikiria sana) kuwa "samaki mmoja akioza wameoza wote". Ukweli ni kuwa samaki mmoja akioza siyo wote wameoza!
 
Rimovie ndio rinaanza hapo kweli allah ni muweza wa kila kitu analipa hapa hapa duniani kesho akhera ni hesabu tuu damu ya ally na daudi zinaanza kuwasakama waliozimwaga
 
Hilo nalo halikubaliki; na polisi wakifanya hivyo tutawapinga vile vile. Ndio maana tunasema haki ni haki hata ya adui yako ni haki. Polisi wanawajibu wa kuwatafuta wahusika. Tukihalalisha hili yatatokea kama yale yaliyokuwa yanatokea zamani (labda siyo zamai sana) na JWTZ ambapo askari wao akipigwa na rais kikosi kinakuja na kufunga mtaa na kupiga wananchi wote kuwakomoa! Sasa leo polisi wakishuka Kitangiri na kuanz akupiga watu ili "wawataje wahusika" tutasema ni haki kwa vile wanalipiza afisa wao kuuawa na raia?

hakika babu umenena ya kuwa hekima inatuita lakini pia babu kwa kila tukio si yatupasa kujifunza?
nilionalo mimi ni kuwa uachapo kuupiga vita uovu ulio ndani yako na kukimbilia kuupiga vita uovu ulio nje yako, hakika uovu ulio ndani hautokubakisha salama na hizi ni salamu kwa IGP!
 
Tangu habari za mauaji ya Kamanda Barlow yalipotokea mwitikio wa watu wengi umekuwa ni kutokujali, kuhalalisha na hata kushangilia ni kama mtu kusema "akome". Wengi wanahalalisha hili kwa sababu wanaamini ujumbe umetumwa kwa polisi na kuwa polisi 'wanaua watu na sasa kimewarudia'. leo kosa la Kamuhanda anahukumiwa Barlow? Leo hii kosa la askari mmoja wanalaumiwa jeshi zima kiasi kwamba leo chochote kitakachompata polisi tunafurahia? Ni lazima tujifunze kuwa na hekima ya kutofautisha kitu kinachoitwa "collective punishment" kwamba tunaadhibu wote kwa kosa la mmoja. Labda ni kwa sababu tunaamini (bila kufikiria sana) kuwa "samaki mmoja akioza wameoza wote". Ukweli ni kuwa samaki mmoja akioza siyo wote wameoza!.
Hali ilivyo sasa, WATU WAMEJAA UCHUNGU, HASIRA, KINYONGO na HAMU ya kuona askari yeyote (mahali pengine hata familia zao) anakumbana na mabaya. Bila shaka hata watu wakiona polisi anapigwa wengi watashangilia badala ya kutoa msaada. Wafanyabiashara waliuawa Dar (hatujui wangapi wameuawa mahali pengine kwa mtindo huu), Bulyanhulu vijana walizikwa hai, Mara, Iringa, Morogoro n.k. Polisi wameua. Na Mwanza polisi hao hao wamekosakosa kuua!.. Kisa hiki na mengine mengi ndiyo chanzo cha hasira!..
 
Mzee Mwanakijiji,unatakiwa urudi bongo kidogo,maana naona uko out of touch.Maneno yako ni ya "busara",lakini ungekuwa bongo na kukutana na unyama wa polisi usingesema hayo maneno.

Kuna watu ndugu zao wameuwawa bila sababu,kuna watu wako jela kwa kubambikiziwa kesi.Polisi wameshajijengea uadui na wananchi wa kawaida.

Si bora uwasemee wananchi hao wanyonge,wacha waseme wanavyojisikia,pengine ndiyo njia yao pekee ya "Retaliatory impulse", kwasababu wao ni wanyonge na wanahisi kuna mtu kawatendea haki.

Usilazimishe watu wasikitishwe na vifo vya askari wanyama na wakati wao wanauwa raia wema each and everday.

Kwanza una uhakika gani kwamba amefia mikononi mwa raia?Tofauti na tunavyojuwa sisi kuwa raia wasiokuwa na hatia wanafia mikononi mwao mchana kweupe na kamera zikimulika?

Ndio tatizo la kuongozwa na hisia, instinct na passion. Binadamu anatakiw aongozwe na 'reason' na siyo hisia zilizoumizwa. Kwa vile kuna watu wametendewa vibaya na polisi kwa namna yoyote ile inahalalisha vipi kwa polisi kufanyiwa ubaya? Leo hii tuna huko NY polisi mmoja amemuua askari wa jeshi akidhania alikuwa anachomoa bunduki. Watu wamekasirika na hilo si jipya huko NY? Hivi umewahi kuona wamarekani wanafurahia kuuawa kwa polisi? Unafikiri hawa Wamarekani (hasa weusi na latino) hawana uchungu wa kibinadamu wanapoona ndugu zao wanatendewa vibaya.

Umeona mwamko wao ni nini? NI kudai reform ya jeshi, uchunguzi na hata kutaka watu wawajibike (yule Chifu wa Florida alikouawa Treyvon aliondolewa)! Sisi wengine badala ya kutaka na kuhalalisha polisi wafanyiwe vibaya kwa sababu baadhi yao wanawafanyia vibaya raia tunakata jeshi lile reformed, Mwema na Chagonja waondolewa na tunataka watu kama kina Kamuhanda watiwe pingu. Tunaliona tatizo lile lile la kiuongozi na kimfumo ambalo linachangia sana kwa askari wa chini kukosa weledi na nidhamu. Hatufikirii ati kwa vile polisi wapo wakorofi basi wauawe au wafanyiwe vibaya ili kutengeneza a moral equivalency of sort.

Pita hisia zako na vionjo na tumia uwezo wako wa kufikiri. Usifikirie kwa msingi wa "mbona sisi wanatufanyia vhivi na sisi tuwafanyie vile"! Ni alama ya kukomaa katika hekima. Ndio maana wapo humu humu watu wanaoona nis aawa kwa kibaka kuuawa na kutiwa moto kwa sababu wamekuwa 'kero'! Kwamba "we hujawahi kuchomolewa ndio maana hujui jinsi walivyo kero"!
 
Mkuu siyo kwamba napingana na wewe,ila sioni haja ya kupingana na raia ,especially kwenye issue ambayo ni wazi inahusisha retaliatory impulse.

Mbona hukuanzisha thread kama hii kwa wale waliokuwa wakihalalisha mauwaji wa Mwangosi?

Pili,ningekuwa wewe,ningewashauri polisi watende kwa namna ambayo haitajenga sura ya wananchi kufurahia jambo baya linapowatokea.Nina uhakika kabisa kuwa waliotoa hisia zao kufurahia hili jambo,wengi wao siyo criminals hata kidogo.

Ninakuhakikishia kuwa hizo ni credible feelings za the oppressed ones.

Wakati wa ubaguzi wa rangi kule SA,ungesema maneno kama haya?

Ndiyo maybe polisi wa kikaburu walipatwa na mauwaji,lakini unataka kuniambia wananchi wangekuelewa kama ungewaambia wasifurahie vifo vyao?

Only kama huamini kwamba tuko kwenye mipambano mithili ya ile ya ukombozi wa Afrika Kusini.
 
retaliatory impulse ndio huko kuongozwa na hisia na vionjo. Ninaelewa vizuri sana suala la revenge. Lakini revenge ni kwa yule aliyetendewa ndiye anaweza kusema anataka kujirudishia haki yake. Sisi wengine tunafurahia mauaji ya Barlow kwa sababu katufanyia nini? Kwmaba kwa sababu "polisi wanafanya hivi na vile" basi polisi wote sasa wauawe? Mbona niliandika vizuri tu kwenye suala la Kamuhanda? Wapo watu wanaamini Kamuhanda angeuawa basi 'haki ingekuwa imetendeka" na kufurahia. Mimi bado nisingefurahia wala kuhalalisha. Hatuwezi kujenga na kutetea jamii ya 'dog eat dog'!
 
Mkuu mwanakijiji,mtu akifiwa,wakati wa msiba,hautakiwi kumwambia mambo ya kusema,unatakiwa kumfariji,na baada ya msiba,kama yakiendelea,then your point is justifiable.Ndiyo maana yangu halisi ya ku mention retaliatory impulse.

Kwenye retaliatory impulse,haina maana kwamba tunakwenda kuuwa mtu kwa kulipiza kisasi kwasababu ya msiba(retaliatory impulse isn't neccessarilly a revenge),bali utaona ni hisia zinazotokana na kitendo cha unyanyaswaji(ie huyu ameuwawa kwasababu hii,ama ameuwa kwasababu hii).

Ndiyo maana nikatolea mfano wa apartheid ya SA.Kwamba maneno kama haya husingeeleweka.

Acha msiba upite,acha watu watoe vilio vyao kwasasa(both ways).

Misiba haiongozwi na hekima,la sivyo isingeitwa vilio,maana ukiongozwa na hekima bila hisia huwezi kulia.
 
Back
Top Bottom