Hekima inapoita: Mauaji ya Barlow yanahitaji kulaaniwa, kukataliwa na yanalia "haki"

Niwe muwazi, toka polisi na viongozi wa serikali waanze kunyanyasa raia, kila anapoondoka m1, huwa nashukuru mungu. sina huruma nao kabisa.
 
Mzee Mwanakijiji nakuunga mkono haki ya kuishi ni ya kila mtu hata kama humpendi kwani hakuna aliyemkamilifu katika kila jambo.
 
Kilings are never justified, na ndo maana death penalty imebakia kwenye karatasi pekee, lkn, iweje police wachukulie vifo vingine kiwepesiwepesi? roho ya Barlow
ni moja na roho ya Mwangosi nayo ni roho moja. both bcame copses, na huo ndo ubinadamu tunaopaswa kuulinda. Leo ukiona raia kauwawa na police 4 whatever reason kesho ukasikia police kauwawa utaona ni jambo la kawaida kabisa. Cha msingi tujitathmini sisi raia lkn hasa viongozi. Ukisigina haki ya mtu wewe hakimu kesho ni rahisi mtu kumgonga na gari mtoto wako makusudi. Kumbuka visasi ni asili ya binadamu. hakuna lenye mwanzo lisilo na mwisho, dhuluma, hii ndo side effect yake. RIP KAMANDA BARLOW, Rudi Tz yangu kisiwa cha amani kilichotukuka kwa utawala wa sheria, masiasa yenu yanayotufanya tuendelee kuwa masikini hukohuko!
 
Nakubaliana nawe Mwanakijiji kwamba binadamu hatustahili kufurahia mauaji ya binadamu mwenzetu. Wa kulaumiwa hapa ni Serikali ambayo utendaji wake katika kulinda na kuhakikisha haki za Watanzania pale wanaponyanyaswa kwa aina yoyote ile Serikali ambayo inatakiwa iwe mtetezi wa Watanzania haifanyi hivyo. Angalia DHAIFU jinsi alivyoshiriki katika kifo cha Kanumba na hata kutoa salaam na mchango za/wa rambi rambi kwa wafiwa, lakini hakufanya hivyo kwa Mwangosi pamoja na kuwa hakuwa na hatia yoyote ile ya kusababisha kupoteza maisha kinyama kiasi kile.

Haya yote yanayoendelea ndani ya jamii yetu kwa asilimia kubwa yanasababishwa na DHAIFU. Watanzania hatuna tabia hizi za ajabu ajabu za kufurahia kifo cha mtu yeyote yule hata kama hatuhusu lakini huku tuendako kama Serikali haikua makini ili kurudisha imani kwa Wananchi wake basi hali hii itazidi kujitokeza kwa kasi kubwa sana kutokana na Watanzania kuvichukia vyombo vyote vya dola vikiwemo polisi na mahakama ambavyo vimekuwa mstari wa mbele katika kuminya haki mbali mbali za Watanzania pamoja na Serikali yenyewe.
 
Ukiona wnanchi, hasa wale wa kawaida sana, wanafurahia kifo cha mtu mwingine, tena kiongozi wa jamii, ujue kuna upotofu mkubwa wa maadili katika mfumo wa Uongozi.

Wananchi wa Tanzania ni watii na wavumilivu, na wasiopenda maovu. Serikali na Polisi yapasa ijisafishe. Iheshimu watanzania na kuwapa kile kitu wao wanakitaka. Serikali iendeshwe kwa mujibu wa sheria (na si kwa mujibu wa hisia za viongozi)

Kwa mfano, sasa hivi hakuna anayejua nini kitafuata baada ya mauaji haya...hatujui kama wataweka tume, ama kamati...ama watafanya mambo kimya kimya au vipi. Hili halivumiliki hata kidogo. Na wakiweka kamati ama tume...hakuna anayejua kama italeta mazao tunayoyategemea...

Bado narudia tena...Viongozi ndio wanaopelekea nchi katika hatima hii. Lazima wajitafakari na wabadilike.
 
Sio wewe uliesema humu 'umetafuna' wake za watu saba?
sasa unashangilia nini hapa?
wewe ufanywaje na wenye wake?
Naungana na watanzania wengine katika kulaani mauaji haya,Marehemu alikuwa kati ya wasomi wazuri sana,ana masters ya sheria,pia kuna fununu kuwa alikuwa amependekezwa kwenda kanda Maalumu ya Dar kuchukua nafasi ya ....,wengine wanahusisha ili na kifo chake.Pamoja na kuunga mkono hoja ya mwanakijiji lakini ni wakato mzuri wa polisi kutafakari upya uhusiano wa jeshi na raia kwa siku za karibuni,hii ni matokeo ya mbegu ya chuki iliyopandwa hivi karibuni na jeshi ilo kwa kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya raia na kwa kufanya kazi kisiasa,si siri raia wako so negative dhidi ya jeshi ilo.Said Mwema alikuwa na lengo zuri sana alipo introduce police jamii lakini lakini kutokana na maingiliano ya siasa kwneye uendeshaji wa jeshi ilo ameshindwa kutimiza azma yake.
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu wangu nakuomba sana ufahamu tabia na hulka za binadamu kabla hujahukumu na kitu gani kinatakiwa kufanywa kwanza ili kuondoa nafasi ya mambo yanayoweza kutokea. wazungu wanasema mahala popote ambapo diplomacy imeshindikana basi fahamu ya kwamba upo uwezekano mkubwa wa vita hata kama swala limeanzishwa na mtu mmoja. Iraq ilishambuliwa kwa sababu ya mtu mmoja tu Saadam na walokufa ktk mashambuliszi hayo wameitwa nani Collateral damage. Mtu mmoja anaweza kabisa kuimaliza jamii nzima, hivyo hekima huanza na watu wenyewe kutofundishana shari.

Binafsi yangu husema kama kuna uwezekano wa kuepusha shari Je, kuna sababu gani ya kupuuza UPENDO lakini tuwe wepesi wa kulaani matokeo wakati mbegu tulizopanda ndizo chanzo na sababu ya matokeo hayo?. Kwa nini tusijifunze kutopanda mbegu chafu ambazo matokeo yake ndio haya..Hivi kweli wewe na wengineo mlitegemea Polisi wanaweza kuua na tukawalaani kwa maneno lakini wananchi wataendelea kuvumilia kuona mauaji yakiendelea na jeshi letu likijenga Chuki na uadui baina yake na wananchi?..

Kosa la kamuhanda linaweza kabisa kuchukua sura mpya ni lazima tujifunze haya, na hivyo kosa la mtoto alokojolea Msahafu linaweza kabisa kuzua vita baina ya Waislaam na Wakristu, kosa la Chadema linaweza kuzua vurugu kubwa baina ya wanachama wa CCM ana Chadema na kosa la Chadema linaweza kuzua vifo vya raia wengine wengi..

La muhimu kwetu sisi ni kujiuliza kama kuna umuhimu wa kuendeleza vitendo vyovyote kwa gharama hizi kubwa ambazo zinajenga chuki baina yetu. Kuna tatizo gani kwa serikali yetu, viongozi wa vyama na serikali na dini kufundisha UPENDO?.. kwa nini kila unapokwenda nchini siasa ni za CHUKI tu.. aidha viongozi kutupiwa mawe, makanisani na misikitini hakuna mafundisho ya upendo isipokuwa upande wa pili ni watu gani. Ukienda Msikitini Hotuba hazizungumzii hadithi za mtume isipokuwa SIASA za chuki, Ukienda makanisani vile vile, Ofisi za CCM na Vijana ni jinsi ya kuwasambaratisha Chadema. CUF ni Uzanzibar dhidi ya bara, JF ni waislaam against wakristu, CCM against Chadema, CUF agaisnt Chadema tena kwa matusi mazito mazito. Hi kweli ndio demokraisa au tunafanya madudu mengine?..Kweli mnategemea kuwepo na AMANI?..

Leo hii katika vyama vyetu wachungaji ndio wanagombea Ubunge, I mean mkuu wangu unategemea nini kutoka kwa mchungaji anayekwenda kanisani kufundisha dini wakati ni mwanasiasa mgombea Ubunge wa jimbo lake?.. halafu tunasema nchi yetu haina dini! huyu ni mbunge ambaye kuna uwezekano mkubwa akawa Waziri kama chama chake kitaingia madarakani..Kwa nini asiache kwanza Uchungaji kama alivyofanya Dr.Slaa na kujishughulisha na siasa lakini unakuta mtu anagombea Uongoz huku akifundisha Gospel makanisani na hata ktk majukwaa ya siasa. jamani tunatafuta nini kama sio kuitaka shari sisi wenyewe?..

mambo mengine jamani sina haja ya kuyazungumza sana lakini ukweli unabakia kwamba sisi wenyewe tunafundisha a chuki, sisi wenyewe ndio tunaochochea hizi CHUKI na HuSUDA ktk mfumo mzima wa siasa zetu na Utawala. Maana sioni tatizo kabisa kwa Polisi nchini kuwalinda wananchi kama walivyoapa badala yake wananchi ndio wanakuwa maadui zao kwa makosa yalofanywa na viongozi wao halafu tutegemee watu watakaa kimya tu....

Hivi unajua mkulu nae alichagua mchungaji mmoja kuwa mbunge kama sio viti maalumu!!
 
i beg to differ on this.....hamna anaependa watu kuuwawa hovyo....hii hata dini zetu haziruhusu......ila linapokuja suala la mfumo wa polisi nchini kuwa wa hovyo na kuruhusu mambo ya mauaji ya raia kutokea bila wahusika kuchukuliwa hatua, hapa lazima watu wawe na hasira kwa polisi.....tena watu wanapoona kuwa wakubwa wenyewe wa polisi wanafumbia macho mauaji ya raia wasio na hatia.....unategemea kweli raia watawapenda kweli polisi??????.....ni kwa msingi huu tu hata mimi naona bora message imepelekwa kwa polisi kuwa oh!!kumbe hata wao waweza kuuwawa!!!......ni kwa msingi huo watu wanaona bora yametokea kwa polisi kama yalivyokuwa yakitokea kwa raia chini ya usimamizi wa hao hao polisi....mimi naona bora wao polisi nao waonje machungu ya mwenzao kufa......ili nao wajue kuna kufa....kwa msingi mzima wa kujali uhai wa wenzao raia.....napata hisia kabisa kuwa waliomuua huyu mkuu wa polisi ni raia tu na wala si majambazi.......maana chuki kwa hawa mapolisi imekuwa juu sana tz....haswa ukizingatia kuwa kelele zinapigwa na raia na wao wanakuwa kimya....na wameshiriki kuua pia......let them die too.......
 
Mheshimiwa mwanakijiji heshima kwako kwa uchambuzi uliotukuka lakini mzee mwanakiji jamii yetu saizi ndio imefikia hapo anakojolea KORAN mtoto wa dhehebu jingine yanachomwa makanisa ya dhehebu mengine sasa Mzee mwanakijiji labda wewe hujaona picha ya huyo mwl.ambayo alikwa na kamanda mtoto katokelezea kweli kamanda amekufa kishujaaa!!!!!!!!!

hyo pcha iko wapi?
 
Nimesema juzi kuwa ukosefu wa hekima ni janga kubwa la kitaifa kwa kweli nilimaanisha hilo. Tangu habari za mauaji ya Kamanda Barlow yalipotokea mwitikio wa watu wengi umekuwa ni kutokujali, kuhalalisha na hata kushangilia ni kama mtu kusema "akome". Wengi wanahalalisha hili kwa sababu wanaamini ujumbe umetumwa kwa polisi na kuwa polisi 'wanaua watu na sasa kimewarudia'. Kauli hizi ndizo zinazothibitisha ukosefu wa hii hekima.Tumeshuhudia kosa la mtoto mmoja kwenda kuhukumiwa makanisa na wakristu; leo kosa la Kamuhanda anahukumiwa Barlow? Leo hii kosa la askari mmoja wanalaumiwa jeshi zima kiasi kwamba leo chochote kitakachompata polisi tunafurahia?

Ni lazima tujifunze kuwa na hekima ya kutofautisha kitu kinachoitwa "collective punishment" kwamba tunaadhibu wote kwa kosa la mmoja. Labda ni kwa sababu tunaamini (bila kufikiria sana) kuwa "samaki mmoja akioza wameoza wote". Ukweli ni kuwa samaki mmoja akioza siyo wote wameoza!

Kamanda Barlow ahukumiwe kwa matendo yake mwenyewe na si matendo ya wengine. Je alikuwa ni kamanda mzuri kwa polisi, je alisimamia haki na utawala wa kisheria kwa kadiri ya uwezo wake (yaani pamoja na mapungufu yake kama alivyoshughulikia hili la koswakoswa la afisa)? Je kuwa dhaifu kiutendaji adhabu yake ni mauti?

Tuna tofauti gani basi na wale ambao wanaona mtu anapigwa na watu kwa sababu kadaiwa ni 'kibaka' na wao bila kuuliza wanachukua jiwe na kurusha au wanauliza "lete petroli" halafu wanaondoka zao huku nyuma mtu anatiwa kiberiti? Tuna tofauti gani na jamii isiyoerevuka ambayo haitaki kutafuta ukweli inaishi kwa imani na hisia tu?

Mauaji ya Barlow kama yalaivyokuwa mauaji ya Mwangosi na ya wananchi wengine wengi yanapaswa kulaaniwa na siyo kuhalalishwa, yanastahili kupingwa na siyo kutetewa na yanahitaji kukataliwa na siyo kuzoeleka.

Ni wazi kuna mapungufu ya kiutendaji na mambo mengi ambayo hayajibu maswali yetu ndio maana wengine tulitaka maafisa wa juu wa jeshi hilo wang'olewe kwa sababu wameligeuza kuwa ni jeshi la kisiasa sasa. Inapofika watu wanaona jeshi la polisi ni la CCM au lisilo na ule ukaribu wa zamani na wananchi basi ni hatari kwa sababu hawatalipa ushirikiano na wakipata nafasi ya kuwatendea polisi wanawatendea! Mwema, Chagonja na wengine wajuu wanapaswa kuondolewa ili mabadiliko ya kweli ya jeshi yaletwe na watu wenye uwezo. Inapofika watu hawaoni huruma ya mtu kupoteza maisha yake tumefika pabaya.

Hivi mauaji haya yana tofauti gani ya Pro. Mwaikusa? yana tofauti gani na mauaji ya yule Mwanasheria miaka michache iliyopita pale Dar; yana tofauti gani na mauaji wananchi kule Arusha, au Songea? Well.. tofauti ni namna tu lakini ni kuwa wote wamepoteza maisha katika mazingira ambayo hayakupaswa kutokea; ni mazingira ambayo yanahitaji kuchunguzwa na kuondolewa ili isije ikafika mahali huko mbeleni tukasikia Waziri auawa, Mwenyekiti wa Chama cha siasa apigwa risasi au Mbunge auawa au hata iwe yale yale ya Afisa auawa au mwananchii auawa akidhwaniwa ni jambazi!

Hekima inatuita tulaani mauaji haya, kuyapinga na kutaka juhudi zote za kuwaleta kwenye haki zifanyike pasi ya huruma au upendeleo au husuda. Hii haina maana watu tunaridhika na utendaji wea jeshi la polisi. Ushahidi ni mwingi mno kuwa jeshi letu linahitaji mabadilikko ya mfumo (structural reform) ili kulifanya liwe la kisasa zaidi, likijali watu na likiwa linaelewa tunu ya kanuni za demokrasia. Mahitaji ya mabadiliko hayo hayalalishi unyama dhidi ya polisi au raia. Na pamoja na hilo mabadiliko ya msingi yatokee ndani ya jeshi la polisi ili lionekane kweli linajali raia.

Binafsi ninalaani vikali mauaji ya kinyama ya kamanda wa polisi na kutaka haki itendeke kuhakikishwa wahusika wanakutana na mkkono wa sheria. Huwezi kupinga mauaji ya Mwangosi na kutaka haki itendeke halafu ushangilie mauaji ya Kamanda.

Haki ni haki hata ya adui yako ni haki. Mwangosi alikuwa na haki ya kuishi kama vile Barlow alivyokuwa nayo na kama mamia wengine walivyokuwa nayo na ambayo ilikatishwa kinyama. Tusivumilie mauaji ya aina hii kwani yana chochea visasi. Itakuwaje kama polisi nao katika kujihami wanaanza kuua kama mbwa na wananchi wanarudishia kisasi kama wana wazimu?

Litakuwa ni taifa la damu. Damu ambayo isipokataliwa itaendelea kutiririka kama kijito kisichokoma.

Mkuu mwache auwawe and let him go to hellllll huyu si ndo juzi alisema ooooh yule afisa wa uhamiaji aliingia kwenye mtego wa majambazi na akaongeza kuwa ana bahati sana maana sie hatulembi juu ya majambazi na akasema sie ni kuua tu majambazi so sheria gani inaruhusu kuua jambazi?Mie siwaungi mkono kabisa majambazi lakini usemi aliotumia ulikuwa mkali haustahili sheria inasema kamata mwizi peleka mahakamani na si kumuuwa so i can say Goes around comes around au na hata Bible imenena mshahara wa dhambi ni mauti kwanza huyo mwalimu alimtoa wapi na kwa nini Police ampe lift raia wa kawaida mie nafahamu only mhalifu ndio utamkuta kwa gari ya Police hata kama ni Private hata Ulaya Police wanaambiwa wasiwape raia lift.Na huyu huyu kamanda si ndo ameshindwa kuwapeleka waliotaka kuto roho za viongozi na wabunge wa CHADEMA hapo hapo Mwanza so alifikiria yeye hawezi kufa mwacheni aende hellllllllllll ati wawatafute wauaji na wale wauaji wa raia alioshindwa kuwatafuta?Sasa kwa kuwa yeye ni kamanda watu wakamatwe bila utaratibu Lol Bongo imeoza ati kisa kamanda.Ama kweli mkuki kwa Nguruwe..............................!!!!!!
 
kama kweli walomuua ni majambazi, naomba niwape kazi nyingine ya Iringa!
Au wizara ya elimu imuhamishe huyu mwl kwenda Iringa najua Kamuhanda naye atanasa tu! Na ndo utakua mwsho wake.
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu wangu nakuomba sana ufahamu tabia na hulka za binadamu kabla hujahukumu na kitu gani kinatakiwa kufanywa kwanza ili kuondoa nafasi ya mambo yanayoweza kutokea. wazungu wanasema mahala popote ambapo diplomacy imeshindikana basi fahamu ya kwamba upo uwezekano mkubwa wa vita hata kama swala limeanzishwa na mtu mmoja. Iraq ilishambuliwa kwa sababu ya mtu mmoja tu Saadam na walokufa ktk mashambuliszi hayo wameitwa nani Collateral damage. Mtu mmoja anaweza kabisa kuimaliza jamii nzima, hivyo hekima huanza na watu wenyewe kutofundishana shari.

Binafsi yangu husema kama kuna uwezekano wa kuepusha shari Je, kuna sababu gani ya kupuuza UPENDO lakini tuwe wepesi wa kulaani matokeo wakati mbegu tulizopanda ndizo chanzo na sababu ya matokeo hayo?. Kwa nini tusijifunze kutopanda mbegu chafu ambazo matokeo yake ndio haya..Hivi kweli wewe na wengineo mlitegemea Polisi wanaweza kuua na tukawalaani kwa maneno lakini wananchi wataendelea kuvumilia kuona mauaji yakiendelea na jeshi letu likijenga Chuki na uadui baina yake na wananchi?..

Kosa la kamuhanda linaweza kabisa kuchukua sura mpya ni lazima tujifunze haya, na hivyo kosa la mtoto alokojolea Msahafu linaweza kabisa kuzua vita baina ya Waislaam na Wakristu, kosa la Chadema linaweza kuzua vurugu kubwa baina ya wanachama wa CCM ana Chadema na kosa la Chadema linaweza kuzua vifo vya raia wengine wengi..

La muhimu kwetu sisi ni kujiuliza kama kuna umuhimu wa kuendeleza vitendo vyovyote kwa gharama hizi kubwa ambazo zinajenga chuki baina yetu. Kuna tatizo gani kwa serikali yetu, viongozi wa vyama na serikali na dini kufundisha UPENDO?.. kwa nini kila unapokwenda nchini siasa ni za CHUKI tu.. aidha viongozi kutupiwa mawe, makanisani na misikitini hakuna mafundisho ya upendo isipokuwa upande wa pili ni watu gani. Ukienda Msikitini Hotuba hazizungumzii hadithi za mtume isipokuwa SIASA za chuki, Ukienda makanisani vile vile, Ofisi za CCM na Vijana ni jinsi ya kuwasambaratisha Chadema. CUF ni Uzanzibar dhidi ya bara, JF ni waislaam against wakristu, CCM against Chadema, CUF agaisnt Chadema tena kwa matusi mazito mazito. Hi kweli ndio demokraisa au tunafanya madudu mengine?..Kweli mnategemea kuwepo na AMANI?..

Leo hii katika vyama vyetu wachungaji ndio wanagombea Ubunge, I mean mkuu wangu unategemea nini kutoka kwa mchungaji anayekwenda kanisani kufundisha dini wakati ni mwanasiasa mgombea Ubunge wa jimbo lake?.. halafu tunasema nchi yetu haina dini! huyu ni mbunge ambaye kuna uwezekano mkubwa akawa Waziri kama chama chake kitaingia madarakani..Kwa nini asiache kwanza Uchungaji kama alivyofanya Dr.Slaa na kujishughulisha na siasa lakini unakuta mtu anagombea Uongoz huku akifundisha Gospel makanisani na hata ktk majukwaa ya siasa. jamani tunatafuta nini kama sio kuitaka shari sisi wenyewe?..

mambo mengine jamani sina haja ya kuyazungumza sana lakini ukweli unabakia kwamba sisi wenyewe tunafundisha a chuki, sisi wenyewe ndio tunaochochea hizi CHUKI na HuSUDA ktk mfumo mzima wa siasa zetu na Utawala. Maana sioni tatizo kabisa kwa Polisi nchini kuwalinda wananchi kama walivyoapa badala yake wananchi ndio wanakuwa maadui zao kwa makosa yalofanywa na viongozi wao halafu tutegemee watu watakaa kimya tu....
Mkandara umenifurahisha kwa uchambuzi wako ingawa unaelekea kuchukizwa na udini lakini ww yaelekea ni mdini sana, au labda c mwelewa mambo ya wengine hv mtu mwenye akili timamu atasemaje mchungaji aache uchungaji ndo akawe mwanasiasa? hujui uchungaji ni cheo kama dr, prof,alhaj, nk baada ya kuhitimu mafunzo ya uchungaji? We unaweza sema mtu aache ulhaji ndo akawe mwanasiasa? Title za watu zisitusumbue, cha kujiuliza je anachapa kazi? tujadili hoja ya MMK tuache udini.
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu wangu nakuomba sana ufahamu tabia na hulka za binadamu kabla hujahukumu na kitu gani kinatakiwa kufanywa kwanza ili kuondoa nafasi ya mambo yanayoweza kutokea. wazungu wanasema mahala popote ambapo diplomacy imeshindikana basi fahamu ya kwamba upo uwezekano mkubwa wa vita hata kama swala limeanzishwa na mtu mmoja. Iraq ilishambuliwa kwa sababu ya mtu mmoja tu Saadam na walokufa ktk mashambuliszi hayo wameitwa nani Collateral damage. Mtu mmoja anaweza kabisa kuimaliza jamii nzima, hivyo hekima huanza na watu wenyewe kutofundishana shari.

Binafsi yangu husema kama kuna uwezekano wa kuepusha shari Je, kuna sababu gani ya kupuuza UPENDO lakini tuwe wepesi wa kulaani matokeo wakati mbegu tulizopanda ndizo chanzo na sababu ya matokeo hayo?. Kwa nini tusijifunze kutopanda mbegu chafu ambazo matokeo yake ndio haya..Hivi kweli wewe na wengineo mlitegemea Polisi wanaweza kuua na tukawalaani kwa maneno lakini wananchi wataendelea kuvumilia kuona mauaji yakiendelea na jeshi letu likijenga Chuki na uadui baina yake na wananchi?..

Kosa la kamuhanda linaweza kabisa kuchukua sura mpya ni lazima tujifunze haya, na hivyo kosa la mtoto alokojolea Msahafu linaweza kabisa kuzua vita baina ya Waislaam na Wakristu, kosa la Chadema linaweza kuzua vurugu kubwa baina ya wanachama wa CCM ana Chadema na kosa la Chadema linaweza kuzua vifo vya raia wengine wengi..

La muhimu kwetu sisi ni kujiuliza kama kuna umuhimu wa kuendeleza vitendo vyovyote kwa gharama hizi kubwa ambazo zinajenga chuki baina yetu. Kuna tatizo gani kwa serikali yetu, viongozi wa vyama na serikali na dini kufundisha UPENDO?.. kwa nini kila unapokwenda nchini siasa ni za CHUKI tu.. aidha viongozi kutupiwa mawe, makanisani na misikitini hakuna mafundisho ya upendo isipokuwa upande wa pili ni watu gani. Ukienda Msikitini Hotuba hazizungumzii hadithi za mtume isipokuwa SIASA za chuki, Ukienda makanisani vile vile, Ofisi za CCM na Vijana ni jinsi ya kuwasambaratisha Chadema. CUF ni Uzanzibar dhidi ya bara, JF ni waislaam against wakristu, CCM against Chadema, CUF agaisnt Chadema tena kwa matusi mazito mazito. Hi kweli ndio demokraisa au tunafanya madudu mengine?..Kweli mnategemea kuwepo na AMANI?..

Leo hii katika vyama vyetu wachungaji ndio wanagombea Ubunge, I mean mkuu wangu unategemea nini kutoka kwa mchungaji anayekwenda kanisani kufundisha dini wakati ni mwanasiasa mgombea Ubunge wa jimbo lake?.. halafu tunasema nchi yetu haina dini! huyu ni mbunge ambaye kuna uwezekano mkubwa akawa Waziri kama chama chake kitaingia madarakani..Kwa nini asiache kwanza Uchungaji kama alivyofanya Dr.Slaa na kujishughulisha na siasa lakini unakuta mtu anagombea Uongoz huku akifundisha Gospel makanisani na hata ktk majukwaa ya siasa. jamani tunatafuta nini kama sio kuitaka shari sisi wenyewe?..

mambo mengine jamani sina haja ya kuyazungumza sana lakini ukweli unabakia kwamba sisi wenyewe tunafundisha a chuki, sisi wenyewe ndio tunaochochea hizi CHUKI na HuSUDA ktk mfumo mzima wa siasa zetu na Utawala. Maana sioni tatizo kabisa kwa Polisi nchini kuwalinda wananchi kama walivyoapa badala yake wananchi ndio wanakuwa maadui zao kwa makosa yalofanywa na viongozi wao halafu tutegemee watu watakaa kimya tu....
Hongera sana mkuu Mkandara, kweli kabisa yanayotokea sana ni mazao ya mbegu mbaya ya chuki iliyopandwa kwanza na jeshi la polisi lenyewe. Mara ngapi tumesikia polisi wakipongezana na kutoa taarifa za hovyo kabisa, eti polisi wamefanikiwa kuwa ua majambazi kadhaa! ni nani huwa amethibitisha kwamba waliouawa huwa kweli ni majambazi? kumbuka hata wale wafanya biashara wa madini waliouawa na akina Zombe pale Dar mara ya kwanza kabla ya uchunguzi waliitwa majambazi!
 
MM tumepata taarifa kumbe alikuwa na mke wa mtu,ilikuwa ni halali yake kutwangwa lirisasi la shingo,Mungu analipiza kwa njia nyingi sana na tunaomba kwa nguvu zote yule wa iringa naye yamkute mabaya kuliko haya

Huna aibu kuongea uongo hadharani? Toa ushaidi mke wa nani? Mzee Mwanakijiji umetoa analysis nzuri sana. Je twalipeleka wapi taifa letu na utu wetu?
 
Hivi kuna uhusiano wa hii kitu na hile ya afisa uhamiaji.. hapo Mwanza?

kuna habari bado nafuatilia hapa, maana huyu kamanda alikuwa ni miongoni mwa makamanda wachache weledi na waliokuwa na ushirikiano mzuri na CDM, Ukweli utajulikana tu lets be patient for a while! issue hii inataka kufanana na ile ya kamanda kombe kipindi kile cha lyatonga
 
Nimesema juzi kuwa ukosefu wa hekima ni janga kubwa la kitaifa kwa kweli nilimaanisha hilo. Tangu habari za mauaji ya Kamanda Barlow yalipotokea mwitikio wa watu wengi umekuwa ni kutokujali, kuhalalisha na hata kushangilia ni kama mtu kusema "akome". Wengi wanahalalisha hili kwa sababu wanaamini ujumbe umetumwa kwa polisi na kuwa polisi 'wanaua watu na sasa kimewarudia'.

Mauaji ya Barlow kama yalaivyokuwa mauaji ya Mwangosi na ya wananchi wengine wengi yanapaswa kulaaniwa na siyo kuhalalishwa, yanastahili kupingwa na siyo kutetewa na yanahitaji kukataliwa na siyo kuzoeleka.

Nakubaliana nawe kwa hoja ya msingi kwamba si vema kuchukua sheria mkononi kwa namna yoyote ile bila kujali jinsi, cheo au nafasi katika jamii.

Lakini hata ukiwalaani hawa wanaoshangilia ni kulaani kilele cha tatizo badala ya kulaani chanzo.
Chanzo kikuu au kiini cha tatizo ni kufa au kushindwa kwa mfumo wa sheria hapa nchini. Leo hii mtu mwenye madaraka anajiona yupo huru kufanya chochote hata kama anavunja sheria kwa sababu anajua hakuna hatua zozote zitakazochukuliwa dhidi yake.

Katika mazingira kama hayo Je unafikiri kama ni kweli kama inavyohisiwa kwamba mauaji yanahusiana na wivu wa kuibiwa mke, je huyo mwenye mke alikuwa na nafasi ya kupata haki mbele ya mfumo wetu wa sheria?.

Waliofanya maovu dhidi ya Ulimboka na Mwangosi kwa kiasi kikubwa wanajulikana na hadi sasa wapo huru, ni kipi kitafanya hali iwe tofauti kwa Barlow?.

Iwapo tuhuma kwamba ''alikuwa anakula mali ya mtu'' ni kweli,basi mauaji yanaweza kuwa yamefanyika kwa sababu kuu mbili.

Sababu ya kwanza ni ya kibinadamu kama walivyo wanyama wengine,iwe ni simba, kuku, au panya bila kujali ukubwa wa mnyama huwa hawapendi kuingiliwa. Wakiingiliwa kwenye himaya yao watapambana hadi kufa au kuua.

Sababu ya pili ni ya mazingira ya sasa ya mfumo wa sheria ambao hutoa haki kwa kuangalia madaraka na fedha bali badala ya kutoa haki kwa kila mtu.

Sababu ya kwanza inaweza kuzuilika kwa 'busara za kibinadamu'' kwa vile binadamu yupo tofauti kidogo na wanyama wengine, lakini hiyo itategemea na jinsi mtu anavyoweza kuhimili kishindo cha athari za kisaikolojia.

Sababu ya pili iko nje ya uwezo wa mtu mmoja mmoja, inahitaji nguvu ya pamoja.

Mwisho: Siungi mkono mauaji ya raia yeyote.

Hata hivyo naungana na wale wanaofikiri kwamba pengine Mola ameamua kutoa somo kupitia kwa kamanda huyu ili kuwaamsha watawala na kusikia kilio cha wengi juu ya ukandamizaji hata kama tuhuma dhidi yake si za kweli.
 
Totafautishe vitu viwili: Kuhuzunishwa na Kufurahishwa. Mimi Sijafurahishwa na kifo cha Kamanda lakini Pia Sijahuzunika

Hivi RPC si wanapaswa kutembea na ulinzi? Walinzi wake walikuwa wapi?

RIP
 
Back
Top Bottom