Hekima inapoita: Mauaji ya Barlow yanahitaji kulaaniwa, kukataliwa na yanalia "haki"

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Nimesema juzi kuwa ukosefu wa hekima ni janga kubwa la kitaifa kwa kweli nilimaanisha hilo. Tangu habari za mauaji ya Kamanda Barlow yalipotokea mwitikio wa watu wengi umekuwa ni kutokujali, kuhalalisha na hata kushangilia ni kama mtu kusema "akome". Wengi wanahalalisha hili kwa sababu wanaamini ujumbe umetumwa kwa polisi na kuwa polisi 'wanaua watu na sasa kimewarudia'. Kauli hizi ndizo zinazothibitisha ukosefu wa hii hekima.Tumeshuhudia kosa la mtoto mmoja kwenda kuhukumiwa makanisa na wakristu; leo kosa la Kamuhanda anahukumiwa Barlow? Leo hii kosa la askari mmoja wanalaumiwa jeshi zima kiasi kwamba leo chochote kitakachompata polisi tunafurahia?

Ni lazima tujifunze kuwa na hekima ya kutofautisha kitu kinachoitwa "collective punishment" kwamba tunaadhibu wote kwa kosa la mmoja. Labda ni kwa sababu tunaamini (bila kufikiria sana) kuwa "samaki mmoja akioza wameoza wote". Ukweli ni kuwa samaki mmoja akioza siyo wote wameoza!

Kamanda Barlow ahukumiwe kwa matendo yake mwenyewe na si matendo ya wengine. Je alikuwa ni kamanda mzuri kwa polisi, je alisimamia haki na utawala wa kisheria kwa kadiri ya uwezo wake (yaani pamoja na mapungufu yake kama alivyoshughulikia hili la koswakoswa la afisa)? Je kuwa dhaifu kiutendaji adhabu yake ni mauti?

Tuna tofauti gani basi na wale ambao wanaona mtu anapigwa na watu kwa sababu kadaiwa ni 'kibaka' na wao bila kuuliza wanachukua jiwe na kurusha au wanauliza "lete petroli" halafu wanaondoka zao huku nyuma mtu anatiwa kiberiti? Tuna tofauti gani na jamii isiyoerevuka ambayo haitaki kutafuta ukweli inaishi kwa imani na hisia tu?

Mauaji ya Barlow kama yalaivyokuwa mauaji ya Mwangosi na ya wananchi wengine wengi yanapaswa kulaaniwa na siyo kuhalalishwa, yanastahili kupingwa na siyo kutetewa na yanahitaji kukataliwa na siyo kuzoeleka.

Ni wazi kuna mapungufu ya kiutendaji na mambo mengi ambayo hayajibu maswali yetu ndio maana wengine tulitaka maafisa wa juu wa jeshi hilo wang'olewe kwa sababu wameligeuza kuwa ni jeshi la kisiasa sasa. Inapofika watu wanaona jeshi la polisi ni la CCM au lisilo na ule ukaribu wa zamani na wananchi basi ni hatari kwa sababu hawatalipa ushirikiano na wakipata nafasi ya kuwatendea polisi wanawatendea! Mwema, Chagonja na wengine wajuu wanapaswa kuondolewa ili mabadiliko ya kweli ya jeshi yaletwe na watu wenye uwezo. Inapofika watu hawaoni huruma ya mtu kupoteza maisha yake tumefika pabaya.

Hivi mauaji haya yana tofauti gani ya Pro. Mwaikusa? yana tofauti gani na mauaji ya yule Mwanasheria miaka michache iliyopita pale Dar; yana tofauti gani na mauaji wananchi kule Arusha, au Songea? Well.. tofauti ni namna tu lakini ni kuwa wote wamepoteza maisha katika mazingira ambayo hayakupaswa kutokea; ni mazingira ambayo yanahitaji kuchunguzwa na kuondolewa ili isije ikafika mahali huko mbeleni tukasikia Waziri auawa, Mwenyekiti wa Chama cha siasa apigwa risasi au Mbunge auawa au hata iwe yale yale ya Afisa auawa au mwananchii auawa akidhwaniwa ni jambazi!

Hekima inatuita tulaani mauaji haya, kuyapinga na kutaka juhudi zote za kuwaleta kwenye haki zifanyike pasi ya huruma au upendeleo au husuda. Hii haina maana watu tunaridhika na utendaji wea jeshi la polisi. Ushahidi ni mwingi mno kuwa jeshi letu linahitaji mabadilikko ya mfumo (structural reform) ili kulifanya liwe la kisasa zaidi, likijali watu na likiwa linaelewa tunu ya kanuni za demokrasia. Mahitaji ya mabadiliko hayo hayalalishi unyama dhidi ya polisi au raia. Na pamoja na hilo mabadiliko ya msingi yatokee ndani ya jeshi la polisi ili lionekane kweli linajali raia.

Binafsi ninalaani vikali mauaji ya kinyama ya kamanda wa polisi na kutaka haki itendeke kuhakikishwa wahusika wanakutana na mkkono wa sheria. Huwezi kupinga mauaji ya Mwangosi na kutaka haki itendeke halafu ushangilie mauaji ya Kamanda.

Haki ni haki hata ya adui yako ni haki. Mwangosi alikuwa na haki ya kuishi kama vile Barlow alivyokuwa nayo na kama mamia wengine walivyokuwa nayo na ambayo ilikatishwa kinyama. Tusivumilie mauaji ya aina hii kwani yana chochea visasi. Itakuwaje kama polisi nao katika kujihami wanaanza kuua kama mbwa na wananchi wanarudishia kisasi kama wana wazimu?

Litakuwa ni taifa la damu. Damu ambayo isipokataliwa itaendelea kutiririka kama kijito kisichokoma.
 
nadhani kwakuwa ni yeye tofauti na wananchi wengine basi watatafutwa hata mbuzi wa kafara wafungwe jela.

Hilo nalo halikubaliki; na polisi wakifanya hivyo tutawapinga vile vile. Ndio maana tunasema haki ni haki hata ya adui yako ni haki. Polisi wanawajibu wa kuwatafuta wahusika. Tukihalalisha hili yatatokea kama yale yaliyokuwa yanatokea zamani (labda siyo zamai sana) na JWTZ ambapo askari wao akipigwa na rais kikosi kinakuja na kufunga mtaa na kupiga wananchi wote kuwakomoa! Sasa leo polisi wakishuka Kitangiri na kuanz akupiga watu ili "wawataje wahusika" tutasema ni haki kwa vile wanalipiza afisa wao kuuawa na raia?
 
Mkuu MMM,

Rules of the game ndio zimepelekea faulo nyingi hata kwenye jambo la utu/uhai kama hili. Wao (polisi) badala ya kusitkitka au kutoa taarifa zenye kuonesha wanajali au kuthamini uhai wa raia wanapokufa mara nyingi wamekuwa wanafanya "dhihaka" kwa matamko yao mepesi tena yenye udanganyifu na ghiliba lukuki.

HATA HIVYO nakubali rai yako, kwamba hakuna uhalali wa kufurahia kifo cha Barlow. Kama jamii ni lazima tuchore mstari/mpaka ktk mambo kama haya.

TWO WRONGS NEVER MAKE ONE RIGHT
 
Nimesema juzi kuwa ukosefu wa hekima ni janga kubwa la kitaifa kwa kweli nilimaanisha hilo. Tangu habari za mauaji ya Kamanda Barlow yalipotokea mwitikio wa watu wengi umekuwa ni kutokujali, kuhalalisha na hata kushangilia ni kama mtu kusema "akome". Wengi wanahalalisha hili kwa sababu wanaamini ujumbe umetumwa kwa polisi na kuwa polisi 'wanaua watu na sasa kimewarudia'. Kauli hizi ndizo zinazothibitisha ukosefu wa hii hekima.Tumeshuhudia kosa la mtoto mmoja kwenda kuhukumiwa makanisa na wakristu; leo kosa la Kamuhanda anahukumiwa Barlow? Leo hii kosa la askari mmoja wanalaumiwa jeshi zima kiasi kwamba leo chochote kitakachompata polisi tunafurahia?

Ni lazima tujifunze kuwa na hekima ya kutofautisha kitu kinachoitwa "collective punishment" kwamba tunaadhibu wote kwa kosa moja. Labda ni kwa sababu tunaamini (bila kufikiria sana) kuwa "samaki mmoja akioza wameoza wote". Ukweli ni kuwa samaki mmoja akioza siyo wote wameoza!

Kamanda Barlow ahukumiwe kwa matendo yake mwenyewe na si matendo ya wengine. Je alikuwa ni kamanda mzuri kwa polisi, je alisimamia haki na utawala wa kisheria kwa kadiri ya uwezo wake (yaani pamoja na mapungufu yake kama alivyoshughulikia hili la koswakoswa la afisa)? Je kuwa dhaifu kiutendaji adhabu yake ni mauti?

Tuna tofauti gani basi na wale ambao wanaona mtu anapigwa na watu kwa sababu kadaiwa ni 'kibaka' na wao bila kuuliza wanachukua jiwe na kurusha au wanauliza "lete petroli" halafu wanaondoka zao huku nyuma mtu anatiwa kiberiti? Tuna tofauti gani na jamii isiyoerevuka ambayo haitaki kutafuta ukweli inaishi kwa imani na hisia tu?

Mauaji ya Barlow kama yalaivyokuwa mauaji ya Mwangosi na ya wananchi wengine wengi yanapaswa kulaaniwa na siyo kuhalalishwa, yanastahili kupingwa na siyo kutetewa na yanahitaji kukataliwa na siyo kuzoeleka.

Ni wazi kuna mapungufu ya kiutendaji na mambo mengi ambayo hayajibu maswali yetu ndio maana wengine tulitaka maafisa wa juu wa jeshi hilo wang'olewe kwa sababu wameligeuza kuwa ni jeshi la kisiasa sasa. Inapofika watu wanaona jeshi la polisi ni la CCM au lisilo na ule ukaribu wa zamani na wananchi basi ni hatari kwa sababu hawatalipa ushirikiano na wakipata nafasi ya kuwatendea polisi wanawatendea! Mwema, Chagonja na wengine wajuu wanapaswa kuondolewa ili mabadiliko ya kweli ya jeshi yaletwe na watu wenye uwezo. Inapofika watu hawaoni huruma ya mtu kupoteza maisha yake tumefika pabaya.

Hivi mauaji haya yana tofauti gani ya Pro. Mwaikusa? yana tofauti gani na mauaji ya yule Mwanasheria miaka michache iliyopita pale Dar; yana tofauti gani na mauaji wananchi kule Arusha, au Songea? Well.. tofauti ni namna tu lakini ni kuwa wote wamepoteza maisha katika mazingira ambayo hayakupaswa kutokea; ni mazingira ambayo yanahitaji kuchunguzwa na kuondolewa ili isije ikafika mahali huko mbeleni tukasikia Waziri auawa, Mwenyekiti wa Chama cha siasa apigwa risasi au Mbunge auawa au hata iwe yale yale ya Afisa auawa au mwananchii auawa akidhwaniwa ni jambazi!

Hekima inatuita tulaani mauaji haya, kuyapinga na kutaka juhudi zote za kuwaleta kwenye haki zifanyike pasi ya huruma au upendeleo au husuda. Na pamoja na hilo mabadiliko ya msingi yatokee ndani ya jeshi la polisi ili lionekane kweli linajali raia. Binafsi ninalaani vikali mauaji ya kinyama ya kamanda wa polisi na kutaka haki itendeke kuhakikishwa wahusika wanakutana na mkkono wa sheria. Huwezi kupinga mauaji ya Mwangosi na kutaka haki itendeke halafu ushangilie mauaji ya Kamanda.

Haki ni haki hata ya adui yako ni haki. Mwangosi alivyokuwa na haki ya kuisha kama vile Barlow alivyokuwa nayo na kama mamia wengine walivyokuwa nayo na ambayo ilikatishwa kinyama. Tusivumilie mauaji ya aina hii kwani yana chochea visasi. Itakuwaje kama polisi nao katika kujihami wanaanza kuua kama mbwa na wananchi wanarudishia kisasi kama wana wazimu?

Litakuwa ni taifa la damu.
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu wangu nakuomba sana ufahamu tabia na hulka za binadamu kabla hujahukumu na kitu gani kinatakiwa kufanywa kwanza ili kuondoa nafasi ya mambo yanayoweza kutokea. wazungu wanasema mahala popote ambapo diplomacy imeshindikana basi fahamu ya kwamba upo uwezekano mkubwa wa vita hata kama swala limeanzishwa na mtu mmoja. Iraq ilishambuliwa kwa sababu ya mtu mmoja tu Saadam na walokufa ktk mashambuliszi hayo wameitwa nani Collateral damage. Mtu mmoja anaweza kabisa kuimaliza jamii nzima, hivyo hekima huanza na watu wenyewe kutofundishana shari.

Binafsi yangu husema kama kuna uwezekano wa kuepusha shari Je, kuna sababu gani ya kupuuza UPENDO lakini tuwe wepesi wa kulaani matokeo wakati mbegu tulizopanda ndizo chanzo na sababu ya matokeo hayo?. Kwa nini tusijifunze kutopanda mbegu chafu ambazo matokeo yake ndio haya..Hivi kweli wewe na wengineo mlitegemea Polisi wanaweza kuua na tukawalaani kwa maneno lakini wananchi wataendelea kuvumilia kuona mauaji yakiendelea na jeshi letu likijenga Chuki na uadui baina yake na wananchi?..

Kosa la kamuhanda linaweza kabisa kuchukua sura mpya ni lazima tujifunze haya, na hivyo kosa la mtoto alokojolea Msahafu linaweza kabisa kuzua vita baina ya Waislaam na Wakristu, kosa la Chadema linaweza kuzua vurugu kubwa baina ya wanachama wa CCM ana Chadema na kosa la Chadema linaweza kuzua vifo vya raia wengine wengi..

La muhimu kwetu sisi ni kujiuliza kama kuna umuhimu wa kuendeleza vitendo vyovyote kwa gharama hizi kubwa ambazo zinajenga chuki baina yetu. Kuna tatizo gani kwa serikali yetu, viongozi wa vyama na serikali na dini kufundisha UPENDO?.. kwa nini kila unapokwenda nchini siasa ni za CHUKI tu.. aidha viongozi kutupiwa mawe, makanisani na misikitini hakuna mafundisho ya upendo isipokuwa upande wa pili ni watu gani. Ukienda Msikitini Hotuba hazizungumzii hadithi za mtume isipokuwa SIASA za chuki, Ukienda makanisani vile vile, Ofisi za CCM na Vijana ni jinsi ya kuwasambaratisha Chadema. CUF ni Uzanzibar dhidi ya bara, JF ni waislaam against wakristu, CCM against Chadema, CUF agaisnt Chadema tena kwa matusi mazito mazito. Hi kweli ndio demokraisa au tunafanya madudu mengine?..Kweli mnategemea kuwepo na AMANI?..

Leo hii katika vyama vyetu wachungaji ndio wanagombea Ubunge, I mean mkuu wangu unategemea nini kutoka kwa mchungaji anayekwenda kanisani kufundisha dini wakati ni mwanasiasa mgombea Ubunge wa jimbo lake?.. halafu tunasema nchi yetu haina dini! huyu ni mbunge ambaye kuna uwezekano mkubwa akawa Waziri kama chama chake kitaingia madarakani..Kwa nini asiache kwanza Uchungaji kama alivyofanya Dr.Slaa na kujishughulisha na siasa lakini unakuta mtu anagombea Uongoz huku akifundisha Gospel makanisani na hata ktk majukwaa ya siasa. jamani tunatafuta nini kama sio kuitaka shari sisi wenyewe?..

mambo mengine jamani sina haja ya kuyazungumza sana lakini ukweli unabakia kwamba sisi wenyewe tunafundisha a chuki, sisi wenyewe ndio tunaochochea hizi CHUKI na HuSUDA ktk mfumo mzima wa siasa zetu na Utawala. Maana sioni tatizo kabisa kwa Polisi nchini kuwalinda wananchi kama walivyoapa badala yake wananchi ndio wanakuwa maadui zao kwa makosa yalofanywa na viongozi wao halafu tutegemee watu watakaa kimya tu....
 
Mheshimiwa mwanakijiji heshima kwako kwa uchambuzi uliotukuka lakini mzee mwanakiji jamii yetu saizi ndio imefikia hapo anakojolea KORAN mtoto wa dhehebu jingine yanachomwa makanisa ya dhehebu mengine sasa Mzee mwanakijiji labda wewe hujaona picha ya huyo mwl.ambayo alikwa na kamanda mtoto katokelezea kweli kamanda amekufa kishujaaa!!!!!!!!!
 
Mzee Mwanakijiji ukweli ni kwamba si jambo la kawaida binadamu kufuraahia kifo cha binadamu mwezake.
Lakini sisi wenyewe ndio tumefikishana mahali ambapo kuna watu wakifa ama wakiuwawa wengine tunashangilia kama si kufurahia kimoyomoyo. Hata hizi tabia za kuwapiga na kuwachoma moto vibaka ni matokeo ya watu waliopewa mamlaka ya kulinda sheria kushindwa kufanya hivyo, kwahiyo wananchi wanaamua kujichukulia sheria mikononi.

Kumekuwepo na matukio mengi ya jeshi la polisi kuwapiga raia wasio na hatia, kuwatesa, kuwabambikia kesi na kuwafanyia kila aina ya manyanyaso lakini wananchi hawaoni hatua madhubuti zikichukuliwa na wenye mamlaka wakiwadabisha askari polisi wanaokiuka haki za kiraia kwahiyo wanaamini kwamba hao wakubwa ndio wanawatuma kutekeleza ushenzi wanaofanyiwa.

Kwahiyo kitendo cha wananchi kutosikitishwa kabisa na kifo hiki, na wengine wanafurahia kifo hiki ni matokeo ya ulegevu wa watawala, kwa kushindwa kusimamia japo sheria tulizonazo, imefika mahala nchi hii imegawanyika matabaka, kuna wale wachache walio juu ya sheria na hawa ni wale wenye vyeo vya juu serikalini na chama tawala, na kuna tabaka la wengi la wananchi wanyonge ndilo liko chini ya sheria na manyanyaso.

Kibinadamu hata mimi nasikitika kwa kifo cha kamanda Barlow lakini kwa kutazama uhalisia wa mambo siwezi kuwalaumu kabisa watanzania kwa reaction zao juu ya kifo hiki. Ni muhimu sana wakuu wa nchi pamoja na jeshi la polisi wajifunze kwa tukio hili, ili kuanzia hapa waweze kujitathmini na kufanya marekebisho/mabadiliko muhimu kwa ajili ya jeshi la polisi ili kujaribu kurejesha uhusiano mwema baina ya polisi na wananchi kwakuwa pande zote mbili zinahitajiana, kwahiyo mahusiano mema baina yao ni jambo la lazima kwa mustakabali mwema wa nchi hii.
 
Last edited by a moderator:
MM tumepata taarifa kumbe alikuwa na mke wa mtu,ilikuwa ni halali yake kutwangwa lirisasi la shingo,Mungu analipiza kwa njia nyingi sana na tunaomba kwa nguvu zote yule wa iringa naye yamkute mabaya kuliko haya
 
Mzee Mwanakijiji mimi siongezi neno. Maana kuna watu wametoa maneno ya ajabu kabisa hadi unaanza kuhoji utu wao uko kwenye nini hasa!!
 
Last edited by a moderator:
Nimesema juzi kuwa ukosefu wa hekima ni janga kubwa la kitaifa kwa kweli nilimaanisha hilo. Tangu habari za mauaji ya Kamanda Barlow yalipotokea mwitikio wa watu wengi umekuwa ni kutokujali, kuhalalisha na hata kushangilia ni kama mtu kusema "akome". Wengi wanahalalisha hili kwa sababu wanaamini ujumbe umetumwa kwa polisi na kuwa polisi 'wanaua watu na sasa kimewarudia'. Kauli hizi ndizo zinazothibitisha ukosefu wa hii hekima.Tumeshuhudia kosa la mtoto mmoja kwenda kuhukumiwa makanisa na wakristu; leo kosa la Kamuhanda anahukumiwa Barlow? Leo hii kosa la askari mmoja wanalaumiwa jeshi zima kiasi kwamba leo chochote kitakachompata polisi tunafurahia?

Ni lazima tujifunze kuwa na hekima ya kutofautisha kitu kinachoitwa "collective punishment" kwamba tunaadhibu wote kwa kosa la mmoja. Labda ni kwa sababu tunaamini (bila kufikiria sana) kuwa "samaki mmoja akioza wameoza wote". Ukweli ni kuwa samaki mmoja akioza siyo wote wameoza!

Kamanda Barlow ahukumiwe kwa matendo yake mwenyewe na si matendo ya wengine. Je alikuwa ni kamanda mzuri kwa polisi, je alisimamia haki na utawala wa kisheria kwa kadiri ya uwezo wake (yaani pamoja na mapungufu yake kama alivyoshughulikia hili la koswakoswa la afisa)? Je kuwa dhaifu kiutendaji adhabu yake ni mauti?

Tuna tofauti gani basi na wale ambao wanaona mtu anapigwa na watu kwa sababu kadaiwa ni 'kibaka' na wao bila kuuliza wanachukua jiwe na kurusha au wanauliza "lete petroli" halafu wanaondoka zao huku nyuma mtu anatiwa kiberiti? Tuna tofauti gani na jamii isiyoerevuka ambayo haitaki kutafuta ukweli inaishi kwa imani na hisia tu?

Mauaji ya Barlow kama yalaivyokuwa mauaji ya Mwangosi na ya wananchi wengine wengi yanapaswa kulaaniwa na siyo kuhalalishwa, yanastahili kupingwa na siyo kutetewa na yanahitaji kukataliwa na siyo kuzoeleka.

Ni wazi kuna mapungufu ya kiutendaji na mambo mengi ambayo hayajibu maswali yetu ndio maana wengine tulitaka maafisa wa juu wa jeshi hilo wang'olewe kwa sababu wameligeuza kuwa ni jeshi la kisiasa sasa. Inapofika watu wanaona jeshi la polisi ni la CCM au lisilo na ule ukaribu wa zamani na wananchi basi ni hatari kwa sababu hawatalipa ushirikiano na wakipata nafasi ya kuwatendea polisi wanawatendea! Mwema, Chagonja na wengine wajuu wanapaswa kuondolewa ili mabadiliko ya kweli ya jeshi yaletwe na watu wenye uwezo. Inapofika watu hawaoni huruma ya mtu kupoteza maisha yake tumefika pabaya.

Hivi mauaji haya yana tofauti gani ya Pro. Mwaikusa? yana tofauti gani na mauaji ya yule Mwanasheria miaka michache iliyopita pale Dar; yana tofauti gani na mauaji wananchi kule Arusha, au Songea? Well.. tofauti ni namna tu lakini ni kuwa wote wamepoteza maisha katika mazingira ambayo hayakupaswa kutokea; ni mazingira ambayo yanahitaji kuchunguzwa na kuondolewa ili isije ikafika mahali huko mbeleni tukasikia Waziri auawa, Mwenyekiti wa Chama cha siasa apigwa risasi au Mbunge auawa au hata iwe yale yale ya Afisa auawa au mwananchii auawa akidhwaniwa ni jambazi!

Hekima inatuita tulaani mauaji haya, kuyapinga na kutaka juhudi zote za kuwaleta kwenye haki zifanyike pasi ya huruma au upendeleo au husuda. Hii haina maana watu tunaridhika na utendaji wea jeshi la polisi. Ushahidi ni mwingi mno kuwa jeshi letu linahitaji mabadilikko ya mfumo (structural reform) ili kulifanya liwe la kisasa zaidi, likijali watu na likiwa linaelewa tunu ya kanuni za demokrasia. Mahitaji ya mabadiliko hayo hayalalishi unyama dhidi ya polisi au raia. Na pamoja na hilo mabadiliko ya msingi yatokee ndani ya jeshi la polisi ili lionekane kweli linajali raia.

Binafsi ninalaani vikali mauaji ya kinyama ya kamanda wa polisi na kutaka haki itendeke kuhakikishwa wahusika wanakutana na mkkono wa sheria. Huwezi kupinga mauaji ya Mwangosi na kutaka haki itendeke halafu ushangilie mauaji ya Kamanda.

Haki ni haki hata ya adui yako ni haki. Mwangosi alikuwa na haki ya kuishi kama vile Barlow alivyokuwa nayo na kama mamia wengine walivyokuwa nayo na ambayo ilikatishwa kinyama. Tusivumilie mauaji ya aina hii kwani yana chochea visasi. Itakuwaje kama polisi nao katika kujihami wanaanza kuua kama mbwa na wananchi wanarudishia kisasi kama wana wazimu?

Litakuwa ni taifa la damu. Damu ambayo isipokataliwa itaendelea kutiririka kama kijito kisichokoma.
Mwanakijiji ni kweli Kabisa. Ndg zetu wa Roman Catholic wanawimbo unasema....Bwana Kama wewe ungehesabu maovu yetu, nani angesimama, nani angesimama, nani angesimama mbele yako.... Taifa haliwezi kuendelea hivi, hatujui yatamkuta nani Kesho.

Sio mambo ya kushangilia haya hata kidogo!. Bado naamini TZ ni kisiwa cha AMANI na Mungu atusaidie na kutulinda. Tuliombee Taifa letu, damu zisiendelee kudai damu ktk ardhi, wana maombi mmenielewa naamini.

Queen Esther
 
Hilo nalo halikubaliki; na polisi wakifanya hivyo tutawapinga vile vile. Ndio maana tunasema haki ni haki hata ya adui yako ni haki. Polisi wanawajibu wa kuwatafuta wahusika. Tukihalalisha hili yatatokea kama yale yaliyokuwa yanatokea zamani (labda siyo zamai sana) na JWTZ ambapo askari wao akipigwa na rais kikosi kinakuja na kufunga mtaa na kupiga wananchi wote kuwakomoa! Sasa leo polisi wakishuka Kitangiri na kuanz akupiga watu ili "wawataje wahusika" tutasema ni haki kwa vile wanalipiza afisa wao kuuawa na raia?

Jeshi hili la polisi ndugu MM unategemea mapya gani tokea kwao, nakuhakikishia ndani ya Saa 24 utasikia raia wasiokuwa na hatia wamekamatwa wakihusishwa na mauaji ya Liberatus , double standard ya Hali ya juu, labda wewe hukai tanzania hulifahamu jeshi la polisi, Mimi kwa dhamira yangu ya wazi nasema to hell, nimeridhika na kilichotokea .
 
"Kamanda Barlow ahukumiwe kwa matendo yake mwenyewe na si matendo ya wengine
." JE wajua kahukumiwa kwa makosa ya nani? ni kweli hatusupport mauaji kwam2 yeyote asiye na hatia, lakin je ulisikia majibu yake juzi kuhusiana na kukoswa risasi kwa yule ofisa wa uhamiaji mwanza? yale majibu yalikuwa ni ya ulinzi shirikishi?
 
Mzee Mwanakijiji mimi siongezi neno. Maana kuna watu wametoa maneno ya ajabu kabisa hadi unaanza kuhoji utu wao uko kwenye nini hasa!!

Majambazi Hawa watasidia kuwakumbusha polisi kuwa nao ni binadamu na ipo siku watakufa pia, kwa unyama ambao polisi wametenda kwa Muda mrefu tena kimfumo, wamechangia familia nyingi kuwa na Watoto Yatima wanaoteseka bila wazazi, potelea mbali acha nao wauwawe tu, my conscious is clear on this.
 
Ukweli husemwa:

Tanzania kwa sasa imekuwa kama kuku aliyekatwa kichwa kidogo na kuachiwa.

Nchi kwa sasa inaombwe la viongozi katika serikali, vyama vya siasa na madhehebu ya dini. Na hakuna kipindi ambacho jamii iko kwenye taharuki kama sasa. Ni hatari pale jamii inapoanza kuwa na fikra na mawazo ya kinyama. Pale jamii inapoanza kutotofautisha lipi tendo ni la kinyama na lipi tendo ni la kibinadamu.

The day is numbered.
 
MM tumepata taarifa kumbe alikuwa na mke wa mtu,ilikuwa ni halali yake kutwangwa lirisasi la shingo,Mungu analipiza kwa njia nyingi sana na tunaomba kwa nguvu zote yule wa iringa naye yamkute mabaya kuliko haya

Sio wewe uliesema humu 'umetafuna' wake za watu saba?
sasa unashangilia nini hapa?
wewe ufanywaje na wenye wake?
 
Back
Top Bottom