Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 10,848
- 2,669
Kila jambo lina chanzo. Katika mfumo wa nchi kama hivi ni rahisi sana kwa hekima kuanzia juu kushuka chini. Lakini ni rahisi pia kwa ukosevu wa uvumilivu kuanzia chini kwenda juu. Tunachoshuhudia sasa ni kukosekana kwa uvumilivu, na hivyo kusababisha moto kuelekea juu. Nini chanzo cha ukosefu wa uvumilivu? Mfumo unajua. Hata wananchi wanajua. Sasa kipi rahisi au ghali kati ya mfumo wa kushuka au wa kupanda? Ni nani kati ya makundi haya mawili atakayepoteza? Upumbavu wa mfumo (unaounda safu ya uongozi wa Dola) ndio chanzo cha hii furaha ya wananchi pale mmojawapo wa wanamfumo anapodhalilika, au hasira na chuki za wananchi pale mmojawao anapodhurika.