Hawa ndio wabaya wa waislamu na uislamu wenyewe kwa Tanzania...

Status
Not open for further replies.
Haisee jamaa wewe naomba ufanye haraka harakati za kuivunja bakwata na kuwaelimisha waislamu wamjue adui yao ni nani,maana umeongea vitu vizito na vya maana sana binafsi nimependezwa na upeo na uelewa ulio nao.safi tunaitaji waislam wenye utashi kama wewe.
 
Kwanza nakupongeza Mtoi kwa kutoa mawazo chanya kuhusu hali halisi ya udini ndani ya Tanzania. Mimi si muislamu lakini nimevutiwa sana na maelezo yaliyotolewa na mtoa mada. Naomba nitoe mchango wangu kidogo.

Kwanza tatizo la kutokuwa na wasomi wa kiislamu wengi miaka ya uhuru kweli ilitokana na historia ya wakoloni kwani Wamisionari waliwekeza kwenye elimu na afya lakini kwa upande wa waislamu waliwekeza kwenye madrasa (elimu akhera tu). Mfano chanzo cha mimi kuwa mkristo ni baba yangu aliyekuwa anaitwa Hosseni kubadili dini kuitwa Godfrey. Kisa ni kuchukizwa na wazazi wake ambao walimkataza kwenda darasa la tano kwani walimtaka akasome dini. Huo ndio ulikuwa mwisho wa elimu yake. Je ni wazazi wangapi hadi leo ambao hawafikiria kutafuta balance kati ya elimu akhera na elimu dunia? Waislamu ni ndugu zangu na naamini wapo wazuri tena sana ambao wanaweza kuleta mabadiliko chanya kwenye vichwa vya waumini wengi wakiislamu ambao wamekuwa wakifuata mikumbo bila kuwa na taarifa sahihi.

Bwana Mohamed Mtoi sifahamu kiwango chako cha elimu ila hiki ulichoandika kimekaa kichadema zaidi kuliko ukweli wenyewe; unataka kuniambia katika mamilioni ya waislamu waliopo Tanzania ambao hawakujaaliwa kusoma walikataa wenyewe au tu ni matatizo ya mfumo mzima uliokuwepo? Kigezo cha kusema raisi na makamu ni waislamu hakina mshiko; tatizo lipo na ni kubwa sana lisipofanyiwa marakebisho litakuwa ni balaa kubwa kwa taifa letu; yapo matatizo yamechangiwa na waislamu wenyewe na yapo ambayo serikali imechangia kwa kiasi kikubwa; hii hoja yako ya kusema tatizo hulioni ni mtazamo wako ambao umeliangalia kwa kiwango cha muuza kahawa.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
mimi kwangu naamini wakiristo na CCM ndio adui wa waislam tz. hivi vitu vikikaa na kuwaheshimu waislam udini utaondoka tz

Kwa maoni kama haya bado tu unakataa kuwa watu kama wewe ndo maadui wa uislam? Wewe ni tatizo kwa wanaokuzunguka na kwako mwenyewe. I wish ningejua ulipo ili upewe msaada maana unaweza hata kujidhuru mwenyewe.
 
Sikiliza redio imaan sasa. Kwakeli makubwa yanasemwa. Ni redio pekee ambayo inasema uhalisia wa udini wa tanzania.
 
Mohamed Mtoi,

Soma historia ya Tanzania kuhusu unatoa mfano wa Bakwata hunajua hiyo taasisi imeundwa na nani na kwa sababu zipi? Hakuna Muislam anayeipenda Bakwata hiyo unayoisema.

Nakuambia maneno machache tu wewe jikite kwenye kuendeleza Chadema lakini usitake kuwasemea Waislam matatizo yao.

Jiulize kwa nini Pro-Chadema wenzako wanakusifia kwa uzi wako? Ukiona adui yako anakusifia kwenye jambo lako basi achana nalo haraka ukiona adui yako alipendi jambo lako basi shikamana nalo sawa sawa.
 
Mohamedi Mtoi,

Hivi hunajua maana ya mfumo unataja majina ya Chade Othman, Mohamed Shein ndio reference yako kupinga mfumo ebu tupe idadi ya mawaziri wa Tanzania na manaibu wake Waislam wangapi na Wakiristo wangapi. Tutajie idadi ya makatibu wa wizara Waislam wangapi na Wakiristo wangapi. Wizara zote za serikali na makampuni ya umma yote yamejaa Wakiristo unadhani ili limekuja bahati mbaya.

Hakuna hata Muislam mmoja anayejitambua anaweza kukubaliana na hii thread yako ya Chadema, wewe ni kama ni Muislam basi ni "Muslim puppet" hata enzi za mitume walikuwepo ndio maana unaona hii thread yako imependwa na Pro-Chadema wenzako na kukusifia ambao wanakutumia.

Kaka, hapa hatumiwi mtu, but this is the fact.
Mawaziri na manaibu wao wanateuliwa from wabunge. So tukianza kuhesabu mawaziri waislamu, itabidi tuanze kwanza na wabunge waislam wako wangapi. Hapo sina shaka umenipata.

Tukija kwa hao makatibu, sijajua unataka kusema nini, maana mteuzi wao ni Rais ambae sina shaka wewe unamkubali. Sasa kama unaniambia ana udhaifu katika chaguzi zake za makatibu, ina maana unaniambia kua unakubali kumtumikia mtu usiemkubali.

Kaka Ritz, tukubali tukatae sis I waislam tuna matatizo pia. Bakwata ingekua strong, serikali yako ya CCM isingetuonea. Angalia jinsi kina Pengo na Malasusa wanavyojitahidi kutoa matamko kwa waislam pale ambapo taasisi za dini zao zinapoguswa, hili hutoona kwa Bakwata, why?

Na-declare ufuasi wa CDM (Sijui kwa MM), but hapa sizungumzii kama Mwana-CDM, but muislam naeguswa na matatizo tulip nayo. Serikali kama baba wa wote, ikitokea akampendelea mtoto mmoja (mkristo) basi usimchukie huyo ndugu yako, anza kwanza na baba yako. Na jibu linaweza likawa kua pengine hujaonyesha kuhitaji kusoma akakulipia Ada.
 
Last edited by a moderator:
AshaDii na Mohamed Mtoi, wanamitazamo yao huwezi kusema matatizo ya Waislam ni Waislam wenyewe nimeongea mwanzo Muislam makini anayejitambua hawezi kubaliana na mawazo yao ya kichadema.

Kama kweli wao wanaona hakuna tatizo la mfumo kristo wagombee uongozi ndani ya Chadema waone na huo Uislam wao Zitto anapendwi Chadema kwa nini?

Ndio maana unaona huu uzi Chadema wote wanauchangia pongezi nyingi lakini dini yetu imetuambia miongoni mwetu wanafiki huwa hawakosi.

Hapa HAKUNA CHADEMA wala nini, KWA Maana hiyo una taka kutuaminisha KUWA CCM NDIYO wanalea MFUMO Kkristo???? Historia ya mkoloni ni historia tu, NDIYO Maana Baba wa TAIFA alitaifisha Shule zote ZA dni pamoja na lawama lukuki anazopewa RIP. Tangu sera huria ianze nitajie id adi ya Shule na hospitali zilizojengwa na dini TOFAUTI TOFAUTI, NDIpo hiyo dhana potofu ya MFUMO kristo, inaweza kujitenga, japo MFUMO huo SI NDIYO wa Issa bin Mariam??? AU kuna TOFAUTI?
 
kwa maoni kama haya bado tu unakataa kuwa watu kama wewe ndo maadui wa uislam? Wewe ni tatizo kwa wanaokuzunguka na kwako mwenyewe. I wish ningejua ulipo ili upewe msaada maana unaweza hata kujidhuru mwenyewe.
huu ndio ukweli. Kama leo ccm inatoa pesa kwa makanisa kwa ajili ya maendeleo ya kanisa
 
Upande mmoja tunaweza kuwalaumu waliowachagua hao majaji wakuu. But tujiulize huyo mchaguzi (Rais) alikua ana wigo gani wa kuchagua??

Kama kila akipepesa macho, haoni muislam basi angefanyaje? Kunaweza kukawepo na njama za kutukandamiza waislam, but njama hizo zinafanikiwa kutokana na udhaifu wetu wenyewe.

Hii inaapply kwa nafasi zingine pia, naamini mtu hapaswi kuchaguliwa kwa merit kwa mfano kama waliopita wote walikua waislam basi jaji anayefuata awe mkristo. Hapo ndipo tunapokosea. Kama waliocompetent zaidi ni wa dini ile ile moja waendelee kuchaguliwa kwa kuwa tunachojali ni utendaji/ufanisi/uzoefu/uelewa wa mtu huyo katika kazi yake na sio kama yeye huwa anaswali Ijumaa au anasali Jumamosi ama Jumapili.

Kuna haja sana ya kubadili namna yetu ya kufikiria. Kwa hali ilivyo sasa, zinasikika lawama nyingi Wakristo wakiwa kwenye nafasi za juu serikalini kuliko wakiwa Waislam. Yako wapi haya maagizo ya kupendelea wakristo? Vipi ndugu zetu wapagani, wahindu, buddhists? Mbona hatuwasikii wakilalamika ama wao hawazitaki hizi nafasi? Tupendane Watanzania.
 
Muslim in christian countries they live peacefully but muslim in muslim countries its a problem.
 
Muslim in christian countries they live peacefully but muslim in muslim countries its a problem.

Shangaaaa???? Syria, Somalia, Egypt, Tunisia etc etc nalo ni MFUMO kristo aka Issa bin Mariam???
 
1. Adui namba moja kwa waislamu ni kutokuwa na mashule na vyuo vingi vyenye kutoa elimu bora kwa vijana wa kiislamu na hata wale wa upande wa pili wanaokuja kuitafuta elimu. Najua kuna watu watapinga sana lakini ukweli mchungu lazima tuuseme ili tupate pa kuanzia, mtakuwa mashahidi hata shule tulizo nazo hazifanyi vizuri sana kwenye mitihani ya kitaifa lakini pia hata mashule yetu hayana mfumo wa kuandaa masheikh walio iva kwenye elimu dunia na akhera. Mimi napendekeza harakati zetu ziwe kwenye kujenga mashule ya viwango pamoja na kuajiri walimu bora bila kujali dini zao ili kuwaandaa vijana bora wanaoendana na kasi ya sayansi na teknolojia kuelekea soko la ajira ya ushindani na pia viongozi bora wa dini.

Mtoi hujiulizi kwanini waislamu hatuna hivyo vyuo na mashule wakati kipindi East African Muslim Walfare Society (EAMWS) watanzania tunajitoa/tunaivunja tulikuwa na miradi ya vitega uchumi mbalimbali? Waislamu wengi wanamuona nyerere mbaya simply ni juu ya maamuzi yake ya kuitoa tanzania kwenye hiyo jumuia na kuianzisha BAKWATA (mind you,aliianzisha yeye ilhali yeye si miongoni mwa hao waislamu E.g Kikwete aanzishe baraza la wakristo Tanzania na kuvunja organization zao zilizopo) na matokeo ya BAKWATA yamekuwa ni kufilisi mali za waislamu na kutetea maslahi ya CCM.

Mimi kuna wakati huwa nasema ni sawa tu ndugu zetu wakristo wakitudhihaki kuwa sisi ni mashetani,hatuna elimu,wazee waubwabwa tende na gahwa na matusi mengine yote yaliyopo duniani maana hivi tuseme ukweli tofauti na kutangaza muandamo wa mwezi kipindi cha mfungo wa ramadhan BAKWATA inafanyakazi gani nyingine kwa waislamu? BAKWATA haijitambui na haijui inadhima gani kwa umma wa kiislamu Tanzania,Sheikh Ponda akisema anaonekana ni mkorofi. Viongozi wake wanachaguliwa kisiasa kwa maslahi ya MAGAMBA.

Mwisho kabisa ningependa kuwashauri na nyie ndugu zetu wakristo mmbadilike jamani,mnawapa maneno mazito sana watoto wenu juu ya uislamu, hili nimelishuhudia mwenyewe mara nyingi sana tangu nipo mtoto mpaka sasa hivi ni mtu mzima.Kitendo cha kuwaambia watoto wenu kuwa uislamu ni ushetani siyo vizuri?hivi unafikiri unamjengea picha gani mtoto huyo pindi atakapokuwa mkubwa kwenye jamii kama hii ya mchanganyiko mkubwa wa kidini?

Tumejikwaa,tujipanguse vumbi,tuondoe kisiki na tusonge mbele! Tanzania siku zote tumeishi kwa ushirikiani na dini haijawahi kuwa kigezo cha kututenganisha.
 
huu ndio ukweli. Kama leo ccm inatoa pesa kwa makanisa kwa ajili ya maendeleo ya kanisa

Rais wako miezi kadhaa iliyopita kule dodoma aliwaambiaje? Anzisheni MOU na ninyi. Mnasubiri nini sasa? I bet kama si wewe basi ndugu yako yeyote ameshawahi pata huduma toka taasisi yeyote ya kikristo na wala hakuulizwa ni dini gani. Ndugu zetu hivi huwa mnashirikisha ubongo kweli?
 
Mohamed Mtoi,

Soma historia ya Tanzania kuhusu unatoa mfano wa Bakwata hunajua hiyo taasisi imeundwa na nani na kwa sababu zipi? Hakuna Muislam anayeipenda Bakwata hiyo unayoisema.

Nakuambia maneno machache tu wewe jikite kwenye kuendeleza Chadema lakini usitake kuwasemea Waislam matatizo yao.

Jiulize kwa nini Pro-Chadema wenzako wanakusifia kwa uzi wako? Ukiona adui yako anakusifia kwenye jambo lako basi achana nalo haraka ukiona adui yako alipendi jambo lako basi shikamana nalo sawa sawa.

Kama Uzi huo Imekaa na unashabikiwa na CHADEMA, CCM NDIYO chimbuko na Mlezi wa MFUMO Kristo aka Issa bin Mariam? Wachangiaji wAna mapenzi na nchi Yao na hawako kisiasa zaidi, hapa ni uzalendo MBELE, Siasa waache we kina Nape, Zito na wafuasi wao
 
Mohamedi Mtoi na AshaDii,

Katika mazingira tuliyonayo inatia faraja sana kuona watu wanakuja na hoja za kufikirisha na zenye mantiki.

Mumeweza kuja na kujenga hoja zinazosimama zenyewe na zinazojieleza. Mumefanya hivyo hata pale ambapo dhamira zenu zinakinzana na fikra zenu. Mumeshinda nguvu ya ubinafsi, mkaongozwa na weledi tena kwa kujiamini na kwa mantiki.

Kwa vile mnasimamia kile kilichopo miyoni mwenu na katika fikra, na kwa vile mnaongozwa na mantiki zaidi ya hisia, wapo watakaowakejeli, kuwadhihaki, kuwatoa katika uumini na kuwakashifu. Hilo lisiwasononeshe kwasababu ajuae dhamira zenu ni Mwenyezi mungu peke yake.

Wanajamvi, Mtoi na Ashadii wametoa fikra zao na mitazamo yao. Tunaweza kukubaliana au kutokubaliana nao hiyo ndivyo inatakiwa iwe. Muhimu ni kuwa kama yupo asiyekubaliana nao basi aje hapa na kutueleza fikra zake kwa 'kushambulia' hoja zao kama walivyozileta na si kejeli matusi au dhana tu kwa vile fulani kasikia ABC kutoka kwa fulani.

Mathalani, mimi nakubaliana na Mtoi kuwa wakati umefika sasa serikali iwaache waislam waamue utaratibu wa kumpata kiongozi wao ambaye wao watamsikiliza na awe kiungo muhimu kati ya Waislam, serikali na jamii zetu zingine.

BAKWATA imepoteza hadhi na dhamana hiyo muda mrefu na sasa ni wakati wa kuangalia suala hili kwa mtizamo mwingine na jicho mujarab.

Kwa vile BAKWATA imepoteza hadhi na heshima miongoni mwa jamii ya Waislam, haya tunayoyaona ni matokeo ya watu wachache kutumia ombwe lililopo katika kuleta mitafaruku. Ndiyo maana taasisi zinazuka na kila moja ikiwa na misimamo yake. Kwa maneno mengine hakuna kiunganishi cha jamii kwahiyo mweleko unakuwa mashariki kaskazini, kusini magharibi n.k. ili mradi mtu apate anachokitaka.

Ni kutokana na hayo ndiyo maana tumeona taasisi zinazoshughulikia mtaa mmoja zikijipa uhalali wa kuwa taasisi za kitaifa. Lakini pia kutokana na kuzuka kwa taasisi hizi kunakosababishwa na Ombwe la uongozi, tumeona taasisi inayosimamia wakfu wa nyumba 3 kariakoo ikijipa hadhi ya kusema kwa niaba ya Waislam wa Tanzania.

Tumeshuhudia makundi haya mengine ya mitaa yakiongoza kwa masilahi binafsi huku yakiwa yamejivika joho la Uislam. Hebu fikiri kidogo! Sheikh aliyesema CCM imewaonea waislam tangu uhuru mwaka 1995-2000, Sheikh huyo huyo amegeuka na kusema CCM inawafaa Waislam mwaka 2005!! Think about it!

Sikubaliani na Mtoi kuwa kiongozi wa Taasisi kama BAKWATA lazima awe msomi. Hoja yangu hapa naijenga kwa njia mbili:

1. Kuna kiongozi wa kiroho ambaye anatakiwa aijue dini yake vema ili kuwaongoza wafuasi wa dini yake kulingana na sheria, kanuni na taratibu. Huyu anasaidiwa na wataalam wengine wanaojua mambo ya dini katika nyanja mbali mbali.

Kwa mfano,Mufti ndiye kiunganishi cha wataalam (ulamaa kama sijakosea) waliobobea katika sharia, tawhid, fiki n.k. Kwahiyo lazima awe kiongozi mwenye weledi wa hali ya juu katika dini.

2. Uongozi wa Taasisi kama BAKWATA ni jumuiya inayowaweka waumini pamoja. Hakuna mahali katika kitabu kitakatifu imetajwa BAKWATA au taasisi nyingine. Ndiyo maana Kenya wa SUPKEM, pengine Zambia na Malawi tofauti.

Kwa msingi huo taasisi inatakiwa iundwe kwa kuangalia Taratibu za dini na mazingira yaliyopo. Hapa ndipo tunaweza kusema anahitajika mtu mwenye elimu katika mambo ya Utawala, viwango kama PhD n.k. ili kukidhi mahitaji ya uendeshaji wa taasisi kwa kuwa kiunganishi cha masuala ya dini na yale ya jamii.

Ukiniuliza Taasisi kama BAKWTA ijengwe vipi, ningeweza kushauri kuwa iwe na vitu vifuatavyo:
1. Mufti ambaye ni mkuu wa mambo ya kidini
2. Mwenyekiti wa Taasisi ambaye ni msimamizi wa shughuli za taasisi kama kiunganishi cha dini na mazingira au jamii.

Na mwisho nakubaliana na Mtoi na AshaDii kuwa umefika wakati wa watu kuangalia dini zinasemaje na si fulani anasema nini. Watu wajiulize je kile wanachotaka kukifanya kina reflect misingi ya dini kama ilivyoletwa kwa kuangalia vitabu vitakatifu, hadithi na sunna (Kwa watu wa imani zote)
 
Last edited by a moderator:
Mkuu chama,
Huyu jamaa ni muslim puppet anakuambia haoni tatizo lolote wala hakuna mfumo kisrto wabaya ni Waislam wenyewe.
Tatizo kwenye mfumo wet lipo, hiyo inafahamika. But tumefanya juhudi gani kujaribu kutafuta balanced system?? Nani wa kufanya hizi juhudi? Katika formal ways, tungetegemea chombo kama Bakwata kichukue nafasi hii, ambapo kimeshindwa.

Hapa ndipo zinapoibuka informal ways like kina Sheikh Ponda, Alhaji Kundecha n.k., na hizi zinapewa support kubwa sababu ya kushindwa kwa formal ways.

Nkuulize, labda we unaona nini kifanyike? Pengine badala ya kushambulia hoja za wengine, embu nawe uje na counter measures against this system.
 
Last edited by a moderator:
Mohamed Mtoi,

Soma historia ya Tanzania kuhusu unatoa mfano wa Bakwata hunajua hiyo taasisi imeundwa na nani na kwa sababu zipi? Hakuna Muislam anayeipenda Bakwata hiyo unayoisema.

Nakuambia maneno machache tu wewe jikite kwenye kuendeleza Chadema lakini usitake kuwasemea Waislam matatizo yao.

Jiulize kwa nini Pro-Chadema wenzako wanakusifia kwa uzi wako? Ukiona adui yako anakusifia kwenye jambo lako basi achana nalo haraka ukiona adui yako alipendi jambo lako basi shikamana nalo sawa sawa.

Hapo kwenye blue unamaanisha kwamba hata viongozi wa Bakwata siyo waislamu? Nenda shule baba, umri unakwenda. Elimu siyo kidonge useme mkipambana mtapewa mmeze
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom