Hawa ndio wabaya wa waislamu na uislamu wenyewe kwa Tanzania...

Status
Not open for further replies.
AshaDii na Mohamedi Mtoi mmezungumza vizuri sana, sasa HAYO NDIYO mafundisho yanayotakiwa kutolewa, KWAsababu masuala mengine yametokana na historia, na NDIYO Maana baba wa TAIFA alichukua hatua ZA kutaifisha Shule zate ZA dini, pamoja na lawama lukuki anazopewa.

Je Shule zisingetaifishwa ingekuwa je??? Iwekwe Mifano ya mafunzo KWA VIONGOZI wa dini, wasomi wasione kazi ya KUWA maalim ni KWA waliomaliza darasa la Saba, washiriki kikamilifu!!!!

Pamoja tutafika, Mungu IBARIKI Tanzania
 
Ni ukweli mtupu.

Wakati tunapata uhuru shule nyingi zilikuwa ni za Wakristo. Wamisionari wao walihakikisha kuwa popote penye Kanisa panakuwa na shule pamoja na hospitali. Waislamu walikuwa na shule chache sana. Haijalishi kuwa nia ya wakoloni wale ilikuwa watupe elimu ya kuweza kuwatumikia tu, lakini ilileta mwangaza kwa walioipata. Mwalimu Nyerere kwa kuliona hilo akaona kuwa wakristo wanaendelea kuanzisha shule mpya na waislamu hawana mpango. Akaona maono ya mbali kuwa taifa litakuwa na wasomi wakristo wenye nuru na waislamu wengi walioko gizani na akafanya maamuzi magumu ya kutaifisha shule zote za wakristo ilo na waislamu nao wasome.

Hata siku za karibuni waislamu walipodai kuwa shule zilizotaifishwa zirudishwe, Kikwete alisema kuwa hilo haliwezekani kwa kuwa itanufaisha makanisa zaidi kwani karibu asilimia 80 ya shule zote zilizotaifishwa zilikuwa zao.

Inanishangaza kuona waislamu wakimwona Nyerere kwa mmoja wa maadui zao wakuu. Hulka ya wakristo ni ukarimu. Hawakumbishia Nyere bali waliona nia yake njema kwa ndugu zetu waislamu na hakuna Kanisa hata moja lililowahi kumlaani mwalimu kwa kutaafisha shule na hospitali zake. Walionufaika ndio wanaomlaani.

Angalia tu mfano wa vyuo vikuu. Baada ya kuruhusiwa tena kujenga mashule na Vyuo vya binafsi, Makanisa yameanzisha mashule mengi sana tena ya viwango. Wameanzisha vyuo vikuu vingi katika kila kanda ya nchi yetu kama si kila mkoa. Waislamu wanafanya nini? Kwa kadri wanavyolalamika kuwa huo ni mfuma Kristo ndio wanavyopoteza muda na huku wakristo wakiendalea mbele. Na elimu ndio ufunguo wa maisha.

Waislamu amkeni. Acheni kutoa sababu za kufikirika na kusadikika tu zisizo na uhalisia. Vurugu hizi ni taswira ya kukosa elimu.

kudu!!!.Huo ndio ukweli wenyewe tatizo sisi waislam ni walalamishi sana kuliko kutenda na tutabaki hivihivi. Bora mimi niliyejiendea shule huo upuuzi wao sina muda nao. Ponda mwenyewe no school sasa kuna nini cha maana atanieleza hata kama mimi ni muislam. Serikali funga hao wahuni Mtume wetu hajatuelekeza tufanye upuuzi huo kwa jina lae
 
Tatizo letu waislam ni kua hatutaki kubadilika. Sitegemei Mufti wa darasa la Saba aweze kuja na vision + mission ya kuipeleka Bakwata mbali kama afanyavyo Doctor Alex Malasusa.

Mi nimesoma A-Level Islamic Seminary, yaani ni bora ukwepe darasa unaweza kupona kuliko kukwepa sala. Watu wanajengwa kiimani zaidi kuliko kidunia, no balances.

Pia kuna tofauti kubwa ya uendeshaji wa taasisi zetu tofauti na wenzetu. Tukijiuliza Mufti wetu anawajibika kwa nani nje ya nchi, jibu hakuna. So akiboronga hakuna wa kumsimamia maana ye ndio Top. But wenzetu mfano Waroma, wao wanawajibika Vatican, hivyo no ujinga ujinga wa kiuongozi.

Sambamba na hilo, hao wakubwa zao wa nje wanawapa musaada mbalimbali, ndio maana kila siku vigango, parokia, usharika n.k. vinafungulia na kuanzishwa. Sisi wakubwa zetu wa kutupa misaada wako wapi? Ni kina nani?

Pia utakuta hata sera ni tofauti. Wenzetu wanatafuta pori a.k.a msitu, wanafyeka na kuweka mission hapo. Hapo zitapatikana shule, hospitality, other economical activities e.t.c, sisi hatuna akili hiyo.

Mimi ukiacha A-level, shule zingine zote nimesoma na hawa ndugu zangu, yaani Waislamu wenzangu nafanya kuwahesabu, wako wapi wengine?? Hawakuchaguliwa? Au hawakuomba? Wali-qualify? Why?

Hivi kuna sababu zozote za kisayansi zinazofanya mtoto awe/asiwe na akili just because of dini yake?? Nikichora graph ya waislamu nlioanza nao primary walioacha shule mpaka nimemaliza shahada ya pili, pyramid ni Kali sana? Where are others??

Fanya research fupi tu;
Pitia kituo cha daladala anza kuuliza jina wale mateja wa pale, utaambiwa Dullah, Muddy, Ally, Ramso and the like. Toka hapo upitie mahakama za chini ambazo kesi mbalimbali kama za wizi wa kuku, kutukanana, kupigana, n.k. zinahukumiwa, majina ni hayohayo.

Tumeshakosea, tufanyeje sasa??
Real inahitajika debate then utekelezaji on this issue.
Duh! Shark we kweli una macho safi,you are hundred percent right!!hawamjui adui yao hawa.
 
Mohamedi Mtoi

Kweli we umenena nahisi elimu inakufanya uwe mstaarabu,ila waambie wenzio elimu ndo itakayo wakomboa mkristo anapeleka mtoto tuisheni nyie mnwapeleka Madrasa je mnategemea mtaringana kielimu badilikeni
 
Huyu mtoa mada ni kweli katembelewa na sauti ya mungu. Kwa mara ya kwanza tangia tupate uhuru huyu mtoa mada kaelimisha umma na kuleta amani ya kweli. Yaani hata kujituma tuu elimu za NBAA madarsa ya jioni, huwaoni wasilamu wengi bali wakristo tuu. sasa leo ukiona wahasibu wengi wana CPA ni wakristo, utalalamika?

Katika shule za kiislamu nyingi, wanwake huwa na madarasa yao na wanaume pia hutengwa . Tena hawaruhusiwi kabisaa hata kuongea pamoja wakiwa Break. Sasa group studdy kam wote wanawake ni vilaza basi humo kuna divison zero. Shule za kiislamu zifanye jitihada za kuajili walimu wa dini yeyote ili kuimarisha elimu.

Nchi kama Senegal, Uturuki, Akgeria, Moroco na Tunisia, ukienda huko wailsmu hufanyia jamii kam vile mtoa mada alivyopendekeza ktk elimu. Ndio maana utakuta nchi hizo hazina matattizo ya kuoingoza dini yao. wanwake Uturuki, senegal hawavai kabisaa hijab wala baibui. Hapo tunisia, Moroco na Algeria wao dini ni seconda topic na wameelimika sana both dini na elimu dunia.ukienda beach, utadhania upo Miami! wewe angalia sana CCTV africa, halafu wakizitaja nchi hizo angalia watu wa mitaani, katika watu mia baraka shehe ni mija tuu au hamna ila dini yao huipenda sana.

watoa mada wa kiislamu waliochangia mada hii kweli ni wamepevuka, mungu awabariki!
 
Tatizo letu waislam ni kua hatutaki kubadilika. Sitegemei Mufti wa darasa la Saba aweze kuja na vision + mission ya kuipeleka Bakwata mbali kama afanyavyo Doctor Alex Malasusa..
Yote aliyotoa mwanzilishi wa thread hii nayakubali ni kweli tupu. Lakini katika post hii ya Shark (nilipomnukuu hapo juu) naona serikali inabeba lawama kwa kiasi fulani. Katika chaguzi za mufti serikali huwa inaingilia sana, hutaka Mufti ambae serikali inamuafiki.

Kama mtakumbuka wakati wa uchaguzi wa Mufti baada ya kifo cha yule Hemed bin Jumaa, kulikuwapo mgombea mmoja msomi sana -- Profesa Mikidadi.

Habari zilisema kwamba serikali, kupitia Usalama wa Taifa, ilihakikisha kwamba Profesa huyu hapati, asiruhusiwe kuongoza Waislamu, ni bora yule wa darasa la saba ambaye hatimaye alipiota kwa ghilba kubwa na mizengwe. Waislamu wengi walimtaka Profesa Mikidadi kwani walimuona ni mtu ambaye angewaendeleza. Lakini kwa kuwa wanaomchagua Mufti ni wajumbe wa BAKWATA kutoka mikoani na wilayani, wengi wao waliweza kununuliwa na Usalama wa Taifa kumkosesha Profesa Mikidadi u-Mufti.

Conclusion hapa ni kwamba inaonekana serikali nayo ina wasiwasi sana Waislamu wakipata kiongozi wao wa juu ambaye ni msomi.

Naomba michango yenu kuhusu hili.
 
mimi kwangu naamini wakiristo na CCM ndio adui wa waislam tz. hivi vitu vikikaa na kuwaheshimu waislam udini utaondoka tz
 


Yote aliyotoa mwanzilishi wa thread hii nayakubali ni kweli tupu. Lakini katika post hii ya Shark (penye red) naona serikali inabeba lawama kwa kiasi fulani. Katika chaguzi za mufti serikali huwa inaingilia sana, hutaka mufti ambae serikali inamuafiki.

Kama mtakumbuka wakati wa uchaguzi wa mufti baada ya kifo cha yule Hemed bi Jumaa, kulikuwapo mgombea mmoja msomi sana -- Profesa Mikidadi.

Habari zilisema kwamba serikali, kupitia Usalama wa Taifa, ilihakikisha kwamba Proifesa huyu hapati, asiruhusiwe kuongoza Waisilamu, ni bora yule wa darasa la saba ambaye hatimaye alipiota kwa ghilba kubwa na mizengwe. Waisilamu wengi walimtaka Profesa Mikidadi kwani walimuona ni mtu ambaye angewaendeleza. Lakin kwa kuwa wanaomchagua mufti ni wajumbe wa Bakwata kutoka mikoani na wilayani, wemgi wao waliweza kununuliwa na Usalama wa Taifa kumkosehsha Profesa Mikidadi umufti.

Conclusion hapa ni kwamba inaonekana serikali nayo ina wasiwasi wasi sana Waisilamu wakipata kiongozi wao wa juu ambaye ni msomi.

Naomba michango yenu kuhusu hili.

Usemayo yana ukweli kiasi flani. Sidhani iwapo serikali iliingilia wakati Dr Malasusa alichaguliwa kuongoza KKKT. Kwa kuingilia uongozi wa Bakwata, ndiyo maana Bakwata yenyewe imekaa ki-CCM CCM tu -- kwa mfano ufisadi nk.
 
chama

Nadhani Mhe Rais wakati wa Eid mwaka Juzi Dodoma? Alisema badala ya KULALAMIKA KUWA hawa wAna MOU leteni na nyinyi muwe na MOU na serikali, sijui hatua gani zimechukuliwa hadi Leo? Wenye hiyo MOU hebu iweke ni hapa tuone hicho kinacholalamikiwa, MOU iliyosainiwa awamu ya Pili!!!! Ingekuwa ni awamu ya kwanza AU ya tatu kesi NDIYO ingekuwa KUBWA zaidi!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: FJM
Bwana Mohamed Mtoi sifahamu kiwango chako cha elimu ila hiki ulichoandika kimekaa kichadema zaidi kuliko ukweli wenyewe; unataka kuniambia katika mamilioni ya waislamu waliopo Tanzania ambao hawakujaaliwa kusoma walikataa wenyewe au tu ni matatizo ya mfumo mzima uliokuwepo? Kigezo cha kusema raisi na makamu ni waislamu hakina mshiko; tatizo lipo na ni kubwa sana lisipofanyiwa marakebisho litakuwa ni balaa kubwa kwa taifa letu; yapo matatizo yamechangiwa na waislamu wenyewe na yapo ambayo serikali imechangia kwa kiasi kikubwa; hii hoja yako ya kusema tatizo hulioni ni mtazamo wako ambao umeliangalia kwa kiwango cha muuza kahawa.

Chama
Gongo la mboto DSM

Unasema kuna tatizo ni lipi? kuna mfumo mbovu ni upi huo? mbona MM amechambua japo kidogo,kama kuna tatizo mahali liainishe tulijadili, afu haya ya uchadema na kuuza kahawa sijui yameingiaje hapa?
 
Bwana Mohamed Mtoi sifahamu kiwango chako cha elimu ila hiki ulichoandika kimekaa kichadema zaidi kuliko ukweli wenyewe; unataka kuniambia katika mamilioni ya waislamu waliopo Tanzania ambao hawakujaaliwa kusoma walikataa wenyewe au tu ni matatizo ya mfumo mzima uliokuwepo? Kigezo cha kusema raisi na makamu ni waislamu hakina mshiko; tatizo lipo na ni kubwa sana lisipofanyiwa marakebisho litakuwa ni balaa kubwa kwa taifa letu; yapo matatizo yamechangiwa na waislamu wenyewe na yapo ambayo serikali imechangia kwa kiasi kikubwa; hii hoja yako ya kusema tatizo hulioni ni mtazamo wako ambao umeliangalia kwa kiwango cha muuza kahawa.

Chama
Gongo la mboto DSM
tatizo la elimu si la waislam peke yao ni nchi nzima na wakristo pis
 
Watu Kama AshaDii na Mohamedi Mtoi Wana upeo wa juu sana wa kuchambua mambo. Ushauri wangu kwenu kwanini msigombee hizo nafasi za bakwata na taasisi nyingine za kiislamu ili hili darasa mnalotoa lisiishie hapa JF tu liwafikie hata hao ambao hawana access ya Internet ?
 
Last edited by a moderator:
Mohamed, I sincerely hope watu (wa dini zote) watasoma post yako wakiwa na fikra huru. Tatizo linalotumaliza Tanzania ni elimu. Kwanza nafasi za elimu ni chache, na ukibahatika kupata nafis elimu ni ya hovyo kupindukia. Ni rahisi sana kumyumbusha mtu ambaye hana elimu.

Kwenye uongozi wa BAKWATA, mimi sio muislam lakini kama mtanzania nina maslahi na uislam maana sote tunaishi pamoja. Nakubaliana na wewe juu ya umuhimu wa viongozi wenye elimu dunia na dini. Na ningesema Sheikh wa msikiti wa Ijumaa lazima awe na elimu walau Diploma; Sheikh wa Wilaya -Advanced Diploma; Sheikh wa mkoa awe na walau degree moja, na Mufti definately awe na Masters. Ni isiwe elimu ya google. Wawe wamesoma kwenye recognised instututions.

Hii kwanza itaondoa hii migogoro ya kugombea misikiti lakini pia itasaidia sana kuweka misingi bora ya namna kuinua taasis zilizo chini ya waislam. Ni ajabu unakuta msikiti uko mahali kwa zaidi ya miaka 20 lakini hakuna hata nursery school! Sasa unawaambia watoto wenu wanasoma wapi? Lakini utakuta sheikh na wazee wenziwe hawana habari hata kidogo.

Mambo yameachwa kwa muda mrefu lakini sasa hakuna ujanja.

Wachangiaji wote wanagusa jambo moja la msingi sana, nalo ni elimu hasa kwa viongozi wa dini pamoja na taasisi zake. Ukweli mchungu lazima usemwe, na mifano lazima iigwe hata kama ni kutoka katika taasisi ambazo kwa mitazamo finyu ya baadhi ya waumini wa kiislamu watawaita "MAKHAFIR". Angalia mifumo ya makanisa ya Kikristo, Waroma kama mfano wangu hapa, Elimu ya chini ya mtumishi anayeitwa PADRE ni elimu ya KIDATO CHA SITA, pamoja na Diploma ya THEOLOJIA. Kwa kima cha chini cha aina hii sina haja ya kuendelea kusema kule juu kunakuwaje! Nilisoma tamko la Maaskofu wa KKKT, juu yaliotokea Mbagala, na pale mwisho waliambatanisha Majina yao. Kuna idadi kubwa mno ya MADOKTA!!!!! Kwa elimu ile huwezi kumtegemea akurupuke katika kufikia maamuzi! Tujifunze, kwa maana madhara ya kuwa na viongozi wenye upeo hafifu wa elimu wanaishia kutulisha shubiri, na kupandikiza chuki miongoni mwetu, badala ya UPENDO na AMANI!
 
Mohamedi Mtoi,

“Uadui” mkubwa wa Uislamu Tanzania ni haya pia…


  • Lugha ya Kiarabu katika Mafundisho ...
  • Kujivua Uislam kwa Waumini wa Waislam
  • Mafunzo ya Vitisho katika Dini
  • Kukosekana kwa ustaarabu
  • Umimi wetu Waislamu

BTW, Nakubaliana na swala la BAKWATA, Hicho chombo inabidi kivunjwe kwa manufaa ya wengi sababu ni asilimia kubwa ya Waislam tunapingana nacho na kuona kuwa hakifai.

I wish...Mola angetupa sote uwezo wa kuchota hekima zako dada AshaDii..

Umenena vyema...wakati inabidi jifunze kiswahili kama lugha ya pili baada ya kinyamwezi chetu..inabidi tujue kiingresa kwa ajili ya kutafuta riziki..lakini kwa imani inabidi tujue pia kiarabu...matokeo yake tulio wengi tunawaachia wachache wanaojua kiarabu ili watusaidie kutafsiri mafundisho kwenye miahadhara..matokeo yake wanafundisha wanayotaka wao.

Mafunzo ya dini yakiambatanishwa na vitisho..mara fulani lakini sio zote huleta nidhamu ya woga na chuki na hii uzaa kwanini yule hayuko kama mimi... so sad!

Umimi Quote "Inakuwa mimi, mimi mimi... Mimi kama Muislam nina haki hii…. Mimi Muislamu matatizo yangu yanasababishwa na huyu… Mimi nakandamizwa… Mimi ndio nastahili sio Yule (hata kama muislamu mwenzio)" end of quote.. I have no comment..sidhani kama naweza kuongeza zaidi ulichosema...well said!

My take.. kama tungesikia busara zako na watu kama kina Mohamed Mtoi..basi wale wahuni wachache hapa duniani wanaochafua image ya dini ya Islam wangekosa wafuasi..
 
Tatizo letu waislam ni kua hatutaki kubadilika. Sitegemei Mufti wa darasa la Saba aweze kuja na vision + mission ya kuipeleka Bakwata mbali kama afanyavyo Doctor Alex Malasusa.

Mi nimesoma A-Level Islamic Seminary, yaani ni bora ukwepe darasa unaweza kupona kuliko kukwepa sala. Watu wanajengwa kiimani zaidi kuliko kidunia, no balances.

Pia kuna tofauti kubwa ya uendeshaji wa taasisi zetu tofauti na wenzetu. Tukijiuliza Mufti wetu anawajibika kwa nani nje ya nchi, jibu hakuna. So akiboronga hakuna wa kumsimamia maana ye ndio Top. But wenzetu mfano Waroma, wao wanawajibika Vatican, hivyo no ujinga ujinga wa kiuongozi.

Sambamba na hilo, hao wakubwa zao wa nje wanawapa musaada mbalimbali, ndio maana kila siku vigango, parokia, usharika n.k. vinafungulia na kuanzishwa. Sisi wakubwa zetu wa kutupa misaada wako wapi? Ni kina nani?

Pia utakuta hata sera ni tofauti. Wenzetu wanatafuta pori a.k.a msitu, wanafyeka na kuweka mission hapo. Hapo zitapatikana shule, hospitality, other economical activities e.t.c, sisi hatuna akili hiyo.

Mimi ukiacha A-level, shule zingine zote nimesoma na hawa ndugu zangu, yaani Waislamu wenzangu nafanya kuwahesabu, wako wapi wengine?? Hawakuchaguliwa? Au hawakuomba? Wali-qualify? Why?

Hivi kuna sababu zozote za kisayansi zinazofanya mtoto awe/asiwe na akili just because of dini yake?? Nikichora graph ya waislamu nlioanza nao primary walioacha shule mpaka nimemaliza shahada ya pili, pyramid ni Kali sana? Where are others??

Fanya research fupi tu;
Pitia kituo cha daladala anza kuuliza jina wale mateja wa pale, utaambiwa Dullah, Muddy, Ally, Ramso and the like. Toka hapo upitie mahakama za chini ambazo kesi mbalimbali kama za wizi wa kuku, kutukanana, kupigana, n.k. zinahukumiwa, majina ni hayohayo.


Tumeshakosea, tufanyeje sasa??
Real inahitajika debate then utekelezaji on this issue.

Ukweli unauma, but huo ndio ukweli..:sad:
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom