Hawa ndio wabaya wa waislamu na uislamu wenyewe kwa Tanzania...

Status
Not open for further replies.
Bwana Mohamed asante sana kwa uchambuzi mzuri sana na kwei uliotupatia Pia nakupa hongera kwa Muislam kuwa mkweli kutambua mapungufu ndani ya jamii yenu!
 
Sikutaka kuchangia lakini imebidi tu japo machache watu kama Chama ndo wanaozidi kukandamiza waislamu kifikra leo unasema MoU zifutwe nani atweza kugaramia afya ya walio vijini kwa garama halisi? Ni kweli wakristo wana taasisi nyingi zinazotoa huduma za kijamii je walijengewa?

Wakristo wana kawaida ya kutoa sadaka za maendeleo, ujenzi, huduma kila jumapili ili zikajenge taasisi za kuwasaidia wahitaji, je waislamu wanajenga nn?

Kuanzi waarabu wa kwanza kufika Africa mpaka leo wenye uwezo waislamu hawajengi taasisi za kusaidia wahitaji wanajenga misikiti tu, je MoU isainiwe kujenga au kutoa huduma misikitini?

Wakristo baada ya mahubiri huwa wanatangaziana shuhuli mbali mbali za maendeleo na jinsi ya kuweka vitega uchumi, waislamu wakimaliza swala ijumaa mawaidha yanayofuata wengi wao wanaanza kukashifu imani za watu wengine then wanaondoka empty headed, huku wakijitapa yule shehe leo kawakomesha wakristo, then what?

-ndani ya kanisa kuutaja hata uislam ni kosa na waumini wantamwo mhubiri hayupo sawa, muda mwingi wanashulika na waliondani ya kanisa kuliko walio nje vice versa kwa waislam.

Naungana na Mtoi waislamu wanatakiwa kuwa na viongozi wenye vision, msamaha wa kodi upo kwa dini zote na taasisi zake tujiulize waislam wanautumiaje? Kwa nini matatizo yenu ya ndani muwabebeshe wengine?

Viwanja mlikua navyo badala ya kujenga taasisi kama afya na elimu mnauza tena kwa waislamu wenzenu then mnaandamana na kulaumu mfumo kristo, nani anaujenga mfumo huo kama si nyie wenyewe kwa kutokuangalia wanakoangalia wenzenu?

Waislamu wanauzi viwanja mpaka vinavyozunguka misikiti kwa wafanya biashara wajenge frem za maduka wakati wakristo wana spea nafasi ili wajenge vyuo

Waislam wanatafuta eneo dogo lenye msongano wa watu na kujenga hapo msikiti ili tu kuwavutia/shawishi au hata kukera jamii ya wakristo walioko pale na hapo wakipata Imanu ambae hajasoma ilmu dunia ni kashfa na mausi kila ijumaa

Wakristo wanatafuta maeneo makubwa ya wazi wanajenga kanisa shule/chuo au hata vituo vya afya ili watu wawafuate

Nimalizie kwa kugusia ubaguzi katika taasi chache za kiislamu kama mashule vyuo na hospitali.

Ajira katika hizo taasisi zinatolewa kwa kuangalia dini ya mwombaji badala ya uwezo kitu ambacho kinazidumaza badala ya kuziendeleza, waalimu na madaktasi wazuri waislam wanaajiriwa ktk taasisi za kikristo.

Na katika vikao wanatoa mawazo mazuri tu ya nini kifanyike huduma ziimarike ila kwa wao kuwa na mwalimu mkristo ni kosa, mwisho wanabaki na watu walele wale na mawazo yaleyale.

Ninaimani waislamu wakikaa chini na kuangalia matatizo yao ndani yao kwanza tutajenga taifa imara, opportunity zipo wazitumie, siamini na ntakua wa mwisho kuamini kama Mufti na timu yake wataandaa MoU ya kusaidia taasisi za kiislam kutoa huduma kwa jamii then serikali ikatae siamini hivyo.
 
sawa sawa Mdhamini nimekusoma,hii thread yako inaonyesha we ni Muislam wa tofauti sana.


Ingawa nina mashaka atapokelewaje na wale wenye msimamo mkali wanaoona mapungufu yao yanasababishwa na Wakristo, kupitia Dr. Ndalichako, MoU, na Mfumo Kristo!!
 
Ndugu zangu.


Kwa mtazamo wangu hawa ndio maadui wakubwa wa uislamu kwa Tanzania.

1. Adui namba moja kwa waislamu ni kutokuwa na mashule na vyuo vingi vyenye kutoa elimu bora kwa vijana wa kiislamu na hata wale wa upande wa pili wanaokuja kuitafuta elimu.

2. Ni kukubali kufanywa nyezo ya CCM kupata uhalali wa kutawala kwa kura za waislamu.
4. Kutokufuata mafundisho ya mtume.

I admire your thinking Brother.. Well said.. Naomba hata viongozi wetu na pia waumini wa dini zote wasome maoni yako..

Hekima na confidence zako ni za pekee..Mola atakupa baraka za pekee..

Ndugu zangu imani zetu zisiburutwe na wana siasa..tujijali zaidi sisi wenyewe na sio wao..wahuni na waroho wa madaraka..
 
Mohamedi Mtoi,

Hivi hunajua maana ya mfumo unataja majina ya Chade Othman, Mohamed Shein ndio reference yako kupinga mfumo ebu tupe idadi ya mawaziri wa Tanzania na manaibu wake Waislam wangapi na Wakiristo wangapi. Tutajie idadi ya makatibu wa wizara Waislam wangapi na Wakiristo wangapi. Wizara zote za serikali na makampuni ya umma yote yamejaa Wakiristo unadhani ili limekuja bahati mbaya.

Hakuna hata Muislam mmoja anayejitambua anaweza kukubaliana na hii thread yako ya Chadema, wewe ni kama ni Muislam basi ni "Muslim puppet" hata enzi za mitume walikuwepo ndio maana unaona hii thread yako imependwa na Pro-Chadema wenzako na kukusifia ambao wanakutumia.
 
Last edited by a moderator:
Hivi hunajua maana ya mfumo unataja majina ya Chade Othman, Mohamed Shein ndio reference yako kupinga mfumo ebu tupe idadi ya mawaziri wa Tanzania na manaibu wake Waislam wangapi na Wakiristo wangapi. Tutajie idadi ya makatibu wa wizara Waislam wangapi na Wakiristo wangapi. Wizara zote za serikali na makampuni ya umma yote yamejaa Wakiristo unadhani ili limekuja bahati mbaya.

Hakuna hata Muislam mmoja anayejitambua anaweza kukubaliana na hii thread yako ya Chadema, wewe ni kama ni Muislam basi ni "Muslim puppet" hata enzi za mitume walikuwepo ndio maana unaona hii thread yako umependwa na Pro-Chadema wenzako ambao wanakutumia.

this is vivid and evidently that .... the problem is ignorance/lack of education
 
...

Hivi kuna sababu zozote za kisayansi zinazofanya mtoto awe/asiwe na akili just because of dini yake?? Nikichora graph ya waislamu nlioanza nao primary walioacha shule mpaka nimemaliza shahada ya pili, pyramid ni Kali sana? Where are others??

....

Hapo kwenye red; imani (a.k.a dini) ina nafasi muhimu sana katika maendeleo ya mtoto hilo halina ubishi. Malezi ya awali (early childhood) ni msingi muhimu sana katika kuamua mustakabali wa baadaye wa mhusika iwe kitaaluma au nyanja nyingine zote. Mtoto aliyefundishwa UPENDO tangu anazaliwa huwezi hata mara moja kumlinganisha na aliyefundishwa UWA, CHINJA, PIGA, MAKAFIRI, n.k.
 
We mohamed mtoi hao makafir watakusifu lkn hata cku moja hawawez kukusaidia kwa chochote kwa sbb wakafir wote wanachuk na uislam kama hakuna mfumo kristo memorandum of understndng ya nin? mashirika ya kusaidia waislam kama o.i.c kwann wanayapinga..makafir hakuna kitu cha waislam wakakikubal angala tangu uhuru mpk leo mawazir wakuu wangap wakristo na waislam? baraza la mawazir tangu uhuru waislam wangap?
 
Since 1961 mpaka miaka miwili nyuma ndio anapatikana jaji mkuu muislamu bakwata na sheehena wao mufulis simba waondoshwe na hao vibaraka wa bakwata washtakiwe kwa kuufilisi mali ya waislamu

Ndugu yangu,fungua macho yako na akili yako,ukiendelea kuamini hivo hata watoto wako watakuja kukulaumu!hakuna kitu kinachoitwa mfumo Kristo,hichi kinachoitwa mfumo kristo kimepandikizwa na losers kwa maslah yao binafsi.mie nimesoma nje ya nchi kwa scholarship ya serikali,marafiki zangu wakubwa walikuwa waTZ ambao ni Waislamu na hata majina yao ni ya Ki-Islam!sasa kama kuna mfumo kristo walipewa vip hizi nafasi?we are still gud friends na ukiwauliza wao hawakubalian na hii dhana ya mfumo kristo.mkuu amka pata elimu dunia,wapeleke watoto shule ili kesho na keshokutwa wasije kukulaumu.
 
Mohamedi Mtoi,

Hivi hunajua maana ya mfumo unataja majina ya Chade Othman, Mohamed Shein ndio reference yako kupinga mfumo ebu tupe idadi ya mawaziri wa Tanzania na manaibu wake Waislam wangapi na Wakiristo wangapi. Tutajie idadi ya makatibu wa wizara Waislam wangapi na Wakiristo wangapi. Wizara zote za serikali na makampuni ya umma yote yamejaa Wakiristo unadhani ili limekuja bahati mbaya.

Hakuna hata Muislam mmoja anayejitambua anaweza kukubaliana na hii thread yako ya Chadema, wewe ni kama ni Muislam basi ni "Muslim puppet" hata enzi za mitume walikuwepo ndio maana unaona hii thread yako imependwa na Pro-Chadema wenzako na kukusifia ambao wanakutumia.

Soma TAFAkuri jadidi ZA MMtoi na AishaDiii bila jazba!!!!! MTU hateuliwi KWA dini AU Kabila lake, Bali uwezo na elimu yake!
 
Last edited by a moderator:
Matatizo mengi ya kidini yatapungua kama sio kwisha kwa kuwapeleka watoto shule na vyuoni.

Hakuna njia ya mkato wala rahisi ya kusawazisha mambo iliyo rahisi zaidi ya kwenda shule na kupata elimu itakayotuwezesha kushindania nafasi na fursa mbalimbali nchini. Kila kona msikiti sasa iwe kila kona shule, na vyuo. Jinsi nchi yetu ilivyo na watu wake walivyo haitakuja kutokea nchi yote ikaendeshwa Kikristo wala Kiislamu ktk miaka michache ijayo. dawa ni kujiweka sawa kugombania kazi na fursa zilizopo za kazi uongozi, madaraka.

Kumbuka wakati mtoto mmoja yuko madrasa anahifadhi Quran tukufu kifuani yuko mtoto mwingine wakati huohuo anayehifadhi Hisabati kichwani. Mwisho wa siku watoto wote wawili watatakiwa wakutane kwenye chumba kimoja na mtihani mmoja wa Hisabati, we unadhani hilo pambano atashinda nani?. Mshindi wa pambano hilo ndo atakaepewa zawadi ya kujiunga na sekondari, chuo, ajira, uongozi na urais ikibidi.

Angalieni sana waislamu fujo hazitatufikisha kule tunakokwenda katika nchi kama yetu yenye dini mbalimbali.
 
Nadhani hujamuelewa Mtoi; amedai haoni tatizo liliopo liwe ni mfumo kristo kama unavyodaiwa au mfumo wa ukandamizaji; cha kushangaza amekuja mawazo ya kurekebisha mfumo ambao hauna tatizo; yeye haoni tatizo la mfumo mzima kwa sababu lengo lake kuu ni kutaka kuishutumu CCM; ushauri ni serikali kuvunja MoU na taasisi zote za kidini hapo ni pa kuanzia tu.

Chama
Gongo la mboto DSM

Mkuu chama,
Huyu jamaa ni muslim puppet anakuambia haoni tatizo lolote wala hakuna mfumo kisrto wabaya ni Waislam wenyewe.
 
Last edited by a moderator:
Tatizo kubwa ni Elimu na Kutokuwa na Ajira.

Angalia wanaoleta vurugu ni raia wa aina gani?- wengi wao hawana elimu na hawana ajira.
 
Nimebarikiwa sana na hii thread. Hii usaarabu natamani ungekuwepo mbagala na kwingineko, yasingetolea yaliyotokea.
 
Hii ni thread ya mwaka.

Sijasoma watu wote lakini mtoa mada na wifi kipenzi AshaDii mmemaliza. Mkiweza kulitambua hilo na kulifanyia kazi hakika maisha yatakuwa ya amani.

Natamani adui yetu sote awe ibilisi. Kitu kimoja cha muhimu sana nilifundishwa, kumuona shetani mbele ya kila jambo baya. Hata mtu aniudhi naambiwa muombee, that way unampalia makaa. Badala ya kupambana head on, unamuombea aone nuru ya Mungu wako. That way unamuachia maswali. Lakini haswa ustaarabu wa dhahiri unahusika. Tunaishi vema na ndugu zetu wa damu wenye imani tofauti, tusishindwe kuheshimiana.
 
Binafsi naamini kwamba matatizo yetu lazima tuyaangalie kuanzia ndani kwetu kabla ya kwenda nje. Mengi yamesemwa kuhusu mfumo kristo na ubaya wa Nyerere kwa waislamu wa Tanzania, lakini tujiulize, je waislamu na wingi wao na nguvu zao za kifedha, wamejifanyia nini katika kuondokana na hii hali?

Mimi ni mkristo lakini nimekulia maeneo ambayo yana idadi kubwa sana ya waislamu(Mabibo na Magomeni). Kitu kikubwa nilichokiona ni mwamko mdogo wa elimu katika marafiki zangu wengi. Kwa mfano nyumba niliyokuwa ninaishi, mzee mwenye nyumba alikuwa na watoto sita na wote walikuwa hata sekondari hawajafika! Mtoto wake wa mwisho alimtoa Dodoma alikokuwa amemaliza darasa la saba, wakati huo mimi nilikuwa nimemaliza darasa la saba, Baada ya muda kidogo akampeleka kujifunza ufundi wa feni. Leo hii mimi nina elimu ya chuo kikuu, sijasomea hizo St Mary's, kupitia hizi za wizara ya elimu(Kibasila & Tambaza), yeye bado anatengeneza feni Magomeni. Kesho nikiteuliwa mkurugenzi kwenye shirika la umma, ni yeye huyo huyo atakayesema haya ni matokeo ya mfumo kristo!!

Mambo mengine yanakera kuambiwa lakini ukweli lazima usemwe. Hii hali ipo kila sehemu, ni kawaida sana kukuta familia nyingi za waislamu ambazo wengi wa wanafamilia elimu zao ni duni sana, wakati wale ambao wazazi wao walipata elimu wanafanya juu chini kuhakikisha watoto wao wanapata elimu nzuri

Waislamu amkeni, hakuna mtu duniani hapa atayekuja kuwaokoa

Hivi leo hii Sheikh Ponda na ushawishi wake wote alionao angeamua kufanya ziara nchi nzima kufanya michango ya ujenzi wa vyuo vikuu, imagine wangepata fedha kiasi gani? Mbona waislamu ni hodari sana katika kujenga majumba ya ibada, wanashindwaje kutafsiri uhodari huo kwenda kwenye elimu? Mna nguvu sana ya pesa, mmehodhi biashara nyingi sana hapa Tanzania lakini kwa namna moja au nyingine mmeshindwa kutafsiri hali hiyo kwenda kwenye elimu. Angalia waluteli kila siku wanavyofanya harambee za ujenzi wa vyuo. Hata hiyo MOU inayolalamikiwa, hata waislamu wana haki nayo, kama Kikwete alivyosema,
"Napenda kuwahakikishia kuwa hakuna kitu cho chote ambacho Serikali itatoa kwa dini moja ambacho dini nyingine itanyimwa. Kwa kweli mbele ya Serikali dini zote zina haki sawa. Kama hujaomba usimlaumu aliyeomba akapewa au aliyempa. Kama yupo anayeamini anazo sifa kama mwenzake aliyepewa aombe naamini atapewa. Iwapo itafanyika vinginevyo dai haki yako kwa mamlaka zinazohusika."


Play your part first
 
Soma TAFAkuri jadidi ZA MMtoi na AishaDiii bila jazba!!!!! MTU hateuliwi KWA dini AU Kabila lake, Bali uwezo na elimu yake!

AshaDii na Mohamed Mtoi, wanamitazamo yao huwezi kusema matatizo ya Waislam ni Waislam wenyewe nimeongea mwanzo Muislam makini anayejitambua hawezi kubaliana na mawazo yao ya kichadema.

Kama kweli wao wanaona hakuna tatizo la mfumo kristo wagombee uongozi ndani ya Chadema waone na huo Uislam wao Zitto anapendwi Chadema kwa nini?

Ndio maana unaona huu uzi Chadema wote wanauchangia pongezi nyingi lakini dini yetu imetuambia miongoni mwetu wanafiki huwa hawakosi.
 
Mohamed Mtoi na AshaDii

hats off to you!

Kuna baadhi ya viongozi wa dini (wakristo na waislamu) hujigeuza wao kuwa ndio dini yenyewe na wengine hata kujiona ndio Mungu mwenyewe. Waumini pia humfuata muhubiri, siyo dini, siyo Mungu. Huwaabudu wahubiri au viongozi wa dini.

Kwa mtazamo wangu, hawa viongozi wa namna hii wa dini ndio hugeuka sumu kwa jamii pale watakapoamua kutafuta umaarufu na sifa badala ya kuhubiri dini. Kwa bahati mbaya, namna yetu kutafuta umaarufu ni kutofautisha waumini wako na wale ambao siyo waumini wako. Kupandikiza chuki,mfitina, uadui, hasira, dharau na kadhalika

sasa hii ya kugeuza waumini kuwa militants, vibaka, na magaidi ndo kilele cha kiongozi wa dini kujigeuza ndio Mungu au dini yenyewe. Hivyo anafanikiwa kuwapotosha waumini wake, kuwapoteza, na kufanya watu wengine kuhoji iweje Mungu aamrishe maovu. Kwa hiyo, mwisho wanakuwa wamemgeuza dini yao na Mungu wao kuwa muovu, mwenye chuki, mhujumu wa binadamu na mali zao.

Consequence of our commands and actions to that very which we strive to achieve. Hapa upeo wa shehe Ponda na Fareed ulikuwa Mdogo sana. Wamedhalilisha dini yetu sana
 
Mkuu chama,
Huyu jamaa ni muslim puppet anakuambia haoni tatizo lolote wala hakuna mfumo kisrto wabaya ni Waislam wenyewe.

Wewe ambaye ni mwislamu wa kweli umefanya nini kurekebisha hiyo hali? Do you believe kuwa kwa kuandamana utawatoa makatibu wakuu wa wizara na wakurugenzi wa mashirika? Tafuteni njia za kutatua matatizo zenye kuleta tija. Nyie kila mtu aliye na nafasi serikali ni puppet. Mwema, Chande, Dau, Kikwete wote hao kwenu nyie ni ma-puppet tu. Ulitaka Jaji mkuu awe Sheikh Ponda?​
 
Umenichekesha nina coaligue mpya alinipa stori yake na nssf. Anaitwa jina la kiislamu. Sasa akaajiriwa harakaharaka. Baada ya mwaka wakagundua sio muislamu, akahamishiwa mtwara akiwa na ujauzito wa miezi 5. Akagoma kuondoka. Akatafuta kazi akaondoka baada ya kukaa mtwara 3 months.Sasa baba unataka tuanze kufanya interview kwa dini? Umeniacha solemba.
Mohamedi Mtoi,

Hivi hunajua maana ya mfumo unataja majina ya Chade Othman, Mohamed Shein ndio reference yako kupinga mfumo ebu tupe idadi ya mawaziri wa Tanzania na manaibu wake Waislam wangapi na Wakiristo wangapi. Tutajie idadi ya makatibu wa wizara Waislam wangapi na Wakiristo wangapi. Wizara zote za serikali na makampuni ya umma yote yamejaa Wakiristo unadhani ili limekuja bahati mbaya.

Hakuna hata Muislam mmoja anayejitambua anaweza kukubaliana na hii thread yako ya Chadema, wewe ni kama ni Muislam basi ni "Muslim puppet" hata enzi za mitume walikuwepo ndio maana unaona hii thread yako imependwa na Pro-Chadema wenzako na kukusifia ambao wanakutumia.
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom