Makete Kwetu
JF-Expert Member
- Jan 8, 2012
- 531
- 165
HUKUMU ya kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wa jimbo la Segerea, yaliyompa ushindi Dk. Makongoro Mahanga (CCM), itatolewa Mei 2 mwaka huu.
Katika kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Ibrahim Juma, aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA, Fred Mpendazoe, anaiomba makahama itengue matokeo hayo kwa vile kulikuwa na kasoro kadhaa.
Jana, Jaji Juma aliamuru kuwa April 11 itakuwa siku ya kukutana kwa pande zote mbili na April 19 mwaka huu, mawakili wa pande zote mbili watawasilisha hoja kwa njia ya maandishi.
Katika utetezi wake jana, Dk. Mahanga alidai kuwa katika Tanzania nzima ni jimbo la Segerea pekee ndilo alilolisikia kuna mtu kakamatwa na masanduku ya kura huku akikana kuhusika wala kuitwa na polisi kuhusiana na wizi wa masanduku.
Dk. Mahanga alisema hayo mbele ya Jaji Juma wakati akijibu swali la wakili wa Mpendazoe, Peter Kibatala, lililotaka kueleza kama alifahamu kukamatwa kwa masanduku ya kura, alijibu kuwa hakuwahi kufika katika kituo cha polisi Buguruni wala kukamatwa na masanduku hayo na kwamba taarifa hizo alizisikia katika vyombo vya habari.
Alipoulizwa kama anakumbuka kutokea mgogoro wowote, alikiri akisema hatua hiyo ilimlazimu yeye Mpendazoe kufika katika kituo hicho na kuongeza kuwa CCM ilisaidia katika uchaguzi kwani ilikuwa na maslahi naye.
Kuhusu alikoipata elimu yake ya falsafa ya udaktari (PhD), Dk. Mahanga alisema kuwa alisoma Washington Marekani ila hakuwahi kupeleka vyeti vyake katika Tume ya Vyuo vikuu nchini iidhinishwe, isipokuwa alivipeleka kwa aliyekuwa mwajiri wake Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Pia alidai kuwa hakuwahi kuiona barua ya malalamiko ya kuchaguliwa kwake na wajumbe wa NEC iliyopelekwa kwa Katibu Mkuu ikiwa ni pamoja na kukanusha madai ya Mpendazoe ya kwamba alipata kura 56,962 dhidi ya 4,404 za Dk. Mahanga.
"Matokeo yalionyesha kuwa mimi nilipata kura 43,554 na Mpendazoe kura 39,150 ambazo ndizo zilitangazwa," alisema.
Source: Tanzania Daima