Hatma ya Mahanga kujulikana Mei 2, 2012!

Tuna taaluma nyingi sana hapa nchini hata kama zimeoza lakini nyingine zinasaidia. Mfano mwalimu anaanza na mtoto hajui kusoma na mwisho wake anasoma na kuandika lakini kazi ambzo watanzania wengi hawaziamini na wanajua wapo kwa ajili ya kutimiza wajibu ni mahakama na mahakimu wao na majaji, ni wachache sana wanaokataa kula na kutoa hukumu ya kweli hata mbele ya macho ya Mungu.
 
Tumsubiri Mungu wetu! Haki yetu ipo ila itacheleweshwa tu! Mungu ibariki Tanzania,ibariki cdm,na watu wake pia.
 
Jamani kama Segerea Mahanga akishinda, navua uraia wa hii nchi natafuta ukimbizi nchi yoyote hata Burundi.
 
ngoja tusubiri hukumu ili tuendelee kujiridhisha kama kweli mahakama zetu zinafanya maamuzi/kutoa hukumu kwa rimoti
 
Magamba wanatumia nguvu ya dola kushinda, serikali yao, mahakama yao, polisi wao, jela zao, tume ya uchaguzi yao na sheria ni za kwao hivyo WATALAZIMISHA KUSHINDA KESI!

Usikate tamaa hakuna jeshi,polisi. vifaru, mabomu mizinga jela nk ziliwahi kushinda nguvu ya umma, makaburu walikuwa na nguvu za ajabu sana lakini walifika mahali nguvu ya uma ikashinda rejea movie ya sarafina! Ni Swala la muda tu juzijuzi tumeshuhudia ghadaffi na madege yake, vifaru makombora askari wengi mbwa farasi mabomu akifa kifo cha aibu tena akijificha chini ya mtaro mfano wa panya! Siku watanzania wakiamua inawezekana!!
 
Tumsubiri Mungu wetu! Haki yetu ipo ila itacheleweshwa tu! Mungu ibariki Tanzania,ibariki cdm,na watu wake pia.

Mungu ameshamaliza kazi yake katupa akili ya kuona tunavonyanyaswa na kunyimwa haki zetu kafungua macho yetu tukaona uonevu, wizi, ufisadi, upendeleo, kulindana ndani yab taifa letu sasa hawezi kushuka kupigania haki hizo ni sisi tuanzishe mapambano na yeye mungu atusimamie maana siku zote yeye husimama upande wa haki!
 
Jamani wanchadema na wanamageuzi wote nchini sote kwa pamoja tumwamini Mungu basi haki yetu itathibitika kwani haki huinua taifa na pasipo haki taifa huanguka.
Thanks u ol and long live CDM.
 
Sintaona ajabu kama Mahanga atashinda kwani inasemekana huyo jaji anayesikiliza hiyo kesi ingawa ana uprofesa lakini ni M-serikari [ wa mkweree]!
 
CCM haiwezi nyang'anywa jimbo hata moja believe me. Ukiacha Kihiyo na Kinyondo ambao kesi zao ziliwashinda na majaji wakaona aibu, Majaji hawa wa JK wote ni walipa fadhila. Sanasana watakachofanya ni ku-neutralise hukumu ya Arusha kwa kutengua jimbo moja ambalo kwa CCM itakuwa rahisi kuchakachua na kushinda.

2015 haitakiwi kutegemea mahakama tena ila wananchi wajue kuwa wakiruhusu mtu akitangazwa mshindi bila kushinda kura zao basi watulie tu kudumisha amani na utulivu maana kwenda mahamani haina maana tena.
 
Kuna habari za ndani Jaji anayesikiliza kesi hiyo kushinikizwa kuitupilia mbali ingawa ushahidi uko wazi.

Kesi hiyo ni ngumu kwa Bw. Mahanga ( Sio Mh. Mahanga) kwani imemkalia vibaya mno na kuna hati hati ya kupoteza Ubunge wake na Uwaziri pia.

Mwenye tetezi zaidi atuwekee humu je, ni kweli.


Watanzania tuwe makini na majaji wetu kwani kuna dalili ya Magamba kuwaingilia katika kazi zao. Kwa mtazamo wangu hii ni kushusha hadhi na heshima ya mahakama nchini mwetu.

Nawasilisha hoja.
 
Wanajf wote kwa pamoja twendeni kusikiliza hukumu ya kesi ya kupinga matokeo ya jimbo la segerea ambapo makongoro mahanga alitangazwa mshindi kwa wizi , mda ni kwanzia saa 4 asubui japo sijui ni mahakama gani twendeni wote
 
Ndugu zangu kwa mwendo wa hizi mahakama zetu nahisi Mpendazoe anaweza chezewa mchezo mchafu kwenye hukumu inayotarajiwa kutolewa tar2 mwezi ujao. Kwa mwenendo wa kesi ile Mahanga hatakuwa na chake kama mahakama itatenda haki kisheria. Je' wewe unahisi kipi chaweza kutokea japokuwa tunasubiri maamuzi ya mahakama?
 
Back
Top Bottom