Hatma ya Mahanga kujulikana Mei 2, 2012!

Makete Kwetu

JF-Expert Member
Jan 8, 2012
531
165
HUKUMU ya kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wa jimbo la Segerea, yaliyompa ushindi Dk. Makongoro Mahanga (CCM), itatolewa Mei 2 mwaka huu.

Katika kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Ibrahim Juma, aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA, Fred Mpendazoe, anaiomba makahama itengue matokeo hayo kwa vile kulikuwa na kasoro kadhaa.

Jana, Jaji Juma aliamuru kuwa April 11 itakuwa siku ya kukutana kwa pande zote mbili na April 19 mwaka huu, mawakili wa pande zote mbili watawasilisha hoja kwa njia ya maandishi.

Katika utetezi wake jana, Dk. Mahanga alidai kuwa katika Tanzania nzima ni jimbo la Segerea pekee ndilo alilolisikia kuna mtu kakamatwa na masanduku ya kura huku akikana kuhusika wala kuitwa na polisi kuhusiana na wizi wa masanduku.

Dk. Mahanga alisema hayo mbele ya Jaji Juma wakati akijibu swali la wakili wa Mpendazoe, Peter Kibatala, lililotaka kueleza kama alifahamu kukamatwa kwa masanduku ya kura, alijibu kuwa hakuwahi kufika katika kituo cha polisi Buguruni wala kukamatwa na masanduku hayo na kwamba taarifa hizo alizisikia katika vyombo vya habari.

Alipoulizwa kama anakumbuka kutokea mgogoro wowote, alikiri akisema hatua hiyo ilimlazimu yeye Mpendazoe kufika katika kituo hicho na kuongeza kuwa CCM ilisaidia katika uchaguzi kwani ilikuwa na maslahi naye.

Kuhusu alikoipata elimu yake ya falsafa ya udaktari (PhD), Dk. Mahanga alisema kuwa alisoma Washington Marekani ila hakuwahi kupeleka vyeti vyake katika Tume ya Vyuo vikuu nchini iidhinishwe, isipokuwa alivipeleka kwa aliyekuwa mwajiri wake Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Pia alidai kuwa hakuwahi kuiona barua ya malalamiko ya kuchaguliwa kwake na wajumbe wa NEC iliyopelekwa kwa Katibu Mkuu ikiwa ni pamoja na kukanusha madai ya Mpendazoe ya kwamba alipata kura 56,962 dhidi ya 4,404 za Dk. Mahanga.

"Matokeo yalionyesha kuwa mimi nilipata kura 43,554 na Mpendazoe kura 39,150 ambazo ndizo zilitangazwa," alisema.

Source: Tanzania Daima
 
Huyu Makongoro Mahanga kumbe hata udokita alionao ni feki! mimi ndio kwanza nimepata habari hizo kupitia magicfm jamani hawa watu mbona wanapenda sana ukubwa ambao hawana wanachekesha kweli!!!!:heh:
 
Huyo jaji wa kesi ya kupinga matokeo ya jimbo la segerea atoe haki,asipo toa haki nitajua kuwa ikulu imeingilia kesi hiyo kama ilivyoingilia kesi ya Lema.
 
Serikali inaingilia uhuru wa Bunge na hata mahakama kwa kuwalazimisha wafanye yale yenye manufaa kwao; mfano ni pale Rais alipoliamuru bunge kubadilisha sheria ya mchakato wa kuandika katiba mpya mara tu baada ya yeye kuridhia!! Kama aliweze kufanya hivyo kwa bunge kitu gani kitamzuia asifanye vivyo hivyo kwa mahakama ambayo yeye ndio mteuzi wao?Jinsi hukumu za uchaguzi zinavyotolewa mwelekeo ni kwamba sasa ccm inatumia mahakama kukandamiza demokrasia na sintaona ajabu huyu jaji akitupilia mbali kesi ya Mahanga!!
 
Mungu atatupigania wanamapinduzi hatuendi msituni wala kushika silaha yeyote lkn machozi yetu atayafuta kwa kutupatia haki yetu
 
HUKUMU ya kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wa jimbo la Segerea, yaliyompa ushindi Dk. Makongoro Mahanga (CCM), itatolewa Mei 2 mwaka huu.

Katika kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Ibrahim Juma, aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA, Fred Mpendazoe, anaiomba makahama itengue matokeo hayo kwa vile kulikuwa na kasoro kadhaa.
Jana, Jaji Juma aliamuru kuwa April 11 itakuwa siku ya kukutana kwa pande zote mbili na April 19 mwaka huu, mawakili wa pande zote mbili watawasilisha hoja kwa njia ya maandishi.

Katika utetezi wake jana, Dk. Mahanga alidai kuwa katika Tanzania nzima ni jimbo la Segerea pekee ndilo alilolisikia kuna mtu kakamatwa na masanduku ya kura huku akikana kuhusika wala kuitwa na polisi kuhusiana na wizi wa masanduku.

Dk. Mahanga alisema hayo mbele ya Jaji Juma wakati akijibu swali la wakili wa Mpendazoe, Peter Kibatala, lililotaka kueleza kama alifahamu kukamatwa kwa masanduku ya kura, alijibu kuwa hakuwahi kufika katika kituo cha polisi Buguruni wala kukamatwa na masanduku hayo na kwamba taarifa hizo alizisikia katika vyombo vya habari.
Alipoulizwa kama anakumbuka kutokea mgogoro wowote, alikiri akisema hatua hiyo ilimlazimu yeye Mpendazoe kufika katika kituo hicho na kuongeza kuwa CCM ilisaidia katika uchaguzi kwani ilikuwa na maslahi naye.

Kuhusu alikoipata elimu yake ya falsafa ya udaktari (PhD), Dk. Mahanga alisema kuwa alisoma Washington Marekani ila hakuwahi kupeleka vyeti vyake katika Tume ya Vyuo vikuu nchini iidhinishwe, isipokuwa alivipeleka kwa aliyekuwa mwajiri wake Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Pia alidai kuwa hakuwahi kuiona barua ya malalamiko ya kuchaguliwa kwake na wajumbe wa NEC iliyopelekwa kwa Katibu Mkuu ikiwa ni pamoja na kukanusha madai ya Mpendazoe ya kwamba alipata kura 56,962 dhidi ya 4,404 za Dk. Mahanga. Matokeo yalionyesha kuwa mimi nilipata kura 43,554 na Mpendazoe kura 39,150 ambazo ndizo zilitangazwa,” alisema.

Source: Tanzania daima
 
Lazima atoswe muhuni huyu, lakini Gamba litahakikisha linauwa kesi kidesign. Loh..! kazi ipo.

Kapata kura 43,554 na Mpendazoe kura 39,150 ???????, wizi mtupuuu.:shock:
 
Makongoro ni waziri hakuna kesi pale asingepewa uwaziri km kungekuwa na kesi itakayohtrsh ubunge wake hapo kalaghabao imekula kwenuuu
 
haya wadau jimbo la segerea.....mambo yamekuwa ni moto hukumu ya kupinga matokeo ya ubunge wa jimbo la segerea
sasa imeiva na hukumu kutajwa may 2 mbili mwaka huu.....je mnadhani yaliyotokea arusha mjini sasa yanaweza tokea jiji la dar es salaam......je jamaa anaweza vuliwa ubunge wake....au atashinda

source...mwanachi,rai,mtanzania,na baadhi ya wanachama wa ccm......
 
Mahanga atashinda kwavile ccm imedhamilia kuhujumu mafanikio ya upinzani kwa bei yeyote ile kwa kutumia mahakama na hasa kwavile hawa majaji wa siku hizi nao wamekuwa kama sekondari za kata!!
 
Bora tupate katiba mpya kwani katiba ya sasa ni kichaka cha uonevu, ufisadi, usaliti. Usishangae kusikia anapeta
 
Buriani makongoro mahanga ,hiyo PHD yako kama sio zile za internet cafee tunataraji kukuona vyuon ukikata pindi!
 
Back
Top Bottom