Wewe ni expert sugu ila tu watu hawajakufahamu kwa sababu hawajui mambo haya na wanapenda kujifariji na umbea mwingi. Nimefuatilia maoni yako kwenye post mbili hivi, nimejifunza kitu kikubwa sana toka kwako....... Big upMkuu walimu ni waajiriwa wa Wakurugenzi, lakini 'MAMLAKA YAO YA AJIRA NA NIDHAMU NI TSD AMBAYO NI SERIKALI KUU' ndio maana hata post zao hazitangazwi na TAMISEMI, wanapandishwa vyeo na TSD Mkurugenzi hawezi kubadili mishahara bila idhini ya UTUMISHI. Mwenye Jukumu la kusimamia MIUNDO NA VIWANGO VYA MISHAHARA YA WATUMISHI WOTE NCHINI NI UTUMISHI, wao wakisema HAPANA hakuna marekebisho yatakayofanyika.
Kwanza sio malengo yangu kupotosha watu, ilikuwa ni katika kushare information kidogo tulizonazo.
Pili ukisoma kipengele cha nne cha barua ile utaona anasisitiza kwamba kwa wale wenye shida kwenye madaraja yao watapandishwa kulingana na waraka mpya na hawataruhusiwa kudai malimbikizo..Swali: Je kulikuwa na haja gani ya kufika kote huko kama swala bado halijakubakiwa na utumishi?
Wewe ni expert sugu ila tu watu hawajakufahamu kwa sababu hawajui mambo haya na wanapenda kujifariji na umbea mwingi. Nimefuatilia maoni yako kwenye post mbili hivi, nimejifunza kitu kikubwa sana toka kwako....... Big up
Ndg yangu inaelekea hujui kabisa mfumo wa serikali, tofautisha mamlaka ya ajira na upandishwaji wa vyeo na nidhamu na upandishwaji wa mishahara. Mwenye dhamana ya kutangaza nyongeza ya mishahara serikalini ni Waziri wa ofisi ya Rais management ya Utumishi wa Umma, na anayetoa waraka ni katibu wake Mkuu, katika kifuatilia bajeti ya serikali umewahi hata sikia waziri wa elimu au hata Tamisemi katangaza nyongeza ya mshahara? Mifumo wa sasa mapendekezo ya kuongeza mishahara hujadiliwa kisekta na kupeleka mapendekezo kwa Waziri mwenye dhamana ili wajadiliane na Waziri wa fedha kabla ya kutangazwa ili baadae utolewe waraka kwa waajiri. Ukisoma document hii tunayosema ni waraka, ni maelekezo ya mkoa kwa walimu kuandikisha majina wale ambao wanafikiri madaraja yao yamekosewa, hivyo hata mleta uzi ametupotosha wote hapa. Nawasilisha
Ki2 kinaeleweka, hebu download upload hizo nyaraka ziko wazi. Tunashukuru kwa kaz nzur
Hii ni barua toka kwa katibu tawala wa mkoa wa Kilimanjaro kwenda kwa wakurugenzi wa halimashauri kuwajulisha juu ya waraka mpya uliotolewa unaorekebisha waraka wa 2002 kuhusu mishara ya kada ya utumishi wa walimu. Pamoja na mambo mengine, unaelezea malimbikizo ya mishara ya nyuma ya walimu kuwa haitalipwa badala yake wataingizwa moja kwa moja kwenye madaraja mapya kulingana na waraka huo. Sasa la msingi la kujiuliza, ni hii hii serekali sikivu ya SSeM ndio waliotoa waraka huo, na kama ni ndio, ni kweli watautekeleza, au ni yale yale ya kuwatapeli watanzania
kwa kauli za maisha bora kwa kila mtanzania? Kumbuka tunaelekea uchaguzi.