Hatimaye yametimia walimu kucheka huu ndiyo waraka mpya.

Wakuu vipi walimu wa vyuo vikuu pia wamo kweye mabadiliko haya ya mishahara..
 
hivi walimu wasomi wazima, mnaweza kukubali uongo uliowekwa na mleta mada hapo juu?kimsingi if u think logically hata haiingii akilini hilo ongezeko la mshahara.Ila kam ni kweli ,basi -heko walimu wa Tanzania ,kwa Afrika mtakuwa wa kwanza kilipwa mshahara mkubwa kiasi hicho.
 
Tatizo mnafikiri ualimu ni kazi ya kifukara, sikatai kwani ndo kazi za watoto wa familia masikini kwani kazi zingine hadi uwenandugu ktk system
 
Walimu wa Tanzania wepesi sana kudanganyika. Hiyo post imewafunga kamba watu wengi.
 
Ndg yangu inaelekea hujui kabisa mfumo wa serikali, tofautisha mamlaka ya ajira na upandishwaji wa vyeo na nidhamu na upandishwaji wa mishahara.

Mwenye dhamana ya kutangaza nyongeza ya mishahara serikalini ni Waziri wa ofisi ya Rais management ya Utumishi wa Umma, na anayetoa waraka ni katibu wake Mkuu, katika kifuatilia bajeti ya serikali umewahi hata sikia waziri wa elimu au hata Tamisemi katangaza nyongeza ya mshahara?

Mifumo wa sasa mapendekezo ya kuongeza mishahara hujadiliwa kisekta na kupeleka mapendekezo kwa Waziri mwenye dhamana ili wajadiliane na Waziri wa fedha kabla ya kutangazwa ili baadae utolewe waraka kwa waajiri.

Ukisoma document hii tunayosema ni waraka, ni maelekezo ya mkoa kwa walimu kuandikisha majina wale ambao wanafikiri madaraja yao yamekosewa, hivyo hata mleta uzi ametupotosha wote hapa.

Nawasilisha
 
hii inawezekana, ukitilia maanani uchaguzi ujao hauko mbali sana. Na hiki chama tawala inaonekana kimeshikwa pabaya!!
 
attachment.php
 
WAPENDWA HAYA NI MAISHA YA WATU,NAOMBA ALIYEFANIKISHA KUUSOMA ATUPE Taarifa unahusu nn?

Nimesoma,una nembo ya jamuhuri ila hakuna muhuri ,anwani ni za mkuu wa mkoa wa kilimanjaro ndiye mwandish kwenda kwa katibu tawala mkoa kilimanjaro,pia nimeona anwani ya afisa elimu same,naona imekaa kisanii.
 
Ndg yangu inaelekea hujui kabisa mfumo wa serikali, tofautisha mamlaka ya ajira na upandishwaji wa vyeo na nidhamu na upandishwaji wa mishahara.

Mwenye dhamana ya kutangaza nyongeza ya mishahara serikalini ni Waziri wa ofisi ya Rais management ya Utumishi wa Umma, na anayetoa waraka ni katibu wake Mkuu, katika kifuatilia bajeti ya serikali umewahi hata sikia waziri wa elimu au hata Tamisemi katangaza nyongeza ya mshahara?

Mifumo wa sasa mapendekezo ya kuongeza mishahara hujadiliwa kisekta na kupeleka mapendekezo kwa Waziri mwenye dhamana ili wajadiliane na Waziri wa fedha kabla ya kutangazwa ili baadae utolewe waraka kwa waajiri.

Ukisoma document hii tunayosema ni waraka, ni maelekezo ya mkoa kwa walimu kuandikisha majina wale ambao wanafikiri madaraja yao yamekosewa, hivyo hata mleta uzi ametupotosha wote hapa.

Nawasilisha

Kwanza sio malengo yangu kupotosha watu, ilikuwa ni katika kushare information kidogo tulizonazo.
Pili ukisoma kipengele cha nne cha barua ile utaona anasisitiza kwamba kwa wale wenye shida kwenye madaraja yao watapandishwa kulingana na waraka mpya na hawataruhusiwa kudai malimbikizo..Swali: Je kulikuwa na haja gani ya kufika kote huko kama swala bado halijakubakiwa na utumishi?
 
Back
Top Bottom