Hamad kufikishwa kamati ya maadili ya CUF, asema Mtatiro

Kwanini Naibu Katibu Mkuu wa Visiwani asikaimu nafasi hiyo automatically? Je, Mtatiro ana full authority ya kufanya maamuzi as Katibu Mkuu au ndio ile ya kukaimu jina lakini maelekezo, maagizo na maamuzi yanatoka kwa Maalim?

Yanatoka kwa maalim seif,si hata hii habari ya kuzuia mikutano ya hamad rashid umesikia seif alimuagiza bwana Julius aizuie kwa kutumia jeshi lao la blue guard?ila mimi nashangazwa na ukimya wa mwemyekiti bwana Haruna,mbona yuko kimy kwenye suala nyeti kama hili?kwanini hawakemei maalimu seif,bwana Hamad na bwana Julius kuhusu kwenda public?je ni kweli hana ubavu kwa maalim?
 
Kamati ya nidhamu na maadili ya chama ipo, labda yeye haifahamu kwa sababu anafanyia shughuli za chama vijiweni na anakwepa kuzifanya kwa kufuata taratibu zilizopangwa. Hakuna watu wanaokimbizwa mikoani kuokoa hali ya mambo. Hakuna tunachookoa zaidi ya kujipanga zaidi na zaidi. Haya masuala ya kina hamad rashid(MB) ni masuala ya vikao vya chama na kamati maalum za nidhamu. Vikoa na kamati husika vinafanya kazi kwa mujibu wa katiba ya chama. Kama kuna mtu amekiuka taratibu za chama na kama mtu ana kampeni ya kukigawa chama na kukivunja katiba ya chama itasimama na vikao vitaitumia kufanya maamuzi. Kwa hiyo, hapa hakuna vita ya mtu na mtu, hapa kuna vita ya kuchezea katiba. Kama kuna mtu mwingine yeyote(hata kama ni mie mtatiro) anakiuka taratibu za chama, chama kitamtendea haki yake kwa mujibu wa katiba, na kwa bahati mbaya CUF haitetereshwi na mtu mmoja, CUF ni chama chenye wafuasi wengi na hivyo hakitegemei mtatiro, wala hamad rashid wala maalim seif wala lipumba. Yeyote yule akichezea katiba ya chama, katiba itamtendea haki.
Sisi hatutatuma wajumbe mikoani kufanya kampeni zozote. Wenye chama huko vijijini wanajua nani anataka kuua chama na wamejionea wenyewe watu walivyo tayari hata kuua kwa mapanga ili kutafuta madaraka kinyume na taratibu za chama.
Kwa ujumla rapsha za juzi hazijakiteteresha chama, chama kinazidi kuimarika na kujipanga zaidi kila kinapopata misukosuko na CUF ni chama cha kipekee ambacho kimepitia misukosuko mingi. Hata hili la hamad rashid litamalizwa kwa utaratibu mzuri na kila upande utatendewa haki na katiba.

Mtatiro,

Wasiwasi wangu ni kwamba utakuja kujikuta wewe ndiye unatimuliwa CUF na kuwaacha wenyewe wakiendelea na maisha kama kawaida.
Sitaki kuamini kwamba Hamad Rashid hajui taratibu za chama, wala sitaki kuamini kirahisi kwamba Hamad Rashid anaweza kushindwana na Maalim Seif.
Kwakuwa kuna maneno mitaani kwamba ma-senior members wa CUF wanaotokea upande wa pili hawakufurahia jinsi ulivyopita pita haraka haraka hadi kufika hapo ulipo, kuwa naibu katibu mkuu na kuwaacha wanachama mahiri na wakongwe ndani ya chama, naona kama kuna zengwe linatengenezwa hapa na usipokuwa makini utakuwa bangusilo.

Kuna hii skendo ya kutumia mamilioni ya chama kule igunga bila idhini ya wenye chama, nayo ni agenda inayokuweka pabaya. Na mbaya zaidi chama chenu kimepata matokeo mabaya sana igunga pamoja na kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha ambacho hamjawahi kukitumia hata kwenye kugombea uraisi. Hapa sikuoni ukichomoka ndugu yangu, wameshakuelekeza kibla!!
 
Mtatiro atangaza kwamba Hamad Rashid na wenzake 3 kuitwa mbele ya kamati ya maadili y Cuf kwa kosa la uasi.

Ch10 news 7pm

Nadhani tunayaona yanayotokea CUF na NCCR, hawa wote walikuwa wanaiandama CDM na kujiona wapinzani wa kweli, leo uweli unadhihirika. Hamad ni mroho wa madaraka kichizi, hana tofauti na Shibuda.

Ukija kwa kafulila laana ya uasi alioufanya CDM inamtafuna, hivi tukisema hivi vyama tunaviongoza kwa akili za hawa jamaa si tungekwisha kabisa???????

Cheki Laana nyingine, wanaolilia Posho kama hawa wa CUF na CCM + Shibuda leo wanaumbuka mbele ya watanzania........... malipo ni humu duniani.


Kwa issue ya Kafulila, hawa jamaa wa ukanda ule wa kigoma hawajifunzi tu?, wajiulize Dr Walid Kaburu yuko wapi?, nahisi ndicho kitakachotokea kwa kafulila na Zito wasipoangalia....

Ila CDM inamvumilia sana Dogo zito umeona NCCR hawakuchukua hata round, wamemtoa out.
 
Pole sana ni wengi wenye mtazamo kama wako, kifupi mimi huwa sitawaliwi na itikadi naangalia haki inapotakiwa itendeke, haki ya mtu haiangalii wewe ni CCM ,Chadema, wala CUF. Kama EL ataonewa nitasema kama Zitto atatetereka nasema kama ninavyosema leo kwa HR, kwa ninavyoifahamu CUF it is just a matter of time HR atakuwa nje ya ulingo. Kuhusu mimi kulipwa for your information EL huwa namuona tu kwenye TV lakini nilimkubali kwenye utendaji wake wakati akiwa PM kwa muda mfupi akaanzisha na kuisimamia project ambayo hadi leo inajulikana kama shule za kata, kifupi alithubutu.

Labda sikukusoma vizuri,kwa hiyo umeamua kumpigia kampeni EDDO awe chairman wa ccm ili amalizie kazi yake kwa kuanzisha na vyuo vikuu vya kata au?kama jibu ni ndiyo ur are very wrong brother kwa nafasi ya uenyekiti hawezi kuanzisha serikali za kata,atatumia muda mwingi kukiimarisha chama chake na kukidhoofisha chako labda kama mna ajenda ya siri hutaki kuitoa mapema mno na huu uenyekiti mnataka kuutumia kama daraja tu.
 
HR anasema tangu chama kianze hakuna kamati ya maadili ndio ameickia jana kutoka kwa mtatiro,do u think kamati ya maadili itakuwa na watu gani ukimtoa HR manake jamaa ni miongoni mwa wazee wa chama
 
CUF chama imara hawawezi kukitikisa kwa kuweka mamluki.idara yao ya Intelegencia yao iko juu sana. Mfano wako wapi hawa 1 mapalala 2. Naila jidawi 3. Fatuma maghimbi 4. Tambwe hiza nk. Wote hao walikuwa vibaraka wamekwishney.ushauri kwa MH Hamad rashd ni kosa kumtuhumu kiongozi wa kitaifa magazetini/kukampeni kabla ya uchaguzi wa chama. Huo ni utovu wa nidhamu.
 
Kwani kuna shida gani akirudi zenji akawa mwenyekiti wa kitongoji si itakuwa poa 2
 
Back
Top Bottom