Hamad kufikishwa kamati ya maadili ya CUF, asema Mtatiro

Pole sana ni wengi wenye mtazamo kama wako, kifupi mimi huwa sitawaliwi na itikadi naangalia haki inapotakiwa itendeke, haki ya mtu haiangalii wewe ni CCM ,Chadema, wala CUF. Kama EL ataonewa nitasema kama Zitto atatetereka nasema kama ninavyosema leo kwa HR, kwa ninavyoifahamu CUF it is just a matter of time HR atakuwa nje ya ulingo. Kuhusu mimi kulipwa for your information EL huwa namuona tu kwenye TV lakini nilimkubali kwenye utendaji wake wakati akiwa PM kwa muda mfupi akaanzisha na kuisimamia project ambayo hadi leo inajulikana kama shule za kata, kifupi alithubutu.

Inaeleweka kumkubali mtu kwa kazi nzuri yenye maslahi ya taifa lakini si kwa kiwango cha kutengeneza bango kwa ajili ya kampeni za mtu wa chama kingine tena bora ingekua kwa level ya urais sio uenyekiti wa chama kisichokuhusu ambacho ni hasimu wa chama chako,mfano wewe kama ni chadema ama cuf,mwenyekiti wa ccm anakuhusu nini?atakusaidia nini hasa ambacho unaona asipokuwa mwenyekiti utakikosa?kwa hilo bango uliloingia gharama kulitengeneza kwa ajili ya kumpigia kampeni 'bila malipo yeyote' ni wazi kwamba umeteleza vibaya sana,kwanini usikifanyie hivyo chama chako kilipokuwa igunga?unadhani ulikitendea haki kwa kuendelea kuzunguka mitaani na bango la kumpigia kampeni lowassa awe mwenyekiti wa ccm huku ukimuacha mgombea ubunge wa chama chako akigalagazwa na yule wa chama cha lowassa? naomba "upime" mwenyewe kama uamuzi wako huo ni wa busara ama la,kama kweli wewe sio kada wa kimya kimya ama hulipwi chochote.Pia kumbuka hapa humsifii lowassa bali unampigia debe waziwazi awe mwenyekiti wa ccm!hiyo ni kazi ya makada wa ccm sio mpinzani.

 
kijana acha hizo mbona we ni gwanda damu nakujua...

Amani nyekele ni mwenyekiti wa uvccm singida, achana naye chap.omb.e huyo. Kwa maelezo yako kuwa wamfahamu nyekele yafaa utuombe radhi kwa kusema uongo!
 
viongoz wengi wa cuf si wapinzani na wapo pale sio kama wana nia ya kujenga na kuongoza taifa but wapo pale ili waendeshe maisha kwa visent wanavyopata. vyama hivi hatuna budi kuviondoa. kama alivyosema kafulila kuwa mbatia yupo pale ili apate mkate aendesha maisha yake na wala si mpinzani.
 
Mtatiro , kaendeleza kuchemka kwani nimemsikia Hamad via TBC 1 akisema kuwa CUF hakuna kamati ya maadili , labda iwe imeundwa leo , sasa huyu kijana inaonekana kaamua kutumia maneno ya kiCCM sijui anaelekea wapi.

Kama hiyo kamatio ingekuwepo kusingekuwa na haja ya Maalim kwenda Lindi Na Mtwara kujipanga , wakati Maharagande katumwa Tanga na wengineo nitawajulisha kesho wamepangwa wapi kwenda kukihami chama .......

Maalim dhambio yake ni kukubali kula kuku wakati wenzake ambao walifilisika na kufungwa pamoja naye wakisota kama huyu Hamad sasa hapo wanajuana vizuri sana na wote ni mawakala wa TISS long time ...
 
HR akija Chadema nahamia CUF rasmi.

Sijaelewa HR anafagiliwa kwa lipi huko CUF kwamba eti ndiye anayeweza rudisha heshima ya chama wakati ndiye ameibomoa zaidi CUF baada ya uchaguzi wa mwaka jana. Wapemba ni watu wa ajabu sana,ni popo wa kisiasa,na sasa nimeanza kuelewa ni kwanini wana CCM wa Unguja wamekuwa na shaka siku zote na Wapemba.
 
Kweli,cuf ni kama NGO ya ROSTAM Kwa muda sasa,jussa amekua akitumika kama kiungo muhimu sana cha mahusiano ya cuf na Rostam kupitia kwa Januari Makamba!hapa kuna mambo mengi sana yanazunguka,mpaka muafaka wa seif na karume uliopelea seif kuhamishia "ofisi ya ukatibu wa cuf ikulu ya zanzibar" na kisa cha shein kuwa rais wa zanzibar na bilal "kuletwa" bara,yote yana mkono wa Rostam na genge lake!lengo likiwa kumpisha njia lowassa amrithi jamaa magogoni indirectly,si mnajua shein kama angebaki bara baada ya mzee wa chalinze kumaliza muda wake ikulu angekua na sifa zote za kumrithi pale magogoni?kina Rostam waliliona hilo mapema mno,wakamleta bilal ambae walijua baada ya miaka mitano atakuwa kishachoka sana na hatakua na nguvu za kuitamani ikulu ya magogoni tena zaidi ya kuombea aendelee kuwa makamu wa rais kwa miaka mingine mitano!


Ni kweli kabisa ulivyoandika. Ndio mbinu yao ya kumwondoa Shein Tbara
 
Kamati ya nidhamu na maadili ya chama ipo, labda yeye haifahamu kwa sababu anafanyia shughuli za chama vijiweni na anakwepa kuzifanya kwa kufuata taratibu zilizopangwa. Hakuna watu wanaokimbizwa mikoani kuokoa hali ya mambo. Hakuna tunachookoa zaidi ya kujipanga zaidi na zaidi. Haya masuala ya kina hamad rashid(MB) ni masuala ya vikao vya chama na kamati maalum za nidhamu. Vikoa na kamati husika vinafanya kazi kwa mujibu wa katiba ya chama. Kama kuna mtu amekiuka taratibu za chama na kama mtu ana kampeni ya kukigawa chama na kukivunja katiba ya chama itasimama na vikao vitaitumia kufanya maamuzi. Kwa hiyo, hapa hakuna vita ya mtu na mtu, hapa kuna vita ya kuchezea katiba. Kama kuna mtu mwingine yeyote(hata kama ni mie mtatiro) anakiuka taratibu za chama, chama kitamtendea haki yake kwa mujibu wa katiba, na kwa bahati mbaya CUF haitetereshwi na mtu mmoja, CUF ni chama chenye wafuasi wengi na hivyo hakitegemei mtatiro, wala hamad rashid wala maalim seif wala lipumba. Yeyote yule akichezea katiba ya chama, katiba itamtendea haki.
Sisi hatutatuma wajumbe mikoani kufanya kampeni zozote. Wenye chama huko vijijini wanajua nani anataka kuua chama na wamejionea wenyewe watu walivyo tayari hata kuua kwa mapanga ili kutafuta madaraka kinyume na taratibu za chama.
Kwa ujumla rapsha za juzi hazijakiteteresha chama, chama kinazidi kuimarika na kujipanga zaidi kila kinapopata misukosuko na CUF ni chama cha kipekee ambacho kimepitia misukosuko mingi. Hata hili la hamad rashid litamalizwa kwa utaratibu mzuri na kila upande utatendewa haki na katiba.
 
Mkuu Mtatiro,

Nina matatizo kidogo na huu mgogoro unaoendelea. Ulianza kimya kimya kwenye magazeti na sasa umeanza kujitokeza kwa uwazi zaidi na hasa unapoona watu wanapigana mapanga. Nina maswali kidogo:

Kwanini CUF wanakuwa wazito kujibu barua za Hamad Rashid mpaka inafika mahali anazipeleka magazetini ili apate sympathy ya wapiga kura (wana chama wa CUF)? Kukaa kwenu kimya kunampa ujasiri wa kuwavuruga zaidi na atawavuruga sana msipofanikiwa kumdhibiti mapema kwa kujibu hoja zake.

Kile kijitabu/kijarida alichokuwa akikisambaza then akasitisha zoezi hilo kwa ahadi kwamba madai yake yangefanyiwa kazi, anasema hakuna kilichofanyika na hivyo ametishia tena kuendelea na zoezi la kusambaza sumu mbaya ya chuki, nyinyi kama chama hamuoni kwamba sumu hiyo mbaya inawamaliza zaidi huku bara?

Katibu Mkuu ni mtendaji mkuu wa chama ambaye anatakiwa kuwa ofisini muda wote kusimamia kazi za chama za kila siku. Tangu Maalim awe Makamu wa Rais, amekuwa bize na nafasi hiyo, hivi shughuli za Katibu Mkuu wa Chama amemkabidhi mtu mwingine au bado huwa anakuja Buguruni kushughulikia maswala ya kichama? Sasa hivi Mwenyekiti hayupo, Katibu Mkuu yuko bize, Hamad Rashid anasema Mtatiro ni mtoto mdogo, je, ni nani ambaye anashughulikia maswala ya CUF?

Kwa sakata linaloendelea huko Visiwani, mtazidi kukiua chama. Nina mashaka watu kama akina Katani [Mbunge wangu wa Tandahimba japo alipokonywa ubunge wake] wakiona haya yanayoendelea wanakata tamaa na inawezekana na wao wanaweza kuingia kwenye migogoro ya siasa za makundi. Mnaweza kumuona Hamad Rashid yuko peke yake, lamesema kuna wengi 19 na wote ni vigogo na wengine ni wabunge wa huku bara. Malizeni hili sakata vinginevyo Pemba nayo mtaipoteza. Sasa hivi CCM wanashangilia tu wanasubiri mavuno.

Mwisho, kama kikao cha Hamad Rashid kilikuwa kwenye ukumbi wa kukodi, hao walinzi wa chama walienda kulinda nini kwenye huo ukumbi? Walinzi wa chama wanalinda wanachama au wanalinda mali za chama na viongozi wao? Je, wanachama ngazi ya tawi wanapoamua kufanya mkutano lazima waombe kibari makao makuu ya CUF au mkoani au wilayani? Hapa kuna matatizo, migogoro haimalizwi kwa ubabe na kutumia nguvu, bali kwa maridhiano ya maongezi.

Blue Guards siyo suluhu ya kumdhibiti Hamad Rashid, itisheni vikao na mjibuni barua zake na hoja zake.
 
Nimeufuatilia kwa karibu sana "Mgogoro" unaoendelea ndani ya chama cha CUF sasa na yafuatayo ni mang'amuzi yangu. Je wewe yako ni yepi?
Ama kweli sikio la kufa halisikii dawa. Mimi si mfuasi wa CUF wala CCM bali ni mwanamageuzi ninayetamani upinzani ushamiri dhidi ya CCM. Kwa muono wangu binafsi Hamad hana kosa katika kupendekeza mabadiliko ndani ya chama chake kwani hiyo ndiyo mojawapo ya misingi ya demokrasia ila naona anakuwa "victimized" na wahafidhina ndani ya chama hicho wanaong'ang'ania madaraka kiasi ya kufubaza mvuto wa umma kwa chama hicho.
Baada ya pigo la Igunga wengi tulidhani chama kingekaa chini, kutafakari na kuja na maamuzi ya kukiimarisha na kukihuisha (Kama ambavyo naamini Hamad anataka), lakini kwa bahati mbaya haeleweki na walevi wa madaraka waliosheheni katika chama chake. Haiingii akilini kwa watu wawili kung'ang'ania madaraka ya uenyekiti na ukatibu Mkuu kwa karibu miango miwili wakati kuna wanachama competent kibao.
Tatizo la CUF linaweza fanana na la wenzao wa CCM ambao kwa miango kadhaa tabaka fulani liling'ang'ania madaraka kiasi cha kulewa chakari na kuanza kujitapa eti CCM ina wenyewe huku wakibadilishana madaraka kiukoo, kirafiki na kifisadi. Sasa wanaonja joto la jiwe na kifo chao kiko mlangoni pao licha ya kutapatapa mithili ya panya aliyeshiba chakula chenye sumu.Kwa mtazamo wangu CHADEMA imedumisha mvuto kutokana na tabia yao ya kubadilisha sura muhimu katika chama (Achilia mbali propaganda za wapinzani wao), kwa mfano Mwenyekiti wao wa kwanza alidumu miaka kama mitano hivi kabla ya kumpa kijiti Bob Makani, na sasa Mbowe ambaye baada ya kutofanya vema katika kugombea urais alimwachia mwanachama mwingine (Dr. Slaa) aliyepeleka kiama CCM na kuipa ladha CHADEMA mbele ya umma. Ni muhimu kwa CUF kufanya mabadiliko makubwa ya ndani na naiona sauti ya Hamad kama ya mjumbe aliaye nyikani. Wasipomsikiliza watakigawa chama na ni wazi kikigawanyika; upande wa Hamad Rashid utakuwa na afya zaidi maana unawakilisha wakereketwa wengi tu wanaoogopa kujitokeza kutokana na udikteta wa Seif.
 
Hana kosa lolote sema hawa wakubwa wa vyama huwa hawapendi kuwa challenged kwenye position wanazoshikilia,kama Hamad Rashid yuko right,seif yuko busy na kazi za ikulu,hawezi tena kukitendea haki cuf kwenye hususan kwenye position ya utendaji zaidi kama katibu mkuu,may be angekua mwenyekiti sawasawa lakini sio katibu,cuf kimekua doro,kazi za katibu mkuu zinafanywa na mtoto ambae hana hata miaka mitatu ndani ya cuf japo huyo mtoto sio kiongozi mbaya na anafanya siasa za kisasa lakini bado anatakiwa kuongozwa na wazoefu!na kwa cuf ilivyo Hamad Rashid haswa ndio anapaswa kumrithi seif kutokana na historia yake kwenye chama hicho,HAMAD is right kwenye hili...
 
Mtatiro anatumika bila kujijua,seif labda kamdanganya yeye ndio atakua katibu mkuu wa cuf,sioni mantiki yeyote hapa ya yeye kumpinga Hamad Rashid,kwa maslahi na afya bora ya upinzani makini alitakiwa kuungana na Hamad anaepigania kuirudisha CUF kwenye ungangari wake,sasa hivi cuf imekua nyonge,cuf nyoro nyoro sio ile ngangari iliyoinyima usingizi ccm mpaka serikali yake ikapiga marufuku watu wasiruhusiwe kupanda malori wakati huko vijijini ndio usafiri wetu wa kawaida,yote ilikua ni kuweweseka cuf!
 
Hana kosa lolote sema hawa wakubwa wa vyama huwa hawapendi kuwa challenged kwenye position wanazoshikilia,kama Hamad Rashid yuko right,seif yuko busy na kazi za ikulu,hawezi tena kukitendea haki cuf kwenye hususan kwenye position ya utendaji zaidi kama katibu mkuu,may be angekua mwenyekiti sawasawa lakini sio katibu, cuf kimekua doro, kazi za katibu mkuu zinafanywa na mtoto ambae hana hata miaka mitatu ndani ya cuf japo huyo mtoto sio kiongozi mbaya na anafanya siasa za kisasa lakini bado anatakiwa kuongozwa na wazoefu!na kwa cuf ilivyo Hamad Rashid haswa ndio anapaswa kumrithi seif kutokana na historia yake kwenye chama hicho,HAMAD is right kwenye hili...

Nimeuliza hili swali mara nyingi sana, kwamba ni nani ambaye amepewa kukaimu nafasi ya Katibu Mkuu? Bahati mbaya sijapata jibu mpaka sasa. Je, unataka kusema huyo mtoto ni Julius Mtatiro? Maana kuna thread moja nilisoma Hamad Rashid akisema Mtatiro ni mtoto mdogo.
 
Nimeuliza hili swali mara nyingi sana, kwamba ni nani ambaye amepewa kukaimu nafasi ya Katibu Mkuu? Bahati mbaya sijapata jibu mpaka sasa. Je, unataka kusema huyo mtoto ni Julius Mtatiro? Maana kuna thread moja nilisoma Hamad Rashid akisema Mtatiro ni mtoto mdogo.
Ni wazi kwamba mtatiro ndio anakaimu automatically kutokana na position yake huku bara ambako angalau nako sasa cuf ndio iko hai,zanzibar hakuna upinzani tena!
 
ccm ilitaka chama kifike hapo yaani wampe sefu umakamu ili awe busy na ackijenje chama, na wamefanikiwa maana cuf ilivyo ni kama tulivyoona igunga, sasa HR ameshtuka na anataka kuirudisha cuf kule ilikotoka lkn ccm wameshanusa hatari kwa hamad kuwa katibu kwani cuf huenda ikaimarika kuelekea 2015 na sasa ccm inapambana nae, lengo ni kuiona cuf ikifa kabisa.
 
Ili kupata majibu ya swali lako, nadhani inabidi twende taratibu ili kuwe na hukumu iliyo ya haki. Mpaka sasa nadhani wengi tunaongea kwa kuwa tumesoma kwenye magazeti stori ya upande mmoja wa Hamad Rashid, hatujasikia upande wa pili wa shilingi ili tuweze ku-balance maelezo.

Sasa ili kuwatendea haki pande zote mbili zinazohusika kuna mambo ambayo yanatakiwa yajulikane:

1. Utaratibu wa kumpata Katibu Mkuu wa CUF ukoje? Je, anagombea au anateuliwa?

2. What if the current Secretary General amepata wadhifa mwingine ambao unamfanya ashindwe kutekeleza majukumu yake ya kila siku, ujazaji nafasi yake unakuwaje? [Maana nimesoma mahali Mtatiro anasema uchaguzi ni 2014, je, chama kibaki bila mtendaji mkuu kwa miaka 3 kusubiri uchaguzi wa ndani wa chama?]

3. Vile vikao vya juu vya chama vinavyofanya maamuzi, huwa vinakutana mara ngapi kwa mwaka? Je, vimekuwa vikikutana regularly? Maana Mwenyekiti hayupo, Katibu Mkuu yuko bize na serikali ya mseto, so, vikao vinasimamiwa nani?

4. Je, Bwana Hamad Rashid ameishapeleka hizo duku duku zake kwenye vikao rasmi vya chama baada ya kuona Mwenyekiti amekaa kimya bila kujibu barua zake?

5. Je, Katiba inasemaje kuhusu namna ya kuitisha vikao vya ngazi za kwenye matawi?

6. Katiba inawatumbua Blue Guards kama ni walinzi wa mali za chama au walinzi wa wanachama na kuzuwia wasifanye vikao?

Kuna mambo mengi sana ambayo hayako sawa na yana ashiria kiza huko mbele ya safari.

Kwa maoni yangu, uongozi wa CUF una matatizo/makosa na Hamad Rashid nae ana makosa, na njia pekee ya kumaliza huo mgogoro ni kupitia vikao rasmi vya chama na siyo kutumia blue guards au mabaunsa wa kukodi.
 
Ni wazi kwamba mtatiro ndio anakaimu automatically kutokana na position yake huku bara ambako angalau nako sasa cuf ndio iko hai,zanzibar hakuna upinzani tena!

Kwanini Naibu Katibu Mkuu wa Visiwani asikaimu nafasi hiyo automatically? Je, Mtatiro ana full authority ya kufanya maamuzi as Katibu Mkuu au ndio ile ya kukaimu jina lakini maelekezo, maagizo na maamuzi yanatoka kwa Maalim?
 
baada ya kukosa nafasi ya kuunda kambi rasmi ya upinzani bungeni kama walivyozoea, wakaamua kwa msaada wa mabwana (magamba) zao kuunda kanuni uchwara ya kuanzisha kambi isiyo rasmi, lkn kwakua si rasmi pia haina maslahi, akashtuka kuwa alichopigania hakina maslahi, sasa anapigania mambo yenye maslahi, sasa kama alikuwa hawajui ccm hgapa ndo atawajua, watamchafua mpaka basi!
 
By Keil
Ili kupata majibu ya swali lako, nadhani inabidi twende taratibu ili kuwe na hukumu iliyo ya haki. Mpaka sasa nadhani wengi tunaongea kwa kuwa tumesoma kwenye magazeti stori ya upande mmoja wa Hamad Rashid, hatujasikia upande wa pili wa shilingi ili tuweze ku-balance maelezo.

Sasa ili kuwatendea haki pande zote mbili zinazohusika kuna mambo ambayo yanatakiwa yajulikane:

1. Utaratibu wa kumpata Katibu Mkuu wa CUF ukoje? Je, anagombea au anateuliwa?

2. What if the current Secretary General amepata wadhifa mwingine ambao unamfanya ashindwe kutekeleza majukumu yake ya kila siku, ujazaji nafasi yake unakuwaje? [Maana nimesoma mahali Mtatiro anasema uchaguzi ni 2014, je, chama kibaki bila mtendaji mkuu kwa miaka 3 kusubiri uchaguzi wa ndani wa chama?]

3. Vile vikao vya juu vya chama vinavyofanya maamuzi, huwa vinakutana mara ngapi kwa mwaka? Je, vimekuwa vikikutana regularly? Maana Mwenyekiti hayupo, Katibu Mkuu yuko bize na serikali ya mseto, so, vikao vinasimamiwa nani?

4. Je, Bwana Hamad Rashid ameishapeleka hizo duku duku zake kwenye vikao rasmi vya chama baada ya kuona Mwenyekiti amekaa kimya bila kujibu barua zake?

5. Je, Katiba inasemaje kuhusu namna ya kuitisha vikao vya ngazi za kwenye matawi?

6. Katiba inawatumbua Blue Guards kama ni walinzi wa mali za chama au walinzi wa wanachama na kuzuwia wasifanye vikao?

Kuna mambo mengi sana ambayo hayako sawa na yana ashiria kiza huko mbele ya safari.

Kwa maoni yangu, uongozi wa CUF una matatizo/makosa na Hamad Rashid nae ana makosa, na njia pekee ya kumaliza huo mgogoro ni kupitia vikao rasmi vya chama na siyo kutumia blue guards au mabaunsa wa kukodi.
Well said mchillo and keil, facts speak on themselves. A wise saying has it that failure to adopt flexibility risks breakage! And this is exactly wahat is happening within CUF now. I also concur with he suggestion that Hamad Rashid is more competent than any member within CUF to take the position of Secretery General.
 
Back
Top Bottom