Hakika watu tunakabiliwa na Magonjwa mengi, kila Ugonjwa unayo Dawa yake

Mokaze

JF-Expert Member
Aug 3, 2018
14,375
14,870
Salam wakuu,

Nilipata kuhadithiwa kisa kimoja cha kweli kilichotokea miaka mingi huko India, nami nimeonelea nikiweke humu ili tupate kujifunza.

Katika miaka ya mwishoni mwa 1800 na mwanzoni mwa 1900 katika kijiji kimoja huko India alitokea mwanamke mmoja aliyepatwa na ugonjwa wa ajabu wa mikono kunyooka kama mtu aliyepigiliwa msalabani, watu walijaribu kuinyoosha kwa njia za kawaida na njia za dawa ya kienyeji na za hospitali nk lakini ilishindikana, alipelekwa kwa waganga wa aina mbalimbali lakini hakuna aliyeweza kujua chanzo cha ugonjwa huo kwani huo kwao ulikuwa ni ugonjwa mpya, masiku, mawiki na miezi ilizidi kukatika mume na ndugu na jamaa walianza kukata tamaa juu ya kupona kwa ndugu yao ikizingatiwa kwamba huo ulikuwa ni ugonjwa wa ajabu kuwahi kutokea kwani hakukuwepo na historia inayoonyesha kuna mtu aliyewahi kuwa na ugonjwa huo huko nyuma.

Binadamu katika mahangaiko huwa anafanya kila kitu anachoshauriwa na watu, wengine walitoa ushauri wa kumpeleka mgonjwa kwa waganga wa kupiga ramli nk huko kote ilikuwa ni kazi bure na kupoteza muda na pesa bila mafanikio ilimuradi kila njia na dawa walizoweza kuzipata zilitumika bila mafanikio.

Kumbuka, huo ugonjwa ni sawa na mtu mlemavu wa mikono yote miwili, mikono imenyooka kama mtu aliyepigiliwa msalabani na akijaribu kuirudisha kwa nguvu anapata maumivu makali sana ya misuli ya mikono hivyo yeye akawa ni mtu wa kuhudumiwa kwa vitu vingi kama mlemavu wa mikono anavyoweza kuhudumiwawa, mbaya zaidi ni ulemavu wa ukubwani.

Inakaribia mwaka zikawafikia habari kutoka kwa mtu mmoja kwamba katika kijiji cha mbali kidogo kutoka hapo yupo mganga mmoja mashuhuri sana ambaye anaweza kutatatua shida hiyo, yule mume katika hali ya kukata tamaa na ukizingatia ameshatumia pesa nyingi bila mafanikio na kiuchumi ameshakuwa hohehahe kwa shingo upande akaamua kwanza aende yeye mwenyewe kumuona huyo mganga ili amuelezee shida ya mgonjwa wake.

Kweli alifika na kumuelezea shida, yule mganga akamsihi huyo mume ampeleke huyo mgonjwa ili amuone kwa macho kitu ambacho mume hakupenda kusikia kwani yeye alitaka kusikia kauli kutoka kwa mganga inayosema kwamba; "ninaweza kumtibu", basi !!, kwakuwa hakusikia kauli hiyo akaona huyo naye ni sawa tu na wale waganga wengine waliomlia pesa zake bila mafanikio. basi akarudi nyumbani huku akiwa hana matumaini na kesho yake akakutana na yule jamaa aliyempa habari za kuwepo kwa huyo mganga maarufu katika kijiji hicho cha mbali, huyo bwana (mleta habari) atakata mrejesho lakini huyo mume akatoa mrejesho katika hali ya kukata tamaa kuonyesha kwamba hata huyo mganga naye ni sawa na wale wengine waliokula pesa zake bila mafanikio, yule mleta habari akamuambia huyo mume kwamba;

"Huyo mganga unayemtilia shaka alishawahi kuwa mganga wa mfalme", mume kusikia hivyo mara moja akapata imani na kesho yake akajikusanya na akasafiri pamoja na mgonjwa hadi kwa huyo mganga, mganga alipomuona mgonjwa akawauliza tu ni muda gani mgonjwa amedumu na ugonjwa huo??, walipomtajia tu basi akawaambia wamtoe mgonjwa nje kumpumzisha .

Mle ndani wakabaki yule mume na mganga, Mganga akamuambia kwamba tatizo la mkewe linaanzia kichwani ndani ya ubongo kutokana mshtuko fulani alioupata na wala halianzii kwenye misuli ya mikono hivyo ili apone anatakiwa awekwe ndani ya chumba peke yake na alazwe juu ya kitanda akiwa mtupu chumba hicho kifungwe mlango na humo chumbani abaki mgonjwa peke yake halafu apatikane mvulana shababi ambaye hajuani na huyo mgonjwa kisha huyo mvulana naye abaki mtupu nje halafu aingie kwa ghafla ndani ya hicho chumba akiwa katika hali hiyo ya utupu alimolazwa huyo mgonjwa, (kumbuka jambo hilo inabidi lifanywe kwa siri wakati huyo mgonjwa hajui kinachoendelea nje), na huyo kijana mara akiingia humo kwa ghafla afanye kama anataka kumbaka huyo mgonjwa.

Itaendelea episode fupi ya pili na ya mwisho.
 
Back
Top Bottom