Dar: Polisi wamsaka Mganga aliyelewesha Watu 16 wa familia moja kisha kuwaibia

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462

Polisi Dar_page-0001.jpg
Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam linachunguza tukio la mtu mmoja aliyejifanya mganga wa jadi huko maeneo ya Mji mwema, Kigamboni, Dar es Salaam kwa kuwanywesha dawa inayodhaniwa kuwa ni sumu na kuwalewesha watu 16 wa familia moja na baadae kuwaibia simu.

Tukio hilo limetokea tarehe 18 Februari 2024 majira ya saa tatu usiku wakati mtu huyo aliyejifanya mganga wa jadi alipofika nyumbani kwa familia ya Mzee Halisi Amani kwa lengo la kumtibia mke wake Fatuma Abdalla (52) aliyekuwa anasumbuliwa na tatizo la miguu. Aliwanywesha dawa iliyowalewesha familia nzima, wakapoteza fahamu na akawaibia simu 5 za mkononi na kuondoka.

Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamtafuta mganga huyo pia limemkamata kwa mahojiano mtu mmoja anayefamika kwa jina la Jalala Ally Said anayedaiwa kushirikiana na mganga huyo.

Wagojwa walilazwa na kupatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni mpaka sasa wagonjwa 13 wamesharuhusiwa na wengine watatu waneendelea kupatiwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.

Tukio lingine limetokea tarehe 9 Februari, 2024 huko eneo la Tuangoma, Mbagala ambapo mtu mmoja aliyejifanya mganga wa jadi aliwanywesha dawa zilizowalevya na baadae kupoteza fahamu watu watano na kuwaibia pikipiki namba MC474, simu 3 za mkononi na Tsh 30,000.

Jeshi la Polisi linawatahadharisha wananchi kuhusiana na kuwepo kwa watu wanaojifanya waganga wa jadi ambao huwalewesha watu na wanafamilia kwa ujumla na baadae kuwaibia.
 
FB_IMG_1708428401737.jpg
 
Wqjinga waliwao

Tena huyo mganga angewandua familia nzima

Ova
HABARI Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam linachunguza tukio la mtu mmoja aliyejifanya Mganga wa jadi maeneo ya Mji Mwema Kigamboni jijini Dar es Salaam na kuwanyeshwa Dawa inayodhaniwa kuwa ni sumu na kuwaibia watu 16 wa wafamilia moja.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Kamishina wa kanda Maalum CP Muliro Jumanne Muliro amesema tukio hilo lilitokea Februari 18 Mwaka huu majira ya Saa tatu usiku wakati mtu huyo aliyejifanya Mganga wa wajadi na kuingia nyumbani kwa familia ya Mzee Halisi Amani kwa lengo la kumtibia mke wake Fatuma Abdallah (52) aliyekuwa anasumbuliwa na tatizo la miguu.

“Aliwanywesha Dawa iliyowalewesha familia nzima wakapoteza fahamu na kuwaibia simu tano za mkononi na kuondoka" amesema Kamishina Muliro

Kamishina Muliro ameongeza kuwa kufuatia tukio hilo jeshi limetoa onyo kwa wanaojifanya waganga wakienyeji kuwa halitosita kuwachukulia hatua.

Katika hatua Nyingine Jeshi hilo limewataka Mamlaka husika inayohusika Sukari kuuza kwa bei elekezi na hatosita kuwachukulia hatua. #EastAfricaRadio
 
Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam linachunguza tukio la mtu mmoja aliyejifanya mganga wa jadi huko maeneo ya Mji mwema, Kigamboni, Dar es Salaam kwa kuwanywesha dawa inayodhaniwa kuwa ni sumu na kuwalewesha watu 16 wa familia moja na baadae kuwaibia simu.

Tukio hilo limetokea tarehe 18 Februari 2024 majira ya saa tatu usiku wakati mtu huyo aliyejifanya mganga wa jadi alipofika nyumbani kwa familia ya Mzee Halisi Amani kwa lengo la kumtibia mke wake Fatuma Abdalla (52) aliyekuwa anasumbuliwa na tatizo la miguu. Aliwanywesha dawa iliyowalewesha familia nzima, wakapoteza fahamu na akawaibia simu 5 za mkononi na kuondoka.

Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamtafuta mganga huyo pia limemkamata kwa mahojiano mtu mmoja anayefamika kwa jina la Jalala Ally Said anayedaiwa kushirikiana na mganga huyo.

Wagojwa walilazwa na kupatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni mpaka sasa wagonjwa 13 wamesharuhusiwa na wengine watatu waneendelea kupatiwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.

Tukio lingine limetokea tarehe 9 Februari, 2024 huko eneo la Tuangoma, Mbagala ambapo mtu mmoja aliyejifanya mganga wa jadi aliwanywesha dawa zilizowalevya na baadae kupoteza fahamu watu watano na kuwaibia pikipiki namba MC474, simu 3 za mkononi na Tsh 30,000.

Jeshi la Polisi linawatahadharisha wananchi kuhusiana na kuwepo kwa watu wanaojifanya waganga wa jadi ambao huwalewesha watu na wanafamilia kwa ujumla na baadae kuwaibia.
Safi sana yaani huyo mganga haina haja ya kutafutwa inabidi atumiwe pongezi maana hauwezi kuchezea hela huku uchumi umeshuka.
 
Mganga wa kienyeji? yani mtu tu from nowhere anakuja nyumbani anajitambulisha kisha mnamuelewa,kumwamini kisha kuanza kuwanywesha dawa? kweli ndg zangu?
 
Wengi tuna-commet as if hatuyajui maisha ya kitanzania,hakuna kitu kibaya duniani kama maradhi halafu uwe umetokana na familia maskini kila utakachoambiwa ambacho ni cha bei rahisi (kwa mtizamo wako) utakifanya.

Ni kweli wameibiwa lakini zipo sababu ambatanishi zimesababisha,unaweza kukuta huyo mgonjwa wa miguu hawajawahi kumpeleka hospital kwa vipimo vya maabara ili kujua ni maradhi ya kawaida au lah sababu ya umaskini waka-opt dawa za Kiswahili.

NB;siungi mkono mambo ya waganga lakini tujue hatufanani hali.
 
Walioibiwa na aliyewaibia ni wapumbavu. Kwa teknolojia ilivyo huyo mganga ni mpuuzi mno kuiba simu.
 
Kiazi kimesepa na simu 5.

Halafu huyu siyo hardened criminal.

Hajawaza hata kuwabaka. Yeye kachukua simu tu akatoweka
 
Back
Top Bottom