Haijawaji kutokea mgao wa umeme mwaka mzima, awamu hii ni kiboko

Hii nchi Sasa inapoelekea ni pabaya, Toka Awamu ya Mkapa, haijawaji kutokea Mgao mkali wa Umeme kama huu Awamu hii inayoitwa ya sita, Mgao ambao umedumu zaidi ya Mwaka Mmoja.

Hii Serikali Sasa ikibidi tu iwashe mitambo ya kifisadi ya IPTL Kwa maana mtu unawezaje kuvumilia Mgao wa zaidi ya Mwaka Mzima, mvua zinyeshe zisinyeshe Mgao upo pale pale.

Serikali itafute Namna hata kuleta Umeme waafuta watakaoweza wanunue watakaoshindwa wakae Giza.

Awamu hii ya SITA Mimi naiita Awamu ya Giza Totoro, Bodi imevunjwa mara tatu, wakurugenzi wamebadilishwa mara mbili, lakini Mgao ni ule ule
Swali lako linajibiwa na jibu hili kwamba nchi haikuwahi kuwa na rais mwanamke ila sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tungeweza kuwaruhusu hawa watu wauze umeme kwenye grid ya taifa ingekuwa vizuri zaidi. Tungewapa watu incentive ya kuweka solar na kuipa TANESCO competition.

Ukiweza kuweka mfumo wa watu binafsi kuuza umeme katika grid ya taifa, utakuwa umetatua tatizo la umeme Tanzania kwa kiasi kikubwa.
Iwe kama kampuni ya sim walivyofanya
Mwamba mkapa sjui kwanini asinge ibinafsisha tanesco au kuiuzulilia mbali

Ova
 
Hi ilikuwa kauli ya Makamba mara tu Baada ya kupewa uwaziri wa Nishati

Aje atuombe radhi Kwa kutudanganya
Ile kauli yake ilikuja sio kwa bahati mbaya ! Ile kauli ilikuwa ni smoke screen kwa yale yote ambayo yangefuata kama tunavyo yashuhudia hivi sasa !!
Ukarabati uliosemwa umekula mabilioni mengi kuliko maelezo !
Fake or whatever Umeme upo vile vile unakatika katika. !
Kipindi cha yule Mwamba inasemekana mitambo ilikuwa haifanyiwi matengenezo lakini ile mitambo ilikuwa ikimuogopa yule jamaa ndio maana umeme haukukatika katika namna hii !!
Mungu anawaona !!
Karma is just around the corner 🙏🙏
 
Na huku maeneo ya mlimani city, goba hadi mbezi sasa mgao imekuwa kila siku usiku hakuna umeme........sijui kuna nini kinaendelea kwenye hii serikali.
Anaharibiwa mtu hapo ili asukumiwe jumba bovu !!
 
Na miezi 6 ilishaisha
Wakaja na blah blah wakadai maji hayaingii bwawani
Maneno maneno mengiii tu
Huu mgawo wanautumia kiupigaji,
Kufanya mauchafu yao tu

Ova
Serikali ya CCM inatuona sisi wananchi ni maboya
 
Walijichanganya wakakata umeme masaki kilichotokea kesho yake bodi ikavunjwa chap!🤣
 
Hii nchi Sasa inapoelekea ni pabaya, Toka Awamu ya Mkapa, haijawaji kutokea Mgao mkali wa Umeme kama huu Awamu hii inayoitwa ya sita, Mgao ambao umedumu zaidi ya Mwaka Mmoja.

Hii Serikali Sasa ikibidi tu iwashe mitambo ya kifisadi ya IPTL Kwa maana mtu unawezaje kuvumilia Mgao wa zaidi ya Mwaka Mzima, mvua zinyeshe zisinyeshe Mgao upo pale pale.

Serikali itafute Namna hata kuleta Umeme waafuta watakaoweza wanunue watakaoshindwa wakae Giza.

Awamu hii ya SITA Mimi naiita Awamu ya Giza Totoro, Bodi imevunjwa mara tatu, wakurugenzi wamebadilishwa mara mbili, lakini Mgao ni ule ule
Pamoja na mvua zote zilizonyesha na kuleta mafuriko, mauaji na watu kukosa makazi lakini swala la umeme limekuwq JIPU ni nini tatizo na tunakwama wapi.
Mbona majirani zetu hawana mashida haya.
Wizara husika si mkuje na jawabu mmeshindwa kazi ondokeni.
Figisu tupu!!
 
Kama ni hujuma anaehusika afungwe jiwe shingoni na kutupwa baharini sehemu yenye kina kirefu, nia asionekane katika uso wa dunia. Walala hoi tunateseka sana, nina saluni yangu na ninategemewa, jioni narudi nyumbani bila shilingi. "Mtanikumbuka". Yametimia!!!.
 
Pamoja na mvua zote zilizonyesha na kuleta mafuriko, mauaji na watu kukosa makazi lakini swala la umeme limekuwq JIPU ni nini tatizo na tunakwama wapi.
Mbona majirani zetu hawana mashida haya.
Wizara husika si mkuje na jawabu mmeshindwa kazi ondokeni.
Figisu tupu!!
Umeme wa maji (Hydro) hautamaliza tatizo la umeme Tanzania, solar power itakumalizia matatizo yako ya umeme wewe na familia yako, sasa Kila mtu ajitetee mwenyewe na kufunga solar tuachane na huu ujinga wa TANESCO na serikali ya CCM, mwaka wa tatu huu sijui bill za TANESCO 100%, bongo Kuna jua kuliko mahitaji
 
Back
Top Bottom