Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,027
- 144,381
Hiki ndicho naweza kusema kuhusu huu mgao wa umeme hapa mkoani Arusha.
Nimefika hapa juzi mida ya saa moja usiku na kukutana na giza nene maeneo ya Usa-River.Umeme ulirudi saa 5 usiku na asubuhi saa 12 kasoro wakakata tukashinda almost siku nzima hakuna umeme.
Leo tumeamka nao(ulirudi usiku) na.ilipofika saa 10 wakakata na mpaka saa hizi tuko gizani.
Jana nako hali ilikuwa ni hiyo hiyo, mchana mzima hamna umeme ukarudi saa 12 jioni na ndio huo tuliamka nao leo hii.
Sina ratiba kamili ya mgao (Kama ipo), ila kwa hizi siku tatu nilizokaa hapa Arusha maeneo ya Usa River, hali ndio hii.
Mwaka 2006 wakati wa Kikwete, hali ilikuwa ni kama hii. Sasa leo hii ikiwa ni miaka 16 baada ya ule mgao, bado tena tumerudi katika hali ile ile. Binafsi najiuliza, katika kipindi chote hiki cha miaka 16, hatukijfunza na kuchukua hatua hali hii isijirudie tena?
Hii nchi inasikitisha sana na Watanzania wenye imani na CCM kamwe huwa siwaelewi kabisa wanatKa mpaka nini kitokee ndio wakubali CCM hii nchi imewashinda na hawafai kuendelea kubaki madarakani hata kwa sekunde moja ijayo.
Miaka 60 ya uhuru bado tunaongele megawatts, wimbo usioisha. Aibu sana!