Hadithi: Penzi la Kiziwi

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Mar 10, 2022
17,796
32,148
-BUSU (KISS)-

(Kutoka Ikulu hadi Kumpenda Kiziwi)
Episode one

Hey! Naitwa Jack, ni mtoto wa kitajiri na nina miaka 24. Nimekulia katika familia ya Baba, Mama na mtoto mmoja ambaye ni Mimi. Baba yangu anaitwa Mr Charles kwahiyo moja kwa moja Mama yangu ataitwa Mrs Charles. Binafsi nimekulia katika familia ambayo haina dhiki ya aina yoyote. Baba na Mama yangu ni wafanyakazi wa ofisi ya Rais hivyo kwetu kula, kulala na kufanya matanuzi mengine ni jambo la kawaida sana. Tunatanua utadhani sisi ni watoto wa Rais.

Sio kwamba najigamba lakini ndio maisha ambayo nimelelewa, tangu nimekuwa sikuwahi kuona mwanamke ambaye anatembea peku, hajapaka mekapu, anayenuka vumba la kuni wala amevaa nguo za kuchanika. Mara zote nilikuwa ni mtu wa ndani nikilindwa na ulinzi kisha nikitoka labda nimeenda kwa marafiki zangu ambao wengi ni watoto wa mawaziri pamoja na wabunge. Zaidi ya hapo ningeenda chuo ambapo nilisoma Kampala, Uganda.

Kukua katika malezi haya kidogo kulinifanya niwe ni mtu mwenye dharau, kejeli na sijali mtu mwinhine. Pia nachukulia kila mtu ambaye yupo chini yangu hawezi kunifanya lolote lile. Hii ndio amri ya kwanza ambayo nilifundishwa na Mama pamoja na Baba yangu. Nikaimeza amri hii na kuifanyia kazi lakini nilikuja kuivunja siku moja ambapo nilikutana na msichana mrembo, mwenye kuvutia.

Nakumbuka ilikuwa Alhamis katika mkesha wa Sikukuu ya ya uhuru ambapo kulikuwa na shughuli za kiserikali kwahiyo viongozi mbalimbali na watu wenye hadhi zao walikutana katika uwanja na shughuli zilifanyika hapo. Katika eneo hili ndipo kulikuwa na binti mzuri, mwenye macho ya kuvutia yenye kubeba haiba, msichana ambaye kwa kumtazama kwa mara ya kwanza hakuzidi miaka 20.

Mrembo huyu alikuwa anapiga mbira wakati wenzake wakiendelea kuimba nyimbo mbalimbali ili kuwabururidisha wageni ambao wamefika eneo lile. Upigaji wake wa mbira ulikuwa tofauti na ule ambao nimewahi kuusikia kwa watu wengine. Nilijikuta namtazama sana, nilimtazama kiasi kwamba hadi Baba ambaye alikuwa pembeni yangu aliniuliza.

“Unatazama nini”🤔

“Nothing daddy”😒 nilimkatalia kwa makusudi sababu nilikuwa namjua Baba yangu, tabia ya kutopenda masikini lilikuwa ni jambo ambalo amerithi enzi na enzi kutoka kwenye koo yake. Kwahiyo pale napo nilifanya makusudi kabisa.

“Hakuna kitu wakati nakuona unamtazama yule masikini, unataka akurithishe dhiki si ndio?🙄

“Mmmh! Nimeona anapiga vizuri”🤗

“Ok, achana naye ni masikini. Huwa wanachukuliwa na kuburudisha kwa siku kama hizi”

“Sawa daddy” Niliamua kumaliza mada maana sikupenda marumbano lakini hii haikunifanya kuendelea kumtaza yule binti.

Kiukweli nilitokea kumpenda, nilitamani awe katika maisha yangu lakini namna ya kumuingia, namna ya kumfanya awe karibu na mimi ndio ulikuwa mziki. Basi, shughuli ilimalizika. Nami nilijaribu kumtafuta yule binti lakini sikuweza kumpata.

Nilichanganikiwa mno, nikawaza wapi ambapo ningeweza kumpata lakini ukweli ni kwamba kwa wakati ule ilikuwa ni ngumu sana kumpata yule binti? Siku iliyofuata nilisumbuka maeneo tofauti tofauti lakini sikuweza kumpata.

Nilipatwa na hasira😠kwanini nimeshindwa kumpata sasa? Basi nilirudi Ikulu ambako ndiko kulikuwa na makazi yetu. Jioni Rais aliniita maana alikuwa anapenda sana kuzungumza na mimi, nilienda kumsikiliza.

“Judy anaweza kurudi hapa akitokea marekani kimasomo” 🤗

“Oh! Nahisi itapendeza maana tutakuwa wawili”💏

“Kweli kabisa au ushapata mpenzi maana kila siku anakuulizia?”🤔

“Hapana, mwambie nipo bado kama ikiwezekana basi tutaoana”😎

“Sawa” Niliamua kumkubalia Rais kwakuwa kwanza alikuwa ni kiongozi wangu lakini ukweli ni kwamba huyo mtoto wake ambaye aliitwa Judith sikuwa nampenda hata chembe. Kulikuwa na ushawishi kutoka kwa Baba pamoja na Mama ambao muda wote hawakuacha kumpigia debe na kuamini kwamba kama tukiwa wawili basi tutapendezana na huenda nami ningekaribishwa vizuri Ikulu kama Rais huko mbeleni.
 
Nakumbuka siku zilienda lakini sikuacha kumtafuta yule binti. Nilifanya vile ambavyo najua ila mafanikio ndio kitu kilikuwa kigumu kukipata. Hatimaye iliingia sikukuu ya Mapinduzi ambayo ilifanyika Visiwani Zanzibar. Nasi tulienda huko, kwa bahati nzuri niliweza kumuona yule binti. Naye alikuwa amekuja na watu wake, alikuwa mnyenyekevu wakato anaomba anasalimia, alikuwa anamtazama mtu mmoja baada ya mwingine lakini sikuona akizungumza neno lolote lile.

Muda wa kupiga mbira ulipofika, alianza kupiga. Macho yangu hayakuacha kumtazama na masikio yalikula aina mpya ya upigaji mbira. Alikuwa anapiga vizuri sana, sa sijui ni kweli au ni mapenzi yangu tu🤦‍♂️ Uvumilivu ulinishinda, kwanza nilitoa simu na kuanza kumpiga picha pamoja na kumchukua video lakini hili sikutosheka nalo. Niliona napaswa kwenda kumshika mkono ili nipate alau harufu yake🤭

Nilijikuta natoa elfu 10 na kuandika namba yangu ya simu katika ile hela kisha nilipiga hatua hadi alipo. Nilijaribu kumsehemsha, niliona yupo kimya. Aliendelea kupiga mbira. Nikashikwa na hasira maana sikuwa napenda dharau😠 nikasema nimrambe makofi nini? Nilipogundua kuwa nipo sehemu ya wazi nilijishusha, nikajiambia kwamba labda yupo katika upigaji.

Basi niliongeza elfu 30 katika ile hela. Ili kutenganisha na watunzaji wengine ambao walikuwa wanaendelea kumtunza, niliamua kuiweka hela ile katika mbira kwa nuu. Niliona ikidondoka chini, hakuikota. Aliendelea kupiga mbira yake.

“Hope utakuwa na simu na utanitafuta” Nilizungumza kwa sauti ya chinichini na kurudi sehemu ambayo nilikuwa nimekaa mwanzo ili niendelee kutazama shughuli inavyokwenda.... ITAENDELEA
 
Nakumbuka siku zilienda lakini sikuacha kumtafuta yule binti. Nilifanya vile ambavyo najua ila mafanikio ndio kitu kilikuwa kigumu kukipata. Hatimaye iliingia sikukuu ya Mapinduzi ambayo ilifanyika Visiwani Zanzibar. Nasi tulienda huko, kwa bahati nzuri niliweza kumuona yule binti. Naye alikuwa amekuja na watu wake, alikuwa mnyenyekevu wakato anaomba anasalimia, alikuwa anamtazama mtu mmoja baada ya mwingine lakini sikuona akizungumza neno lolote lile.

Muda wa kupiga mbira ulipofika, alianza kupiga. Macho yangu hayakuacha kumtazama na masikio yalikula aina mpya ya upigaji mbira. Alikuwa anapiga vizuri sana, sa sijui ni kweli au ni mapenzi yangu tu Uvumilivu ulinishinda, kwanza nilitoa simu na kuanza kumpiga picha pamoja na kumchukua video lakini hili sikutosheka nalo. Niliona napaswa kwenda kumshika mkono ili nipate alau harufu yake

Nilijikuta natoa elfu 10 na kuandika namba yangu ya simu katika ile hela kisha nilipiga hatua hadi alipo. Nilijaribu kumsehemsha, niliona yupo kimya. Aliendelea kupiga mbira. Nikashikwa na hasira maana sikuwa napenda dharau nikasema nimrambe makofi nini? Nilipogundua kuwa nipo sehemu ya wazi nilijishusha, nikajiambia kwamba labda yupo katika upigaji.

Basi niliongeza elfu 30 katika ile hela. Ili kutenganisha na watunzaji wengine ambao walikuwa wanaendelea kumtunza, niliamua kuiweka hela ile katika mbira kwa nuu. Niliona ikidondoka chini, hakuikota. Aliendelea kupiga mbira yake.

“Hope utakuwa na simu na utanitafuta” Nilizungumza kwa sauti ya chinichini na kurudi sehemu ambayo nilikuwa nimekaa mwanzo ili niendelee kutazama shughuli inavyokwenda.... ITAENDELEA
Endelea mkuu...
 
Episode Two

Nakumbuka baada ya sikukuu kuisha tulirudi Dar es salaam ambako tulikaa kwa siku moja na siku ya pili tuliingia Dodoma. Kwa siku zote hizo sikubahatika kupata simu kutoka kwa yule msichana wala meseji sikuiona.

Nikajiuliza itakuwa hajaiona ile namba ama kuna nini? Kiukweli maswali yalikuwa mengi sana kwa upande wangu, lakini sikuweza kupata jibu hata moja. Niliumia moyoni maana nilitaka awe anawasiliana na mimi ili nijue nampataje lakini naye alileta ujuaji.

Niliendelea kumtafuta, nikajaribu kutazama video zangu na kupita kwa baadhi ya watu mtaani nikiwaulizia kama naweza kumpata yule binti ila bado kulikuwa na ugumu. Sikufanikiwa kumpata hadi nilihisi kuchoka sasa, nilianza kukata tamaa.

Ijumaa moja ambayo ilikuwa tulivu hivi, majira ya Jioni Mama aliniita, tulikaa wawili tu. Ilikuwa ni kawaida kwetu kuzungumza sababu Mama yangu ananipenda sana, ananichukulia kama jicho lako. Kwahiyo siku hii Mama nilimuuliza mara baada ya kuongea kwa muda mrefu.
“Mapenzi ni nini mama?”
“Kujitoa”
“Kwa namna gani?”
“Kujitoa kwa hisia nzito ambazo haziwezi kuzuilika na mtu yoyote. Kumpenda mtu bila kujali ana mali, pesa, gari au elimu yake. Lakini unampenda na kumjali?” Nikasema Mama tayari ameingia kwenye line yangu, nilimuuliza.
“Kuna uwezekano wa mimi kuoa mtu mwingine kutoka nje ya Ikulu?”
“Unazijua Protocal za kuwa chini ya Rais?” Niliona Mama ananiuliza swali ngumu nilishindwa kumjibu, naye akanigongomezea msumali mwingine akisema.
“Kila mmoja ndani ya hii ofisi anafahamu kwamba una mwanamke ambaye ni Judy, naye anarudi kwa ajili yako”
“Lakini mama, simpendi Judy na hayupo katika moyo wangu”
“Jack acha ujinga wako, tumewaandaa muda mrefu ili muje kuwa wapenzi na anarudi ili mfunge ndoa mkaishi Marekani”
“Marekani tena?”
“Unajitia kutokufahamu si ndio?”
“Sio chaguo langu sasa
“Chaguo lako ni nani sasa?”
“Upo tayari nikuoneshe?” Nilimuuliza hapo nikiwa na wasiwasi mno maana nilijua nini kitaenda kutokea

Mama aliniambia sawa kama nikiweza nimuoneshe, basi nilitoa simu yangu na kuchezea. Nilipotazama sehemu ya picha na video sikuzikuta. Nikakumbuka, siku moja nyumaa siku ilichukuliwa na Baba, aliniomba na kusema kuna data anataka kuziangalia.

Nikajua hakuna ambaye amefanya hili la kufuta picha kama sio yeye? Nilipatwa na hasira, niliondoka kwa Mama na kwenda kwa Baba ambapo alikuwa amekaa na Rais hata sijui walikuwa wanazungumza jambo gani? Waliponiona walisimamisha mazungumzo yao.
“Bora umekuja sasa” Aliniambia Baba, ikanibidi nipoe. Hasira zote niliziweka pembeni maana sikutaka kulianzisha mbele ya Rais
“Kuna nini Baba?”
“Judy anawasili kesho hapa, kutakuwa na watu mbalimbali ambao watakaribishwa ili kumpokea. Nawe ukiwemo” Rais alitoa maelezo
“Oh! Kumbe”
“Ndio, kwahiyo nategemea utajiandaa kuwa naye”
“Sawa” niliondoka mahala pale maana sikutaka kukaa.

Nilienda chumbani kwangu ambako nilijifungia na kuanza kuangua kilio. Nililia mno maana sikupenda kile ambacho kimefanywa kuhusu picha pamoja na video. Nikiwa chumbani, Baba alikuja. Alifungua mlango na kukaa kitandani, akiniangalia aliuliza.
“Unaichukia”
“Kwanini umefuta picha?”
“Nafanya hili ili kulinda hadhi yako, hadhi ya Rais na heshima yetu kama wazazi
“Ndio ufute picha?”
“Rais amekuamini ndio maana amekupa Judy, kwanini unataka kutufanya tuonekane wapuuzi?”
“Ni wewe ndio ulinilazimisha lakini mimi sipo tayari”
“Najua umeumia lakini hupaswi kuwa na picha za masikini katika simu yako” Baba alisisitiza na kuondoka.

Usiku wa siku hii ulikuwa mrefu sana, nilipatwa na hasira vilivyo juu ya kile ambacho kimetokea. Sikukupenda kwakweli lakini ningefanyaje kama picha tayari zimefutwa? Sasa nikawa nawaza wapi ambapo ningeweza kumpata yule binti? Nilijiuliza maswali mengi sana lakini sikuweza kupata jibu.

Asubuhi ilipopambazuka, watu mbalimbali walikuja Ikulu wakitokea maeneo tofauti tofauti. Nami nilifuatwa na mtu wa mavazi ambaye alinitaka kwenda kupima suti, si unajua tena mambo ya Prince kwakuwa natakiwa kuwa mpenzi wa binti wa Rais.

Alipomaliza nilimuulizia kuhusu mpiga mbira kama amewahi kumsikia lakini alisema hajawahi. Alinikera na yeye namuulizia masuala ya muhimu halafu hajui lolote. Basi, muda ulienda wageni nao hawakuacha kuporomoka pale Ikulu. Kwa bahati nzuri kulikuwa na watu ambao wangepiga ngoma ili kumburudisha Judy akiwa kama binti mfalme.

Miongoni mwa watu hao alikuwepo pia Mpiga mbira lakini jambo la kushangaza ni kwamba, walimzuia getini na kumtaka asiingie hadi aende akabadilishe nguo maana alivaa nguo za kuchakaa, lakini ukweli haukuwa hivyo. Bali Baba alitoa amri ya kumzuia mtu yule ili mimi nisiweze kumuona.

Habari ikanifikia kwa haraka sana, nami nikaipeleka kwa Rais.
“Hana kazi ingine zaidi ya hii, kwanini asiruhusiwe?” nilimwambia
“Unamfahamu?”
“Ndio” Nilijiongeza kama kuna lolote ambalo lingetokea huko mbeleni basi ningejua natatuaje. Kwa bahati nzuri binti aliingia kwa ajili ya kupiga mbira. Siku hii nikajiambia kwa namna yoyote nitahakikisha najua wapi mrembo huyu anakaa ili iwe rahisi kwangu hata nikimtafuta basi naweza kumpata....... ITAENDELEA
 
Episode Three

Wageni waliendelea kutiririka Ikulu, watu walikuwa wengi mno kana kwamba kulikuwa na mkutano hivi. Wapo ambao walikuja na familia yao, wapo ambao walikuwa wenyewe. Wapo ambao walikuwa ni walinzi lakini hawa wote walikuja kwa ajili ya kumpokea binti Rais ambaye aliwasili kwenye majira ya saa 11 jioni hivi.

Ilikuwa furaha kwa Baba, ilikuwa furaha kwa Mama pamoja na Rais na hata mke wake pia ambao walikuwa wanamtaza binti huyu. Nami nilipomuona sikutaka mambo mengi, nilijua sitapata muda wa kuzungumza na Mpiga mbira. Nilijitoa ufahamu.

Nikaenda kwa mmoja wa wafanyakazi wa ndani ambaye aliitwa Anna, huyu tulimzidi cheo kwahiyo ilikuwa rahisi kumtumikisha ana akanielewa.
“Unamjua yule mpiga mbira?”
“Ndio”
“Nataka ujue wapi ambapo anaishi, ila hii iwe siri yetu”
“Unanipa Tsh ngapi?”
“Unapenda hela, nataka unisaidie bhana”
“Sawa hakuna shida” Anna alinielewa nami sikumuacha bure nilimwahidi kama atajua wapi anakaa basi ningempa kiasi cha laki mbili kama posho. Alinikubalia na nilirudi Ikulu kuzungumza na familia.

Nilikuta sehemu ambayo sherehe ya mapokezi ya Judy ikiwa imejaa, mida ya saa moja usiku ilikuwa kama saa sita usiku. Sauti ya muziki haikuacha kusikika huku wasanii mbalimbali wakiendelea kutumbuiza.

Baba, Rais, Mama, Mama Judy walikuwa wamekaa meza moja huku Judy akiwa amesimama akizungumza na Kijakazi wake. Nami nilipiga hatua hadi karibu yake, nilimsalimia kabla ya kurudisha macho kwa Mpiga Mbira ambaye alikuwa amesimama kwa pembeni akitutazama.
“Anaonekana mzuri, ngoja nikamsalimie” Nilijiambia moyoni na kumuaga Judy ambaye aliniuliza naenda wapi? Lakini nilimdanganya, akanielewa.

Nilienda hadi kwa Mpiga mbira, nikajaribu kumsemesha lakini hakujibu lolote. Nikamuuliza mbona hakunitafuta lakini alikausha tu. Alinikera mno hadi nilipayuka.
“Kila siku nakuongelesha na huongei, au unapenda navyoteseka kukutafuta?” Nilidhani kwamba angechukia lakini hakuonesha dalili hizo.
“Ondoka, rudi sehemu yako” Sauti ya Mama kutoka nyuma yangu ilipenya kwenye masikio yangu. Niligeuka na kumtazama.
“Mama namuongelesha muda wote lakini haongei?
“Unaongea kwa sauti, Rais atakusikia na utamweka mwenzako sehemu mbaya Muache”
“Sawa” Nilirudisha macho kwa Mpiga mbira.

Yule binti alishika mbira yake na kuanza kupiga taratibu, sauti ambayo ilikuwa inatoka ilipoza kabisa hasira zangu. Alikuwa anafuatisha wimbo nzuri ambao sikuwahi kuusikia kabla, nilijikuta nikisimama na kugeuka. Nikamtazama, naye aliweka tabasamu huku akiendelea kupoga mbira. Nikahisi kama hakuna kitu ambacho kimetokea. Basi ilinibidi nirudi lakini sio kwamba sikuwa na hasira.

Nakumbuka siku hii nilimtazama sana huyu binti, nikataka kumchukua video lakini sikuwa na simu maana Baba aliichukua muda tu. Nikachukia kuanzia mwanzo wa shughuli hadi ilipoisha kwenye majira ya saa sita hivi.

Watu mbalimbali waliondoka katika eneo lile nami nilikuwa wa mwisho kabisa. Kutokana na kuwekeza macho kwa Mpiga mbira, kwa muda mrefu. Judy alihisi jambo maana hata muda niko naye sikuwa mtu wa kuzungumza kama ilivyokuwa kawaida yangu. Macho nilimpa yule binti na sio Judy tena. Hii ilimkera lakini alishindwa kuniambia.

Basi asubuhi ilipofika, tulitoka na Judy kuelekea kwenye hotel moja hivi ambako huko tungekutana na marafiki zake. Lakini tukiwa njiani sikuacha kuwaza kuhusu yule binti. Nilitamani kumuona mpiga mbira wangu. Nilijikuta naangaza kila sehemu ila wapi? Sikumuona.
“Unaonekana kama mtu ambaye hujafurahishwa na ujio wangu?”
“Kwanini?”
“Nimehisi hilo, tangu jana usiku hunipi muda kabisa”
“Hapana sio kweli, nimependezwa na Baba anasema kwamba mpango wa ndoa upo tayari”
“Upo tayari kunioa?”
“Kwani ushapata mchumba?”

“Hapana ndio maana nimerudi kwa ajili yako”
“Nami nipo kwa ajili yako pia” Niliamua kumzuga lakini sikuwa na lamaana ambalo namaanisha.

Basi, tuliendelea na safari hadi tulipofika kwenye hotel ambako Judy alinitambulisha kwa Marafiki zake kibao ambao walinipenda na kunipa pongezi kwa kuwa na mwanamke mzuri. Licha ya pongezi zao, ila binafsi ilikuwa nikimtazama Judy namuona ni mwanamke wa hovyo na hayupo katika moyo wangu.

Tuliporudi Ikulu, muda wa chakula cha jioni. Anna alikuja na kuninong’oneza.
“Tayari nimeshajua wapi anakaa”
“Usiniambie..?”
“Ndio” Ilinibidi nitoke na Anna nje ili tuzungumze vizuri maana kwa jambo kama lile hatukupaswa kuongea mbele ya watu.

Tulitoka hadi nje ambapo tuliweka kituo kwenye bembea, kila mmoja akawa tayari kumsikiliza mwenzake.
“Umejua na jina lake?”
“Ndio, anaitwa Jane” Niliposikia jina tu, nikasawazika moyo. Nilikuwa napenda niwe na mwanamke ambaye jina lake linaanzia na J, kama ilivyokuwa kwangu.
“Woow! Naitwa Jack then ye ni Jane, kama titanic hivi”
“Kwani umempenda?”
“Ndio”
“Jack unapendaje mwanamke kiziwi, hasikii wala aongei?”
“Kiziwi?”
“Ndio ni kiziwi”
“Mungu wangukwanza anaishi wapi?”
“Karibu na nane nane lakini ni mtoto wa kimaskini sana, anaokota makopo na yupo na mwanamke ambaye anaishi naye kama Mama yake lakini sio mzazi”
“Oh! Mama yake mzazi kafa au kamtelekesa?”
“Nimeambiwa kafariki muda tu lakini pia huyo mwanamke ni kipofu. Pia ana ndugu yake ni kibubu. Msaada pekee upo kwa Jane ambye anategemea mbira ili kuwalisha hao wengine” Nilihisi Anna ananiongopea, anataka kunipa hadithi za kale za kipofu, bubu na kiziwi. Nikajiambia, kesho nitaenda na kuhakikisha nampata ili kujithibitishia kama ni kweli ama anataka kuniongopea..... ITAENDELEA
 
Endelea kutupia episode mzee
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom