Je, unakumbuka penzi lako la mbali liliishia wapi?

buzitata

JF-Expert Member
Apr 11, 2017
1,997
7,068
Habarini

Leo nimekaa nikitafakari sana juu ya mambo ya muda kidogo yaliyopita juu ya safari ya mapenzi

Miaka ya nyuma lilikua ni jambo la kawaida kuwa na mahusiano na mtu ambaye hujawahi kumuona lakini ukawa na upendo naye sawa na unaishia naye jirani.

Nakumbuka wakat fb,bbm,na Whatsapp zimepamba moto nilidondokea kwenye penzi zito na Binti Fulani kutokea Kanda ya kaskazini

Kisa Cha kuanzisha mahusiano.

Nilikua na ndugu yangu ambaye tulikua tunawasiliana mara Kwa mara na sikusave namba yake kwasababu ya simu yangu ilikua imejaaa( yes zaman had smartphone zilikua na limit ya kusave majina)

Sasa wakat naandika namba ya huyo ndugu yangu Ili nimpigie kwabàhat mbaya zile namba nikawa nimezigeuza kwaiyo nikawa nimempigia mtu tofauti, huyo ndiye aliyenifanya niandike Uzi.

Alivyopokea niliongea naye kidogo halaf nikakata, na baadae nikamtafuta Tena na kuanzisha urafiki hatimaye penzi zito, tulikua tunapendana haswaaaaaa, kipind hicho hakuna maswala ya kutumiana picha ilikua ni mwendo wa kuulizana kama ww ni mweupe au mweusi,umbo, kimo, baada ya hapo unamuumba mwenyewe kichwani mwako kwamba huyu atakua hivi

Miaka ikapita tukiwa tunawasiliana baadae kidogo tukapotezana, siku Moja nikamtafuta akanambia aisee unabahati sana kipindi ulipokuwa kimya nilikua naumwa sana ilibaki kidogo nifaliki, sikuweza kutilia maanani sana nikampa pole halaf penzi letu likaendelea Kwa muda Fulani halafu tukapotezana Tena na Miaka ilivyosonga Mimi nikaoa na sikua namkumbuka kabisa

Kuna siku nilikua nimekaa na wife tunapiga stori za kawaida ghafla yule ndugu yangu ambaye namba yake ilipelekea kukutana na mpenz wa mbali akawa amenipigia, baada ya kuongea naye alivokata nikasema ngoja nitafute Ile namba ambayo ilikua inamilikiwa na mpenz wangu wa mbali kama inapatikana. Nilivopiga akapokea mdada akiskika yupo kwenye makelele ikabid nimtumie sms Ili nijitambulishe kama hiyo no ni yake au tayari IPO na mtu mwingine

Mara boooooom, yule mdada akasema ni kweli huyo unayemtafuta alikua mmiliki wa hii namba ila Mimi ni mdogo wake Kuna siku simu ilikua inamsumbua kwaiyo akanipa Mimi pamoja na line na yeye tayar ameshafariki Kwa ugonjwa wa kansa, alifariki(2018)

Sio Siri niliumia sana nilipoambiwa hivyo na ukizingatia tulikua tunatiana moyo sana Miaka ya nyuma

Mwisho wa yote mwanga wa milele umuangazie japo nilitaman sana kumuona àkiwa hai ila ndo ivo Tena kazi ya mola Haina makosa
 
Aisee umenikumbusha mbali sana ndgu.
Kipindi niko form two, kumiliki simu ilikua anasa, japo nilikua nasoma day school ila walimu bado walikua wanatukazia kinoma.

Ni wachache tulikua nazo enzi hizo, tulikua na ujinga wa kubunibuni namba then unapiga, akipokea dem mnakomaa nae akipokea men mnakata.
Huku na huko ikabahatishwa namba ya bidada mmoja, kila mtu akaichukua ile namba tulikua kama mtu 5 hivi.
Kila mmoja akamtongoza yule manzi kwa wakati wake ila ikatokea akanielewa mimi wakati huo yeye yuko form 4 nadhani.

Nilidumu na yule she kwa miaka 2 bila hata kumuona sura, ila kila kitu kuhusu yeye nilikua nakijua.
Tulipotezana nilipokua bize na kitabu, nikaja muona fb wakati huo tushaachana.
 
M pia nimo, kuna dada nilikuaga nachat nae fb mpaka tukawa kama wapenzi na akaniambia niend ila hela ikawa uchawi m nilikua chuga ye yupo tabora. An ilikua kila saa 12 asubuhi lazima anicheki
 
Aisee umenikumbusha mbali sana ndgu.
Kipindi niko form two, kumiliki simu ilikua anasa, japo nilikua nasoma day school ila walimu bado walikua wanatukazia kinoma.

Ni wachache tulikua nazo enzi hizo, tulikua na ujinga wa kubunibuni namba then unapiga, akipokea dem mnakomaa nae akipokea men mnakata.
Huku na huko ikabahatishwa namba ya bidada mmoja, kila mtu akaichukua ile namba tulikua kama mtu 5 hivi.
Kila mmoja akamtongoza yule manzi kwa wakati wake ila ikatokea akanielewa mimi wakati huo yeye yuko form 4 nadhani.

Nilidumu na yule she kwa miaka 2 bila hata kumuona sura, ila kila kitu kuhusu yeye nilikua nakijua.
Tulipotezana nilipokua bize na kitabu, nikaja muona fb wakati huo tushaachana.
huu mchezo wa kubuni namba hadi leo nnao sijauacha
 
Kuna mwanamke aliwahi kukosea namba kipindi hicho , aisee alinipenda sana alikuwa mtu kutoka Tanga jina lake aliitwa Amina makazi yake alikuwa anaishi kawe mwaka 2014,..

Aliniambia yeye ni bikra na anahitaji hiyo zawadi anipee mimi ila tulikuja kupotezana baada ya Mimi kwenda jkt ile miezi 6 ya koz na kuny'ang'wa simu ndo ikawa basi tena maana line yangu ilifungwa.

Kuna kipindi alinitumia mpaka picha nikiwa jkt ,aisee alikuwa ni mtoto haswaa yaaani
Utotoni ni kama malaika ngoja mzijue hanasa sasa, Hapendwi mtu tena 🤣🤣🤣
 
Kuna mwanamke aliwahi kukosea namba kipindi hicho , aisee alinipenda sana alikuwa mtu kutoka Tanga jina lake aliitwa Amina makazi yake alikuwa anaishi kawe mwaka 2014,..

Aliniambia yeye ni bikra na anahitaji hiyo zawadi anipee mimi ila tulikuja kupotezana baada ya Mimi kwenda jkt ile miezi 6 ya koz na kuny'ang'wa simu ndo ikawa basi tena maana line yangu ilifungwa.

Kuna kipindi alinitumia mpaka picha nikiwa jkt ,aisee alikuwa ni mtoto haswaa yaaani
Watu mnadanganywa sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom