HERY HERNHO
Member
- Mar 4, 2022
- 70
- 313
Tangu tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.8 liikumbe Uturuki na Syria tarehe 6 Februari, na kuua zaidi ya watu 44,000, kumekuwa na mamilioni ya machapisho kwenye Twitter yakishiriki habari, picha na video za maafa hayo.
Lakini imgegundulika kwamba baadhi ya machapisho hayo yameilaumu kwa njia isiyo sahihi HAARP, kisambaza data chenye nguvu kilichoko Alaska, Marekani, kwa kusababisha tetemeko la ardhi.
HAARP Ilianzishwa na jeshi la Marekani mnamo 1990 na imekuwa ikiendeshwa na Chuo Kikuu cha Alaska Fairbanks tangu 2014.
Kufuatia tetemeko la ardhi kulikuwa na ongezeko la idadi ya akaunti zinazochapisha kuhusu HAARP kwenye Twitter.
Katika moja ya machapisho, mwandishi aliuliza: "Ni nini hasa kilitokea Uturuki... Walitumia urekebishaji wa hali ya hewa ya Geo-engineering HAARP!"
Mtumiaji mwingine alishiriki video ya ndege na kusema kwamba wanyama walikuwa "wakitenda vitu vya ajabu" kabla ya tetemeko la ardhi, kisha akauliza ikiwa Uturuki "ilishambuliwa na HAARP?"
Watu pia walikuwa wakichapisha picha za mawingu, wakidai kuwa zilionekana Uturuki kabla ya tetemeko la ardhi na zilitengenezwa na HAARP.
HAARP ilianzishwa awali ili kutafiti athari za tabaka la angahewa ya dunia ambayo ina mkusanyiko mkubwa wa ayoni na elektroni na ina uwezo wa kuakisi mawimbi ya redio (ionosphere) kwenye mawasiliano ya kijeshi na kiraia na mifumo ya urambazaji.
Usumbufu unaotokea kwa kawaida katika ionosphere unaweza kuvuruga mawimbi ya redio yanayopitishwa kutoka duniani, ambayo ni muhimu kwa aina nyingi za teknolojia ya kisasa, ikiwa ni pamoja na satelaiti za GPS, mifumo ya Wi-Fi na vyombo vya anga na mawasiliano ya redio.
Mnamo 2022, mafuriko yalipopiga jiji la Bulgaria la Karlovo, kulikuwa na madai kwenye mitandao ya kijamii kuwa mvua hiyo kubwa ilisababishwa na HAARP.
HAARP pia ililaumiwa kwa mafuriko mabaya nchini China na moto mkubwa wa misitu nchini Uturuki mnamo 2021.
katika coment nimekuweka taarifa jins HAARP inavyofanya kazi