Tetemeko ardhi lenye nguvu limeripotiwa katikati mwa Uturuki tena

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
21,713
35,539
Tetemeko jipya la ardhi lenye nguvu limeripotiwa katikati mwa Uturuki.

Utafiti wa Jiolojia kutoka Marekani unasema tetemeko lenye ukubwa wa 5.5 lilikuwa katika kina cha kilomita 10 (maili 6) karibu na mji wa Golbasi.

Wakati huo huo, Kituo cha Ulaya-Mediterranean Seismological Center (EMSC) chenye makao yake nchini Ufaransa kiliweka nguvu ya tetemeko kuwa karibu na Golbasi 5.6, na kuongeza kuwa lilikuwa katika kina cha 2km.

Mashirika yote mawili yalisema tetemeko hilo lilitokea saa 03:13 GMT siku ya Jumanne. Hawakutoa maelezo zaidi.

Eneo la Kusini-Mashariki mwa Uturuki limekumbwa na mfululizo wa mitetemeko kufuatia tetemeko kuu la ardhi karibu na mji wa Gaziantep Jumatatu asubuhi.
 
Hii dunia ni kama msukumo wa chini umeongezeka nguvu....
Acha tu mamii.. Huku ni majanga ya hali ya juu, vijumba vyetu tumejenga chini ya ubora, hatuna bima.. Tupo tupo tu.. Ikitokea vifo vitakuwa vingi, wengi tutaingia kwenye ukosefu wa makazi, watu kurudi nyuma(mtu una kijumba chako) ushamliza kisha kikabomoka si umasikini huu.
 
Tetemeko jipya la ardhi lenye nguvu limeripotiwa katikati mwa Uturuki.

Utafiti wa Jiolojia kutoka Marekani unasema tetemeko lenye ukubwa wa 5.5 lilikuwa katika kina cha kilomita 10 (maili 6) karibu na mji wa Golbasi...
Wagalathia na Wakurdi washapata majanga tayari.

Tumsikilize Receyp Tayyip Erdogan atadata apo
 
Acha tu mamii.. Huku ni majanga ya hali ya juu, vijumba vyetu tumejenga chini ya ubora, hatuna bima.. Tupo tupo tu.. Ikitokea vifo vitakuwa vingi, wengi tutaingia kwenye ukosefu wa makazi, watu kurudi nyuma(mtu una kijumba chako) ushamliza kisha kikabomoka si umasikini huu.
Nani kakuambia majanga ya asili bima itakulipa
 
Hii dunia ni kama msukumo wa chini umeongezeka nguvu

Ikiwa hivyo huko kwa wenzetu wenye vifaa vya kupima na wataalam wa kuweza kupunguza nguvu za mwendo wa matetemeko, je huku kwetu itakuwaje ?

Mungu tulinde.
Hakuna mtu anaeweza kupunguza nguvu za mtetemeko mama, wanachofanya sasa ni research and development ya structure za majengo na miundombinu mengine kama madaraja ambayo yatapunguza madhara ya uharibifu unaotokana na earthquake
 
Vifo vya watu 20000 is not a joke aisee. Hili janga nadhani niworld record.

Turkey inahitaji msaada wa hali na mali toka jumuia ya kimataifa.
 
Vifo vya watu 20000 is not a joke aisee. Hili janga nadhani niworld record.

Turkey inahitaji msaada wa hali na mali toka jumuia ya kimataifa.
Mkuu 2010 Haiti walikufa watu 300000 (laki tatu) usiku mmoja Port Prince. Oooooooh
 
Back
Top Bottom