Haaaa Mzee Mengi!!

Status
Not open for further replies.
ndugu zangu great thinkers, after discussing the road to IPP and its parking as compared to that of TBC what have we gained materially, what have we learned from that.

Tujiuilize je wananchi wamefaidika vipi na mjadala huo, je wameacha kuokota chupa za plastiki na makopo matupu ya bia, je zahanati zao zina dawa , je mazao yao yanafika mijini kwa urahisi na kununuliwa kwa bei ya kuridhisha, je watoto wao wanaenda sekondari na kulipiwa ada, je wakifaulu kwenda vyuoni bodi inawapa mikopo au ndio longolongo ya kila siku.

i would expect great thinkers to dig deep on issues of the like not barabara ya IPP, ambayo hata angeamua kuweka ya dhahabu bado watu wangesema tu. Tubadilike wakati ni huu miaka karibu 50 baada ya uhuru kunajadili vitu vya ajabu visivyo na tija
 
Nyie Wapambe wa Mengi,
Haya yambo kayapigia sana kelele humu ndani Mzee Mwanakijiji. Haya mambo ya ohh mbona siko peke yangu, ohh ni jukumu la serikali, ohhh kifo cha wengi harusi, ndiyo yanayotufanya milele tubaki palepale.

Mengi ni mtu maarufu sana na milele popote alipo ataonekana yeye. Kusema kuna wengine pale basi si awaite na kuwaambia wachangie kujenga hiyo barabara? Anasubiri na yeye kila kitu maana kashalipa kodi?

Nikiwa naishi Ilala Flats, tulikuwa na jirani yetu mmoja Mhandisi, Mzee Ngonyani. Kutokana na mabomba ya maji machafu kuziba, maji taka yalikuwa yakimwagika nje na kutoa harufu mbaya sana, wenyewe wakisema MAFURIKO. Yakitokea kinachofanywa mnafunga madirisha ya upande huo. Mhandisi huyo alifika point akachoka, akaja kuitisha mkutano kuwa ataenda kununua mabomba na kugharamia ujenzi wake. Wanaotaka kumsaidia wamsaidie na wasiotaka waache. Huwezi amini, wote walitoa hela. Tatizo dogo lipo kwa Msomali, yeye siku zote anasema "hana muda, wampe gharama na yeye atatoa pesa - Yes alitoa hela..." Wakati mwingine ni vitu viko ndani ya uwezo wetu ila tunakosa KIONGOZI. Kila mtu au anaona hilo HALIMHUSU au anasubiri FULANI aanze.

Tusiwe waoga namna hiyo. Mwambieni Mzee ashirikiane na jirani zake hao wenye mashine za kufulia sijui, na wenye viwanda wengine, unaweza kukuta wakapata hata msaada kutoka EU kama wao ni masikini saana na ile barabara ikajengwa kwa Zege ili kuhimili mizigo mizito kutoka kiwandani. Cement Tanzania ipo, mawe na mchanga upo, shida iko wapi? Ni pesa tu. Hao watu kama wameweza kuwa na Viwanda, kinawashinda nini kujenga barabara au Parking?
Mnaweza kumtetea sana ila ukweli ni kuwa UJUMBE UMEMFIKIA. Na kama nyie ni Wapambe wake basi MFIKISHIENI. Siku anafungua na aseme kuwa wameijenga kwa ushirikiano na wenzake. Labda itakuwa mfano kwa watu wengi huko mitaani kushirikiana na kuweka mazingira yao katika hali safi. Tunaisubiri saana serikali wakati serikali yenyewe ni ya CCM (Chama Cha Mafisadi).
kwa hiyo unataka mengi aitishe mkutano awaambie mwananchi wachangie, au mengi ni kiongozi wa mtaa ziliko ofisi IPP wa kitogoji, kwani jukumu la usafi au kujenga barabara ni mengi?..atajenga barabara ngapi maana ninavyojua mengi anamakampuni mengi sana..huna lolote wewe umetumwa na mafisadi tu
 
Dah payroll inafanya kazi kweli kweli!!!!
 
Unajua nini? Kuna misemo miwili huwa naipenda sana:
1) Watanzania "tumerogwa" na kuachiwa akili za kuvuka barabara tu ili tusigongwe na magari.
2) Watanzania "tumerogwa" kiasi kwamba kadri tunavyokojoa basi mkojo unatoka ukiwa umechanganyika na chembechembe za akili (i.e akili zinapungua kadri tunavyokojoa).

Sasa basi, ni dhahiri watu wengi pengine jazba zao zimewazuia kujua haswa lengo la hii mada au wanafanya makusudi kutotaka kujua. Jamani mimi sijasema sitambui mchango wa huyu mzee kwenye jamii yetu (tena kuna mahali nimekiri kuwa yeye ni role model wangu kwenye masuala ya kijamii). Na kwa sababu hiyo hiyo ya ujihusishaji wake kwenye jamii katika masuala ya mazingira, basi ndivyo hivyo hivyo nilivyokuwa nategemea kuona mazingira yanayomzunguka kuwa mfano wa kuigwa.

Ni kweli kuwa ile barabrara inatumiwa na viwanda vingine vilivyopo maeneo yale. Sasa basi, kwa bahati mbaya au mzuri, kati ya wamiliki wote wa viwanda maeneo yale, Bw. Mengi ndiyo ni kioo ambacho jamii yetu inatumia kujiangalia. Leo hii kukitokea kitu cha kihistoria eneo lile, jamii itatumia Ippmedia kama kigezo cha simulizi la eneo la tukio hilo. Kabla ya jina la Subash Patel, Alpha au mengineyo, utasikia jina la Mengi kwanza likitajwa. Hii inadhihirisha prestige aliyokuwa nayo kwenye jamii yetu.

Kwa hiyo kama alivyosema Sikonge, mzee Mengi angeweza kabisa kutumia influence yake kuwakusanya wakazi wenzake maeneo yale ili kuweza kushughulikia ile barabara (iwe kuishinikiza serikali au wao wenyewe kupitisha harambee). Hilo halina ubishi.....yeye mwenyewe analijua hilo kabisa.

Kuhusu parking ya Ippmedia, jamani ile media stream imekuwa kwenye business kwa muda gani sasa? Vyombo vyake vya habari vina rank namba ngapi kwenye jamii yetu? Hebu niambieni kuna watu wangapi mashuhuri ndani na nje ya nchi wameshawahi kwenda pale au kuifagilia vyombo vile? Jamani yaani mnataka kuniambia kwa hadhi ya vyombo vya habari vile (pamoja na hadhi ya mmiliki wake) katika jamii yetu (na nje) ni sawa kabisa kuwa na parking ikiwa katika hali ile? Eti wengine mnathubutu kusema kuwa suala la parking ni sula dogo sana. Parking ya vyombo vya habari ambaye mmiliki wake ni kioo bab'kubwa katika jamii iko longolongo vile, lakini bado mnaona poa tu? Duh basi tunasafari ndefu....

Labda kwanza niulize maswali kadhaa- hivi Bw. Mengi bado ni mmoja ya wanahisa wakubwa wa Coca Cola Tanzania? Kama jibu ni ndio, sasa mbona njia ya kwenda Coca Cola ina rami (kuanzia pale kwenye kona mpaka kwenye get la coca cola)? Kama ni serikali iliyojenga, ni nani aliyeishinikiza kuweka rami kwenye kile kipande? Ni vipi ku-assume kwamba, kwa sababu Coca Cola ni ya wazungu ndio maana wanathamini mazingira yake; na kwamba kwa sababu Ippmedia ni ya mwenzetu ndio maana anaona mazingira yake sio ishu sana? Je ni sawa kutumia hiyo assumption hapo juu kuelemea kwenye ule msemo wa Miafrika Ndivyo Tulivyo?

NB: Kwa wale wanaofikiri kuwa nimeanzisha hii mada kwa agenda zangu binafsi (au nimetumwa), basi wamenoa. Mimi ni mmoja ya watu wanaozimia sana mafanikio ya yule mzee katika ujihusishaji na mambo ya kijamii. Kama kuna kitu ambacho ningependelea yule mzee anifunze basi ni njia mbalimbali za kuweza ku-give back to the community. Kwa wale wanaonijua ambao pia wanajua mipango yangu ya siku za usoni kwenye jamii, basi wanajua ni jinsi gani ninavyoweza kumhitaji yule mzee kwa ushauri.
 
Nchi nzima iko shaghalabagala sasa kwa nini unam single out Mengi? Mavumbi umeyaona ofisini kwake tu? Sinza hakuna mavumbi? Tandale hakuna mavumbi? Upanga hakuna mavumbi? Sengerema hakuna mavumbi? Kisesa je?

Sasa kama mavumbi ni commonplace Tanzania kwa nini umlaumu yeye tu? Tujilaumu sote kama taifa na si mtu mmoja mmoja kwa vile tu wanahadhi fulani.
 
Ngabu,
Kwa bahati mbaya, watu au maeneo yenye wakazi ambao wanakipato cha juu yanakuwa singled out. Unajua kwa nini? Kwa sababu huko ndiko ambako mtari umechorwa juu sana. Hivi unajua kwa nini watu wanaponda barabara za mitaa ya Mikocheni na Mbezi Beach? Ushasikia watu wanaponda njia za mitaa ya Manzese, Tandika, Buguruni, na kadhalika?

Kwa hiyo, mzee anakuwa singled out kwa sababu ya hadhi yake pamoja na uongozaji wake katika masuala ya kijamii. Ndo bei ya hadhi hiyo!
 
Ngabu,
Kwa bahati mbaya, watu au maeneo yenye wakazi ambao wanakipato cha juu yanakuwa singled out. Unajua kwa nini? Kwa sababu huko ndiko ambako mtari umechorwa juu sana. Hivi unajua kwa nini watu wanaponda barabara za mitaa ya Mikocheni na Mbezi Beach? Ushasikia watu wanaponda njia za mitaa ya Manzese, Tandika, Buguruni, na kadhalika?

Lazima kuwe na standard moja. Miundombinu kama barabara lazima iwe mizuri kotekote maana hata huko Tabata, Mivinjeni, Mlalakuwa na kwingineko kuna binadamu wanaoishi kama huko Mikocheni na Mbezi Beach.

Hii dhana ya kuwa na standard tofauti tofauti ndio hujenga matabaka ya walionavyo na wasionavyo! Siipendi kabisa mimi. If you are going to hold Mengi to a higher environmental standard so should be the case to others as well. There shouldn't be a double standard when it comes to that.
 
Watanzania kweli nchi yetu imejichokea, na hatujui nini kazi ya kodi zetu. Sasa leo hii Mengi awakusanye wenye viwanda wenzake wafanye harambee wajenge barabara na kodi wanazolipa zitafanyia nini?
 
Watanzania kweli nchi yetu imejichokea, na hatujui nini kazi ya kodi zetu. Sasa leo hii Mengi awakusanye wenye viwanda wenzake wafanye harambee wajenge barabara na kodi wanazolipa zitafanyia nini?

Amini amini nakuambia, kwa Tanzania hii na kama ikiendelea kuwa ilivyo, ukisubiri hela ya kodi ije ijenge hizo barabara, zitakuja kuanza kujengwa siku moja kabla ya Yesu kurudi kuihukumu dunia. So keep in waiting.
 
kwa hiyo unataka mengi aitishe mkutano awaambie mwananchi wachangie, au mengi ni kiongozi wa mtaa ziliko ofisi IPP wa kitogoji, kwani jukumu la usafi au kujenga barabara ni mengi?..atajenga barabara ngapi maana ninavyojua mengi anamakampuni mengi sana..huna lolote wewe umetumwa na mafisadi tu

Kwani Jumamosi atapokuwa Nzega kutoa hiyo Misaada kwenye majimbo ya hao wabunge kipenzi chake (afike na Sikonge basi aache hizo pesa zake watu tuongeze wake) kwani yeye ni kiongozi wa MITAA ya Nzega? Kama angelikuwa Mzungu angelikuwa kajijengea hata kwa kuweka vitofali vya cement (pavements) ambavyo siku hizi watu kibao wanajijengea. Mkuu yaani UNACHEMKA PUMBA za ovyo hata nguruwe watazigomea kula.

Nchi nzima iko shaghalabagala sasa kwa nini unam single out Mengi? Mavumbi umeyaona ofisini kwake tu? Sinza hakuna mavumbi? Tandale hakuna mavumbi? Upanga hakuna mavumbi? Sengerema hakuna mavumbi? Kisesa je?

Sasa kama mavumbi ni common place Tanzania kwa nini umlaumu yeye tu? Tujilaumu sote kama taifa na si mtu mmoja mmoja kwa vile tu wanahadhi fulani.

Nyani Ngabu, uko sawa Mkuu, MITANZANIA NDIVYO ILIVYO. Heri kuiacha na Mivumbi yao, huku ikizubiri Mvua kupunguza hilo Vumbi na hapohapo kutumia advantage ya maji ya mvua ili kutapisha vyoo.... akhhhhh puuu!!!

ACHA WAFU WAWAZIKE WAFU WENZAO.
 
Watanzania kweli nchi yetu imejichokea, na hatujui nini kazi ya kodi zetu. Sasa leo hii Mengi awakusanye wenye viwanda wenzake wafanye harambee wajenge barabara na kodi wanazolipa zitafanyia nini?

Ni kweli kabisa hii nchi imejichokea kabisa sijuhi mtoa hoja kama kaziona parking zingine za mjini, kabla hujafika kwa Mengi ukitokea Morroco unafika pale kwenye makao makuu ya tume ya Science na Technologia, sijuhi mkuu kama ameiona ile parking pale, ukifika makao makuu ya wIZARA YA ULINZI NA MAKAO MAKUU YA JESHI PALE UPANGA SIJUHI KAMA PARKING AMEIONA, kuna parking kubwa pale AVALON SIJUHI KAMA MKUU KAIONA ILE, SINA UHAKIKA NA LUGALO JESHINI? KUNA PARKING NYINGINE IPO PALE MBELE YA STATISTICS, UPIMAJI NA RAMANI NADHANI NA WIZARA YA FEDHA PARKING IPO PEMBENI YA BAHARI,
HIVI MKUU KESHAIONA PARKING YA PALE MAKAO MAKUU YA POLICE (CENTRAL),
MIMI NADHANI KAMA HAUKUWA NA NIA MBAYA NA BWANA MENGI BASI UNGEWEKA TOPIC YAKO IWE OPEN NA TUJADILI UBOVU WA PARKING NA BARABARA ZOTE ZA DAR NA SIO KUMCHAGUA MENGI TU, KAMA MENGI NI ROLE MODEL HATA SAIDI MWEMA NI HIVYO HIVYO LAKINI OFISI ZAKE PARKING NI MBOVU zaidi ya za Mengi
nawasilisha
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom