Umeona kwa Mengi tu? Hiyo barabara inakwenda kwenye nyumba za kuishi watumishi wa serikali akiwepo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mawaziri, Wakurugenzi n.k. Hivyo inatakiwa serikali itengeneze. Huwezi kulinganisha na TBC kwani TBC wanatumia kodi zetu ambazo ni pamoja na anazolipa Mengi. Hata hivyo kila mtu ana mipango ya biashara yake na inawezekana parking kutengenezwa ipi kwenye process. Mengi anafanya kazi kubwa sana hasa ya kusaidia jamii yenye mahitaji. Ofisi zake zinafikika na hata parking gari zina park lakini kumbuka kuna watu wenye mahitaji muhimu zaidi ya kujenga parking. Barabara ni ya serikali na hilo eneo ni industrial area.