Haaaa Mzee Mengi!!

Status
Not open for further replies.
Hapa suala la barabara ni la serikali kupitia;kuhusu parking ana-option ya kupa-decorate au lah!Hata hivyo kama ni suala la vumbi sehemu gani hapa nchini TZ hakuna vumbi?
 
kwa hiyo ulitaka mengi awafukuze mama ntilie na vibanda vyao....
lowasa ofisi zake ziko kwenye ile barabara na alikuwa pm mbona umtaji
chuki binafsi....
anyway siyo chuki bali uko kazini

Au wale nanihii pale pembeni ya white house yetu mbona wanatesa kama kawa?
 
Ile barabara kwani inaenda kwa Mzee Mengi peke yake? Kule chini kuna akina Subbash Patel na watu influential kibao. Lakini kwa kuwa watu wamezoea Mengi huwa anajitolea basi wanataka ajenge. Hata kama hamumpendi huyu mzee tumtendee haki kidogo,kazi ya barabara ni ya wakusanya kodi,otherwise mtu ajitolee mwenyewe siyo tuanze kuleta siasa hapa eti ajenge.
 
Nyie Wapambe wa Mengi

Mkuu Sikonge mie sio mpambe kabisaaa wa mzee Pua ndo maana katika thread ile nimesema matajiri wa Kibongo wanajisikia ufahari wanapo toa michango yao public lakini mfuate kwa pembeni kuwa unashida unauguliwa kama utapewa thubutu hapo hapo utakuta mtu katoka kutoa 150mil lakini unashida ya 100000 unanyimwa.
 
kama umeona serikali imeuza loliondo na watu wanachomewa nyumba hawana pa kukaa na iko kimya?huna haja ya kuongea kuhusu parking ya mengi,inadhuru au kuhusiana vipi na mahitaji ya wananchi?licha ya hivyo MZEE MENGI ni msaada na ni mtu mzuri sana katika kusaidia na kujali ubinadamu unapomfikia,kusema kweli jamani mi kuhusu huyu mzee nampa heshima yake,ni tofauti kabisa na hao watu mnawaita viongozi.kuhusu ufisadi na kilakitu nani si fisadi tanzania?MWACHENI MZEE APUMZIKE,ANA THAWABU NYINGI KULIKO LAANA MNAZOMTUPIA,NA NI MFANO KATIKA JAMII

Wee Mtu vipi? Umeni-quate maneno yangu na hukusoma hata kimoja nilichoandika. Mbona unanipandikiza maneno ambayo mie sikusema? Hebu soma tena ujumbe wangu na urudie tena. Mbona wakimshambulia huwa anakuja kwetu kuanza kulialia? Sasa sisi tunasema kuwa "badala ya kugawa pesa, awe mfano wa kuigwa kwa watu". Awaonyeshe watu jinsi ya kuvua samaki na kugawa ndoano badaya ya samaki (pesa) ambazo siku zote zinalemaza watu.
Ombi langu kwa Mengi ni dogo sana:-
1. Awe mfano kwa kutunza mazingira sehemu anayokaa na anayofanyia kazi.
2. Awe kiongozi kwa kuwaongoza watu kutunza mazingira sehemu wanazokaa.

Nani hapa anaongelea Serikali ya CCM? Ile hamna cha kuongea tena maana tumeongea saana na hakuna kinachoendelea. Kama watu wakianza kupata mwamko wa kubadili maisha yao, itakuwa ni shule nzuri sana ya kufahamu ni kiongozi gani anawafaa kuwaongoza. Tatizo unapoishi sehemu kunanuka vinyeshi (maana mvua ikinyesha watu wanatapisha vyoo) na unakwenda kwa Mengi unakuta hayo maji taka yanapita mbele ya Ofisi yake na yeye kapumzika ndani (na watu kama wewe wanasema tumwache apumzike) unafikiri nitapata shule yoyote? Mengi ni Bench Mark ya Watanzania wengi kuwa kama yeye Mpingo mwenzetu kaweza, basi na sisi tunaweza. Wasukuma wengi sana kwa sasa wanafanya kazi usiku na mchana ili kushindana na Wachaga/Mengi. Kama huyu asingelikuwepo, si na wao wangebweteka? Mengi inabidi aongeze urefu wa eneo la mashindano na ikibidi hata uwanja wa mashindano aubadilishe.
Mengi hawezi kupumzishwa maana UMAARUFU UNA GHARAMA ZAKE.
Halafu hizi HESHIMA unazompa, naona hata akikutia kidole machoni, wala hutaona maana UMESHAKUWA KIPOFU. Mengi ni binadamu tu kama wengine zaidi ya kuwa MASHUHURI, Pesa, kutoa ajira na misaada kibao. Ombi ni kubadilisha tu namna ya kutoa misaada.
UNAFAHAMU KITU HIKI: European Union wanatoa saana misaada kwa nchi members. Ila wote huwa wanaambiwa kitu kimoja. Ukitaka msaada kujenga barabara basi tafuta Euro 1M na sisi tutakupa 3M. Kama huwezi kupata hiyo 1 Euro, hizo 3 Euro huzipati. Hapo watu huchakalika saana ili kukusanya Euro za kutosha kupata 3 zaidi katika kila moja. Ila wakija Afrika (na Mengi anafanya hivyo) wala hawaweki masharti..... chukua tu mwanangu ukaolee mke wa pili. Misaada, My A**.
 
Mkuu Sikonge mie sio mpambe kabisaaa wa mzee Pua ndo maana katika thread ile nimesema matajiri wa Kibongo wanajisikia ufahari wanapo toa michango yao public lakini mfuate kwa pembeni kuwa unashida unauguliwa kama utapewa thubutu hapo hapo utakuta mtu katoka kutoa 150mil lakini unashida ya 100000 unanyimwa.

Mkuu Fidel nilikuwa namaanisha kweli WAPAMBE na siyo wewe. Ukisoma vizuri utaona kuwa NAKUBALIANA NA WEWE na si NAKUPINGA. Tupo pamoja kwa hilo.
 
Ile barabara kwani inaenda kwa Mzee Mengi peke yake? Kule chini kuna akina Subbash Patel na watu influential kibao. Lakini kwa kuwa watu wamezoea Mengi huwa anajitolea basi wanataka ajenge. Hata kama hamumpendi huyu mzee tumtendee haki kidogo,kazi ya barabara ni ya wakusanya kodi,otherwise mtu ajitolee mwenyewe siyo tuanze kuleta siasa hapa eti ajenge.

Kama kuna watu wachafu kwenye maeneo yanayowazunguka basi ni Wahindi. Amini usiamini angelikuwa Mzungu angelikuwa kajijengea kibarabara kizuri kabisa. Mhindi ataajiri watu watunze kwake tu ila maji machafu yanakwenda wapi, taka zinamwagwa wapi hilo yeye halimhusu.

Narudia tena, kama wangelikuwa Waingereza wawili mmoja Mengi na mwingine Patel na wana nguvu kiasi hicho basi huko kungelikuwa na sewage system, barabara na parking nzuri. Ila bahati mbaya kuna Mpingo mwenye nafuuu na Mhindi ambaye kwao uchafu ni damudamu.

Ninaamini ingelitoka gazetini picha ya mazingira Patel na Mengi wanakofanyia kazi, basi na ugomvi wao wote wangelikutana na kuanza kujipanga ili wajenge hiyo barabara. Na huu ungelikuwa mwanzo mzuri.
 
Mkuu Fidel nilikuwa namaanisha kweli WAPAMBE na siyo wewe. Ukisoma vizuri utaona kuwa NAKUBALIANA NA WEWE na si NAKUPINGA. Tupo pamoja kwa hilo.

Nimekupata mkuu Sikonge unajua kuna watu humu iwa wanashindwa kabisa kujizuia ushabiki wao hata pindi linapo kuja swala la ukweli na uwazi kabisa hivi Mengi ni kweli anashindwa kuweka karami pale??? Watu wangapi tunaona wanajiwekea rami, maendeleo sio lazima tusubili serikali ikuletee hapo ulipo jishughulisheni sidhani kama mtu anajitolea kujenga barabara atakatazwa na serikali kwa nini unafanya hivyo hiyo siamini.
 
Hivi kwani Mecco kazi yao nini? Kama Mecco hawawezi kazi si wapewe Kajima au Konoike....
 
Hivi kuna mtu alishindwa kupata parking kwenye hizo ofisi? Kama vumbi ni swala la muda tu kwani elinino inakuja!(jokes)

Mkuu,
Yaani umemaliza yote. Umeandika kuwa ni JOKE ila ndiyo UKWELI. Kila kitu tutakuwa na sababu ya kusema kwa nini tumefanya hivi au vile. Sababu zenyewe za kitoto...... eti ELNINO yaja.

Unakuta jitu linazaa watoto kama utitiri na ukimwambia sasa utawatunzaje anakujibu "Mgomba hauzidiwi uzito na Mkungu wake" ila siku nyingine unakuta Mgomba huo huo umewekewa nguzo ya Y ili kuusaidia maana Mkungu ni mzito hadi Mgomba umepinda. Ni Ubishi tu na kibaya zaidi siku zote tunajifanya Much know, wheyaaa (where ya Kiganda).

Nyani Ngabu uko sawa "MIAFRIKA NDIVYO TULIVYO"
"MIHINDI NDIVYO ILIVYO".
 
Mjomba QUEMU embu jaribu kumlindia heshima huyu mzee,we unafikiri kodi na michango yote ya kijamii anayoitoa huyu bwana kuna watanzania wangapi wanaikwepa,mengi ni mfanya biashara by profession,hakuwahi kufanya engineering katika shule yake na pia hana kampuni inayodeal na construction,embu muonee huruma huyu mzee wa watu!!!
 
Hivi kwani Mecco kazi yao nini? Kama Mecco hawawezi kazi si wapewe Kajima au Konoike....
NN,
Huwezi kuamini MECCO ndiyo walijenga majengo kama Soko la Kariakoo, Kitega Uchumi (kama sikosei) nk na wahindisi wakiwa akina Mponzi. Hili shirika kama yalivyo mengine lilikuwa linaliwa hadi unalionea huruma. Mara ya mwisho nilikuwa MECCO wakijenga nyumba za wafanyakazi pale DSA (chuo cha bishara/Uhasibu Dar es Salaam). Hakukuwa hata na shine moja na sijui hata pesa za faida zilikuwa zinaweza kulipia wafanyakazi. Naona kama kawaida ya mashirika mengine, ilikufa ili kutoa nafasi kwa mashirika ya Wahindi kama ya akina DB Shapriya na wengine wa miaka hiyo ya 80 na 90. BIASHARA MBELE, NCHI YANGU NYUMA.
 
Huyo jamaa ana lake jambo. Kama angekuwa mfuatiliaji na km amefika ktk maeneo ya ofisi yanayomilikiwa na IPP media asingepost maoni hayo kutokana na unadhifu na matunzo yake. Lakini maeneo anayoyazungumzia si miliki yake, japo kuna wakati wenye viwanda maeneo hayo walikusanya nguvu na kugharimia uwekaji wa kokoto ktk barabara kuu iendayo huko, baada ya halm. kutotoa kipaumbele. Huyo Bw. Acheki pia na parking ya Alfa dry cleaners ya mzee wa kazi hapohapo jirani
 
Kutokana na maelezo na member humu unapata ufasaha wa hii "MIAFRIKA NDIVYO TULIVYO" kutoka kwa komredi Nyani Ngabu.
 
Mzee anahisi anawajibika zaidi kwa jamii. anawajibika kwa wanaohitaji, wanaohitaji zaidi ya barabara na parking nzuri. kwake hivyo haviongezi lolote kama kumsaidia anaehitaji Tsh. 60,000 pale Nzega ili aweze anzisha japo biashara ya vititumbua ili japo aweze somesha mwanae mlemavu ambae serikali imentelekeza. Aweze mpeleka mwanae hosipitali mana alie mtangulia alifariki kwa malaria baada ya kukosa huduma hosp kwakua hawezi kulipia etc. etc etc...........

Lazma tujifunze kuwaibika zaidi kwa jamii inayo tuzunguka kwani huo ndio uzalendo halisi. Kwako unahisi angefanya hivyo maana unakiona kizuri kwakua huna uwezo wakukifanya ila lingekua ndani ya uwezo wako lingeshuka thamani na ungekua na vipao mbele vingine zaidi. Ningeona mkuu unabusara kama ungempongeza kwa level of sucrificealofanya kwa kuacha yake binafsi na kuipa jamii.

Tusipo badilika kimitazama na kujenga uzalendo kama anayoonyesha mzee wetu Mengi sidhani kama tutafanikiwa kupambana na umasikili uliokithiri kwa sasa, maradhi na kukuza taaluma.

Tunahitaji mabadiliko ya kifikra kabla hatujafikiria mabadiliko mengine yeyote

Yetu macho
 
Mzee anahisi anawajibika zaidi kwa jamii. anawajibika kwa wanaohitaji, wanaohitaji zaidi ya barabara na parking nzuri. kwake hivyo haviongezi lolote kama kumsaidia anaehitaji Tsh. 60,000 pale nzega ili aweze anzisha japo biashara ya vitymbua pale nzega.

Huu siyo MSAADA, huku ni KUDEKEZA watu.

Angeliweka masharti kadhaa kabla ya kuwapa pesa. Huku anakofanya na alikofanya Kikwete ni KULEMAZA watu. Hawa watu hata plan ya biashara hawana, sasa unampa hela za nini? Aolee mke mwingine?
Hii misaada inayotolewa mbele ya WAANDISHI WA HABARI hata Yesu alisema ni BATILI. Angeliweka walau MASHARTI rahisi kwa watu kusaidiwa na siyo kugawa tu kama pipi....... Wengine wataenda kununua ukimwi.
 
Nadhani na wewe una ajenda yako. Ulitaka Mengi awafanyie kazi jiji wao waendelee kuponda raha wanakusanya kodi na kutafuna bata. Yeye alipe kodi, alafu ajenge barabara kwa kumfurahisha nani??

Wewe umejenga chochote wapi???


Mkuu mweleze huyo. Hizo ni barabara za mitaa, tena haziendi kwa IPP house peke yake, zinaenda kwenye Viwanda pia?? Kwa nini usiseme basi washirikiane na wale wenye viwanda maeneo yale na kuna shwahiba wa SSM na kiwanda cha Nondo halafu unataka Mengi ajenge peke yake??? Hao wenye viwanda pesa yao kubwa iko banked nje ya nchi na ya Mengi ni hapa inakusaidia mimi na wewe kupata mikopo benki na multiplier effect kwenye uchumi iko felt halafu unasema nini wewe mleta hoja?? Magezi, naona tumshauri huyu mtu afikirie kwanza kabla ya kunena!!!

Na kama anatoka Dar basi atuambie anashiriki vipi ku-repair barabara za mitaa hata tu kufukia shimo?? Kama anatoka kijijini na atuambie anashiriki vipi kuchimbia mashimo hasa baada ya mvua wakati hata wale wa vijijini ile ari ya ujamaa na kujitegema imekwisha ndiyo maana zile kazi za harambee mara nyingi ilikuwa Jumatatu kushughulikia matatizo ya kijiji imekufa fiiiiiiiii. Hakuna kitu kama hicho.

Na tuambie mleta mada kodi za mengi zinaenda wapi??? Tena walipaswa wahusika wajenge barabara zile maana zina wateja walipa kodi, niki assume na wale wahindi wenye viwanda kule wanalipa kodi!!!!!

Mleta mada acha fitina wewe??? Naona tangu jana kuna vibaraka wametumwa kumchafua Mengi hapa!!!! Mara ohh safari ya Nzega, mara ohhh Mishahara!!! Mna lenu jambo.
 
Lakini maeneo anayoyazungumzia si miliki yake, japo kuna wakati wenye viwanda maeneo hayo walikusanya nguvu na kugharimia uwekaji wa kokoto ktk barabara kuu iendayo huko, baada ya halm. kutotoa kipaumbele. Huyo Bw. Acheki pia na parking ya Alfa dry cleaners ya mzee wa kazi hapohapo jirani

Mkuu Kapongo,
Hili ndiyo haswaa tunalosema. Je unaweza kutujulisha walifikia wapi? Ilitakiwa wawahusishe watu wote wanaoishi huko au kuwa na biashara. Kama huna pesa walau nenda kafanye kazi za mikono kusaidia kujenga. Amini usiamini, watu hawa wangelikuwa wamebadilika sana kifikra leo hii na wangelikuwa too proud na barabara yao kwani NI WAO WAMEJENGA.
 
Kwa nini usiseme basi washirikiane na wale wenye viwanda maeneo yale na kuna shwahiba wa SSM na kiwanda cha Nondo halafu unataka Mengi ajenge peke yake???

Mkuu unategemea Mengi aketi na Subash Patel meza moja wajadili hili????

 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom