Baada ya kuisambaratisha vibaya CCM kwenye uchaguzi wa udiwani wa kata nne jijini Arusha mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA Godbless Lema kesho atahutubia mkutano mkubwa wa hadhara mjini Mbalizi Mbeya vijijini.
Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya mkutano huo Kissman Mwangomale amesema Lema amealikwa kuwa mgeni rasmi na wanachama wa mjini Mbalizi kwa kuthamini kazi kubwa anayofanya ndani ya Chadema.
CHADEMA inaongoza vijiji vyote vilivyoko katika kata za Utengule Usongwe na Nsalala zote za mjini Mbalizi.
Mkutano huo utafanyika katika viwanja vya mahubiri vilivyoko Tazara mjini Mbalizi.
Lema mbali ya kuhutubia mkutano wa hadhara anatarajiwa pia kufungua matawi ya CHADEMA na kupokea mamia ya wanachama wapya.
Kiongozi huyo wa ngazi ya juu ya CHADEMA anatarajiwa kusindikizwa na wabunge maarufu wa Kanda hiyo Mchungaji Peter Msigwa,Davidi Silinde na Joseph Mbilinyi anayejulikana kwa jina maarufu la Rais wa Mbeya.
Source:Tanzania Daima.