Godbless Lema kutikisa Mbeya Vijijini

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Baada ya kuisambaratisha vibaya CCM kwenye uchaguzi wa udiwani wa kata nne jijini Arusha mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA Godbless Lema kesho atahutubia mkutano mkubwa wa hadhara mjini Mbalizi Mbeya vijijini.

Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya mkutano huo Kissman Mwangomale amesema Lema amealikwa kuwa mgeni rasmi na wanachama wa mjini Mbalizi kwa kuthamini kazi kubwa anayofanya ndani ya Chadema.

CHADEMA inaongoza vijiji vyote vilivyoko katika kata za Utengule Usongwe na Nsalala zote za mjini Mbalizi.

Mkutano huo utafanyika katika viwanja vya mahubiri vilivyoko Tazara mjini Mbalizi.

Lema mbali ya kuhutubia mkutano wa hadhara anatarajiwa pia kufungua matawi ya CHADEMA na kupokea mamia ya wanachama wapya.

Kiongozi huyo wa ngazi ya juu ya CHADEMA anatarajiwa kusindikizwa na wabunge maarufu wa Kanda hiyo Mchungaji Peter Msigwa,Davidi Silinde na Joseph Mbilinyi anayejulikana kwa jina maarufu la Rais wa Mbeya.

Source:Tanzania Daima.
 
Hivi CHADEMA uchaguzi wa Arusha kumbe ulikuwa na maana sana kwenu?

Mimi nilijua imani yenu kuwa Arusha ni ngome yenu itafanya kazi!?

Mbona tena mnajitutumua kushangilia ushindi kwa kata ambazo kimsingi zilikuwa zenu?

Arusha ni yenu, kata ni zenu, kwanini mshangilie kuiangusha CCM?

Acheni hofu kwa CCM jamani, hizi ni siasa tu.
 
...aluta continua,tunawachapa mijini,tunawachapa vijijini,mpaka kieleweke,go, go gooo lema gooo..! Go cdm go chama langu, kwangua magamba mpaka yatoke damu...
 
Hivi CHADEMA uchaguzi wa Arusha kumbe ulikuwa na maana sana kwenu?

Mimi nilijua imani yenu kuwa Arusha ni ngome yenu itafanya kazi!?

Mbona tena mnajitutumua kushangilia ushindi kwa kata ambazo kimsingi zilikuwa zenu?

Arusha ni yenu, kata ni zenu, kwanini mshangilie kuiangusha CCM?

Acheni hofu kwa CCM jamani, hizi ni siasa tu.

nazani wanashangilia kwa sababu ccm mlitaka kuwanyanganya kata zao kwa kuwapiga mabomu,kwa mtutu wa bunduki..kununua shahada za kupigia kura..kuwanunua wazee wa kimasai..kuhairisha uchaguzi mara kadhaa..
 
Chama cha CHADEMA Leo kitafanya mkutano wa injili maeneo nzovwe mbeya mjini msikose waumini wote.
 
Chama cha CHADEMA Leo kitafanya mkutano wa injili maeneo nzovwe mbeya mjini msikose waumini wote.

Siasa zenu hizi ndiyo matokeo ya kura za CUF kwenye uchaguzi wa Kata.Na bado!
 
Baada ya kuisambaratisha vibaya CCM kwenye uchaguzi wa udiwani wa kata nne jijini Arusha mjumbe wa Kamati Kuu Chadema Godbless Lema kesho atahutubia mkutano mkubwa wa hadhara mjini Mbalizi Mbeya vijijini.

Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya mkutano huo Kissman Mwangomale amesema Lema amealikwa kuwa mgeni rasmi na wanachama wa mjini Mbalizi kwa kuthamini kazi kubwa anayofanya ndani ya Chadema.

Chadema inaongoza vijiji vyote vilivyoko katika kata za Utengule Usongwe na Nsalala zote za mjini Mbalizi.

Mkutano huo utafanyika katika viwanja vya mahubiri vilivyoko Tazara mjini Mbalizi.

Lema mbali ya kuhutubia mkutano wa hadhara anatarajiwa pia kufungua matawi ya Chadema na kupokea mamia ya wanachama wapya.

Kiongozi huyo wa ngazi ya juu ya Chadema anatarajiwa kusindikizwa na wabunge maarufu wa Kanda hiyo Mchungaji Peter Msigwa,Davidi Silinde na Joseph Mbilinyi anayejulikana kwa jina maarufu la Rais wa Mbeya.

Source:Tanzania Daima.

Jaman waoneni huruma kidogo hao SISIEMU jaman watakufa na presha
 
Habari yako! Ndiyo weekend inakwenda hivyo! Umeshapokea buku 7 yako hapo Lumumba?

Hivi CHADEMA uchaguzi wa Arusha kumbe ulikuwa na maana sana kwenu?

Mimi nilijua imani yenu kuwa Arusha ni ngome yenu itafanya kazi!?

Mbona tena mnajitutumua kushangilia ushindi kwa kata ambazo kimsingi zilikuwa zenu?

Arusha ni yenu, kata ni zenu, kwanini mshangilie kuiangusha CCM?

Acheni hofu kwa CCM jamani, hizi ni siasa tu.
 
Hivi CHADEMA uchaguzi wa Arusha kumbe ulikuwa na maana sana kwenu?

Mimi nilijua imani yenu kuwa Arusha ni ngome yenu itafanya kazi!?

Mbona tena mnajitutumua kushangilia ushindi kwa kata ambazo kimsingi zilikuwa zenu?

Arusha ni yenu, kata ni zenu, kwanini mshangilie kuiangusha CCM?

Acheni hofu kwa CCM jamani, hizi ni siasa tu.

roho inakuuma jamaa wao kila siku ni mchakamchaka hata hawawaachi mukapumua?
 
Jembe la a town linapiga kazi kweli, kwe2 karatu leo katika uwanja wa kilimatembo mbunge kipenzi cha wanakaratu mh Israel natse akiambatana na mbunge kijana vitu maalum cesilia paresso watawasha moto mkubwa sana magamba hamna chenu tena
 
Pamoja sana kamanda Lema, namkubali sana huyu jamaa. Speech zake hua ni za kuhamasisha ukombozi wa fikra. VIVA CHADEMA.
 
Lema kufanya siasa ni ishara ya utawala bora wa Chama Cha Mapinduzi na uongozi bora wa Jakaya Kikwete. Hivi mnajua kuwa kuna nchi ambazo wezi wa magari hawatakiwi hata kupiga kura, achilia mbali kuwa wabunge?
 
It is impossible for CCM to survive, CCM needs some blood to suck. CCM used to be like an eagle, but now it's more like a vulture. It used to be strong enough to go and suck anybody's blood whether they were strong or not. But now it has become more cowardly, like the vulture, and it can only suck the blood of the helpless. Now the CCM has fewer victims, less to suck, and it becomes weaker and weaker. It's only a matter of time in my opinion before it will collapse completely.
 
Lema kufanya siasa ni ishara ya utawala bora wa Chama Cha Mapinduzi na uongozi bora wa Jakaya Kikwete. Hivi mnajua kuwa kuna nchi ambazo wezi wa magari hawatakiwi hata kupiga kura, achilia mbali kuwa wabunge?

utakuja kufungwa kwa kauli zako...we fikiri huwezi kupatikana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom