Godbless Lema kuanza maombi ya kufunga na kuomba kwa siku saba

wakristo tumefundishwa kusamehe sasa sielewi ni Mungu gani atakayepokea hayo maombi ya kulipiza kisasi

Atayapokea tu mkuu kwa kuwa anasema yeye ndiye awezaye kulipa kisasi kwa kiwango kinachofaa, hivyo alipokataza mwanadamu kulipa kisasi, alijua hatuwezi kufikia viwango timilifu.
Kwa hiyo usiwe na wasiwasi kamanda, kesi imefika kwa hakimu wa HAKI.
 
Kwa ugumu wa mioyo yao Mungu atawapiga tauni
Nadhani kuna kuteleza kidogo. Tunatakiwa tumuombe mungu ili mapenzi yake yatimie (na sio kulipiza kisasi). Kama mungu ataona inafaa sasa kuwazuia wale wote wanaosababisha maisha ya watanzania kuwa magumu basi kupitia sala tunatakiwa tumuombe aingilie kati kulingana na mapenzi. (baba yetu ...... utakalo lifanyike duniani kama mbinguni...)
 
MH LEMA jana alitangaza kuanza maombi ya kufunga na kuomba kwa siku saba kuanzia jumatano ya tarehe 11 April 2012 na kuomba kila mwananchi anayependa haki kwa imani yake kumuunga mkono katika maombi hayo ya kufunga na kuomba. Pia aliomba maombi hayo yaendane na kuwasaidia maskini na wajane na wale wasiojiweza kwa vile vitu ambavyo Mungu ametubariki kwavyo.

Lengo kuu la maombi hayo ni kumuomba Mungu aingilie kati na kulipiza kisasi kwa wale ambao wametumia nafasi zao kushinikiza hukumu isiyo ya haki ambayo ilitolewa hivi karibuni na kumfanya aende likizo katika nafasi yake ya ubunge na pia maombi ya shukrani kwa Mungu kwa yote yaliyotokea. Hayo aliyasema jana katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya NMC jijini Arusha.
Tusipoteze muda kutetea makosa yaliyotendeka...na sala zake na hio funga yake aombe mungu wake amsaidie asiwe mropokaji na mchochezi amuombe ampe hekima zaidi ..ukweli siku zote utabaki hivo kama ulivo...na nyeupe haiwezi kuwa nyeusi hata siku moja....mshaurini Lema kuwa siasa si ugomvi wala matusi, aache jazba ya kupayuka hovyo...amekua na tabia ya kupayuka hovyo na maneno yake hayana ukweli ila ya kijiweni zaidi na ndio haya yalio sababisha kuvuliwa ubunge...haya yaliandikwa na kurikodiwa wakati wa kampeni .wakati wa kampeni zake zilitawaliwa na udhalilishaji wa wanawake na mgombea wa CCM kama mwanamke na muislam tena kwa kubadili dini!!, ni kweli alimdhalilisha kwa sababu ya jinsia yake na dini yake...huu ni ukweli...kulaumu hukumu na hakimu haisaidii kitu jadili jee lugha ya lema wakati wa kampeni ilikuwa inavunja masharti ya sheria za uchaguzi ama la? hili ndio la kujadili ...
lugha yake na maneno yake hata baada ya kuwa mbunge yamekua tata chadema wanahitaji kumweka chini....wamfuze siasa za ustaarab na kuropoka hovyo sio sifa ya kiongozi bora na makini..kuchaguliwa na kuwa na sapport katika jimbo sio hoja...hata Hitler alikuwa na supoort ya karibu 90% ya Wa Germans...na maneno yake ya hovyo na msimamo ya kibabe iliitumbikiza dunia katika vita vikuu vya pili...na wajerumani kukumutwa na dunia nzima...na ndipo walipokuja kujua ubaya wa Hitler na hotuba zake za hovyo...Uchochezi kuvunja amani ama kuasi au kuchukia mtu kwa jinsia yake ama dini yake ama asili yake ndio iliyokua dhambi ya Hitler lakini pia ndio ngazi aliyotumia kujipandisha mpaka akawa Kiongozi wa Germany....
Jaji amefanya kazi yake tujadili facts zilizopo kosa limeshatendeka na kamanda wenu anahitaji kujifunza sio kuendelea kufanya makosa yale yale ya kuropoka ati kikwete ndio alomvua ubunge..haya ni maneno rahisi sana...
 
lema anafunga ili situkane tena!! chadema huyu mtu ni msanii na wenye mature mind tunaona kama comedian fulani tu

tangu lini kufunga unatangaza?
 
Yani kabisa,sio udini tu,ukabila pia.hawana busara kabisa hawa watu.wananchi wanatakiwa kuwa na umakini wa hali ya juu ktk kuchagua viongozi wao.mi kuna sehemu naenda nakuta kabisa wanaongea kichaga.utafikiri tanzania ni ya wachaga.

Hivi wakiwepo wachaga kadhaa na wote ni member wa Chadema kuna ubaya gani wakiongea kichaga? Mbona hata CCM, UDP member wao wakiwa ni wakabila moja huongea kikwao tu kwani kuna nini? Na aliyekwambia kwamba wachaga wote wanaelewana ni nani? hivi Mmarandu na Mmachame au mkibosho pamoja na kuwa wote ni wachaga unadhani wanaongea kichaga cha aina moja?

Mnapenda sana CCM kiasi kwamba hata yale mnayo watuhumu Chadema mtakuwa CCM wanayo even worse, angalia kwa mfano suala la Udini, hivi CCM unaweza kusema sio chama cha kidini? Wakipata shida sehem yeyote hukumbilia kwa viongozi wa Dini, tena wa aina moja, kweli nimeamini, ukipenda, hata Chongo we utasema ni Kengeza! Suala la Kuomba ambalo Godbless Lema amelitangaza mbona ni zuri sana, kila dini huwa na maombi ya kufunga, Waislam wanafunga, wakristo hali kadhalika hata Freemason nao wanafunga, hapo cha ajabu ni nini? au mnaogopa kwa ville mlitenda hiyana kwenye hiyo kesi na mnajua akiachiwa Mungu basi ataleta haki?
 
Tusipoteze muda kutetea makosa yaliyotendeka...na sala zake na hio funga yake aombe mungu wake amsaidie asiwe mropokaji na mchochezi amuombe ampe hekima zaidi ..ukweli siku zote utabaki hivo kama ulivo...na nyeupe haiwezi kuwa nyeusi hata siku moja....mshaurini Lema kuwa siasa si ugomvi wala matusi, aache jazba ya kupayuka hovyo...amekua na tabia ya kupayuka hovyo na maneno yake hayana ukweli ila ya kijiweni zaidi na ndio haya yalio sababisha kuvuliwa ubunge...haya yaliandikwa na kurikodiwa wakati wa kampeni .wakati wa kampeni zake zilitawaliwa na udhalilishaji wa wanawake na mgombea wa CCM kama mwanamke na muislam tena kwa kubadili dini!!, ni kweli alimdhalilisha kwa sababu ya jinsia yake na dini yake...huu ni ukweli...kulaumu hukumu na hakimu haisaidii kitu jadili jee lugha ya lema wakati wa kampeni ilikuwa inavunja masharti ya sheria za uchaguzi ama la? hili ndio la kujadili ...
lugha yake na maneno yake hata baada ya kuwa mbunge yamekua tata chadema wanahitaji kumweka chini....wamfuze siasa za ustaarab na kuropoka hovyo sio sifa ya kiongozi bora na makini..kuchaguliwa na kuwa na sapport katika jimbo sio hoja...hata Hitler alikuwa na supoort ya karibu 90% ya Wa Germans...na maneno yake ya hovyo na msimamo ya kibabe iliitumbikiza dunia katika vita vikuu vya pili...na wajerumani kukumutwa na dunia nzima...na ndipo walipokuja kujua ubaya wa Hitler na hotuba zake za hovyo...Uchochezi kuvunja amani ama kuasi au kuchukia mtu kwa jinsia yake ama dini yake ama asili yake ndio iliyokua dhambi ya Hitler lakini pia ndio ngazi aliyotumia kujipandisha mpaka akawa Kiongozi wa Germany....
Jaji amefanya kazi yake tujadili facts zilizopo kosa limeshatendeka na kamanda wenu anahitaji kujifunza sio kuendelea kufanya makosa yale yale ya kuropoka ati kikwete ndio alomvua ubunge..haya ni maneno rahisi sana...

Mungu si mjinga wala hajawahi kuacha kutenda haki, kwa wanaoonewa, kila siku amesimama kati akiwainua wanyonge,hakuna CD wala audio ya matusi ya Lema yaliyopelekwa mahakamani Kuthibitisha hayo matusi yake,Huyo Mkangaa ni shetani lucifero amezoea,alisababisha Makongoro apoteze ubunge ,sasa tumejua yeye ni ajenti wa Usalama wa Taifa , na wewe ni mwongo unathibitsha jinsi unavyoshabikia dhuluma,na maonevu ya watawala,watawala wenye dhuluma,uonevu na unynyasaji duniani pote kabla hawajafa Mungu huwapa adhabu stahiki,unaweza ukamuona Lema mwehu lakini anachosema ana mantiki kila chozi litolewalo na wanyimwa haki hakika inakuwa ni laana wale wanaohukumu wenzao kwa Simu wakiwa IKULU

Ukweli IKULU hawatakaa milele na hawana siha yeyote ya heshima ya Mungu kwani hawajatenda mema yeyote kwenye utawala wao .kila pembe ya nchi ni vilio,wananhhi wanalilia damu zao zinazomwagwa kutokana na amri zao watawala wakiua wananchi wanao lilia nchi yao,kukataa kuporwa madini yao,mashamba yao,ardhi yao,kunyimwa haki za msingi,maendeleo,elimu,ulinzi,mapatano n.k

Hakika hakuna mwivi wa haki za wananchi aliyesimama mbele ya kiti cha mwenyezi mungu akapokelewa,ukweli wengi wamejikuta wakimaliza maisha yao wakiwa na machnungu tele

Dhuluma haijawahi kushinda haki ,mwacheni Lema amlilie Mungu wake na atamsikia
 
tuko pamoja na mungu atajiobu maombi kwa kuwa huwa hamtupi mja wake. Lema tuko nmyuma yako tunakuombea
 
Iaonyesha ni jinsi gani cdm mtakapobahatika kuingia ikulu mtakavyoiharibu híi nchi
 
Akifunga kwa lengo hilo la Mungu kulipa kisasi hatafanikiwa. Katika Agano Jipya Huko nikuomba vimbaya. Bora asamehe na aombe Mungu Aingilie kati kwenye rufaa yake.

Mpeni ushauri Lema, vita ya kiroho nitofauti sana na vita ya mwili. Maana ya kufunga nikupata uwezo wa kuingia katika ulimwengu wa roho ili kuweza kurekebisha mambo yasiyoenda sawa yakae vizuri. Mojawapo ya masharti ya kuingia katika ulimwengi huo ni kusamehe.
 
Jamani mbona pro-ccm hampendi kusikia habari za Mungu? Au mna mapepo? Kwani ni dini gani isiyomjua mungu? Na kwani kufunga na kuomba ndio kosa na ni dini gani isiyofanya hivyo koz hata freemasons wenyewe na ushetani wao wanamjua mungu! KWELI CCM MMEFIKA PABAYA SANA KAMA NDO HIVI MKISIKIA MUNGU BASI MNAANZA KUTOKA POVU.
mimi nimeshajifunza kwamba kuna watu ambao hawaelewesheki na kuwaelewesha ni kupeteza nguvu bure,hawa jamaa nazani suluhisho ni kuwaacha walivyo maana wanaweza anza toka nje ya mada muda si mrefu ukaanza kusikia anasema Yesu sio Mungu, Ukristo sio dini,au Paulo sio mtume,wewe achana nao
 
Naona maombi ni siri binafsi ya mtu na siyo kutangaza hadharani.

Natoa angalizo kwa CDM. Kwanini mnaruhusu majukwaa yenu ya siasa kuongelea habari za maombi? Kama ni kufungua kwa dua sawa ila mtu kuitisha maombi? Anatoa picha gani kwa wanachama na ambao si wanachama?

Hebu geukeni kidogo - teueni na wale wa dini nyingine and stop keeping quiet when one of ur leaders talks abt religion, siasa siyo dini...na msigeuze dini kuwa mtaji wenu. La sivyo itakula kwenu...mnaelekea walipokuwa CUF. A good strategist hahitaji kutafuta wapi pa kuwapiga, hapo hapo kwenye udhaifu wenu.

Don't give me ur list of MPs sijui viongozi gani mnao wa dini gani, am not interested.

Tatizo lako ni upeo mdogo.LEMA katoa wito wa kufunga na kuomba kwa Mungu siyo dini fulani kama ulivyomezeshwa.MAANA YAKE NI DINI ZOTE ZA KIGENI NA ZA JADI KAMA ILE YETU WASUKUMA WA JADI YA KUTAMBIKA.Tayari Babu yangu kasha mwandaa ng'ombe dume mweusi ili tumtolee tambiko mh Lema na TZ kwa ujumla kama alivyowahi kutambikiwa Baba wa Taifa enzi za kutafuta Uhuru.Tunaamini Mungu atapokea dua zetu
 
Ni lazima Nape au Mwigulu waje humu watujibu hili swali,
hivi ni kwanini pro-ccm hamtaki kusikia neno Mungu? Kwa hali hii basi mtasema makanisa na misikiti ni CDM kwani wote wanataja Mungu.
KAMA PRO-CCM MMEANZA KUPIGANA VITA NA MUNGU! Basi hii ni kazi kweli kweli

Kuzimu kunaingoja ccm na wa2wake
 
Ni lazima Nape au Mwigulu waje humu watujibu hili swali,
hivi ni kwanini pro-ccm hamtaki kusikia neno Mungu? Kwa hali hii basi mtasema makanisa na misikiti ni CDM kwani wote wanataja Mungu.
KAMA PRO-CCM MMEANZA KUPIGANA VITA NA MUNGU! Basi hii ni kazi kweli kweli

Kuzimu kunaingoja ccm na wa2wake wakiongozwa na mkapa
 
Mwambie Wassira,Komba na Lucinde wakatubu,maana video za matusi yao tunazo.LEMA hakutukana wala ushahidi haupo.
Wapo nyomi sana wakutubu,ukiachilia mbali hao wa matusi, wapo wanao sababisha vifo vya wtz kwa ugumu maisha,huku wao wakifaidi keki ya taifa mfn:MKAPA.
 
Utusamehe Makosa Yetu,kama Nasi Tunavyowasamehe Waliotukosea,na Usitutie Majaribuni Bali Utuokoe Na Yule Mwovu!
 
MH LEMA jana alitangaza kuanza maombi ya kufunga na kuomba kwa siku saba kuanzia jumatano ya tarehe 11 April 2012 na kuomba kila mwananchi anayependa haki kwa imani yake kumuunga mkono katika maombi hayo ya kufunga na kuomba. Pia aliomba maombi hayo yaendane na kuwasaidia maskini na wajane na wale wasiojiweza kwa vile vitu ambavyo Mungu ametubariki kwavyo.

Lengo kuu la maombi hayo ni kumuomba Mungu aingilie kati na kulipiza kisasi kwa wale ambao wametumia nafasi zao kushinikiza hukumu isiyo ya haki ambayo ilitolewa hivi karibuni na kumfanya aende likizo katika nafasi yake ya ubunge na pia maombi ya shukrani kwa Mungu kwa yote yaliyotokea. Hayo aliyasema jana katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya NMC jijini Arusha.

Mungu hawasikii wenye dhambi.Kwa moral standard ya Lema,anashinda njaa bure,nothing will happen.
 
TONGUE TWISTERS AT WORK.
hawaambii ukweli huyo, anafunga na kuomba TOBA kwa mungu wake kutokana na mabaya aliyoyafanya katika maisha yake.
kukatisha uhai wa watu wasio na hatia wakati akiwa kwenye zileee shughuli zake alizozizoea(...........))
kupora mali za watu walizozichuma kwa jasho.....
kusababisha UYATIMA kwa watoto wasio na hatia kwa kuwarestisha in peace wazazi wao.
kalagabahooo. hamuambiwi ukweli na kwa sababu vichwa vyenu vinafanana na huyo MINIKABANG, ni lazima mumuamini
 
Back
Top Bottom