Gharama ya kutengeneza kisima Dar

Wana JF Naomba kama kuna anayefahamu gharama za kuchimba kisima kwa Dar
anipe picha kamili,ikiwa nikuanzia kupima mkondo maji,Site ni Bunju karibu na mpiji
natanguliza shukrani.

Lady,
Gharama zinatofautiana kati ya kampuni na kampuni, lakini kati ya eneo na eneo kutegemeana na umbali wa maji chini ya ardhi. Kwa maeneo ya Kitunda, let say kuanzia Banana hadi ndani ndani kwenda Msongola, maji yapo kati ya meta 60 hadi 150 chini ya ardhi na uchimbaji wake unaweza kukugharimu kuanzia milioni 3 na kuendelea. Hiyo milioni 3 ni gharama za uchimbaji na mabomba ya kuleta maji juu, gharama za pampu, tangi na mabomba ya kusambaza maji ni nje ya hiyo m3. Normally kazi wanaimaliza ndani ya saa 24, kama kila kifaa kimeandaliwa

Kwanza kabisa nawashukuru wote kwa mchango wenu.Mwenzetu wewe uliyechimbiwa na wajasilimali
ullichimbiwa maeneo gani? je unaweza kutuunganisha na hao wajasilimali ?tutawapataje?

Kwa upande wangu, hizo gharama nilizoandika hapo juu ni kisima ambacho kimechimbwa kwa ndugu yangu, Kitunda, mwezi Desemba mwishoni, 2011. Mhusika anaweza kukupa namba za wachimbaji, anapatikana kwa 0764 518 851

Wadau kuna yeyote ambaye amechimba kisima na hao jamaa wa Drilling and Dam Construction Agency (DDCA) wa ubungo? Naomba atupe tathmini yake kama wanafaa (kwa kufanya survey na kisha kuchimba). Watu wamezungumzia diameter ya kisima, kisima kikubwa kabisa (kulingana na mabomba yaliyopo sokoni) ni kipi? Mfano kama nahitaji kisima kwa ajili ya biashara (kama nahitaji maji mengi sana) nahitaji kuchimba kisima cha diameter kiasi gani?

Hawa jamaa wanaaminika, kwa sababu ni taasisi ya serikali. Wana takwimu za kutosha za maji kuhusu maeneo mbalimbali ya Dar, kwa hiyo kwao inakuwa rahisi sana kukujulisha gharama za uchimbaji kwa eneo husika ndani ya muda mfupi. Niliwakuta mahali wanachimba, around mwaka 2009 na nilihojiana nao sana. Wao walianiambi kwamba wanafuata procedure zote za uchimbaji kisima, kabla hawajachimba, i.e. wanafanya survey ya eneo, wanalinganisha na taarifa zilizo ktk ramani zao. Wanachukua sample ya maji wakishachimba kisima, kabla hujaanza kutumia, wanapeleka maabara kwa utafiti wa usalama, kisha wanakuruhusu kutumia iwapo yako poa. Ni lengthy procedure ambayo wengi hatupendi, ila ndo ya kuaminika zaidi.

jamani me napenda kufahamu na bei ya matank kuanzia lita 1000 na kuendelea????????
La kwangu la lita 4000 nimenunua 600,000/- mwezi Januari mwaka huu
 
Hii ni mada nzuri kwani imekuja wakati muafaka ambapo watu wengi wanaweza kujitafutia mbinu mbadala za kupata maji kuliko kutegemea DAWASA n.k n.k. Msisitizo uwepo kwenye ushirikishwaji wa utaalam wa uhakika yaani wahandisi wa maji kuanzia awali (sehemu za kuchimba) hadi hatua ya kudhibitisha kwamba maji yatakayopatikana ni salama kwa matumizi ya binadamu. Muhimu pia ni udhibiti wa uchimbaji kwani kama ilivyo kwenye uchimbaji wa madini, ni vizuri kufahamu madhara (kama yapo) yatokanayo kwenye safu za miamba iliyo chini ya ardhi. Nimeshasikia ikizungumzwa kuwa DSM (hasa Kariakoo) ni janga linalonyemelea kwa kasi kutokea kutokana uchimbaji holela wa visima vya maji pasipo kuangalia na kujali umbali wa kisima hadi kingine. Tukizingatia kwamba kitendo cha kuchimba miamba kinasababisha udhaifu (iletwayo na mipasuko) kwenye hiyo miamba ingefaa wataalam watoe mchango wao kwenye kutuhakikishia kwamba zoezi hili linafanyika sawasawa. “Majuto mjukuu”
 
Nilipotaka kuchimba kisima changu na kuona haya makampuni yanavyochimba mikwara ya utafiti tu nilichoka na kuishiwa nguvu. Nikakumbuka jana yake jirani yangu aliponiambia kuna kikundi cha vijana wajasiri mali wanachimba kisima kwa gharama nafuu na wana uzoefu wa kujua kama maji yanapatikana au laa katika eneo hilo. Nikaamua kurudi niwatafute hao vijana, na kweli walipofika eneo hilo wakafanya utafiti kutokana na visima vilivyochimwa awali na wakasema 90% maji yapo chini ya ardhi Ft 80 - 100.

Ingwawa ilikuwa risk nilijilazimisha kuwaamini kutokana na majirani wa hapo kuwa na visima vingi tu vya maji. Bila ajizi vijana wali-drill kisima cha maji kwa zana zao za kimachinga na walipofikia Ft 55 dalili za maji zilianza na wakanihakikishia wanataka wafikishi ft 80 ili kupata maji baridi bila chumvi.

Nikuhakikishie hadi leo napata maji safi baridiii toka Ft 80 chini ya ardhi kwa gharama nafuu sana, kwani gharama zote za kuchimba kisima na kukamilika kuweka pump ilinigharibu Tz Shs 1,200,000. Gharama hii ni tofauti na ile waliyoniambia wataalamu maana wao utafiti tu zaidi ya laki tatu zingenitoka.
  • Mambo ya msingi yanayotakiwa uyaandae ni kujaribu kuangalia waliokutangulia maeneo hayo kama wana maji ya visima na pia kujirishisha kwamba eneo lako haliko kwenye mwinuko zaidi ya wenzako walio na visima eneo lako.
  • Ukubwa wa kisima chako ni diameter ngapi kulingana na mabomba mengi yanayopatikana ambyo kwa kawaida ni mabomba magumu ya Plastic yatakayozamisha ili kuhifadhi maji ndani ya kisima chako.
  • Kuna mchanga wa pekee wa kutiwa kwenye basement ya kisima chako na kando ya bomba ili kuchuja maji yawe maangavu zaidi, wachimbaji wa visima wanajua wapi kwa kupata mchanga huo hasa kandokando ya vijito vya maji, na kuna wauzaji mitaani wa mchanga huo ila hakikisha umehakikiwa na wazoefu wa visima vya maji usijechukua mchanga unaotoa vumbi k uchafua tena maji yako zaidi.
  • Mabomba yatakayounganishwa hadi chini ambayo ni ya plastic ya kuhifadhi maji tokana na chemchemi.
  • Kifuniko cha juu kwenye kisima chako ili kulinda na kuhifahdi kisima kisiharibiwe na maji machafu yasiingie tena.
  • Pump ya maji na tank la maji.
Maelezo hayo ni kwa kisima ambacho ni drilled ambacho pia ni salama kwa familia yako tofauti na kisima chenye shimo kubwa la kuchimbwa ambalo pia si salama kwa famili na huweza sababisha mmommonyoko wa ardhi.

Kama nafasi inakuruhusu kuwatumia wataalamu zaidi ni bora tu ila ujue gharama nazo zinaendana na kiwango cha ukubwa na elimu ya mtu.

Jamani tuwe wa kweli tusichangie kufurahisha tuu hii figure ya 1.2M ni dnogo sana kimsingi mimi nakifanyia ukarafati kisima changu cha 70M gharama za kununua control box, DP switch, AVS, stabiliser pamoja na pump [pump ya kawaida sana] tu ni lakhi 9 na hapo sijaweka gharma za cable ya 2.5 ya mita takribani 80 na kila mita ni 5,000/= ambapo tunapata ukijumlisha na ufundi na ikumbukwe hapa nafanya ukarafati wa kisima kilishochimbwa sasa jamani tuache porojo 1.2M is not enough otherwise am stand to be corrected!

Evaluation ya kama maji yapo au hayapo ni 200,000TShs nilifanya 2009 nadhani kama itakuwa imepanda sio sana na mimi nipo Kisarawe so i gues maeneo yako inaweza kuwa ktk hayohayo mazingira.
 
i think this is one of the most useful thread for this year...thanks LadySwa for bringing this one

what if nataka kufanya small scale irrigation?? nina eka kama kumi hivi kweny udongo wa kichanga
 
Nilitaka kuchimba kisima kwa ajiri ya irrigation Dodoma nikawafuata hao jamaa wa DDCA wa pale geti la kuingilia chuo mlimani cost ya kufanya survey tu ya maji wakaniambia 2.5M kwasababu ya umbali nadhani kiherehere chote kikaniisha ila hao jamaa ni wa ukweli sana kazi zao ni nzuri tatizo ni cost zao zipo juu sana,kwa anayejua kampuni nzuri ya drilling Dodoma tupia contacts hapa tafadhali
 
Jamani tuwe wa kweli tusichangie kufurahisha tuu hii figure ya 1.2M ni dnogo sana kimsingi mimi nakifanyia ukarafati kisima changu cha 70M gharama za kununua control box, DP switch, AVS, stabiliser pamoja na pump [pump ya kawaida sana] tu ni lakhi 9 na hapo sijaweka gharma za cable ya 2.5 ya mita takribani 80 na kila mita ni 5,000/= ambapo tunapata ukijumlisha na ufundi na ikumbukwe hapa nafanya ukarafati wa kisima kilishochimbwa sasa jamani tuache porojo 1.2M is not enough otherwise am stand to be corrected!

Evaluation ya kama maji yapo au hayapo ni 200,000TShs nilifanya 2009 nadhani kama itakuwa imepanda sio sana na mimi nipo Kisarawe so i gues maeneo yako inaweza kuwa ktk hayohayo mazingira.

Gharama halisi za kuchimba kisima kwa mitambo ya gari ni kati ya shs. 50,000/= hadi 70,000/= kwa mita moja. Gharama hizi hazihusu pump ya kuvuta na kusukuma maji, wanachimba na kufunga mabomba na kusafisha kisima kwa kupuliza upepo ndani ya kisima, wanatayarisha report na kupima maji.
 
well kwa ujumla naona uchimbaji wa dar ndo umezungumziwa hapa..................kuna yeyote mwenye taarifa za mikoani hususan Dodoma?
 
Je wapi naweza kupi maji ukiachia pale chuo cha maji, gharama zao niliona ni juu sana. asante
 
Sasa nimekua najiandaa toka mwaka jana,ndo mda wa kufanya kazi.
Nashukuru kurudi hapa na kukuta mambo mengi yame wekwa wazi.
Sasa kazi tu.
 
Kwa wale wenye mashamba na mifugo, nilibahatika kumpata mchimbaji kutoka Kigamboni, huyu bwana nilimfahamu kupitia jukwaa hili. Kisima alichonichimbia ni cha ringi kina urefu wa ft 60, kwa saa moja kinatoa maji lita 2000. Gharama yake ni 950,000/=

Anaitwa Mzee Madomado 0786 796571 au 0768 607161

Bado sijapata pump ya kuvuta maji, tafadhali kama yupo mwenye ujuzi wa pump anifahamishe kwa eneo lisilokuwa na umeme.

Maji ya chumvi yanafaa kwa mifugo na kilimo?
 
Je wapi naweza kupi maji ukiachia pale chuo cha maji, gharama zao niliona ni juu sana. asante

Mkuu kama hujapima bado jaribu sehemu zifuatazo.
1. TBS wana maabara ya kemia na microbiology
2. Ardhi University wana maabara ya mazingira (environmental lab.) na wanapima both chemical and biological
parameters
3. TIRDO (ilipo bodi ya mikopo), wana maabara ya kemia na microbiology.

Uzuri wa TIRDO na TBS maabara zao zimekuwa accredited kwahiyo ni nzuri zaidi.
All thes best.
 
mkuu samahani.. nilikuwa nataka kujua hayo maji baridi ni maji yasio na chumvi? Mimi niko Dar maeneo ya tabata na ninahitaji kuchimba maji ila juz juz hapa nimefatilia nikaambiwa million tatu na nusu hivi kuanzia survey mpaka uwekaji wa pump..
sasa nilikuwa nakuomba unisaidie mawasiliano ya hao vijana.
asante
 
Back
Top Bottom