Ghala la silaha Gongo la Mboto lalipuka!

Kova yupo laivu itv, anasema watu watulie na warudi majumbani mwao! Anasema ni ajali.
 
Waziri wetu mkuu Pinda aandae "machozi" mengi yakumwaga ili aweze kuseek "simpathy" ya Watz
 
Wamekufa watu kibao wao wanasema ni mmoja tu? huyu RC vipi?
 
Tetesi: Kesho asubuhi bungeni, Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama, Rais Mtarajiwa na Waziri Mkuu Shujaa, Edward Ngoyai Lowassa, atatoa taarifa kuhusiana na tukio la Mbagala na kutaka Waziri wa Ulinzi na JKT, Dk. Hussein Mwinyi ajiuzulu na uchunguzi wa kina ufanyike haraka wakati kamati yake inaunda Kamati Ndogo ya Uchunguzi itakayoongozwa na yeye mwenyewe.

Rais mtarajiwa? Mmh bao la kisigino.
 
Mkuu wa mkoa Dar anaongea redio one!!
Anasema wananchi wasogee hadi maeneo ya tazara! Mienendo ya ndege katika uwanja wa taifa umesimamishwa!! Kwa mujibu wa jeshi la polisi Mtu mmoja amepoteza maisha, na majeruhi 43!! Wamepelekwa hospilati za Temeke... Na wakizidi watapelekwa mwananyamala na Muhimbili
 
Kamanda wa polisi,Kova ametoa tamko juu ya mabomu yaliyolipuka gongo la mboto,na kusema ni ajali 2,na uchunguz unaendelea kufanyika!wa2 wa2lie majumban mwao
 
KOVA kupitia ITV anasema eti ni ajali tuu,watu wasizagae warudi majumbani!huku shimbo anasema 10km radius kusiwe na watu!tushike lipi tuache lipi?
 
wadau naingia jamvini muda huu nikiwa ni muathirika wa mambomu na nilikuwa huko na ndipo napoishi, nimeendesha gari pasipo kujijua na sijui nyumba yangu itasalimika ama la, imenilazimu niingie jamvini niwape hali halisi na si kuhadithiwa, NI HATARI SAANA WADAU.
Sasa rasmi ninailaani serikali hii, ni adha kubwa na nimeiharibu mpaka gari kwa hamaki ya kuinusuru my family.

jamani poleni.
Nasikia mmeambiwa mkimbilie mjini.
Sipo huko ila roho yangu haina amani. Watu wangu wapo huko.
Hakuna walioumia?
 
This is no longer bearable. This gov has to go. Why did they not learn from mbagala experience? Kuna nchi nyingine uzembe kama huu unatokea?
It has happened in mozambique with a big loss of life.Actually it happened three times in maputo and the last one in i think 2008 was really bad.
If we have no clue on how to store explosives we should not own them.
 
subirini kesho itaundwa tume ya kuchumbuza mabomu ya gongo la mboto, na mtaambiwa pia, mabomu yemekorofisha mfumo wa umeme! Yangu masikio
 
mimi sitaki details, nasubiri tume nyingine kuchunguza hii nayo! Ile ya mbagala je!? Aah hapa bongo historia haina uhusiano na maisha yetu ya sasa!
 
this is serious!
Nina ndugu zangu kibao maeneo ya Gongolamboto, Kipunguni na Ulongoni....Simpati hata mmoja!
 
mmmmhhhhh inatisha!!!! how safe are we in this country??
Michelle mwulize mkwere na serikali yake zembe na pumbavu mpaka watu wasio na hatia wanapoteza maisha. Kama sababu ni umeme RA, Lowassa, Ngeleja, Kikwete hii damu ijuu yenu. Mimi nakasirika kupita maelezo.
 
Jamani naomba kuulizia hali za watoto wa PUGU secondary ikoje coz hiyo shule huwa inapakana kwa karibu na eneo hili la jeshi, sasa sipati picha wale watoto watakuwa katika hali gani.

Mungu wangu ile shule Jamani jamani..........!!!! Eeeh mungu weeee...!
 
Dr Hussein mwinyi ametangaza kupitia clouds fm kwamba ni magala ya mabomu ndo yamelipuka na sasa wanadhibiti moto usiendelee maeneo mengine
 
Back
Top Bottom