Ghala la silaha Gongo la Mboto lalipuka!

Habari za uhakika ni kuwa mabomu yamelipuka tena, safari hii sio mbagala bali ni kambi ya jeshi gongolamboto
 
Me nimetoka nje, dizain ni mabomu kweli kwani mitaa ya huko kunaonekana moto mkubwa unaonekana juu
 
Mweh..... Mimi niko mitaa ya K'yama na nasikia hasa hili la sasa ni kubwa mno mpaka nyumbayangu imetingishika na madirisha yametaka kung'oka hvi, Mweh nimchukua mwanangu nimetoka nae nje maana alikuwa kalala....!!!!!:twitch:

Wa Ukonga jamani Poleni maana mi niko huku nimetishika hv sasa nyie wa G'mboto je... Poleni sana na wengine ambao mtakuwa mmezthirika pia nawapa pole nyingi sana mwenyezi mungu awalinde
 
Hali ni mbaya sana. Nimeongea na mshikaji yuko Kigamboni, watu wakimbia kimbia hovyo. Milipuko ni mikubwa sana na inatisha.
 
milipuko mitatu imesikika mpaka sasa hali inaonekana ni mbaya na imetokea baada ya kukatika kwa umeme
 
Nyie watu mbona mnaturusha roho huu sio uongo kweli!!?
Sema nasikia milipuko!!!
 
Kwa nini Mabomu yanawekwa kwenye sehemu za kuishi watu? unyonge wetu ndio unatu-cost sasa.
 
Back
Top Bottom