GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 4,916
- 6,686
Mikoa yote miwili, Geita na Njombe, inalingana kiumri. Ilianzishwa mwaka 2012.
Kila mkoa una rasilimali ya kipekee tofauti na mkoa "mwenzake". Njombe kumeshamiri kwa kilimo, hasa miti ya mbao na nguzo pamoja na kilimo cha parachichi, wakati Geita inatamba kwa uchimbaji dhahabu.
Kwa utajiri mkubwa ulio nao, utajiri wa dhahabu, Geita ilistahili kuwa miongoni mwa mikoa iliyoendelea sana.
Nimekuwepo Njombe kwa siku kadhaa sasa. Inaonekana mji unakuwa kwa kasi. Kuna uwekezaji mkubwa sana kwenye kilimo cha miti na parachichi, uwekezaji ambao unaendelea kukua kwa kasi.
Nimeiona stendi yao. Ni nzuri kuliko ya Geita.
Katika tembea yangu maeneo mbalimbali, sijafanikiwa kuona nyumba iliyoezekwa kwa nyasi.
Inaonekana watu wa huku Njombe wana hulka ya kupenda maendeleo. Wanaonekana ni wachapa kazi.
Japo sojapita maeneo yote ya huu mkoa , lakini kwa maeneo machache niliyofika, inaonekana ni mkoa wenye future nzuri.
Geita, pamoja na utajiri wake mkubwa wa dhahabu, usipokuwa makini, itakuja kupitwa mbali sana na Njombe, mkoa wa kilimo.