Nimemkwaruza jamaa kidogo tu ubavuni, we, we, we we, nilijuta. Akashuka mbio tukaanza kubishana, Traffic akawa anatuangalia kwanza tunavyobishana, kisha akasogea karibu akasema hebu pakini pembeni mna sababisha foleni, jamaa anakomaa hapana hadi upime.
Traffic akapima fasta tuka park pembeni, mimi nikawa muungwana nikamwambia jamaa, mkuu nikupe shingi ngapi ukarekebishe, akasema eti yeye sio fundi, hawezi kukadiria, nikamwambia tuongozane nikamrekebishie akaniuliza wapi?
Nikamwambia garage akaniambia eti yeye anagereji yake na hatakubali gari yake itengenezwe na mafundi asio wafahamu.
Yule traffic akaja tena akauliza mnataka nini, nikamwambia mimi sitaki kupotezeana muda ntamrekebishia gari yake, jamaa akaongea ongea na traffic badae akakubali Nikampeleka garage nnayo ifahamu mimi nikaongea na fundi nikamlipa, jamaa akaanza utata tena, eti nani atasimamia gari ikiwa inatengenezwa?, heee" nikamwambia mi nishalipa wewe baki hapa usimamie kwakuwa mimi sijui maswala ya ufundi kwa hiyo sina cha kumuelekeza fundi.
Fundi akaingilia akamwambia acha namba yako ya simu ikiwa tayari ntakupigia, akaacha namba kwa shingo upande, siku iliyo fuata akaenda kuchukua ugonjwa wake wa moyo. Nilishangaa mtu anaiona gari kama binadamu!!!!!!.
Hahahahaaa kama upo humu am sorry.
pole sana mtoa mada japokuwa nimechelewa lakini huyo mtu hajakosea,hata kama gari lake la mkopo lakini kumbuka ni hela yake ambayao anakatwa kidogo kidogo,2 ulitaka mlipane palepale amsema kwel yeye hajui makadilio ya palipo haribika,pia kumbuka wengi wanaomiliki magari wanakuwa na mafundi wao waliowazoea na kuwaamini, la msingi kuwa makini barabarani