Fursa za Ajira kwa Vijana Zinasaidia Kuongeza Kodi kwa Serikali

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
MHE. GEOFFREY MWAMBE ASEMA FURSA ZA AJIRA KWA VIJANA ZINASAIDIA KUONGEZA KODI KWA SERIKALI

"Nakishukuru Chama Cha Mapinduzi kinachoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutupigania watanzania na Jimbo la Masasi kuhakikisha changamoto za Masasi zinaondoka na Masasi sasa hivi ni mpya" - Mhe. Geoffrey Mwambe, Mbunge wa Jimbo la Masasi

"Kwa Serikali, kipaumbele cha kwanza ni Ajira kwa vijana. Tukitengeneza fursa pana za ajira kwa vijana tunaongeza kodi za moja kwa moja kwa vijana kutoka kwenye mishahara yao (Personal Income Tax) na Makampuni watalipa kodi (Cooperate Income Tax) ambayo ni ya uhakika kabisa" - Mhe. Geoffrey Mwambe, Mbunge wa Jimbo la Masasi

"Tukifanya hivyo tunaweza kutoa fursa kubwa sana kwa Serikali kukusanya kodi ambayo inaweza kusaidia kwenye matumizi. Hii inaendana na adhma ya kupanua Tax Base kama alivyosema Mhe. David Mwakiposa Kihenzile" - Mhe. Geoffrey Mwambe, Mbunge wa Jimbo la Masasi

"Tun walipa kodi wachache sana nchini. Sensa imeonyesha tupo watanzania million 61 lakini walipa kodi ni kama Milioni 3 tu wenye Active TIN ambayo ni watu binafsi na makampuni. Matokeo yake msongamano unakuwa ni mkubwa, wachache wanaolipa kodi wanalazimika kulipa na kukamuliwa kodi sana ili kufikia malengo ya nchi" - Mhe. Geoffrey Mwambe, Mbunge wa Jimbo la Masasi

"Tungetanua Tax Base tungerahisisha na kufuata sheria tano za usimamizi wa kodi kwamba kodi lazima kuwe na Finance, Adequacy(Itosheleze Serikali), Simplicity (Urahisi wa ulipaji), Transparency na Administratively (Easiness) ili kusaidia vijana kupata ajira na kupata fedha za kutosha" - Mhe. Geoffrey Mwambe, Mbunge wa Jimbo la Masasi

"Nchi yetu asilimia 60 mpaka 70 ni Mfumo sekta, kule kodi hazipatikani kirahisi kwasababu siyo sekta rasmi. MKURABITA lengo kubwa ilikuwa ni kutengeneza utaratibu wa makampuni mbalimbali na watu binafsi shughuli zao ziweze kurasimishwa ili waingie kwenye mfumo kamili kulipa kodi" - Mhe. Geoffrey Mwambe, Mbunge wa Jimbo la Masasi
 

Attachments

  • Eoe4rw5XcAEKjyY.jpg
    Eoe4rw5XcAEKjyY.jpg
    35.4 KB · Views: 4
Back
Top Bottom